Rais: Jakaya Mrisho Kikwete a.k.a JK
Makamu wa Rais: Dk Ali Mohamed Shein
Waziri Mkuu: Mizengo Kayanda Peter Pinda
1. Waziri wa Nchi (Utawala Bora): Bi. Sophia Simba
2.Waziri wa Nchi (Menejimenti ya Utumishi wa Umma): Bi. Hawa Ghasia.
3.Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Masuala ya Muungano): Bw. Mohammed Seif Khatib.
4.Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira): Dk. Batilda Buriani.
5.Waziri Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): Bw. Philip Marmo
6.Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI):Bw. Steven Wasira - Naibu ni Bi. Celina Kombani.
7.Waziri wa Mipango na Fedha: Bw. Mustapha Mkulo - manaibu ni Bw. Jeremiah Sumari na Bw. Omar Yusuph Mzee.
8.Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii: Profesa David Mwakyusa - Naibu ni Dk. Aisha Kigoda
9. Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi: Bw. John Chiligati.
10.Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi: Profesa Jamanne Maghembe - Manaibu ni ]Bi. Gaudentia Kabaka na Bi. Mwantumu Mahiza.
11. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia: Dk Shukuru Kawambwa - Naibu wake ni Dk. Maua Daftari
12. Waziri wa Miundombinu: Bw. Andrew Chenge - Naibu ni Dk. Makongoro Mahanga.
13.Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo: Kapteni George Mkuchika - Naibu ni Bw. Joel Bendera.
14. Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana: Profesa Juma Kapuya - Naibu ni Bw. Hezekiah Chibulunje.
15. Waziri wa Maji na Umwagiliaji: Profesa Mark Mwandosya - Naibu ni Bw. Christopher Chizza
16. Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Waziri: Profesa Peter Msola - Naibu ni Dk. Mathayo David Mathayo.
17. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto: Bi. Margaret Sitta - Naibu ni Dk. Lucy Nkya
18. Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi: Bw. John Pombe Magufuli - Naibu ni Dk. James Wanyancha.
19. Waziri wa Maliasili na Utalii: Bi. Shamsha Mwangunga - Naibu ni Bw. Ezekiel Maiga.
20. Waziri wa Mambo ya Ndani: Bw. Lawrence Masha - Naibu ni Balozi Khamis Kagasheki
21.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa: Bernard Membe - Naibu ni Balozi Seif Idd.
22. Waziri wa Nishati na Madini: Bw. William Ngeleja - Naibu ni Bw. Adam Malima.
23. Waziri wa Katiba na Sheria: Bw. Mathias Chikawe.
24. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa: Dk. Hussein Mwinyi - Naibu ni Dk. Emmanuel Nchimbi.
25. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki: Dk. Diodorus Kamala - Naibu ni Bw. Mohamed Abood Mohamed
26. Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko: Dk. Mary Nagu - Naibu ni Dk. Cyril Chami.


hivi huyo sofia simba yupo makini kweli? mi naona kama anabebwa tu, i doubt! anyway kikubwa asiwe fisadi tu, kwasababu tutamlowasa tu!
ReplyDeletekumbe jk kabadili makamu wa rais mbona hatujaskia?
ReplyDeleteKazi nzuri Bro Michu kwa kutupasha habari moto moto zinazojiri huko nyumbani.
ReplyDeleteUbarikiwe kwa kipaji ulichojaaliwa
Ina maana waziri wa Sheria hana Naibu?
ReplyDeleteBARAZA LIMEJAA WASOMI KIBAO!!!! MA DAKTA WAKO JUMLA YA KUMI NA MBILI(12) MAPROFESA WATANO(5)DOooooo!!!!!!! SO TATIZO LINAKUWA WAPI??????????????? UZALENDO HAKUNA CHAPENI KAZI BASI.
ReplyDeleteWe anany 11:48 uko makini kweli!! i doubt, Makamu kabadilishwa wapi, makamu wa zamani alikuwa nani na wa sasa ni nani!!!
ReplyDeleteLabda kwa sababu walishakubaliana huko sijui,
ReplyDeleteKwangu, hiyo Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni kamzigo fulani ambako si ka lazima.
Je ni wizara gani inashughulikia ushirikiano wa maeneo mengine kama Kusini au Kaskazini au Mashariki au Magharibi ya afrika au Ulaya au Marekani au mbinguni n.k.?
