
Kaka Michu!
Habari za kazi na shughuli za hapa na pale.
Ni yule yule tena mdau wa Ukerewe nimewaletea wadau email address ya hawa mafisadi ili tuzidi kuweka wazi wajue nini makosa yao na pia kwenye zile picha mbili za mwanzo naona yale maelezo ya picha ya pili hayaonekani vizuri sasa nimeyakuza zaidi ili wadau waone nini hawa jamaa walivyovulunda na kuzidi kuongopa waziwazi.
Labda wadau wangesoma wenyewe ndiyo mzuka uwapande zaidi na wayaone machungu niliyokuwa nayo.
Ngoja ninukuu mstari mmoja ' Compared to Mt.Kenya (Africa's highest mountain), Mt.Kilimanjaro is a relatively easy climb.' mwisho wa kunukuu.
Hizi ni contact zao za ziada kama utapenda kuwarushia na waya kabisa au barua:-
15 Lawrence Bell Dr.,
Amherst,
NY 14221800-387-7702
Fax: 800-387-9930
Mdau Ukerewe hapa,
kama kawaida kaka Michuzi email kapuni.
Michuzi ni vema ungepelaka copy kwa waziri wa utalii na Jk kama utaweza.
ReplyDeletejamani watanzania tutaendelea kulala hadi lini? kwanza tunaburuzwa na viogozi wetu hata tuburuzwe na jirani zetu!!
ReplyDeletehiyo sentensi inaonyesha kuwa wamekusudia kusema kwamba mount kenya ndio mlima mkubwa afrika! na pia wameudharau mount kilimanjaro kuwa ni "easy climb" ili wageni wakapande mount kenya sio!
hivi ni vita .....tuwajibikeni
Wajinga duniani sio wabongo peke yetu. Hivi sasa uki search Mt. Kilimanjaro on google utapata site nyingi sikielezea mlima Kilimanjaro, mojawapo maarufu ni wikipedia.
ReplyDeletehttp://en.wikipedia.org/wiki/Mount_Kilimanjaro
Sasa sijui hawa walioandika ni vipofu. Ndio maana wanatudanganya kuwa wajerumani ndio waliokuwa wa kwanza kuvumbua mlima Kilimanjaro. Hivi kweli mtu atoke huku aende Tanzania agundue mlima? si uongo huo? Wanahistoria wa mambo ya kale kutoka Marekani wame fanya research mlimani na kukuta vithibitisho kuwa kulikuwa na activities zinaendelea mlimani karne nyingi zilizopita hata kabla hao wakoloni hawajatia mguu wao Africa. Na kuna simulizi ambazo simefanyiwa research na kuthibitisha kuwa kweli karne nyingi zilizopita wakazi walioishi maeneo karibu na mlima walikuwa wakiupanda ajili ya shughuli za kimira.
Hawa wazungu wametudanganya vitu vingi sana na hata kuficha ukweli kwamba Africa was the mother of civilization. Wametudanganya kwa miaka mingi kuwa Egyptian Pharaos walikuwa weupe mara waarabu sasa imekuja kugundulika kuwa walikuwa ni weusi na lugha waliyoongea kipindi hicho inalingana na ki wolof pia kiyoruba kinachoongelewa sasa. Imebadilika baada ya waarabu kuingia.
Asante kwa email hapo juu. Ngoja niwakomalieni sasa hivi. Waache za kuleta
kwa tafsiri yangu, kichwa cha habari kinaonyesha milima 2, yaani Mt Kilimanjaro na Mt Kenya. Sina ushahidi wa kuthibitsha kwamba heading inaonyesha mt Kili upo Kenya.
ReplyDeleteJambo jingine, hivi Mt. Kilimanjaro si uko mpakani mwa Tanzania na Kenya? Je wa Kenya hawana haki na mlima ambao sehemu upo kwao na sehemu upo TZ.
Tuache kulaumu, tuangalie wapi tunakosea ili tutafute mbinu za kufanya watalii kuja TZ kuuona mlima huo.
MIMI NARUDI KULEKULE.SERIKALI TUNAOMBA KAMA MNAWEZA KUBADILISHA KATANGAZO KETU KALE KA CNN,WEKA LINGINE TUWAVUTIE WATU.ONYESHA VITU VINGINE.TANGAZO LIMEKAA KIPICHAPICHA SANA.NDO WAKATI WETU WA KUWAKOSHA WAZUNGU WAJE KUNGAMUA MACHO BONGO NA TUPATE KITU KIDOGO.
