hizi ni baadhi ya vifaa feki vilivyobambwe kwenye maduka mbalimbali kwenye
operesheni maalumu inayoendelea nchi nzima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Mungu atunsuru!

    ReplyDelete
  2. Kwanza nawapongeza waendesha zoezi hili maana ni gumu na la hatari ila nina imani kwamba sheria itawalinda. Pamoja na pongezi zangu nawaomba hili zoezi lisiwe la kuzima moto, liendelee siku zote kwa sababu vitu feki ni chanzo kikubwa cha umasikini na vina athari kubwa kiafya na kimazingira. Wakati wanasiasa wakipambana na umasikini kivyao, watendaji wengine nao watambue kwamba hii vita ni kubwa na inafaa kupiganwa na kila mtu na kwa silaha yeyote. Fikira mtu amepata pesa yake kwa shida halafu anakwenda kuuziwa dawa feki, TV feki, radio feki, vifaa vya ujenzi feki n.K. Kwangu mimi huu ni uaji mkubwa na unafaa kukemewa kwa nguvu zote. Waingizao bidhaa feki wanapaswa kupewa adhabu kali sana. Tusipowashughulikia hawa watu watatua na kutufanya tuwe masikini siku zote.

    ReplyDelete
  3. NAWAPONGEZA SANA YAANI KAMA HUYO JAMAA ALIVYOELEZEA HAPO JUU INATIA HASIRA SANA.KINGINE CHA KUCHOMWA MOTO NA KUSHTAKIWA NI VIPODOZI VINAVYOWACHUBUA WANAWAKE MIMI NI MSICHANA AMBAYE NA JIVUNIA RANGI YANGU NYEUSI TENA SIO USHAMBA KAMA WENGI WANAVYOCHUKULIA MAANA NIMEZALIWA (MJINI)OCEAN RD NA NIMEKULIA MJINI SASA KWELI KAMA SI HAKI ZA BINADAMU NINGESEMA WANAOJICHUBUA WACHUKULIWE SHERIA EBU WAANGALIE NYWELE ZINAWAOTA USONI WANAKUWA NA MABAKA KAMA CHUI


    NADHANI HATA MICHUZI UTANISUPPORT HII MAANA INGEKUWA HIVYO USINGEENDA KUOA MY WIFE WARANGI NANI SIO?

    ReplyDelete
  4. Microscope fake ni hatari kwa afya ya watu kwani kunapelekea matokeo ya vipimo vya magonjwa. Pongezi kwa waendesha zoezi!

    ReplyDelete
  5. kiswahili kimenigonga naomba msaada bidhaa feki ni vitu vimeingia kimagendo bila kibali? au feki nikwamba zimetengenezwa sio kitaalamu?? au ni pia ktk mpango tu watu wasijuchubue? mfano hizo cream na lotion Naomba kueleweshwa

    ReplyDelete
  6. Bro Michu, hiyo picha ya pili ivo vitu sio feki. Wapigie simu wahusika waliomo pichani wakueleze ni vitu gani. Kwa kifupi hivyo ni vifaa vya mahospitalini ambavyo hao jamaa pichani walivikamata ndani ya maduka ya dawa ambamo haviruhusiwi kuwemo. Wapigie basi na urekebishe kama ulivofanya kwa subashi

    ReplyDelete
  7. Anon March 2, 2008 12:33:00 aswa tunawalenga nyie mnao jichubua soon hakuna cream itakayokuwa inaingia nchini tanzania hizo zenye hydroquin sijui kwahiyo iyajibi muanze kutumia mchanga kujichubua

    ReplyDelete
  8. Hao wanaotaka kujichubua watumie majivu na mchanga, mbona tukisugulia masufuria yanatakata? Na wao watatakata tu wasiwe na haja ya kutumia makemikali, au watumie stiliwulu (steelwool ati?) watatakata kama sufuria iliyokoshwa na mmakonde. Si unajua wamakonde kwa kusugua sufuria! Mpaka inatoboka!

    Sasa mtu unajichubua ngozi ili iweje! Kama shida ni ngozi kuwa soft, basi watumie riwa, na siku hizi kuna maji ya riwa yanauzwa, mtu akiwa mweupe au mweusi anapendeza vizuri mwororo! He hivi kuna mtu mweupe? (Weupe si ni rangi inayofanana na karatasi au kama hii niliyoandikia haya makoment yangu? Sasa watu ni rangi nyeupe au pinki au brown?)

    ReplyDelete
  9. Pangu, Pangu Watanzania ndio maana hatuendelei kabasa..ninyinyote mlio ongelea kuhusu kujichubua hamna SERA, SERA ZENU ZIMEPAUKA PAUUU.Kupaka krimu ni maamuzi ya mtu mwenyewe na sio biashara ya Taifa zima.. watu wote wanaopaka krimu natumaini ni watu wenye umri zaidi ya 18. Nawaomba sana Watanzania tuwaze jinsi ya kukabiliana na umasikini uliopo nchini KWANI WENGI WANAOJICHUBUA NI MATAJIRI SANA TENA MNO KRIMU JAMANI NI BEI MBAYA SIO MCHEZO, HIVYO TUSI WAGASI WATU NA MAHELA YAO, TUWAFIKIRIE WETU WAMASIKINI WASIO HATA NA HELA YA MLO MMOJA WA SIKU..MUNGU AWATIE NGUVU NA AWAPE HEKIMA WOOOTE. AMEN, AMEN.

