Dear Michuzi,
Kwanza napenda kukupa hongera kwa kazi nzuri unayofanya ktk kutuhabarisha habari mbali mbali na pia kuto maoni mbalimbali ya mambo yanaendelea ktk dunia na pia hapa nyumbani kwetu. hiyo ni kazi kubwa kweli kweli.
Mimi nina tatizo moja tu ambalo nataka wadau wa blog hii wachangie mawazo yao ktk kunisadia kulitatua hili jambo japo wengine huwa wanakandia mambo fulani fulani lakini sitakosa maoni mawili matatu ambayo yatanisaidia hivyo ndivyo mimi naamini.
Mimi umri wangu ni miaka 33, nina mtoto wa miaka 4, i am still single woman, ninafanya kazi na ninajitegemea nisingenda kuongelea undani wangu sana nataka kuja kwenye point ambayo imenileta hapa.
Mnamo January nilikutana na kaka mmoja kwenye chat room, na tulipofahamiana zaidi yeye alikuwa na umri wa miaka 37, na ni mtanzania ambaye hanafanya kazi hapa hapa Tanzania lakini kwa sasa yuko nje ya nchi ambapo ni hapa hapa Africa, kwa upande wake yeye bado hajaoa na hana mtoto.
Kwanza napenda kukupa hongera kwa kazi nzuri unayofanya ktk kutuhabarisha habari mbali mbali na pia kuto maoni mbalimbali ya mambo yanaendelea ktk dunia na pia hapa nyumbani kwetu. hiyo ni kazi kubwa kweli kweli.
Mimi nina tatizo moja tu ambalo nataka wadau wa blog hii wachangie mawazo yao ktk kunisadia kulitatua hili jambo japo wengine huwa wanakandia mambo fulani fulani lakini sitakosa maoni mawili matatu ambayo yatanisaidia hivyo ndivyo mimi naamini.
Mimi umri wangu ni miaka 33, nina mtoto wa miaka 4, i am still single woman, ninafanya kazi na ninajitegemea nisingenda kuongelea undani wangu sana nataka kuja kwenye point ambayo imenileta hapa.
Mnamo January nilikutana na kaka mmoja kwenye chat room, na tulipofahamiana zaidi yeye alikuwa na umri wa miaka 37, na ni mtanzania ambaye hanafanya kazi hapa hapa Tanzania lakini kwa sasa yuko nje ya nchi ambapo ni hapa hapa Africa, kwa upande wake yeye bado hajaoa na hana mtoto.
Baada ya kufahamiana zaidi tulielewana zaidi na kwa kweli he was very gentleman, alikuwa ananijali mimi na mwanangu sio kwa mapesa ila kwa salamu nyingi na simu, na alinitumia picha yake na mimi nikamtumia yangu na mwanangu, alifurai sana na mimi pia.
Katika maongezi yetu alikuwa amepanga aje huku mwezi huu wa 3 kuna shughuli zake binafsi na pia tungepata muda wa kufahamiana zaidi, nilimpenda sana kwani alikuwa na maneno matamu yanayoweza kumtoa nyoka pangoni; lakini kitu ambacho kilikuwa kinamuuzi ktk maongezi yetu ya mara kwa mara ni mimi nilikuwa nikimwambia kuwa mpaka sasa hatuwezi kusema mimi na wewe tuna uhusiano wa kimapenzi kwani bado hujaniona mimi naujue kama hutaweza kuwa na mimi au la! lakini yeye alisema kuwa yuko tyr kuwa na mimi kwani haitaji unzuri wa mwanamke ila hanaitaji mapenzi ya kweli, na kwangu hanahisi atayapta hayo matrue love kutokana na maongezi yetu kitu ambacho mimi nilikuwa nakiping mpaka hapo tutapoonana!!!
Siku yamwisho ambayo ndio anajiandaa kuja TZ tulichat naye na akakasirika baada ya kumwambia mpaka aje tuonane ndio tufanye maamuzi, akidai kwamba mimi sina confidence!! na akasema hawezim kuwa na mwanamke ambaye hana confidence!! na kwa sasa yuko hapa TZ lakini hakuna mawasiliano mimi sina no yake ya TZ, lakini yeye anayo na hajapiga mpaka leo!
Je, wadau naombeni mawazo yenu je maamuzi yangu siyo sahihi au ni kweli sina confidence??? tafadhali nisaidieni. kwa sababu nafsi yangu haina raha kama ni mimi ndiye nimefanya makosa!!!!
Mdau wako wa nguvu
Mdau wako wa nguvu
PS: wadau kunradhi, barua hii ilikuwepo awali ila niliiondoa kwani kuna mtu aliingia kwenye sehemu ya maoni na kuchafua hali ya hewa, na hakukuwa na dawa ila kuiondoa posti yote ili kumtoa. kunradhi kwa usumbufu - michuzi
Pole sana dada.
ReplyDeleteKutokana na ulivyojieleza hapo,kwa hakika hujiamini kabisaaaa.ama sio mlimbwende unahofia kukubaliana na jamaa,eti kisa hujakutana nae..!!wakati umashapeperushiana picha.hapo unachotaka nini?
watoto wa pwani wana sema "UNALO HILOO .....Doa"
*KISODA*
Pole sana dada yangu kwa yaliyokusibu. Tatizo kubwa ninaloliona kwako hapa ni kuwa ulikuwa na msimamo mkali sana bila sababu. Isingekuwa tatizo wewe kukubaliana naye provided hayupo kisha huo msimamo ungeuweka moyoni bila yakuuonyesha that much direct kwake. Ukiona mtu kakupenda wewe na mtoto ambaye sio wake, jua amemaanisha. Lakini basi kama kitumbua kimeingia mchanga Mungu atakupatia kingine ila hilo ni somo kuwa ukilinde kisije ingia mchanga tena. God bless you!
ReplyDeleteasilimia 90% ya mapenzi yanayoanzia kwenye chat room ni longolongo, yatakuumiza moyo, utajutia muda wako na mbaya zaidi unaweza achiwa ukimwi..
ReplyDeleteni mbaya kumpenda mtu ambaya hata sura humjui, halafu anaposema yuko huku mara kule, ikawa uongo mtupu kumbe anaweza kuwa kwenye cafe next to your house ila hamjuani. carefull lady you might leave to regret.
dada pole sana,wallah jamaa hafai hata kwa kulumagia na ugali,huna kosa dada jamaa ndio mjinga,tena shukuru Mungu umeona vibwanga vyake bado mapema,kuliko angeficha alafu uwe nae uje juta baadae.