ReplyDeletewewe anon wa Friday, March 14, 2008 9:30:00 AM EAT,utakuwa unaumwa tena ugonjwa mbaya sana au utakuwa sio mtanzania, au na wewe ni fisadi hatutaki kukuona humu bloguni. mm@#$%^&@#&&zi kabisa
ReplyDeleteWe anony 9:30 AM, To visit or climb Kilimanjaro u have to officially be with Tanzania authorities, pia ninachojua mlima wote upo ndani ya Tanzanian boarders, ila can be viewed from some part of kenya. Ku advataizi mlima uko Kenya is totally wrong.
ReplyDeleteKwanza Kabisa mtumaji tuanaomba tujue ni gazeti gani na tarehe ngapi ukurasa wa ngapi na heading ya topic, ndo tunaweza kuwaandikia tukiwatgaka watoe marekebisho kwani walichoandika hapo si sahihi?, Pili kwa kuandika habari za uongo...., hili gazeti haliwe kushtakiwa na Serikali ?, kwani kwa kufanya hivyo itakuwa fundisho kwa magazeti mengine..
ReplyDeletenaomba kuuliza kwani huo mlima kili si unapandiwa tanzania sasa wao wakiutangaza uko kenya itawasaidia nini au kenya pia kuna sehemu ya kuupanga huo mlima? labda na kenya wanaupanda kwa upande wao. naomba majibu wadau
ReplyDeleteHuyo Anonym.. hapo Juu sijui hata Jiographia kasomea wapi. Ni mwalimu gani aliyekufundisha kuwa Mlima kilimanjaro nusu upo Tanzania na Nusu upo Kenya? shwaini weye...ch*&%$$#p wee, Koma na ulegee. Halafu Umeona kabisa pale chini ya Picha kumeandikwa Mt. Kilimanjaro, Kenya au macho yako yana matege?
ReplyDeleteKwa Taarifa yako ukisimama upande wa Kenya unaona kichuguu tu wala ile peak yenye snow huwezi iona kabisaa. afu ni shrubs tu zimejaa na arid vegetations kule maana upande huo ni leeside ya mlima afu Tanzania ni windside ambapo kuna misitu,mvua, na peak yenye snow and easy to climb, na kwamba woote mlima upo Tanzania. refer ur map.
ReplyDeleteWazungu wengi wajinga hawapendi kujua mambo ya Africa wakenya walishalijua hilo ndiyo maana wako tayari kuwatapeli chochote.Kuwaambia Zanzibar iko Kenya,na Mlima Kilimanjaro uko Kenya.
ReplyDeleteKutokana na UJinga wa Wazungu twaweza watangazia kuwa Jangwa la Sahara liko Dodoma na Singida nchini Tanzania waje kutembelea waone mifugo ya jangwani (Mbuzi) na wakaja kweli.Wazungu watu wa ajabu sana!
Wakenya majasiri kutapeli kuliko watanzania! Ndiyo maana wanawapata wazungu sana kwao kuliko Tanzania.
Wazungu wana akili kwenye mambo mengine lakini Jiografia ni sifuri kabisa.
Anonymous wa friday,March 14, 2008 1:52:00 PM EAT upo sawa kabisa. Mlima wa Kilimanjaro upo Tanzania wote, hakuna sehemu ya mlima iliyopo Kenya. Shida inakuja ukikaa Kenya unauona mlima Kilimanjaro, sasa kwa kuwa hawa wenzetu wazungu na wajinga kuliko waafrika tunavyoweza kufikiri (kwao wanafundishwa history na Geography ya Europe and North America only), wakenya wanatumia nafasi hiyo kuwadanganya. Kuwa mlima upo kwao ila haupandiki kwa upande wa kwao mpaka kwanza uingie Tanzania then urudi mpakani ukapandie kwa upande unaotazamana na Tanzania. Kwa kweli inabidi wahusika washughulikie hili, na kama kuna mahakama ya kimataifa ya mambo ya biashara ni bora kupeleka kesi huko ili wakenya waache kutuibia kwa kuwa huu ni wizi wa raslimali ya watanzania
ReplyDeleteKwa kweli inaumiza MOYO. Nimesoma maoni ya wadau wengi, na ni kweli Tanzania sasa tunahitaji kuanza kushindana, si katika utalii tu, bali kwa kila jambo. NAPENDA kumuunga mkono mdau mmoja aliyesema tubadili jina mlima, iwe Mt. Tanzania. Mi naona hilo wazo ni zuri. Itakuwa ni ngumu kwa mtu, hata mjinga, kudanganywa kuwa Mt. Tanzania uko Kenya. MT. TANZANIA, wadau mnasemaje????? mi binafsi nimelipenda. Kama vipi, ipelekwe Bungeni (ama taratibu zinazotakiwa zifuatwe) tubadili jina kuanzia mwakani. FULL STOP.
