JK akimpongeza mai waifu wake Mama Slama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kuchangia shilingi milioni moja katika mfuko wa elimu wa wilaya ya Bagamoyo wakati wa harambee iliyofanyika katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam Ijumaa jioni.Katika Harambee hiyo zaidi ya shilingi milioni tisa zilichangwa.Katikati ni Mwenyekiti wa harambee hiyo Bwana Subhash Patel.
*PS: Wadau kunradhi awali niliandika kwa makosa jina la kwanza la Bw. Patel kuwa ni Jeetu Patel. Hivi sasa nimerekebisha na naomba radhi kwa usumbufu uliotokea....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Safi JK. Mpongeze mama bwana!! Hongera mama watoto... Hongera mpenzi... hongera sana!!

    ReplyDelete
  2. Michuzi umekosea thats subash patel..kasoma na muungwana huyo wametoka mbali usianzishe msala...

    ReplyDelete
  3. Imekuwaje leo mama huyu hakuweka lishuka?

    ReplyDelete
  4. Afadhali leo Salma hujatundika ule mshuka begani, huwa siupendi kama nini! Umependeza mama, achana na fasheni ya kutundika shuka begani inakuzeesha, uwe unavaa hivi kama leo, au vyovyote unavyotaka lakini mambo ya kukunja shuka na kuibeba begani achana nayo!

    ReplyDelete
  5. Msaada kwenye glob,

    Samahani, ulimaanisha Jeetu Patel yupi??

    Yule mwizi wa fedha za EPA, au??

    ni hilo tu

    ReplyDelete
  6. Michuzi weka comment yangu....

    ReplyDelete
  7. mkubwa hata comments inakuwa issue mbona huweki comments zetu au mpaka umjue mtu nini si ndo mambo ya ukabila haya?au mpaka uwe maarufu?si mambo bwana

    ReplyDelete
  8. Wazungu weusi wasiopenda lishuke, hivi nyie hivyo mnavyovivaa kila mtu anavipenda? Kila mtu anavaa akipendacho kuna fasheni watu wanavaa na wengine hawazipendi lakini hawawaambii eti usivae hiyo fasheni.

    Unachokipenda wewe mwengine hakipendi na unachokichukia wewe mwingine anakipenda!Na sio lazima kila kitu kuiga wazungu!

    Hiyo mishuka ndio jadi yetu waafrika!

    ReplyDelete
  9. Ok kumbe kumbe umelitambua kosa lako na kujisahihisha lakini napata wasiwasi kama serikali itamuwajibisha Jeetu Patel mdogo wake Subhash Patel wakati kaka mtu ni swahiba wa JK na huwa anatoa michango mikubwa kwa CCM hadi Ndg.yake Jeetu Patel akapewa deal la udalali wa ile rada kisha leo wanajifanya wamemuita kumuhoji kama si kiini macho ni nini?

    ReplyDelete
  10. INNER CIRCLE, INSIDE JOB NA MANENO MENGINE MENGI YANAYOFANANA NAYO NI MANENO YA KAWAIDA LAKINI NI MANENO YANAYOTUMIKA SANA KATIKA UFISADI. FISADI HAWEZI KUZUKA TU HIVIHIVI NI LAZIMA ATAKUWA KARIBU SANA NA WAHUSIKA AMA ATUHUSIANA NA MTU ALIYE KARIBU SANA NA WAHUSIKA, SASA NIMEELEWA KWANINI JEETU ALIPATA TENDA NA HAKAMATIKI.

    ReplyDelete
  11. Habari kaka michuzi, ahsante kwa blog yako ya nguvu kwa kweli watuhabarisha sana na kwa wakati na kwa umakini. Kaka michu kwenye habari hii umesema michango zaidi ya milioni tisa, yaani ina maana walichopate ni kati ya tisa na kumi. wakati wama wametoa milioni moja na nmb wametoa kumi mpaka hapo ni zaidi ya mil 11 zingine najua hazijatajwa, ningeshauri hili kadirio liwe la juu ya milioni kumi. naomba muongozo wako.
    nawasilisha.
    ETM

    ReplyDelete
  12. Subash ndo mwenye sea cliff, ila michuzi ulijificha wapi mbona sijakuona.

    ReplyDelete
  13. jamani huyu mama hajui kuvaa. Wangeniajili imi waone nitakavyo mtengeneza!

    ReplyDelete
  14. hivi kwa nini kila mke wa raisi awe na taasisi yake binafsi. kwa nini kila first lady aje na taasisi yake na aondoke nayo? kwa nini kusiwe na moja tu kila first lady anaikuta, anashughulika nayo na anaondoka na kuiacha...???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...