ReplyDeleteDada watu wanaoomba uhusiano kwenye mtandao wako DESPERATE achana nae utampata wako atakaekufaa kama yupo. Achana nae kabisa utu umekwisha siku hizi asije akawa ni mfanyabiashra ya kuuza watu
ReplyDeletewajameni hasa wadada be careful na wachumba wa website,wengine wapo kwa kupoteza mda tu na sio serious looking.unaweza ingia mkenge usiotegemewa.huna kosa dada tht dude ana matatizo ya akili
ReplyDeleteDada nahisi huyo Bro ana kilema.
ReplyDeletePia we jiamini tu kutana nae kama kuna tatizo lolote si utadeside huko mbele ili mradi picha umeiona na umeridhika nae.
kama atakuletea gozi gozi utambadilikia tu huko mbele kwa mbele.
Ila wote wawili hamjiamini
wewe huajimi nae hajiamini asilani.
Kama hajiamini mbona hajitokezi kwako.
Kala ng'ombe mzima anashindwa mkia.
pole dea kwayaliyokukuta ila wewe hujiamini kabisa mmesha tumiana picha inamaana tayari mmekubaliana na huyo kijana huwezi kujua kuwa anafamilia hapa Tanzania ndiyo maana kakukaukia ushauri wa bure jali maisha yako kwani tayari unamtoto haya baba yake yuko wapi? unajua mwenyewe kama unataka mtoto wa pili endelea tu kuumia roho kwaajili ya mtu wa watu. kwaheriiiiiiiiiii
ReplyDeletemwanamme ana 37yrs,alafu ni single mtanzania si kweli atakuwa na tatizo,au anaficha kitu fulani kuhusu yeye.kwa kweli dada huna kosa huyo jamaa ni mpumbavu na anataka kukufanya wewe bwege,eti ukubali kuwa ni wapenzi, kusudi akija bongo apate uroda kiulani kwa kuwa si utakuwa umeshamhalalishia?anataka akupe ngoma huyo hana lolote.be smart sista wenye virus wapo wengi wanatafuta pa kuvisambaza,nakupa moyo endelea kutafuta taratibu wala usiwe na pupa ya mume kwanza tayari una mtoto.
ReplyDeleteukisikia mfumo dume ndo huo sasa,yani mwanamke hana haki ya kutoa mawazo yake yakaonekana na maana.damn...
ReplyDeleteKWA MAONI YANGU MIMI HUYU JAMAA ATAKUWA AMEOA NINAVYOFIKIRIA MIMI SAA INGINE UNAKUWA NA COMPANION WAKO KWA VITU TOFAUTI KAMA VILE KUCHAT ONLINE ESPEACILY UKIWA NCHI ZA NJE KWASABABU YA KUTOKUZOEA MAZINGIRA NA JAMII NI TOFAUTI NA YA KWAKO SO FROM MY POINT OF VIEW IS MARRIED NAUKIRUDI KWENYE UMRI WAKE PIA POSSIBILITY NI KUBWA.HII ITAKUDISSAPOINT KIDOGO:- KAMA ALIJUA UNAKAA WAPI AU WAPI UNAFANYIA KAZI KUTOKANA NA MAZUNGUMZO YENU YA MUDA MREFU ALIKUFUATILIA AKAKUONA AKAINGIA MITI KWASABABU LABDA AJALIDHIKA NA WEWE AMBACHO NI KITU CHA KAWAIDA KILA MTU ANAPENDELEO LAKE SIAJABU HATA WEWE USINGEMPENDA,MFANO MIMI NILISHAWAHI KUKUTANA NA MTU ONLINE TUKAPANGA TUKUTANE PALE PPF TOWER NILIVYOMUONA TU ANAKUJA KUTOKANA NA DESCRIPTION YAKE NILIWASHA GARI NIKAONDOKA BOMBA BAADA YA HAPO SIKUWAHI KUPOKEA SIMU YAKE TENA STORY IKAISHA.KWANZA UJAKUWA KWENYE RELATIONSHIP NAE SO NEVER MIND A LOT TO COME IN FUTURE.
ReplyDeleteHILDA MAPEPE
shenzi kabisa wanaume wa namna hii ndio wale wale kama nimeona jana kwa house maid wetu ambae ni mke wa mtu yani mumewe anapigiwa simu mkewe anaumwa tumbo na kutapika mume anajibu kwa simu mwambieni anywe maji mengi na anaendelea kukauka mpk tunachukua jukumu la kumpeleka hospital na kutundikiwa drip ,vile vile hafiki hata kumuona hosp.dada usife moyo na wachumba ni wengi ila kuna wapo walio serious na fake,so be careful.wish u all the lucky dada but sio kwa huyo mjinga
ReplyDeleteKwani hao watoto baba zao wako wapi. huyo atakuwa anakudanganya tu hakuna mwanaume anayeweza kukupenda kwa sababu tayari umezaa na wanaume tofauti inaonyesha huna confidence. jitunzie wanao na siku hizi mdudu kaenea
ReplyDeletesie wasukuma hatuwezi kusema pumbavu tunasema tumbafu kabisa huyo mwanamme hafai dada anza wala usisononeke kwanza humjui na huna kosa changamka utapata tu mwanamme mzuri.tumbafuuuuuuuuuuuuu by msukuma
ReplyDeletewallah mfumo dume mwenyezi Mungu tunusuru, ni unyanyasaji huu wa kijinsia
ReplyDeletehellow dada!,
ReplyDeletepole sana kwa hayo yote,kiukweli dada angu kutokana na maelezo yako nahisi umeenda sawia na maadili ya kiafrika kwa mwanamke,huenda mwanamme wako aliyekuzalisha mwanzo alikutenda sasa uko makini zaidi,sijui!!,na vilevile nakupa a bit of pongezi kwani uko makini mno,wanaume bwana sisi hatueleweki sometimes siwezi jua huenda alitamani ki2 kutoka kwako labda umbo au whatever,namaana akutumie na akuache,then huwezi jua kama ni kweli yuko bacherol au vp,nahisi kama alikuwa anakupenda angejaribu ku stand na yote unayomwambia then mngekutana face 2 face kisha mngeyaongelea hayo yenu,vile vile kama kweli ana upendo na nia nzuri nawe bila kujali lolote,i swear atakutafuta tu!!,ila ngoja nikunongoneze.....,mdatishe,if u really love him dont afford to leave him,men are dogs,women are supporsed to teach them new tricks they are easy to learn and adapt new things,but they are very mad and go crazy when thy are not well treated!,ni hayo tu,
Am out!