ReplyDeleteDaniel, London
Michuzi fanya uchunguzi wa gazeti na na mwaka wa hiyo kalenda,ukipata ukweli peleka kwenye ofisi ya maliasili na utalii kwa sekretari yeye atawakilisha kwa viongozi wanaostahili!kenya wamechukua mali ya Tanzania nyingi sana,Masai Mara ni yETU na Mombasa pia...lakini kutoa no moyo
ReplyDeleteUkipigana na ukututa utaumia mwenyewe .
ReplyDeleteCha muhimu ni kuishauri nchi yetu kuitangaza zaidi nchi na kuonyesha kuwa huo mlima upo bongo. Hao wanafanya biashara sasa kama wanadanganya watu wengine ili kupata hela ni biashata yao.
na serikali ingeweka ulinzi mkali wa mtu anayetaka kupanda mlima huo lazima aingie Tanzania na kupitia point of Entry sasa kama watu wataweza kuupanda huo mlima kupitia Kenya bila kuwa na Visa ya Tanzania ndio sisi wenyewe tunaharibu.
Na pia ukiangalia Mbuga ya wanyama iliyoko Kenya wakichukua picha za mlima huo zinaonekana vizuri sana.Sasa hata wakisema huo mlima uko Kenya huwezi kukataa.
Ni sisi wenyewe tunaachia hii na ndio maana kama mtu alipanda mlima kwa kupitia Kenya akiondoka ataandika kuwa upo Kenya. Angalia hii picha wamepiga kutoka Kenya- amboseli....http://www.flickr.com/photos/markeveleigh/117963750/
By the way sasa hivi ninavyoandika hii nimeona Tangazo letu kwenye CNN...Limeanza kwa kuuliza where is Mt Kilimanjaro.........Kila siku wakitangaza hivi wenye kutaka kwenda huko watakua na maswali mengi na itawatoa macho hao wanaoadvetise hivyo
Hata tukibadili jina tukaita mt Tanzania bado tatizo litakuwepo coz sio watalii wote wanajua what is Tanzania, vilevile florida kuna saloon inaitwa Tanzania.
ReplyDeletewadau, ukikaa kenya amboseli national park unapata picha nzuri sana ya mlima na wenzetu wanachukulia faida hiyo
Kwanza napenda kuwapongeza watani wetu na kuwashukuru kwa kazi kubwa ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania. Inasikitisha kuona maoni ya wachangiaji wengi kuwalaumu wakenya kwa kutangaza vivutio vya kwetu vya uatalii badala ya kuwapongeza.
ReplyDeleteBinafsi nimekua nikiyachambua haya maoni ya wachingiaji na mengi yameleekea kuilaumu serikali na wakenya katika ili suala bila ya kuonyesha wao kama watu binafsi wanafanya nini au ni mikakati gani ifanywe ili kuongeza kipato cha utalii tz.
Binafsi hawa wakenya ndio wamekua chanzo kikubwa kwa kipato cha utalii nchini kwetu kwani kila mtalii anayeingia kwenye vivutio vyetu ni lazima kulipa ada ya utalii na vile vile wamekua wakitumia hotel zetu na wananchi wetu kutoa huduma kwa hawa watalii. hii ni kutoa ajira kwa wazawa na kodi kwa serikali.
Changamoto ni kwa sisi watanzania kuendeleza ujasirimali kwenye sekta ya utalii na kutangaza kwa nguvu vivutio vya utalii vya nchi yetu huku tukiendelea kuvuna mapato yanayotoka Kenya. soko bado ni bichi. tuache tabia ya kulaumu na kuelekeza kila kitu kwenye serikali na tuanze tabia ya kutetea utaifa wetu kwa vitendo. Mawazo machache ya namna ya kuanza.