Hiyo ingekuwa tu na Kamishna au Mkurugenzi ndani ya wizara husika ya mambo ya ndani na ushirikiano wa Kimataifa!
Pili next time wizara husika na hatimaye Bunge wapitie sheria husika kuangalia namna ya kuboresha uendeshaji wa Tawala za mikoa, wilaya na Halmashauri maana hapo napo kuna vimizigo na vikonfusheni kibao!!
Mimi ningependekeza kuunganisha ofisi za wakuu wa Wilaya na Halmashauri, kwanza ingepunguza migongano na pia kupunguza gharama za kiofisi na rasilimali Wanadamu; wote wanasimamia kitu kile kile (MAENDELEO YA MWANADAMU)kwenye Wilaya/Halmashauri!; Huku unakuwa na DAS kule unakuwa na Afisa Utumishi wa Halmashauri vurugu tupu! Mara Mkurugezi anawajibika kwa Mwenyekiti wa Halmashauri Mara anaitwa na DC na kupewa maagizo vurugu tupu!!! Tena ni wakati muafaka kukawepo viwango vya sifa (kielimu na uzoefu) za Wenyeviti wa Halmashauri (ambao kwangu ndio wangekuwa ma-DC)ambao wangeajiriwa au kupandishwa vyeo Watumishi wenye sifa badala ya kuvifanya vyeo hivyo kuonekana kama vya kisiasa zaidi.
Nimesoma eti Kinje Ngombale Mwiru ameamua kustaafu siasa,Duuh jamaa kazeeka sana toka nazaliwa yupo kwenye system na mpaka now nipo rijali mzee yupo tuuu.Afadhali Kinje umeamua kupumzika vile vile tulikuwa tumeshakuchoka sana.
ReplyDeleteBig up Michu, lakiki tuwekee pia picha zao.
ReplyDeleteKila la heri
Wee Anony wa Feb 13, 1: 49,
ReplyDeleteMjitahidi muwe munarudi nyumbani mara moja moja kuangalia kinacho endelea. KINGUNGE NGOMBARE MWIRU ndiye mzee wetu aliyejiuzulu. KINJEKITILE 'KINJE' NGOMBARE MWIRU ni mwanaye. Upo?
hapo kwa William Ngeleja/.jamani hivi huyu william ana umri gani?maana kuna kabinti chuo cha pale IFM kanasema katoto kangereja na bado kanatumia jina lingine,au baada ya kuwa waziri ndio kamajua kuwa ni baba yake?acha hizo mary.
ReplyDeletena wewe anon wa feb13,1:49 kama hujui kitu nyamaza,toka lini kinje akawa waziri?ni baba yake anaitwa Kingunge Ngombare Mwiru.na its good kaamua kujitoa katumia busara ccm wamemtumia sana.na Mungai Big -up,mnajua nini maana ya madaraka inafik atime inatakiwa kukubali kwamba umri umekwenda.
jamani angalau wamepungua sasa mbona zile nyumba zao ni nyingi sana,za mikocheni,masaki na victoria?watupangishe basi hahahhhahah
ReplyDeleteHivi humu ndani hakuna requirement ya kuwa na atleast elimu ya darasa la saba? kama hakuna naona bro Michu uanze kudai certificate ya elimu ya msingi kabla ya kupost.. Sasa huyu mdau wa Feb 13 1:49 pm anayesema Kinje kastaafu, mbona mimi najua Kinje hana hata miaka 40? Nadhani anamwongelea Kingunge ambaye ni baba mtu. Jamani Waswahili tumesoma sasa tupunguze kuposti vepa.
ReplyDeleteMdau - Boston, US
Hivi Kinje aliingia kwenye baraza la mawaziri lini? huyo jamaa hapo juu anajua tofauti ya Kinjeketile na Kingunge? Jamani lakini haya majina nayo kwa kweli Mungu atusaidie, maana yanawachanganya watu.
ReplyDeleteKinje ni mtoto na Kingunge ni Baba yake Kinje, sasa wewe uliyemchoka ni Baba mtu na sio mtoto. Au labda useme umechoka kulipa parking ya gari lako mtaani kama unalo, hapo utakuwa unamuongelea Kinje. Ukiingia kwenye serikali, ujue umegusa Baba mtu.