wadau kunradhi, sikuaga ila niko huku kwa ujiji (ujerumani) kwa vekesheni kidogo. tatizo kuna kiwinta na fulana inachelewaga kukauka. hapo ni siku ya kwanza, ya pili na ya tatu....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. Karibu sana kwetu.

    ReplyDelete
  2. mmh! Michuzi kwa vekesheni sikuwezi ndugu yangu!!

    ReplyDelete
  3. inamaana hizo siku tatu tu,ulizo kaaa huko ujiji ndio umekuwaga mweupe namna hiyo?amakweli ujiji kuzuri

    ReplyDelete
  4. nakuona Michuzi ndani ujiji,yaani hapo unanikumbusha kule kwetu tokyo(mwakaleli)

    ReplyDelete
  5. MISUPU BANA AU JK ILE TRIP YA UJERUMAN NDIO HIYO? KULA KUKU KAKA MAISHA NDIO HAYA HAYA.ENDELEA KUTUHABARISHA .

    ReplyDelete
  6. No misoup no no no no yaani hutoki bila ze t-sheti hadi majuu unatutia aibu.uroho tu

    ReplyDelete
  7. Jamani hakuna dryer? mpaka usubiri muda wote huo fulana!!!

    ReplyDelete
  8. Karibu sana Mithupu! Nitakutafuta!

    ReplyDelete
  9. Niletee simu ya Nokia yenye kamera ......
    Mwantumu

    ReplyDelete
  10. Tafuta basi Tshirt nzuri kama ya abou na wewe ningekuwa yeye siku ya kuondoka nailoweka kwenye maji. Hehe na wewe umechemsha kama falaviana matata kuenda bika koti utawajua wabeba boksi. Ila kweli dryer nehi? ingekuwa summer ningeelewa kuanika nguo nje hata wakati wa baridi? ua umeme ulikatika?

    ReplyDelete
  11. Mhhhh mkuu michuzi big up umejitahisi sana sio mchezo yaani ujurumani au sio babu kubwa kula kula kuku kwa mlija hamna kulaza kitu peleka vyote

    ReplyDelete
  12. Mithupu kun'guta hiyo fulana bwana ikauke, kwani wewe umefikia hakuna drier huko!!! Angalia haka kawinta hakakaushi nguo haka katakugandishia fulana yako tu iharibike bure, mie nitasikitika sana Mithupu!

    ReplyDelete
  13. mIchuzi bwanaaa!!kumbe uko safarini ndio maana blog inatawaliwa na manka na mchumba wake!!ebu rudi bwana,tumechoka kusoma love story hapa za manka mushi

    ReplyDelete
  14. hizo fulanazz ni midebwedo za thailandi unataraji nini alitengeneza ajalipwa na kama kalipwa amepunjwa na aliyeleta bongo kakwepa ushuru sasa hizo kukauka mpaka pesa ya epa na richmond zirudi zote na hizo ndio zitakauka hata ukiweka ktk dryer maana ni za kifisadi hizo,na hizo hizo kila siku wewe misupu

    ReplyDelete
  15. sasa vidate vinadai simu na laptop kila mtu anadahi ulichohaidi misupu,umekula vya watu sasa walipe,na my wife wako anaona sasa ni soo kilo kumi hiyo misupu

    ReplyDelete
  16. eish !!! shabash !!

    ReplyDelete
  17. michuzi kiboko karibu ujerumani na asante sana wka kutupa haabri ukiwa uko ubarikiwe sana.

    ReplyDelete
  18. Issa Michuzi. Leo vaa hiyo flana yako Liverpoolfc ikicheza inaonesha flana ya bahati nzuri hiyo, leo Bwawa la maini ikifungwa wataongea sana humu. ukirudi Michuzi niletee Viatu vya mpira Size 10 na Jezi ya Bwawa la maini Na Simu Mpya ya Video Camera Sawa. usipoleta Blog tutaiwekea Virusi LOL!. Inshallah urudi salama.

    ReplyDelete
  19. Hahaha Issa Michuzi Koti kubwaaa! unasubiri Vibajaji nini hapo hawatoi Lifti huko Vibajaji hakuna toa pesa upande Taxi LOL!. Vibajaji oyeee kudadadadeki. angalia vizuri wale wabaguzi mipara ya hitler huko noma.

    ReplyDelete
  20. sasa hapo council estate...hata kukausha nguo zilizofuliwa,mpaka mgoje jua mwezi Julai...kabla hivyo hayo mafulana na vyupi kwanza vitaganda!!!kweli ulaya ushamba tuu...bora sisi wasafwa...tunaenda kando ya mto...pigapiga na mawe,na bila pasi..tayari kuvaaaa...

    ReplyDelete
  21. Michuzi vaa sweta mzee, baridi hiyo isikuumize tukakosa habari.

    ReplyDelete
  22. dah hayo magari ya yuropa ovyo kama ya bongo.Kweli Usagara kunatesa.

    ReplyDelete
  23. dah hayo magari ya yuropa ovyo kama ya bongo.Kweli Usagara kunatesa.