Kwanza watanzania wengi kuanzisha biashara ya kuhudumia wataliii
Pili kujifunza kutoka kwa wakenya kutokana na mafanikia ya na ikiwezekana kuanzisha ubia wa kibiashara na watani
Tatu kampuni za kitanzania kuhudhuria kwenye maonyesho ya kimataifa ili kuweza kutangaza utalii wetu
Nne kwa sababu hii mikakati niliyotaja hapo juu inaitaji fedha, Watanzania inabidi kurisk kwa kutafuta mitaji kwa kutumia rasilimali walizo nazo. Mfano kutumia nyumba kuombea mikopo na kufanyia biashara.
Kwa upande wa serikali kutenga fungu na kutumia balozi zetu kutangaza vivutio vyetu vya utalii. na kwa njia hii tutakua kwenye nafasi nzuri ya kuwapiga bao watani wetu.
Kwa sasa sasa naomba watani waendeleze libeneke ya kutangaza vivutio vyetu ili na sisi tuongeze kipato
kuita mt tanzania ni sawa sawa na kulia mahakamani badala ya kujitetea wewe unalia, hakimu lazima akufunge tu, kila kitu ni mambo ya marketing na ma-advertisements sio kubadili jina , unaweza ukabadili jina ukawapa jamaa point ile mbaya watu wakaja kupanda mlima kilimanjaro wewe ukabaki na mlima tanzania wako, lazima tukiulize kilichotushinda mpaka tunafikiria kubadili mlima jina hehehe! mjini shule wakubwa
ReplyDeleteDaniel wa 5:41pm nimecheka kwa jinsi ulivyo hamasisha watu kuita Mt.Kili uwe Mt. TZ. Tupo na wewe pamoja nalipenda jina la Mlima Kilimanjaro.Nafikiri serikali yetu ingechukua hatua za kudhibiti rasilimali zetu.Na Michuzi angekua anatumia nafasi yake kufikisha ujumbe wetu kwenye vyombo husika ili kufanyia kazi. Na pia ideas za watu wanazotoa kwenye glob hii za kuleta maendeleo wangezifanyia kazi.
ReplyDeleteKWA KUADVERTISE MLIMA UKO KENYA, WAKENYA HUPATA FAIDA KUBWA,
ReplyDeleteHOTEL,
TOURIST ENTRY FEE TO KENYA
SHOPPING,
TRANSP0RTATION,
HALAFU WAO HULIPA TANZANIA SEHEMU KIDOGO YA PESA KUPITISHA WATALII KUPANDA MLIMA KILIMANJARO.
NILISHASEMA HAPO AWALI KUTOKANA NA TANZANIA KUWA BONGO LALA KWA MIAKA MINGI TUTAENDELEA KUWA TUPO TUPO WENZETU WANAKIMBIA SISI NDIYO KWANZA TUNAAMKA HII NI KALI YAKE KIBAYA ZAIDI KENYA KWENYE UTALII KWA KUWA TUNALILIA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI NDIYO WATAKAOKOMBA MAPATO YOTE YA KITALII JAMANI TUACHANE KWANZA NA EAC,TUJENGE NCHI YETU KWANZA
ReplyDeleteWenzetu labda mna Atlas inayo onyesha mlima Kilimanjaro uopo Kenya.Tuambieni inapatikana wapi na sisi tukanunune.VIJANA wa Kitanzania msitutie aibu katika hadhira ya Kimataifa!Ni mtalii gani au Mzungu gani aliyedhamiria kuja Afrika au Afrika Masharriki au Tanzania au Kenya mtu aliyekwenda shule asiyetambua kwanza jiografia ya kule alikokusudia kwenda kabla hata ya kuianza hiyo safari?Tusiwe wajinga kupindukia.Hivi nani asiyejua tofauti baina ya misemo hii miwili:Mt.Kilimanjaro,Kenya na msemo mwingine wa Mt.Kilimanjaro in Kenya ?Kama hujatambua tofauti yake basi itakuwa kazi kukuelimisha hapa.Lingine, mtambue kwamba katika biashara ya utalii hakuna mipaka.Mtanzania unaweza kukuza biashara yako ya kitalii kwa kuwavutia watalii waje watembelee vivutio vilivopo nchini Tanzania lakini pia utaweza hata kuongezea vivutio vilivyopo katika nchi za jirani na maeneo mengine ili mradi tu uwahakikishie watalii