    ReplyDelete
  10. Chonde chonde Watanzania wenzangu, Taifa linalo kazi kubwa sana ya kulinda haki na usawa wa binadamu na kuhakikisha viongozi wanafanya kazi nzuri. Hayo mambo ya Cream,Kujichuua,Mikorogo na bla-bla nyingi nyinginezo hayana Uzito kabisa katika jamii. Hao wanaojichubua ni yao mambo na siyo ya mtu, kama madhara ni yao kabisaaa haya husiani na barabara, hosipitali,umeme na maji vitu ambavyo ni VERY IMPORTANT TO THE SOCIETY. THANK YOU VERY MUCH.

    ReplyDelete
  11. Mdau uliyeulizia kuhusu dawa na viambata vilivyopigwa marufuku, tafadhali rejea tovuti ya TFDA (Tanzania Food and Drug Administration)hapa (bofya) au hapa (bofya)

    ReplyDelete
  12. Anon Sunday, March 2, 2008 11:07:00 thank you subi nimesoma hiyo kweli ni hatari sasa kwanini watu wanatumia hivi vitu

    ReplyDelete
  13. Kuna mdau hapo juu kasema kiswahili akijui vizuri anaulizia maana ya neno "feki" sasa mimi nakujibu feki imetokana na neno "fake" sasa sijui nikiswahili ujui vizuri au ni english au vyote viwili.manake hamna kitu nisichopenda kama kumsikia mtanzania anajifanya hajui kiswahili vizuri.

    ReplyDelete
  14. WEE' mdau hapo juu Halooo halooo tafadhali soma tena comet yangu na uielewe sijasema kua silijui neno ''feki'' nalIjua maana yake sana au najifanya sijui kiwahili kwataarifa yako mimi nilikua mwalimu wa kiswahili najivunia sasa kiswahili kuliko lungha nyingine yoyote japo niko majuu soma tena halafu ukitaka kunielewesha Si vibaya poa tuu

    ReplyDelete
  15. ASANTE SAANA MDAU ''SUBI'' UMENIJIBU VIZURI SWALI LANGU KABALA SIJAONDOKA HIZI BIDHAA ZILIKUA ZINAUZWA KAKA KAMA KAZI NILIKUA NASIKIA TU KUPGWA MARUFUKU. MAANA KUNA ALIYEKRUPUKA KUA SIELEWI NENO ''FEKI'' NAJIFANYA KISWAHILI KIMENIGONGA WAKATI YEYE HAKUELEWA SWALI AONYESHA ANAPENDA USHARI

    ReplyDelete
  16. Kiiruuu, jamani, hao wanaotengeneza bidhaa feki watatuua wana wa wenzao siku si zetu! Wee unafikiri kupakaa mafuta ya Transoma kila siku usoni na mwilini ukifikiri kuwa ni cream, baada ya miaka kumi hiyo sura na huo mwili utakuwa na hali gani? Kaazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  17. Wewe mwalimu wa wapi mbona juu umeuliza tu vizuri bidhaa feki ni zipi? Kuingiza kitu kwa magendo toka lini ikatoa maana ya bidhaa kuwa feki? .kama ulikuwa unajua usingeuliza lile swali juu. Mwalimu gani hajui bidhaa inapewa jina la kuwa "feki" kupitia kigezo gani.

    ReplyDelete
  18. Swali kwa anony. wa Sunday 2.57, hiyo riwa ndiyo nini? Tangaza biashara kama inafaa watu watu wataanza kutumia hiyo badala ya madawa yanayochubua ngozi. Maana nafikiri wengi shida yao ni kuwa na ngozi nyororo.

    ReplyDelete
  19. ALIENDIKA RIWA HAIITWI RIWA INAITWA LIWA.LIWA IPO YA UNGA NA SIKU HIZI WANAZIUZA KWENYE TUBE ILA HIZI ZA TUBE NAMASHAKA NAZO ITAKUA WATIA MAMBO MENGINE KUHARIBU UASILIA WA LIWA.LIWA INAWEZA KUWA KWENYE KIPANDE CHA MTI UNASUGUA KWENYE JIWE NA MAJI HALAFU UNASUGUA USONI AU UNANUNUA ILIYOKUA ISHASAGWA UNACHANGANYA NA MAJI UNASUGULIA USO.TAFUTA MADUKA YA WAZANZIBARI AU WANGAZIJA WATAKUA WANAUZA LIWA KWA WINGI.
    LIWA NI KAMA MANJANO(TURMERIC)KWA WAHINDI,HIZI ZOTE NI NATURAL FORMS OF CREAMS BADALA YAKUUNGUZA NGOZI NA HIZO STEROIDS/HYDROQUINONE CREAMS.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...