JK amewateua Majaji wanne wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo inasema kuwa majaji walioteuliwa ni Jaji Steven James Bwana, Jaji Bernard Michael Luanda, Jaji Mohammed Chande Othman na Jaji Sauda Mjasiri.
Taarifa hiyo iliyotangazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inasema kuwa uteuzi huo umeanza leo hii (Jumatatu, Februari 4, 2008).
Kabla ya uteuzi wake, Jaji Bwana alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha. Jaji Bwana ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 1999, pia amepata kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Jaji wa Mahakama Kuu ya Visiwa vya Seychelles, na Katibu Sheria wa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Jaji Bwana pia alikuwa Jaji Mfawidhi wa kwanza Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Biashara.
Naye Jaji Luanda, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Biashara, mjini Dar es Salaam. Jaji Luanda amepata kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, na aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka 2000.
Jaji Mjasiri alikuwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Biashara, Dar es Salaam kabla ya uteuzi wake. Jaji Mjasiri ambaye amepata kuwa mwanasheria katika Shirika la Sheria Tanzania (TLC), na mwanasheria wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA), aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka 2002.
Kabla ya uteuzi wake, Jaji Othman alikuwa katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam. Jaji Othman amepata kuwa mwanasheria katika Chama cha Msalaba Mwekundu (IRC), amepata kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Visiwa vya Timor Mashariki, na pia kuwa mwendeshaji mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda (ICTR) mjini Arusha. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka 2004.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...