je, wamkumbuka bahati iddi nzimano? yule dada wa tabora aliyezaliwa bila mikono na ambaye amekataa kuwa ombaomba mitaani kutokana na ulemevu wake? basi bahati bado anadunda na pamoja na shida ndogo ndogo za kawaida kwa binadamu yeyote anaendelea na maisha kama kawaida. hivi sasa yeye ni mjumbe wa taifa wa mkoa wa tabora katika mkutano mkuu wa chama cha wenye ulemavu nchini na mwaka juzi kwenye uchaguzi mkuu nusura aukwae ubunge kupitia viti maalumu vya wenye ulemavu. bahati haikuwa yake aliambulia kuwa mtu wa tatu. hivi sasa yupo dar kikazi na leo nimebahatika kutembelewa naye ofisini ambako hakusita kutuonesha namna anavyoweza kumudu maisha kwa kutumia miguu - kwa kupiga simu ya mkononi kwa kutumia miguu. usikose kusoma makala yake maalumu wikiendi hii kwenye gazeti la habarileo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. What a perfect world!!

    ReplyDelete
  2. Mseamakweli ni mpenzi wa mungu, Kwa kweli nimemmaind huyu dada ana mguu mzuri sana, mungu huwa hamnyimi mtu vitu vyote. Ningeomba email yake au kujua kama bado yuko single au vipi. I promise you will not regret if you will accept me. I love you.

    ReplyDelete
  3. Mungu mwema sana,wananchi inabidi tujifunze kupitia kwa huyu dada kwani kuna watu wengi sana ambao wamejibeteka tuu,na hawana ulemavu hata mmoja ndungu zangu mfano huo hapa juu,dada yetu Mungu wetu mwema akubariki naakuzidishie nguvu na uvumilivu!!!!

    ReplyDelete
  4. Mkuu kweli huyu mama ni wa ajabu! Simu inanyanyuliwa kwa unyayo na kusikiliziwa sikioni kama kawaida? Sijapata kuona. Tupe taarifa zake zaidi, na ninaamini anaweza kuandikiwa kitabu kikauzwa kikamsaidia kumwuongezea kipato.

    ReplyDelete
  5. NINAMKUMBUKA WAKATI AKISOMA ENZI HIZO ZA MIAKA YA THEMANINI NA TULIAMBIWA KUWA ANGEPATA MSAADA WA KUJENGEWA NYUMBA NA SERIKALI ALIPOKUWA AKIISHI NA MAMA YAKE SIJUI KAMA HILO LILITIMIZWA. HEKO MAMA KWA KUTOJIBWATIKA.

    ReplyDelete
  6. Yaani mzuri kuliko Manka

    ReplyDelete
  7. kweli Mungu wa ajabu,walemavu wengi huwa wana vipaji sana hata kama hana baadhi ya kiungo mwilini mwake lakini utakuta ni creative sana wengi wao

    ReplyDelete
  8. Hongera sana Bahati.

    Michuzi I clearly remember this inspirational lady's story. She is an exemplary citizen and role model, forget about Bongoflava and such malarkey.

    Michuzi, could you find out if there is a phone handset which could make her life much easier. And we, your blog-readers, must buy it.

    Mungu mbariki Bahati

    ReplyDelete
  9. Yaani Mi hapo ndipo ninapoungana na Vitabu vya dini kuwa tusinung'unike, bali Tumshukuru Mungu kwa kila Jambo. Maana kuna watu wana vijitatizo vidogo tu, halaf full kulalamika, oh tumbo langu kubwa, oh nina mikono minene, angalau hivyo unaweza kurekebisha kwa mazoezi, but kuna watu kweli wana majaribu / mitahani katika maisha yao. Mungu awajaalie. Tuache Kulalamika, Tumshukuru Mungu kwa Kila Jambo.

    ReplyDelete
  10. huyu dad ni mfano wa kuigwa, anatuonesha kuwa one can overcome anything and achieve what they want.

    ReplyDelete
  11. Mchangiaji hapo juu..yaani mlokole wa UK..Nakupa point kwa kufukiria wanablog wachangie hand set mpya..lakini nadhani mawazo yako yangeenda mbali kidogo kujiuliza huyu Bahati anaishi vipi?? Na pia ungemuuliza bwana Michuzi kama ataweza fanya nae interview..na kuona wanablog tutaweza kumchangiaje kiuchumi..kwani hawezi kubeba mabox lakini anajitahidi kugombana na ulemavu..Big Up ..Bahati!!

    ReplyDelete
  12. Dada Bahati
    Sisi watanzania wenzako tupo pamoja
    na wewe !usikubali kuwekwa nyuma kwa sababu ya ulemavu wako!hayo
    yote ni mambo ya mungu,
    hakuna alikamilika

    ReplyDelete
  13. Michuzi,
    umenikumbusha mbali sanaaa...
    nakumbuka wakati niliposoma taarifa ya huyu dada mimi nilikuwa ni mtoto mdogo. enzi za magazeti ya chama na serikali kama sikosei... kipindi hicho nae dada Bahati alikuwa bado 'msichana' mbichi kabisa. sasa hivi naona umri nao umesonga kidogo..