Habari
ReplyDeleteDada yangu mimi ni mwanaume nipo ughaibuni ,mimi nadhani sisi wanaume tuna tabia ya kumuambia mmwanamke unapenda wakati hata hujamuona kwa sura, ambalo ni jambo la kushangaza, unaweza kupenda maongezi ya mtu lakini huwezi kusema kimapenzi hadi utapomuona mtu na kumjua ndio useme unampenda, vinginevyo huyu jamaa anakutamani bali sio kukupenda, kuna love at first site
najua kuna wadau watakataa lakini hiki kitu kimenitokea mimi na niko na huyu msichana kwa miaka 7 na hatujawahi kuwa na tatizo lolote lakini tulikuwa tunaonana kama marafiki japo ilichukuwa muda yeye kukubali ombi langu lakini mwishoni tupo wote hadi leo,sasa dada yangu huyu jamaa inawezekana ana mke tanzania pili labda amekuona wewe na haukuwa chaguo lake, licha ya hivyo kama binadamu angekuambia ukweli mngeonana na mkawa marafiki tu.
your true love will come and your baby is one thing you can hold on to.
cheers
mshoboke
Dada pole sana na matatizo, mie hapo sijaona kama umekosea kitu chochote na kuna kitu kinaitwa "instincts", you should know to trust your own usisahau, manake kwa maisha ya sasa hivi unaweza ukafikiria jamaa yuko nje kumbe yuko hapa hapa akawa anatumia picha ya mtu mwingine na nini mie nimefurahi sana ulivyoshtuka. Wala usisikitike wewe piga hatua mbele, kama huyo bwana kweli anakuhitaji atakuja one way or the other huyu inaonyesha tena wewe hauko peke yako manake angekua mwingine angefanya vitu kiutu uzima taratibu ili muelewane.
ReplyDeletemimi ni mwanamke kama wewe, na kwa kweli upo sawa, sio swala la kutokuwa na confindence, but you are acting in the right way!!! yeye anaonyesha sio mvumilivu!! picha pengine ulipiga miaka ya nyuma ulipokuwa mzuri na kwa sasa pengine umenenepa!! you have to see each other face to face before anything goes on!! achana nae, naona ni mbabaishaji tu na analake jambo. uskonde, i dont think he was meant to be, and if he was, he would realise his mistake. usikimbilie kumtambulisha mtoto kwa mtu amabaye hamajafahamiana. it would bring him a bad picture of u, or confuse him!! all the best.
ReplyDeletenana
Picha huwa zinadanganya na wakati mwingine hasa kwa kina dada ni kuwa huwa wanapaka make up na kubadilika kabisa. Ulikuwa uko sahihi kumwambia kuwa mpaka muonane face to face ndio mseme mna uhusiano, maana ungekubali kuwa na uhusiano halafu akaja akasema 'mhu nilifikiri kuwa una wowowo kumbe umepigwa pasi, au kumbe usafiri wenyewe wasi wasi' Wakati mwingine asingesema hayo yote ila angekulamba kisha akaingia mitini ukashangaa kilichomsibu wakati sukari guru umeshampa kulamba. Yeye ndio hana confidence ameogopa kukutana na wewe uso kwa uso.
ReplyDeleteGirl you were right and you are right, usijali utapata mtu atakayekupenda wewe mwenyewe na sio hao wababaishaji. Kwanza wala kulikuwa hakuna ishu ya kumfanya mtu akasirike, hajakua huyo utoto bado unamsumbua akikua ataacha!
Jamani naombeni tumsaidie, how can she get this man back?? sio kumcheka kwani amejua she missed up! kwa hiyo kinachotakiwa ni jinsi ya kurudisha uhusiano wake, cause still she has the amil and phone no. mpeni maneno matamu ya kumrudisha huyo jamaa anayempenda! mimi ningekushauri mtumia email nzuri za kumbembeleza sawa dear pole sana
ReplyDeleteDADA YOU ARE NOT SINGLE WOMEN !!YOU ARE SINGLE UKAJIREJESHA KULE ULIKOKWISHA PITA SISHANGAZWI NAHUYO JAMAA KWA NINI AKAKUPIGA NA CHINI
ReplyDeleteachana nae huyo mamii,naamini mapenzi hayalazimishwi ni chemistry kati ya wawili,kama we unaona mawazo yenu hayaelekeani basi usilazimishe,atakupigia akijisikia na nina uhakika kama bado ana nia na wewe atakuelezea kilichomfanya asikupigie baada ya kuja hapa dar....amini usiamini mama haya mambo ni nature tu!!!!
ReplyDeleteMhh!Sijui katika mawasiliano yenu ya muda mrefu iliyopelekea hata kutumiana picha lengo lake lilikuwa lipi, I guess lilikuwa muwe wapenzi. Mliwasiliana mkakubaliana na ninahisi kuwa hata ulimfanya aamini kweli tayri nyie ni wapenzi, sasa iweje kigugumizi cha ghafla? Ni kweli huna confidence!
ReplyDelete"Mdau"
hebu tuondelee upuuzi wako huo. Si umesema anakujali na anakupa maneno ya kumtoa nyoka pangoni sasa kama ume accept hiyo hali kwanini ulishindwa kumhakikishia kuwa mtakuwa pamoja. Ni kweli huna confidence ndio maana unatapa tapa. Na ulipokuwa unatuma picha ulifikiri unamtumia nani?
ReplyDeleteSITAKI NATAKA hizo ndizo zilizokuponza mama. na Ukome kumtafuta huyo ni mume wa mtu elewa.
Sio kutokujiamini tu, bali ni tatizo la kasumba!! Kwani hata kama hujaonana naye ukimwita "mpenzi" utadhurika nini... Mmekutana: Nae kama anakupenda angekutafuta; hajiamini.
ReplyDeleteNyote hamjiamini. Kukubali kuwa wapenzi japo hamjaonana sio ndoa, ni matamshi tu, tena yasiyoshuhudiwa. Cha kufanya, mtumie email, mwandikie hivi: 'MPENZI WANGU ... NAKUMITHI MENDHIO, UKO TZ, MBONA THIKUONI MPENZI...'
Neno MPENZI ni la kawaida tu. Nakutakia kila la kheri dada yangu mpenzi.