    ReplyDelete
  24. Michu, hako kafulana katakauka siku ya kurudi Bongo, bora kanunue nguo za baridi hapo Ujerumani.

    ReplyDelete
  25. mi nina wasiwasi nawe michuzi utakua mtu wa usalama wa taifa na ndio mana habari zako nyingi zinawanyanyapaa wazungu,na kwa nini nasema hivi mana popote aendapo waziri mkuu,ama rais basi we hua huko kabla,kama wafanyavyo wazee wa kazi ambao mwajiriwa wao ni CCM na si serikali,ila yote ya yote fulanaz mpk iongee mwaka huu bwana la maini naona linafanya kufuru huko maeneo ya milano

    ReplyDelete
  26. Kaka michuzi karibu kwetu ujiji, ila tafadhari hii fulanazz mi na wasi wasi nayo, we m2 wa pwani sio...? siku nyingine iache kwenu huko huko, isije ikatuingilia sisi tulio kwenye vekesheni daily.

    ReplyDelete
  27. Sasa Michuzi mambo yakuanika nguo mpaka ujerumani duuu...kwani host hana dryer au ndiyo utabidi ulipie halafu fulanazzzz ni moja hahahaha pole bro. Mdau T-Dot

    ReplyDelete
  28. Dah nmecheka mpaka basi IoI sasa ni kwamba itaisha nguvu ya bagamoyo ikiingia kwa dryer au host anabana matumizi jamani mishiko yote hiyo IoI haya kaka karibu London tukurushe kama uliacha vidole ubalozi.
    Londoner

    ReplyDelete
  29. Michuzi wewe na Liongo wote bonge la wakulima.

    ReplyDelete
  30. Jamani misupu kauka nikuvae mpaka Majuu?

    ReplyDelete
  31. Michuzi nae kwa kutuchuuza!!! eti ni 'siku ya kwanza ya pili na ya tatu' wakati mi nikiangalia background za siku ya pili na ya tatu ni ile ile ikimaanisha kuwa picha zilipigwa almost ndani ya tofauti ya dakika chache kwa sababu magari yaliyoonekana siku ya pili na hiyo inayodaiwa ni siku ya tatu ni yaleyale! Acha kutuzuga bwana hata sisi tuna macho si watoto wadogo wasiotofautisha!

    ReplyDelete
  32. Hongera kaka michu kwa kuwa ndani ya ujiji, nakutakia kheri, kaka katika picha ya tatu kuna kagari kadogo sana kanaonekana kwa mbali naona ni ajabu kidogo unaweza kutupa habari zaidi tupate kujua vikoje hasa kwa picha ahsante nategemea utatupa uhondo. nataka kujua ni vya watoto au watu wazima? au wadau wa ujiji nisaidieni.
    ETM

    ReplyDelete
  33. Dah mshkaji misupu, yaani wewe umekulia town na umesafiri sana lakini still bado ni bonge la mshamba sijawahi kuona!! Unatutia aibu sana mshkaji, badilika kidogo at least. Hallelluya wallah!!

    ReplyDelete
  34. Karibu sana kaka Michuzi.Naona umekuja pazuri baridi sio kali mwaka huu. Sasa huyu mwenyeji wako hana tumble dryer?

    Karibu sana

    ReplyDelete
  35. Hallow michuzi, Mimi kwakweli namzimia huyo Aboubakar, naomba umuulize kama vipi nitume CV yangu, ni mtanzani mwenzake. Au ameshapata jiko??

    ReplyDelete
  36. Kaka michu, siku mbili tuu umenawiri hivyo safi sanaa. Naona unakula nchi kaka...angalia tu hio account yako isije wekwa under survelance kama mafisadi au ndio unaamua kula vivakesheni vya mwisho mwisho wasije kukushtukia....Basi tumia vifweza hivyo kununulia replacement tishetis mshakaji...noma bwana kigaga hichohicho tu...na mavakesheni yote hayo...LOL wewe unaniua mbavu mkweli kaka yangu kwa katisheti kako hako, na kale ka Liverpool umekabeba nako mbona hatukaoni basi....

    ReplyDelete
  37. Michuzi Pls pls tutafutie picha kwa ajali ya theutamu za wabongo wa uko Ukerewe

    ReplyDelete
  38. Michuzi bila shakha nawe umekuja kujaribu BOX au sio... asikudanganye mtu, box linalipa babake. hapo unaonekana hivyo baada ya siku mbili je ukikaa mwezi utakuaje, maana utatakata kuliko presidaa wa FM academia. Im sure wala vumbi hawajafurahishwa na safari yako, soma comments zao!!??

    ReplyDelete
  39. Mdau uliyeulizia kale kagari kadogo: kanaitwa Smart, ni kadogo na CC zake siyo kubwa na kanatumia mafuta machache sana lakini kanapiga masafa marefu kishenzi, na kama unavyojua waropa wanamaindi environment, kale kagari hakachafui mazingira kwa sana.

    ReplyDelete
  40. michuzi kaka yangu vipi hakuna mashine za kukaushia nguo au vipi,au huko ndio kutunza mazingira?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...