

Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
We Michuzi acha kutuyeyuha hapa! Huyo mwenye mkangafu (Tom Mweuka) alikuwa anafanyia Television gani wakati huo?!! Kulikuwa hakuna television zaidi ya ile ya Zenj! Zetu za tisini mwanzoni
ReplyDeleteWe Michuzi acha kutuyeyuha hapa! Huyo mwenye mkangafu (Tom Mweuka) alikuwa anafanyia Television gani wakati huo?!! Kulikuwa hakuna television zaidi ya ile ya Zenj! Zetu za tisini mwanzoni
ReplyDeleteMjomba Michuzi katika siku Uliyonikuna basi leo kwa kutoa picha hizi, Huyo mzee anayekunja Shati ni mjomba wangu alijulikana Kwa Jina La Mzee Sheni ambaye alikuwa mpishi Hotel Kilimanjaro enzi hizo. Mzee huyo sasa ni Marehemu kwa watu wa Kagera Rangers Mwembe chai watamfahamu na alikuwa na Bar Yake mtaa wa Mengo na Kagera ikiitwa Sheni Bar enzi hizo. Ahsante bwana michuzi ni mimi Mbegu tena
ReplyDeleteWatu wengine wanapenda kubisha kila kitu, hata kama haitakiwi kufanya hivyo. Soma habari vizuri kabla hujatuma comment yako.Michuzi hajaandika kwamba huyo bwana alikuwa kwenye kituo cha Television, kaandika kwamba alikuwa akifanya kazi kituo cha habari, P'se!!
ReplyDeleteMtoa maoni Anonymous wa 8.55pm
ReplyDeleteUnaejiita Mbegu wewe ni Mbegu uliyesoma Lugalo Primary School?
Historia ya picha hii!
ReplyDeleteMohamed Ali alkuja Tanzania kama mjumbe wa Marekani. Mwaka huo Marekani alikuwa inafanya kampeni ili nchi zisusie michezo ya Olympic yaliyofanyika Moscow, USSR. Sasa ilikuwa ilikuwa ni uvamizi wa USSR nchini Afghanistan.
Huyu anayekunja ngumi alikuwa kocha ngumi Tanzania. Ninamkumbuka kwa jina mmoja tu, BADRU.
kumbukumbu nzuri
ReplyDeleteBadru Hussein aliyekuwa kocha wa Bandari alimkunjia ngumi Mohamed Ali uwanja wa ndege siyo Kilimanjaro Hotel. Huyo pichani si Badru Hussein inawezekana akawa Mzee Sheni kama alivyosema anon..
ReplyDeleteMohamed Ali alipata mapokezi ambayo yalimfundisha kuwa Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kwenye ukombozi wa kusini mwa Afrika. Waandishi wa habari walimuita kikaragosi cha wazungu.
Wanaokumbuka tunaomba habari zaidi.
F M Tungaraza.
Anon uliyesema huyu Mzee alikuwa anaitwa Mzee Sheni umenikumbusha. Kama sikosei huyu Mzee Sheni wafanyakazi wenziye pale Kilimanjaro Hotel walikuwa wanamuita jina la utani Mzee Binaisa.
ReplyDeleteAsante,
F M Tungaraza.
Issa Michuzi huyo ni Mzee Sheni, Sio Badru Issa michuzi pic zengine wewe ulikuwa ukisoma bado, unapoweka fanyia uchunguzi kwanza. Issa Michuzi tunaomba tafuta za Malcolm X alipokuja Tanzania ila namjuwa mtu anayo ya Malcom X na Abrahman Babu aliyekuwa NCCR walipiga pamoja.
ReplyDeleteNi mimi Mbegu tena narudi Kwanza napenda kumjibu jamaa aliyeniuliza kama nilimaliza Lugalo la Mimi nilimaliza Karume Primary School na ndio maana namjua vizuri sana huyo mzee Sheni kama nilivyosema ni mjomba wangu na lingine ni kwamba hiyo picha sio kama hapa kwa michuzi ndio mara ya kwanza kuiona niliona na Nakumbuka Mohamed Ali alivyokuja hapo Bongo, Picha hiyo ilitolewa kwa mara ya kwanza ktk Gazeti la Michezo lililokuwa likitolewa kila Mwezi kama sikosei na hata Marehemu Mzee sheni mwenyewe alikuwa na Original copy ambayo alikuwa ametunga Sitting Room kwake. huyo jamaa aliyesema huyo Badru si kweli, Mdogo wake mzee badru tunayehapa Coventry, UK Khamisi Badru naye amekataa, Ni kwamba huyo ni mzee Sheni na kama mdau alivyosema wafanyakazi wa Kilimanjaro wakimtania Binaisa. Ana Watoto Watatu Moshi Sheni, Selemani Sheni na Tabu sheni ulizia Kagera Rangers Mwembechai.
ReplyDelete