SEV
Yes you are a coward..hujiamini na bahati ndo ka ivo ishapotea..mtu kakwambia he loves you like you are then bado unamwambia asubiri mpaka akuone? au huna miguu nini ulimtumia passport size?. Anyway just forget and life goes on..next time elewa kwamba love flows in the air. pole sana kama vipi ntafute.
ReplyDeleteWenger
Pole
ReplyDeleteMimi naona wewe ulikuwa unatafuta kitu maana huo ndio mtindo wa wanawake wetu wa hapa mjini.Wenzetu walioendelea sana huwa wanafuata nafsi na sio kingine.Kwa ushauri mi nakushauri umuombe msamaha huyo bwana halafu ukae ukisali huenda akabadili mawazo vinginevyo .....
Dada nakushauri kuwa sana mwangalifu kuhusu mahusiano ya kwenye mtandao, maana huwezi kuhakikisha habari unayoaambiwa. Kuna watu walisha wahi kuuawa kwa njia hiyo.
ReplyDeleteUmri wako usikufanye uwe 'desperate' na kuolewa, kama mtu anakupenda kweli angekua na nia ya kukuona na kuwa na mawasialiano zaidi.
Achana na huyo kaka kabisa, utampata mwingine atakaye kupenda kweli.
Pole sana sister kwa situation iliyokukuta lkn mi am believe una confidence za kutosha coz mi naona hana sababu ya kushindwa kuonana na wewe if the man is real love u atakutafuta unless otherwise atakupotezea muda mapenzi gn bila kuonana live? the man is nt serious stay calm n u wil get another real man
ReplyDeleteMimi nakuunga mkono. Ingawaje kweli mliwasiliana mkapeana hata picha zenu, lakini huwezi moja kwa moja ukaingia kwenye mkataba-hasa wa kiurafiki ambao hatima yake ni mapenzi bila kuonana.
ReplyDeleteYeye kwanini aogope kuonana na wewe kwanza (Sina maana kuonana kimwili, hata yeye sidhani nia yake ilikuwa hivyo.
Hicho kipengele kisiwe kikwazo cha urafiki wenu kama kweli alikuwa na nia na wewe. Na kama yupo hapa Dar,kuna ugumu gani wa wewe na yeye kukutana. Nahisi kuna `kimtego' fulani, au walakini fulani! Be careful.
MAAMUZI YAKO NI SAHIHI KABISAAA, ILA HUYO HATA AKIKUPIGIA SIMU ACHANA NAYE KABISAAA, MAANA INAONEKANA YEYE NDIYO ANA MATATIZO NA ANATAKA KUKUUZIA MBUZI KWENYE GUNIA HUYOOO.HAPO MIMI SIONI TATIZO LAKO NI NINI? KWANINI HUYO KAKA HATAKI MUONANE KWANZA NDIYO MKUBALIANE? LAZIMA ANA MATATIZO HUYO ACHANA NAYEEE.
ReplyDeleteKWA MAONO YANGU, HUYO KAKA ALITAKA AKISHUKA BONGO TU HAKUNA MJADALA ZAIDI YA URODA, SASA HUYU DADA AKAONA SI USTAARABU AT LEAST TUONGEE TUJUANE ZAIDI..DADANGU HUYO DUME NI MRAFI WA NGONO, WALA HUJAKOSEA, HAKUNA MWANAMKE MWENYE AKILI ANAYEWEZA KUKUBALI MOJA KWA MOJA NA HALI YENYEWE HII SIKU HIZI UPEPO UMEGEUKA, UMEFANYA BUSARA SANA, MUME MWEMA ANATOKA KWA MUNGU..HUYO KATOKA KWA SHETANI!! MUANGE ALE URODA MITAANI HUKO NA KUJIFANYA BADO MTOTO..TULIA NA MWANAO BABU..CONFIDENCE UNAYO SANA, YEYE TU NA KUKURUPUKA KWAKE.. NI SEX MANIAC..ACHANA NAYE!!!
ReplyDeleteNakushauri kwa sasa umwache ili yeye akutafute tena hasa kwa kuwa huna namba yake ya hapa, kama hatakutafuta ujue mambo yameisha na uendelee na mambo mengine na kama atakutafuta maongezi yaanzie mlipoishia i.e. kutokuwa na confidence. Lakini kwa namna ya kawaida kwa mtu ambaye anaishi mbali na amekuja hajakutafuta nadhani maelezo yako wazi.
ReplyDeleteHuyo kaka ni mzinzi, mkimbie kama ukoma, matende na mabusha!!!
ReplyDeletehey sioni umuhimu wa kukubali bila ya kumuon huyo kaka una uhakuka gani kama picha alliyokutumia kabla ni yake dada nakushauri kama vipi huja fanya makosa kama kweli anakupenda atakutafuta wewe usiwe na haraka haraka hasarawalinena wahenga ila pole kwani anaonekana hakujali moyoni bali anakujali kwa maneno tu
ReplyDeleteMI MDAU
Anin kirenga (Day)
Dada kutokana na experience yangu katika maswala ya mahusiano, sioni tatizo lako. I don't see what was the problem. Swala la wewe kutokudeclare upenzi sio chanzo cha mheshimiwa kukasirika, bali ana mambo yake personal yaliomsababisha kufanya hivyo.
ReplyDeleteVile vile ukweli ni kwamba mapenzi ya kupatana kupitia chat room huwa haya dumu. (Source by eharmonny.com).
Sioni tatizo la convidence kwenye swala lako, hasa hasa naona your strong woman sababu ulikataa kudiclare relationship which never existed anyway.
Ushauri wa kitaalamu ninaokupa ni huu, kwanza kabisa punguza mgandamizo wa mawazo kuhusiana na swala zima, sababu jamaa alishaonyesha excuses zisizo na kichwa wala miguu. Ongeza mapenzi kwa mtoto wako mpendwa. na mwisho, omba kwa mungu akuongoze kumpata mpenzi atake kupenda wewe na mwanao kwa vile mlivyo.
Kutokuwasiliana na wewe dada nadhani amekupunguzia matatizo tuu. Kwanza ulikuwa unaitaji kumfahamu on one to one basis zaidi, na hili lingekuwa gumu sababu bingwa angetaka mfahamiaene baada ya kufanya tendo. Kitu ambacho ni simu ya kufahamiana, kwani kinachofuata ni kuungana kwa kupitia kitanda.
Good Job mwana dada, wacha aende zake huko aliko.
Wewe na yeye wote mna akilia sawa,
ReplyDeleteWe utampendaje mtu kwa email tu, hata kama alikutumia picha, kama sio yeye je.
