bango la ziara ya mama afrika
mwanamazingaombwe pekee wa kike bongo akanashe yumo pia na ndiye mama afrika
baadhi ya wasanii wa mama afrika
akanashe joan, ambaye kasomea china mambo ya mazingaombwe, akijitambulisha kwenye moja ya shoo huko ughaibuni, na chini akifanya moja ya vimbwanga vyake vya kufanya meza ielee angani huku yeye kakamata kitambaa chake tu...

je una habari kwamba hivi tunavyoongea kuna kundi la wasanii wa kibongo wakitesa ughaibuni kwa shoo za muziki, sarakasi na mazingaombwe chini ya jina mama afrika? basi ndo hivyo tena. hivi sasa wako ujerumani na ratiba inaonesha wikiendi ijayo, yaani tarehe 9 machi watakuwa hamburg na siku itayofuata watakuwa bonn. kazi kwenu wadau wa huko na kwa habari zaidi cheki www.circus-from-africa.com utaipata. ukipitia google bonyeza translate upage ung'eng'e.
aidha, kuanzia mwezi wa juni mwaka huu mama afrika itafanya ziara ya maonesho 100 hapa bongo kwenye mikoa mbalimbali, na mambo yakienda mswano huenda watakuwa arusha wakati wa mkutano wa sullivan ambao mambo yake yote yanapatikana www.thesullivansummit.go.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ehhe dada mzuri anafanya mazinga ubwe lakini ni kazi kama kazi zingine ila kwa sababu tumechukulia wengi walikuwa hawasomei hii kazi kama wakina kababayeee.yaani nilikuwa sielewi kwanini watu walikuwa wanapenda hivi vitu mimi tangia nikiwa shuleni siendi kwenye vitu kama hivi nilikuwa sioni umuhimu wake

    ReplyDelete
  2. Duh jamani,hayo mazingaombwe na kandomblei...labda wanasiasa wetu wajifunze hayo mambo au vipi?

    ReplyDelete
  3. Mazingaobwe yanasomewa pia? Sasa akimaliza masomo atakua na degree gani? ...B.Sc in mazingaobwe na minor in sarakasi

    Halafu watu hawatamwamini huyo..mzuri sana...mtu wa mazingaombwe anatakiwa awe mbaya anatisha sanaaaa

    ReplyDelete
  4. Jmani hongera sana mpenzi.. mungu aendelee kukusimamia katika kazi zako mamaa.....

    wewe hapo juu haijalishi ni namna gani unaonekana ama laa.. ninamna ambavyo unaweza kupeleka utaalamu wako kwa watazamaje... kazi ni kazi mladi mkono uende kinywani...

    Big up Joan Endeleza fani ikewezekana rudi tena shule uendelee kuwarusha watu hewani

    ReplyDelete
  5. Mi naomba mnieleweshe yale mazingaumbwe yanakua ni nini ? mara kinatokea kitu litambaa mara mtu anabadilishwa mara hivi, Ni nguvu za uchawi au ni ujanja flani? naomba nieleweshe dada Joan

    ReplyDelete
  6. Joan-mama, hongera sana na maendeleo yako.Nimefurahi kuona unaendelea vizuri. Hongera Sana.
    Mwanao.

    ReplyDelete
  7. mimi ninavyoelewa mazingaombwe yanahusiana na uchawi,kwa sababu nakumbuka nikiwa primary walikuwa wanakata mtu kichwa wanaweka kwenye sinia na kile kichwa kinaendelea kusema wakati kimetenganishwa na kiwiliwili,alafu baadae wanarudishia.sipendi coz imejaa nguvu za giza tupu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...