wako kwamba una uwezo wa kuwafikisha kote huko uliko kutaja.Na wakati mwingine ni watalii wenyewe watakao kupa mahitaji yao kwa mfano kwamba nataka nianzie Masaai Mara(ipo Kenya),kisha niende Serengeti(ipo Tanzania),kisha Mlima Kilimanjaro(upo Tanzania),kisha Gombe(ipo Kigoma Tanzania),kisha pwani za Pemba(iko Tanzania),kisha Cabora Basa(iko Msumbiji) orodha ni ndefu.Kwa hakika ni mtalii mwenyewe ndiye atakaye pendekeza umpeleke wapi.Hizi kelele mnazopiga vijana wetu ni za kijinga tu kutojua biashara ya utalii inaendeshwaje.Wakenya wa kawaida hawanufaiki lolote na biashara hiyo kama ambavyo hata sisi watanzania wa kawaida wasivyonufaika na biashara hiyo.Siyo serikali ya Kenya inayo fanya promosheni hizo za Tourist Packages mnazoziona zikitangazwa na wafanya biashara binafsi kama ambavyo wewe na mimi ambavyo tungeweza kufanya.HIVI KWA NINI HAMTAKI KUELEWA?TUMESHA LIELEZA SANA KUPITIA BLOG HII.Acheni huu ujinga wenu na kutaka kuchonganisha pande mbili ambazo ni ndugu na zina ushirikiano mkubwa na wa kihistoria katika nyanja mbalimbali za kibiashara.Badala ya kuendelea kupoteza muda wenu hivyo mngeanza mikakati ya kuanzisha kampuni za kuleta watalii kutoka huko mliko kuja huku nyumbani Tanzania.Its high time you grow up mentally ana assume your civil responsibilities of contributing to the progress of your beloved country.Mmetuchosha sasa njooni na nyingine mpya!Pleeeeeeeeeeaase!
ReplyDeletemaelezo mbona hayajajifunga kiivyo? hapo ni kwamba, kwa wale wanaoelewa kuwa kili iko bongo, watajua cha kufanya, na wale wanaojua kuwa kili iko kenya nao watjua cha kufanya. juzi nimeona nadhani kwenye blog hii balozi wa bongo UK akiwa na mabasi yenye mlima kili. pia nasikia ujerumani. pia tuko CNN. wabongo hofu yenu nini? wakenya wanatusafishia njia kama mlikuwa hamjui.
ReplyDeleteIYO MJANJA ALIYO SEMA MT KILIMANJARO IWE MT TANZANIA NDO MBONGO HALISI. IMEPITISHWA!! AWA WATU HAWA WANAJUA KUWA MBONGO PIGA UA BADO ANAWAZIDI UJANJA TU.
ReplyDeleteMT TZ. INASOUND BOMBA. SASA TUNAANZA KUWAONESHA SINDIMBA NA VITA ZAO ZA UKABILA AWA.TUTACHUKUA MOMBASA WAKILETA MCHEZO AWA. KWANZA WATU WA MOMBASA WASWAHILINA ATA WENYEWE MIOYONI MWAO WANAJIJUA KUA NI WATZ. WE WE WE LETE MCHEZO.
Mdau wa Ukerewe hili la Kilimanjaro na Zanzibar kweli linakera, but si hayo tu!! ukimaliza hilo nadhani tuanze kufuatilia waheshimiwa walioondoa maneno muhimu ktk The Safari larger yaani 1.Urithi wetu
ReplyDelete2.Asili yake Tanzania.
Je hawa watu walikua na maana gani? Je wakenya wakisema Safari asili yake Kenya tutawalaumu? This is serious maana nasikia Safari ipo ktk level ya kimataifa.
Mdau Sao Paulo
michuzi kama baadhi ya watanzania kujiunga na vyama vya wakenya ughaibuni ni sawa, basi matokeo yake, wakenya wanaweza kuzidi kusema mlima uko kao, kuna chama fulani cha wakenya hata raila odinga aliyekuwa mgombea uraisi kenya anakijua, sasa hapo nadhani pia ni mdhamini sina uhakika, ni swali tu kama walishamuhusisha hata odinga, inakuaje, na wakati huyo ndie mmoja aliyesababisha vurugu kenya, kweli tuwe makini na vyama vya wakenya nje ya nchi kwani vinaweza kulete madhara siku moja.
ReplyDelete