Nae pia ni hivyo hivyo,
utakuja uziwa mlio uambiwe ni mbuzi kumbe njemba imebana kichochoroni inaigiza sauti ya mbuzi,
we achana nae tafuta mwengine lakin si kwa email,
Ukikosa kabisa basi njoo hata kwangu kwan nami pia natafuta mke,
Nimemaliza
"Too much advise comfuse" dada yangu.
ReplyDeletePia "kosa ni kurudia kosa" kwani natumaini mtoto huyo ana baba!.
Kina dada wengi wakishafikia umri wako wanakua kama wanaolazimisha ushindi vile,hakika hupata wakati mgumu sana. Kwa sie wakatoliki(samahani kwa watakaokwazika) msichana akiwa katika hali kama hiyo hushauriwa kusali kwa nia thabiti kwa kuweka novena ya sala,aghalabu huambatana na mfungo wa muda wa siku zisizopungua 9.Ukiweza kufanya hili kwa imani yetu tunaamini mungu hurudisha majibu kwa maombi yako kwa namna yatakavyokufikia.
Pointi ya msingi hapo ni kumshirikisha mungu katika wakati huu,naamini utafanikiwa kumpata mume bora. Ushauri wa bure kwako usiende kwa kalumanzira kwani amelaaniwa yule amtegemeae mwanadamu....
George
"Too much advise comfuse" dada yangu.
ReplyDeletePia "kosa ni kurudia kosa" kwani natumaini mtoto huyo ana baba!.
Kina dada wengi wakishafikia umri wako wanakua kama wanaolazimisha ushindi vile,hakika hupata wakati mgumu sana. Kwa sie wakatoliki(samahani kwa watakaokwazika) msichana akiwa katika hali kama hiyo hushauriwa kusali kwa nia thabiti kwa kuweka novena ya sala,aghalabu huambatana na mfungo wa muda wa siku zisizopungua 9.Ukiweza kufanya hili kwa imani yetu tunaamini mungu hurudisha majibu kwa maombi yako kwa namna yatakavyokufikia.
Pointi ya msingi hapo ni kumshirikisha mungu katika wakati huu,naamini utafanikiwa kumpata mume bora. Ushauri wa bure kwako usiende kwa kalumanzira kwani amelaaniwa yule amtegemeae mwanadamu kama kinga na wokovu wake
George
Dada pole sana....
ReplyDeleteMimi kwa maoni yangu naona umefanya sahihi kabisa. sababu kubwa ni kwamba, ku-chat hakuchukui nafasi ya kumwakilisha mtu "physical talk" na pia, ukikutana na mtu face 2 face kuna vitu vingi vitajieleza zaidi ya picha na chat. kwa misingi hiyo, huyo jamaa ndiye ambaye hajiamini hata kidogo.
Keep it up lady, msimamo wako ni sahihi kabisa.
Pole sana dada huyo si mwanaume yeye angekuwa ana mapenzi na wewe si angekusikiliza kwanza, na kweli ulivyomwambia mpaka muonane ndio uone je kweli huyu naweza nikaishi nae sasa yeye anakwambia hauna confidence, achana nae atakupotezea bure wakati.
ReplyDeletePole sana sister, mi nakusihi usiwe na papara, fanya mambo taratibu, usikubali kupelekwa puta kwani wahenga walisema haraka haraka .. na subira huvuta .. Isije ikawa ana lake jambo anataka kukuharibia mambo yako bure. Plse take your time to study the guy na kama kweli yuko interested hawezi kuku turn down kwa staili hiyo. Mbaya zaidi mi nahisi ana mpenzi mwingine hapa hapa bongo ndio maana hajakupigia mpaka sasa. BE CAREFUL!
ReplyDeletekwa nini uondoe...labda ndiyo ulikuwa upande wa pili wa shilingi?
ReplyDeletehaya ni maoni ya upnde mmoja tu.upande wa pili hatuna kwa sababu si wewe michuzi wala huyo kipusa anayelalama humu ndani aliyeweza kutuwekea maoni ya mdaiwa.
leo unataka maoni na mawazo... kulikoni. si bure hapo. pafukutapo moshi kuna moto!
pengine jamaa kafumania. au pengine mtoto hafanani naye kuna kila sababu. hakuna mtu anayeweza kukataa mtoto bila sababu.
asha kum si matusi. kama nitakuwa nimekutukana basi nisamehe;
hivi wewe dada huna wazazi mpaka uje humu kwa michuzi kutafuta msaada wa mawazo?
kabla ya kuvunja ungo uliwahi kufundwa na wazazi wako ukaelemishwa tabia ya MAMBO YA NDANI wewe?
kama uliwahi kupitia huko, sidhani kama ungejitia humu na kuanika UCHAFU wako kwa kisingizio cha kutaka mawaidha....UNALO HILOOO...no 2
Shosti mi naona wala hujakosea. Mbona ni jambo la kawaida tu jamani. Maana mngeweza kuonana, mkajuana vizuri then ndio muendelee au msiendelee na relationship. Maana bwana mngeweza kuonana then maybe kuna kitu kwake ambacho wewe usingekifurahia & vice versa (mfano labda body odour, posture etc)
ReplyDeleteMi naona tu jamaa alikuwa anakuchezea akili au labda yawezekana yupo busy kidogo atakutafuta au labda amepoteza namba yako ya simu.
Kwanini usijaribu kumuandikia e-mail uone kama atakujibu ili uondoe hilo sononeko la moyo. Akikujibu mambo poa, asipokujibu do not waste your time maybe he was just playing you!
helo there,mimi sidhani hana confidence it was jus normal sense u liked eachother il ahuwezi sema mko pamoja mpaka mkutane mkakubaliana n all ,i think he is a bit childish unless alikuwa anatafuta kitu cha kufanya muda uende haraka huko alipokuwa mbali lik talking to you......if he is out there n love u ,feels his heart was with u he should call u !!!stay strong ,believe ur insticts donlet no one make u have self low esteem.
ReplyDeletethanks
lynn
pole sana dada na nakupa moyo kwa yaliyokukuta,naanza kuwa, uamuzi uliouchukua ni mzuri kwa kuwa huyo jamaa hujamjua vizuri mpaka umkubalie kwa kuwa hujui ana madhumuni gani katika maisha yako.sio kila kinachokuchekea ni kizuri kwako na kina mpango mzuri na wewe.
