dar inazidi kuwa tambarare kwa majengo mapya na ya kisasa kama hili ambalo ni mojawapo ya majengo yaliyo pembeni mwa jiji. hapa ni kijitonyama makumbusho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Michuzi ,haya ndo yanayotakiwa ,kujenga majengo mapya pembeni ya mji ili sura ya mji mkongwe wa dar es salaam iendelee kuwepo.haya mambo ya kuvunja majengo ya kihistoria katikati ya jiji kwa kisingizio cha kujenga majengo ya kisasa ,ni ushamba.Michuzi wewe umetembea nchi nyingi duniani,nadhani umeona mwenyewe katikati ya majiji mengi kuna majengo hadi ya miaka 1000 iliyopita,hii yote ni historia kwa vizazi vijavyo,na kivutio kizuri cha utalii.Huu ni wakati wa mamlaka zinazohusika kuliona hilo,ili majengo mapya na marefu basi yajengwe nje ya mji ili kupanua mji,na kuhifadhi historia ya majengo ya zamani.

    ReplyDelete
  2. Bongo Tambarare??!! majengo ama maisha bora kwa kila mtanzania?? msitupotoshe tukarudi bongo tukaacha mabox, Tsh 25000 kwa saa, kwa siku masaa 8 nina kama Tsh.200,000 za kibongo kwa siku.Hapo bado overtime, Sirudi ng'o !!

    ReplyDelete
  3. sasa hiyo tambalale unayozungumzia sijui hipi hapo juu umeonyesha wanafunzai wanakaa chini darasa mmoja wapo zaidi ya 100 sasa sijui unavyo sema tambalale sijui unakusudia nini na hayo majumba wanayo jenga kwa pisa za wizi wakati watoto wetu wana pata elimu duni?

    ReplyDelete
  4. Ndugu yangu Michuzi kwanza hali yako mwana Bwawa mwenzangu. misoup nashangaa kutuambia bongo tambarare wakati hapo juu umetuwekea picha ya wanafunzi wakiteseka kwa kutoka suguri za makalio hivi akianza darasa la kwanza mpaka la saba mwanafunzi kama huyo atakuwa mzima kweli?. pili tukirejea kuhusu majengo naona mkuu umechemsha . ukitizama majengo mengi mapya ya Dar mengi yao hayana lift, milango ya moto (fire exit) nakadhalika watu wanajenga magorofa kariakoo wakati system ya mifereji ya maji machafu ni ya mwaka 57 wakati huo Dar ilikuwa na watu laki moja. na sasa Dar ina watu mamilioni matokeo mifereji kushindwa uwezo na kupasuka kumwaga mimaji michafu na kuleta magonjwa ya miripuko. nitakuwa upande wako ukiniambia kwamba Bongo tambarare kwa wingi wa mafisadi na kuzidi kwa gonjwa la ukimwi. nakutakia Pasaka njema na ushindi wa Kops (Liverpool)Plz kaa mkao wa kujidai tuna goli 2-1 kesho (Torres na Kuyt).

    ReplyDelete
  5. JE MWENYE JENGO HILO NI NANI? JE NI FISADI AU HAPANA? KAMA NI FISASI, SI LIUZWE WATOTO WA SHULE WAPATE MADAWATI NA VITABU/WAALIMU?

    ReplyDelete
  6. Hii ni matokeo ya EPA bongo....kuna baadhi ziliwadondokea kama hivyo. Jengo likikamilika na bank inakuwa ya kwanza kuwa mpangaji! Utashangaa kila kukicha bank na Bureu de Change kibao zinaibuka kila corner ya mji! kwa mzunguko upi wa kibiashara hadi hivyo? kama siyo EPA.

    ReplyDelete
  7. Anoni wa Saturday, March 22, 2008 5:01:00...WELL SAID!!!

    ReplyDelete
  8. Wewe mbeba box acha uwongo, ukibeba box sana sana unalipwa £6.5 kwa saa kabla ya kodi labda uwe unafanya kazi yenye kisomo kama ualimu au tutor. Wee ukitoa hiyo kodi uanbakiwa na ngapi wakati rate ni £2250 kwa £1. Inafikaje hiyo 25000 kwa saa? Anyway ipo nje ya mada lakini acheni kusema uwongo kupotosha watu.

    ReplyDelete
  9. Mlivyo wapumbavu huo ndo utambarare wenu,Majengo!!!!Wake up men mbona wabongo mnakuwa wapumbavu hivyo??hebu tujitahidi 2010 tufanye kama Kenya jamani tupunguze mafisadi.Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...