JK – na “Perestroika” ya Tanzania
Salute JK – Ninfahamu fika kwamba kazi hii si yake peke yake lakini hekima zake za uongozi ndiyo zimetufikisha hapa tulipo leo tukishuhudia hukumu na sauti za wananchi zilivyo na nguvu zenye hoja madhubuti na hata kurekebisha yale ambayo labda kwa kipindi Fulani yalionekana tayari yamekuwa si tabia njema kuyakemea wala kuyazumgumzia maana yaliwahusu watu wenye dhamana kubwa ndani ya uongozi wetu wa nchi.
Huwa inatokea kwamba binaadamu taratibu anajenga mazoea ya mazingira yake mara anapojihusisha na kujilengesha zaidi na mazingira hayo kwa dhamira ya kujikimu, na mara kwa mara hupambana ili tu mambo yake yawe yakienda kwenye msitari uliyo mbele ya maisha yake kwenye kipindi hicho.
Sasa, kwa kipindi cha takriban miaka kumi na mitatu Watanzania kwa ujumla wao walijikuta wakibadili mifumo ya maisha yao bila ufahamu mkubwa kwamba madiliko haya yanaletwa na tabia ya binaadamu kujikimu na kuambatanisha maisha yake na mazingira yaliyo mbele yake, ama kwa kusema “heri nusu ya shari kuliko shari kamili”. Hapa, sina maana ya kumlaumu Mtanzania yeyote, kusudio langu ni kujaribu kutafakari miongo ambayo huleta matabaka ya kuwa na wenye uwezo mkubwa, uwezo wa kati na wasio na uwezo kabisa wa kujikimu kimaisha. Tofauti na siku za nyuma za utawala wa Mwl. JK Nyerere, utawala baada yake umekuwa ukijaribu mambo mengi lakini si kujifunza kutokana na uzoefu na historia ya mambo ya nyuma bali kubunu kabisa mitaala mipya yenye uzoefu mdogo na hata kufikia hali ambayo tumeiona hivi karibuni kwamba kwa mpigo (tofauti ya dakika) mawaziri watatu wamejiuzulu ikiwemo Waziri kiongozi wa shughuli za serikali (Waziri Mkuu). Na si kwa sababu walipenda ama walitaraji, bali yote yaliyojiri mpaka wao kufikia uamuzi huu yalikuwa ni mambo ya utendaji dhaifu na wa aibu kwa nchi.
Ninashukuru watanzania na hasa wabunge kwa mioyo ya subira kusikiliza utetezi dhaifu hasa wa Mheshimiwa Msabaha na Mheshimiwa Karamagi hasa pale walipokuwa wakifanya mzaha wa maneno ya utani na kejeli mbele ya swala zito ambalo limeathiri wananchi wengi kama si umma wote wa watanzania nje na ndani ya nchi.
Hakika mpaka hivi sasa ninajiuliza, kweli mtu mzima kwa makosa kama haya ya kutesa wananchi anaweza akasimama na kutoa utani wa kikabila kwa Mheshimiwa Spika wakati ana jambo zito mbele yake la kulitafakari?
Mimi ningelitegemea kwamba angetoa maneno ya kuomba radhi kwa kusema “kama binaadamu nami nina mapungufu na si kwamba tulifanya yaliyojiri kwa makusudi mazima bali ni mapungufu yetu sisi kama wanaadamu, hivyo kwa hili ningependa kuchukua fursa hii kuwajibika na kujitolea kuwa pamoja nanyi kwa ufuatiliaji wa swala hili mpaka hapo litakapo rejea kuwa na majawabu sahihi” Hakika haya yangekuwa maneno yenye busara nyingi na siyo ambayo yalisemwa na mheshimiwa mmoja katika hili jopo la uwajibikaji wa aina yake nchini kwetu. Nina amini kwamba huyu ni samaki aliyekauka hakunjiki, hivyo mengine tuyaachie dunia itoe funzo lake.
Nina furaha na faraja nikiwa ninaandika makala hii, na si kwa sababu nimepata nafasi kuyanyooshea kidole mapungufu ya hawa viongozi wetu, bali sasa panaonekana kwamba mbele yetu “Light at the end of the Tunnel” siyo taa ya gari moshi linakuja bali ni mwangaza wa nuru, tunakwenda kwenye kheri….. Salute JK.
Nina imani kwamba mabadiliko haya ambayo yanaendelea kwenye uwanja wa Siasa nchini kwetu yataleta chachu na hata kutizama tena dira yetu ya Maadili ya Uongozi inaelekea wapi kabla mambo hayajawa mabaya kiasi hiki. Tuache tabia ya “Rais ameagiza” ama “Waziri Mkuu amemuagiza..” ila tufuate taratibu za uongozi na miiko yake. Hivi kwa nini tusirudie Azimio la Arusha jamani? Kwani lina matatizo gani? Nani alikaa chini akachambua kitaalamu ili atuelezee kwamba katika Azimio la Arusha miiko ya uongozi ilipitwa na wakati!!! Ama kitu kingine chochote ambacho kweli kipo “obsolete”. Ikibidi basi tuwe na mizani ya kupima hata wabunge wetu maana nimeona kuna watu amabo wapo huko vijijini mwetu wana uwezo wa kujieleza na kulezea matatizo ya jamii zao kwa ufasaha mkubwa kiasi kwamba unatahayari kwa kusema kwa nini huyu mtu asipewe hiyo nafasi ya uwakilishi?
Kwa mtizamo huu, mimi binafsi ningependekeza Serikali ianzishe utaratibu wa kuwa na wawakilishi wa kutoka ngazi za chini kabisa ambao wanatoka kwenye mshina hasa ya maendeleo ya wananchi wapewa nafasi ya kutoa mchango wao moja kwa moja kufika kwenye sehemu ya uwakilishi bila ya kupitia kwa wabunge hawa ambao timeona picha ya baadhi tu huku nikiwa nina imani kabisa hata hawa wengine nao wana mambo yao ila tu wakati haujafika tukayapata bayana. (Kazi unayo Dr. Slaa na Mheshimiwa Kabwe kufuatilia na kuibua)
Salute JK.. Kila la kheri katika hii “PERESTROIKA” ya Tanzania.
kolazarzar@yahoo.com

jammeni wadau, hebu acheni ku post comment ndefu ka mpo kwenye gazeti la mzalendo, inachosha jamani, time time, unaweza sema kwani nimeng'ang'anizwa soma?? sio hivyo ila inachosha jaribuni kufupisha kidogo mhh, mmezidi sasa,
ReplyDeleteafadhari hii, kuna yule mtu mwingine wa sydney sijui, yani mzalendo tatu, sijui hamna kazi za kufanya, halafu mnarudia rudia maneno tuu, michu piga marufuku hii kitu.
michuzi uwe unapost mistari mitatu tu, zaidi ya hapo mwenye coment alipie, sisi ni wazembe wa kusoma ndo maana tunapenda news za picha, tukiona picha tunajenga habari wenyewe kichwani, jamaa kama mna maelezo mengi anzisheni blog zenu muwe mnaeleza hapo, hii ya picha tuwachieni wachovu wa kusoma.
ReplyDelete