ReplyDeleteKama still huyo jamaa ana nia nzuri na wewe basi atakutafuta coz mapenzi ni maelewano na sio kuforce.......kama anashindwa kukuelewa kwa hilo dogo la kufahamiana vizuri kwa undani cdhani kama atakuelewa kwa mengine.Kaa chini vuta fikira na umuombe Mungu akuonyeshe mtu alie muaminifu na atakaekupenda kwa dhati.Jiamini kwa kua ulichokifanya ni chema na ungekurupukia tu mwanaume na ukiangalia na magonjwa haya.....
kaka michu, humu ndani mapenzi yamezidi sasa.... haukuna vingine!! inaonyesha jinsi dada zetu wanavyohangaika kutupata karne hii!!!
ReplyDeleteJT
Huyo mwanaume alikuwa anakudanganya, anao wengi tu aliokuwa akichat nao na waliomtumia picha pia, alipokuja hata tanzania anawapitia wote, kabla hamjajijua wote mnakuwa wake wenza. Shukuru Mungu katambua unaakili na ameogopa utamgundua mbinu zake hapo baadaye. Kama kweli alikuwa amezimia kwako pekee, kulikuwa na kazi gani kusubiri muonane? He never was committed. Wala usiuhaungaishe moyo wako kwa kuwaza hilo, move on, wako wengi sana kwenye chat rooms, utawapata wengine.
ReplyDeleteDada, nakupa pole sana kwa kudanganywa kifikra na huyo jamaa, alikuwa hayuko serious na wewe, kwani angekuwa amekumind kwenye picha lazima angekuwa na hamu ya kukuona live, that is common sense, kifupi alikuwa anacheza na akili yako tu.
ReplyDeleteThe guy can't be serious move on girl .... You can do better than that, trust me!
ReplyDeleteKuna kitu umekiacha... unasema siku ya mwisho ulimwambia mpaka aje muonane ndo mfanye maamuzi ndo akaanza kukasirika.... Ni maamuzi gani hayo? Inawezekana hayo maamuzi uliyomwambia ndo yamefanya aone huna confidence.
ReplyDeleteLkn pia huwezi jua labda ni wengi mliompeperushia picha, akaona kigoli kingine,ikabidi aende huko...
kusema ukweli siamini kabisa internet dating... na haswa zikiwakutia wasanii. therefore dada usihofu huyo jamaa for your info amekupunguzia mashuzi. Sometimes anaweza akawa mtu anayekujua anakuchezea tuu. cause is very possible kubailisha jina na kila kitu..i have done that kufanya utafiti fulani na nilifanikiwa asilimia 100 ila nilishindwa kwenda kumeet na huyo mtu kwa kuwa face 2 face nisingeweza hide my true identity unless otherwise.
ReplyDeleteSo people ni vizuri kuwa carefuly kuna watu wako addicted na web chatting and they can do anything... mdada umefanya vizuri sana kumuonyesha jamaa you need to make decision mara mtakapoonana. Manake waswahili wa are good in "I LOVE YOU" hata kama kaona picha tuu which is lie kwani unampendaje mtu bila kumjua... kitu kipi kinakufanya ummind bila kumuona... you need to know a person well enough (usokwa uso, kuishi pamoja, same area or under one roof, au to do lots of things together - then you get to know them better) na ndio kuanza kumwambia unampenda
Pole sana dada..ila kaa chonjo wahuni/matapeli ni wengi dunia hii angalia Mungu anavyokupenda kakuepusha.
ReplyDeleteMme mwema anatoka kwa Mungu keep on praying na Mungu atakupa believe me achana na huyo kajambanani alitaka aitwe mpenzi kabla hamjaonana ili akija ale uroda kiulaini atoke nduki ndo zao wanaume wakware na ameshindwa na kulegea.
Huyo atakuwa na mke, mpenzi,amezimika pengine au si rizk kwa nini hajataka muonane?
Ushauri wangu achana kabisa na Wanaume wakuchati muombe Mungu huku ukihudhuria function,kanisani misibani na sehemu mbalimbali zenye mikusanyiko ya watu mbalimbali wapo wanaume kibao wenye heshima zao watakutaka i believe.
Mimi nilishawahi kufikwa na dizaini kama hiyo ila sasa jamaa alikosea namba akapiga kwangu nilipomwambia mimi ni mtu mwingine tofauti na aliyemkusudia akasema sorry, siku ya pili akapiga ohhh dada nimependa sauti yako mara ohhh tukutane break point nikamwambia sorry mimi ni jini alinitumia msg kama kumi za kuomba sorry.
Achana nae huyo atakuletea ngoma tu!
Unanifurahisha sana!!!
ReplyDeleteUna miaka 33 na unaifikiria kabisa kukaa kwenye computer upate mwanaume mwenye akili timamu, na mwenye sifa nzuri ya kuwa mume wako. Umepoteza muda wako kwa kuwasiliana na watu wa mitandaoni na sasa unazidi kupoteza muda wako na watu wengine kuuliza maswali ambayo majibu yake unayo mwenyewe. OK sasa kama hujajua mpaka sasa huyo bwana alitaka kukuongezea kwenye orodha yake ya wanawake rahisi, rahisi. Alichotaka ni kukuteka mawazo na hisia zako ili akija tu kabla hajaonana na wale aliowazoea akufanyeeeeeeeeee, halafu aende zake. Na una maana gani unaposema ni gentleman??!! Halafu unafikiaje uamuzi wa kusema anakupenda wewe na mwanao? Upendo huo uliuona wapi?? Mama yako si alikwambia usimwamini wanaume usiowajua wewe?!! Inakuwaje unaenda kuparamia wanaume wa kwenye mitandaoni. You are 33 for God's sake. Grow up and get yourself something to keep you busy.
women = feelings, feelings, feelings.. yuck, let that sucka go and save yourself a heart attack.. damn!!!
ReplyDeleteBRO MICHUZI HI
ReplyDeleteHONGERA KWA KUWA NA BLOG NZURI YA KUTUPA HABARI MBALIMBALI.
NASHAURI KAMA INAWEZEKANA WAFUNGULIE WATANZANIA BLOG NYINGINE YA KUSHAURIANA AMBO MABLIMBALI YA MAISHA IKIWA NI PAMOJA NA MAMBO YA MAHUSIANO HUSUSANI MAPENZI.