    Wadau,
    is there anything we can do for this inspirational citizen of our nation?

    Michuzi hebu kusanya maoni ya wadau tumfanyie kitu huyu dada ili awaze kuendesha maisha yake vyema. sitakosa nakala ya habari leo la weekend hii.
    Naamini hapo ofisini kwenu hamkumwacha aondoke hivi hivijapo kitu kidogo mlimtoa

    ReplyDelete
  14. Mwendo mdundo dada inapendeza sana unavyo jituma jipe moyo na mungu atazidi kukusaidia.

    ReplyDelete
  15. Dada Bahati, Mungu akubariki akuzidishie kila baraka. Yaani Michuzi nakuomba hakikisha hii picha inawafikia kampuni za simu.Tunataka watu kama Dada Bahati ndio wawekwe kwenye mabango yao ili iwe inspiration kitaifa na kimataifa. pia iwe fundisho kwa ombaomba na sie wote

    ReplyDelete
  16. Michuzi,huyu binti kama sikosei aliwahi kuishi caritas hostel Tabora niliwahi kuishi hapo miaka ya 89 naamini ni yeye,anastahili pongezi za hali juu hii inaonyesha wazi binadamu anaweza kuyamudu maisha yake pamoja na kuwa pungufu kimaumbile,je hao ombaomba waliopo Dar hawaoni aibu?Michuzi tafuta siku uwapitie wakupe maoni yao labda wao wanaupungufu mkubwa kimaumbile ambayo hatuyaoni .Bahati keep it up!!!

    ReplyDelete
  17. Amam kweli mungu wa maajabu. Bahati mie namkumbuka sana alikuwa akiishi hostel ya masista wa huruma (Tawi la mama Theresa) pale Caritas Tabora. Mama yake hakuwa na uwezo, kama sijakosea nafikiri baba yake kama vile aliwakimbia. Naona sasa kawa dada wa nguvu kweli. Hebu fanya fanya Michuzi uongee naye tujue anaishi vipi na afanya nini, na kama anahitaji msaada zaidi aweze saidiwa...
    Ama kweli ulemavu sio mwisho wa maisha.

    ReplyDelete
  18. i like the idea ya wanablog kumsaidia dada mlemavu, hii inaonyesha hii blog can turn to be something productive......
    pamoja na majungu na fitina iliyomo, hehehe kuna majungu ya kufa mtu humu
    keep it up michuzi

    mimi pia ntatoa hela ya mabox kumsaidia na wala sitanii, tena pound kabisaa!

    ReplyDelete
  19. Maneno ya Sabah "Mungu hakupi kilema akakukosesha mwendo", tusipende kulalamika ikiwa watu kama dada Bahati anapigana na maisha bila kinyongo.Mwm nakubaliana na wewe, ni role model wa wengi wenye viungo vyao na wasio na viungo.
    WE ARE ALL SO PROUD OF YOU.Huku ulaya tunawaona walemavu kama dada Bahati na wanapewa kila kitakacho weza kuwasaidia kurahisisha maisha yao.Moja ambalo naona lingemsaidia dada yetu huyu niku hakikisha ana angalia uzito wake, zoezi la mwili ni muhimu katika kuhakikisha anaishi maisha bora na marefu.
    Nakuombea kila la kheri na afya njema.

    ReplyDelete
  20. Michuzi,

    Asante sana kwa update! Namkumbuka toka miaka ya 80 alivyoanza kututembelea Daily News. Je, ameolewa? Ana watoto?

    ReplyDelete
  21. Nashaurikwamba Uwekwe utaratibu mzuri na unaoaminika, ili misaada imfikie Mlengwa-Dada Bahati.kwa pamoja nina imani tutaweza kumsaidia ili apate UNAFUU wa maisha.Mungu ametujalia Moyo wa Imani na Ushirikiano that's TANZANIA.

    ReplyDelete
  22. Michuzi inaonesha watu wengi wanataka kumsaidia dada bahati.sasa hima hima fanya yafuatayo.mpeleke pale EXIM bank as a special case wamfungulie akaunti na kumpa CREDIT CARD ya master card(wanazo).akishapaipata post details zake kwenye globu ili watu wamkandamizie mihela.Pili msaidie afungue personal blog awe ana post picha za maisha yake ya kila siku,that way itakuwa rahisi wadau kufuatilia maisha yake na kumsaidia,maana nisingependa hii post iwe one off.by the way Che Mponda kwa nini kauliza kama Bahati ana mtoto?i wonder!

    ReplyDelete
  23. Yaani nimempenda halafu yuko kwenye style kishenzi. Check gauni alilovaa..Vintage style yaani yko IN style kishenzi spring time colors etc etc


    I like her

    ReplyDelete
  24. Inatia moyo kuona watu wana moyo wa kumsaidia huyu dada. Nakuomba sana Michuzi usiishie hapa, tupe taarifa zake mara kwa mara. Hata mie niko tayari kutoa mchango

    Mdau
    UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...