KWA MFANA DADA HUYU ANAWEZA AKAWA ANAHITAJI MSAADA LAKINI WATU WAKACHUKULIA MASIKHARA NA AKASHINDWA KUPATA ALICHOKUWA ANAHITAJI
KWAKO DADA POLE NA YALIOKUKUTA
MIMI ANDHANI UNA NDUGU KIBAO PAMOJA NA MARAFIKI WENGI SANA NA KAMA WEWE NI MUUMINI WA DHEHEBU FULANI BASI KUNDI ZIMA LA WATU WANAOKUZUNGUKA LINGETOSHA SANA KUKU SHAURI KULIKONI KUJA KUJIANIKA HADHARANI KWA WATU WASIOKUJUA WAKUSHAURI MIMI NAGHANI UMEPOTEA NJIA
MTAFUTE MANKA AKUFUNDISHE VIGEZO VYA MWANAUME HALAFU NASIKIA ANAFUNGUA MANKA MUSHI MATCH MAKER SOOON MWE AKILI KAMA YAKO
ReplyDeleteMOH
kwanza mapenzi ya chatroom ni matatizo kweli...mie nakushauri achana nae coz angekuwa anakupenda "kweli" angekubali msimamo wako kwani sio muda mrefu mpaka anaenda huko tz
ReplyDeletedada yangu mpendwa!!nakushauri usiumize kichwa chako na kuumia moyoni.achana na huyo mtu asiye na mwelekeo wewe angalia mwanao ambaye ni kitu cha muhimu kwa sasa,kama yupo mtu ambaye atakupenda na kutaka kuwa nawe kimaisha basi wakati utafika naye atajitokeza.mambo haya hayana haraka,angalia usijevamia mtu mabaye atakuwa mwiba kwako na kwa mwanao.
ReplyDeletedada kwanza kabisa una confidence, unajiamin tena sana, na dada naomba sana nkupongeze kwa hilo, natambua baaadhi ya wadau mtakuwamnanishangaa kwa nini nimesema dada anajiamin,ila huo ni ukweli na utaendelea kuwa ukweli mpaka siku ya mwisho.
ReplyDeletehongera kwa kuweza kuonyesha msimamo wako mpaka saaa ya mwisho, na hiyo ndo confidence.
huyu kaka alikuwa anang'ang'ania kuwa mpo kwenye uhusiano wa kimapenzi ili tuu akija tanzania aweze kulala na wewe naakiondoka ndo sahau.
what i can assure you ni kwamba huyu mlume alikuwa hakupendi hata kwa tone, kwan angekuwa anakupenda kwa moyo na wala si kwa kichwa then asingeweza kukaa tanzania walau cku mbili bila kukutafuta.
huyu jamaa huwezi jua alikuwa anatumia fedha za kampuni kukupigia cm, au alikuwa anakupigia pale anapouwa mpweke, au labda kuna maneno alikuwa anayasikia kutoka kwako na hajawahi kuyasikia kwa mwingine, ni c kwamba alikuwa ANAKUPENDA KAMA UDHANIAVYO.
dada if you love someone let him go if he comes back he was yours and if he wont then he was never ment to be your dada.
peace of advice dada, natambua kwa sasa wataka kuwa makini sana kwa sabb una mtoto, na ili kweli upate mme wa kukuoa yabidi ufanye kazi ya ziada, kazi yenyewe ni kujiheshim na kuuheshim mwili wako, wanaume kwa sasa wanajali sana maisha yao, na hivyo hutafuta wanawake wenye kujua dhamani ya maishi, wenye kujiheshim, wenye kutambua maisha, mume utampata, tena mume bora tuu, la msingi jiheshim, na fanya waliokuzunguka wakuheshi,
usije kuwa na mtu kwa sabb huna choice, kwa sabb mtu kamnunulia mtoto wako pipi, kwa sabb mtu anakujulia hali, kuwa na mtu kwa sabb anakujali, kukuheshim wewe na hisia zako.
mungu akubariki sana katika maisha haya ya ktafuta utakayeishi nae
ila nakuomba usemi wa bahati haiji mara mbili wala usije kuwa kichwan mwako kwan nyingine huwa c bahati bali.....
wadau sor huwa kama ntakuwa nimemkwaza mtu
Mimi ni mwanamke na sijasoma maoni yeyote hapo juu bali ujumbe wako tu. Uamuzi wako ni mzuri sana. Alichokua anaharakisha ni kimoja na unajua wee. Alitaka aje hapo bongo na ajifanye ni mpenzi mzuri apate anachotaka halafu akiondoka tena ni kwaheri...
ReplyDeleteUmefanya la maana...alizania kwa vile una mtoto na umri wako basi ni easy target kwake kupata anachotaka....Thanks God you are smarter than that....
Kama ni mpenzi kweli kwanini asiku email au hata kukupigia simu kama ana contact zako...??? Just think about that...mtu aliyekua anakupenda few days ago leo hata salamu na yeye yupo hapo!!! Hakuwa na mapenzi ya kweli huyo...
Na si ajabu mlikua kumi kwenye mtandao kama wewe anawakejeli wote tu...
Mimi ni mkubwa zaidi yako, sijaolewa na sina mtoto. Nina elimu na kazi nzuri. Na baadhi ya wanaume wa kibongo wakishaona una miaka zaidi ya 30 basi wanazania unaharaka ya kuolewa kwa the so called clock ticking.... Watakutaka kwa jambo moja tu wakiona msimamo wako wanakukimbia kama nini. Na pia wanakua wananata, wanajidai, kukuringia, kusumbua kwa vile wanajua unataka mwanaume wa kukuoa kwa the stupid idea ya wajinga na wanafikiria they are your only savier...I am telling you wajinga wajinga achana nao. Keep your head sraight, mimi nimepersevere until now I have the real man that I have been looking for all these years and the wedding bells are soon ringing.
Just hanging there...peace and Good luck
kunashida nyingi walizo nazo watu lakini wanakataa ukweli kuziweka wazi ili wasaidiwe.wanao kukatisha tamaa achana nao,hapa kuna watu wanamitizamo kuanzia hafifu hadi bora.wenye upeo mdogo hadi mkubwa. hivyo utaokota linalo faa,lisilo faa utachuja.
ReplyDeletenikweli umri wako umeenda,lakini uzuri tayari unamtoto.mtunze mwanao. na ukipata mzazi kama wewe anaye tafuta mke mnaweza fanya familia nzuri maana mna share the commons.
OMBI:MR. MICHUZI au YEYOTE MWENYE KUWEZA KUFANYA HILI, ANZISHENI DATING WEBSITE YA KIBONGO ILIWATU WAWEZE KUWA ACCESS WANAO WAFAA.
msijifanye kuwa hili tatizo hamlioni,wakati sign&symptoms zake tayari zinaonekana hapa. warahisishieni watu kutafutana na kufikiana,sio lazima wakutane church,misibani,au ktk sherehe.this can make the best to unite singles and get time to know each other.otherwise itakuwa ile mnatka lakini kusema hamtaki, ooh MFICHA UCHI HAZAI! japo sikuhizi kisayansi anaweza kuzaa,lakini pia lazima watalaam pia huo uchi watauona tu.
kiuno.
ACHANA NAYE HUYOO DADA YANGU, NDIYO MATATIZO YA MAPENZI YA ONLINE HAYO, WAKWELI NI MMOJA KATI YA ELFU MOJA.HUYO LAZIMA KAOA TUU, WENGI WANATAFUTA WA KUPITISHIA SIKU TU LAKINI HAWAPO SERIOUS NA AHADI WANAZOTOA.NA HATA HIVYO MARA NYINGI HUWA HAWACHAT NA MWANAMKE MMOJA TUU LAZIMA ALIKUWA ANACHAT NA WENGI SASA HUWEZI KUJUA LABDA KUNA MWENZIO PIA ALIAHIDIWA HIVYOHIVYO NA AKAONYESHA PICHA PIA NA JAMAA USIKUTE KAANZIA HUKO KWA MWENZIO NA AKANOGEWA, MUNGU ATAKUSAIDIA UTAPATA MWENZAWAKO MWENYE HERI NA WEWE, ACHANA NA HAO WA ONLINE KABISA MAANA HAWAKO SURE NA NINI WANATAKA. MAPENZI YA ONLINE SIYO SAFE JAMANI, NI MARA CHACHE SANA KUPATA MTU MUAFAKA OHOOO.
ReplyDeletehongera sana kwa kuwa na msimamo, unajua watu wengi walio nje ya TZ kwa kweli ni wapweke, sasa wakipata mtu wa kupoteza nae muda ataact kama kweli lakini ni uongo na kujifariji na mikazi ya kubeba box. Nakuomba achana nae endelea kumwomba mungu tuu atakupa mume bora.
ReplyDeletemdau UK
DADA...HUYO KIDUME ALIPOTUA TU WENZIO WAKAMUONA WAKAANZA MAWASILIANO YA USO KWA USO NA YEYE KIDUME INAELEKEA "..ANAMSHAWASHA.."...HONGERA KWA MAPENZI YAKO YA INTERNET.."..IN ......WASWABIRINAH.." BIBIE
ReplyDeleteDada msimamo uliochukua ni sahihi acha kupoteza muda. Fikiria mambo ya maana, songa mbele na maisha achana na matapeli.
ReplyDeletewala usiwe na pressure my sister, achana na wapenzi fake wa kwenye net, utapata matatizo, wa kwako yuko, mungu kakuwekea.
ReplyDeletemfano hai, kuna jibaba moja linaishi ughaibuni, kazi yake kutafuta wanawake wa kitanzania kwenye net, akija likizo anahama nyumba hadi nyumba kwa hao wanawake, kula bure, kulala bure na mengine ya bure, kutwa card ya ATM imesahaulika nyumbani au sijui pesa zimefanyaje, nitumie credit kwenye simu maana nilipo hakuna, ili mradi siku zinaenda kwa bure. yalimkuta rafiki yangu, bahati nilimshtua mapema, ila nasikia kuna dada mwingine yeye ndio alitiwa short ya shs. 2m za kitanzania na mkaka mpenda dezo akapanda ndege bila kuaga kurudi ughaibuni ambapo pia habari za kuaminika anatunzwa na jimama la huko. huyu dada aliamua kushitaki kwenye vyombo vya sheria, ila sijapata habari kama alifanikiwa kupata pesa zake. hivyo shukuru my dear, huwezi jua mungu kakuepushia nini. mara nyingi matapeli wana kauli nzuri sana mdomoni.
WE MCHANGIAJI WA march 18, 9:01 INAONEKANA UNA KIBURI SANA NDO MAANA IMECHUKUA MUDA KUOLEWA HIVYO, MAMBO YA ELIMU NA KAZI NZURI YAMETOKA WAPI? (MANKA TYPE), INAWEZEKANA KIBURI CHAKO CHA ELIMU NA KAZI NZURI NDO KIMEKUFANYA UCHELEWE HIVYO.MTU UNA ZAIDI YA MIAKA 33 NDO UMEPATA MCHUMBA MWAKA HUU, AIBU. INAONESHA NA WEWE ULIKUWA NA MISIMAMO YA KIJINGA NDO MAANA ULICHELEWA HIVYO. ANGALIA SANA ISIJE KUWA HATA HUYO ULIYE NAE SASA AKAWA ANAKUDANGANYA TU.
ReplyDeleteBIG SAM
DEAR Mzee Michuzi nina kitu kimenisikitisha sana naomba wa Tanzania wenzangu tutoe jibu. juzi niliona maandamano makubwa hapo dare es salaam watu wakilalamika kuhusu islaer kumbom mpalestina waliweza kuingia balabalani na kuandamana lakini wanashindwa kukumbuka kwamba uko sudani darful watu si chini ya weusi million nakitu waislam wa meuawa na wa Arabu nyumba zao kuchomwa moto wame zuia hata UN KUTOA MISAADA kwenye kambi za wakimbizi sijaona wa islamu wa tanganyika ama zanzibar wa kiandamana kuomba dua kwa hao ndugu zetu wa darful wanao umia mpaka leo kukosa sehemu za kuishi chini ya utawala wa wa arabu wa sudani egepty tunisia and more country in africa wanaishi wa arabu lakini sijawai kusikia wa africa tukiwafuza kwamba warudi kwao kwani wanashindwa nini kushi na hao wa jewish kama sisi wa africa tilivyo weza kuishi nao kwenye nchi zetu kwa amani wewe kama binadamu na akili zako una tegemea kwamba wamarecani wakimfukuza black ata kwenda wapi kwani ajui alitoka sehemu gani ya africa au south africa wakimfukuza mzungu ajui nchi gani alitokea ndi maana sisi weusi tume muacha mmzungu aishi africa ingawa tunajua na tuna kumbuka mambo yote aliotoufanyia hayo ndio mambo ninayo kuomba bwana michuzi sisi kama watanzania kuyajadili kabla atujaingia kwenye ma andamano.
ReplyDelete