NAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUWATAKIA WADAU WOTE POPOTE MLIPO DUNIANI PASAKA NA MAULIDI NJEMA. NI FURAHA ILIOJE KUADHIMISHA SIKUKUU HIZI TAKATIFU HUKU TUKIENDELEZA LIBENEKE KAMA KAWAIDA.


SI RAHISI KUMTAJA KILA MMOJA KWANI WENGI NI 'MAANONY' ILA KWA UCHACHE NIWATAJE MH. BARAKA WA CHIBIRITI PAMOJA NA ANTI SUBI NA BIBIE MANKA MUSHI AMBAO BILA SHAKA NDIO WAMEKUWA WAKITUCHANGAMSHA KWA MADA ZAO MOTO PAMOJA NA UVUMILIVU WA HALI YA JUU KWA UTANI MWINGI AMBAO WABONGO TUMEJAALIWA NAO, NA AMBAO BAADA YA SULUBU LA KUZUNGUSHA GURUMU LA MAISHA HULETA VICHEKO KATIKA KILA KONA.


VILE VILE NAPENDA KUWAARIFU KWAMBA MDAU WA MILIONI 4 ANAKARIBIA HIVYO SI VIBAYA TUKAANZA SASA KUPANGA NAMNA YA KUMPATA ILI KUONDOA UTATA AMBAO UMEKUWA UKIJITOKEZA KWA NAMNA MOJA AMA INGINE, HASA IKIZINGATIWA KWAMBA MFADHILI AMEONESHA NIA YA KUONGEZA DAU TOKA DOLA 500 HADI DOLA 1000 KWA ATAKAYEBAHATIKA KUWA MDAU WA MILIONI 4.


NAKARIBISHA MAONI YA NAMNA YA KUMPATA MDAU HUYO WA MILIONI 4 NA TUTAPOKUBALIANA, KWA NAMNA YA WENGI WAPE, IWE HIVYO PINDI MUDA UTAPOWADIA.


VINGINEVYO SINA LA ZAIDI ILA KUWASHUKURU SANA WADAU KWA KAMPANI YA NGUVU MNAYONIPA KIASI NAJISIKIA NIKO KILA SEHEMU DUNIANI NA SI BONGO PEKEE.
OMBI LANGU KWA WADAU WOTE NI KUENDELEA KUPENDANA NA KUKOSOANA PASIPO KUCHAFUA HALI YA HEWA, NA IELEWEKE KWAMBA KILICHO CHEMA KWA BATA MZINGA NI KIBAYA KWA KUKU. HIVYO SI RAHISI KWANGU KUWEZA KUMRIDHISHA KILA MMOJA WENU HATA IWE VIPI. HIVYO NA TUVUMILIANE KWA LOLOTE KATIKA KUENDELEZA LIBENEKE.


NATOA SHUKKRANI ZA DHATI KWA WACHANGIAJI WA MADA NA PICHA AMBAO PIA NI WENGI NA SINA UBAVU KUWATAJA WOTE, HIVYO NAOMBA MPOKEE SHUKRANI ZANGU KWA MPIGO HUKU NIKIACHIA MLANGO WAZI KWA MICHANGO YA MADA NA PICHA KWENYE GLOBU HII YA JAMII KUPITIA issamichuzi@gmail.com
NITAKUWA MTOVU WA FADHILA NISIPOWASHUKURU PIA SPONSA WA GLOBU HII YA JAMII WAKIWEMO TIGO, EASY FINANCE, BANG! MAGAZINE PAMOJA NA ARISE BEAUTY SUPPLY AMBAO NAWAAMBIA ASANTE KWA KUNIWEZESHA KUENDELEZA LIBENEKE NDANI NA NJE YA BONGO


ASANTENI WADAU WOTE, MOLA AWE NANYI DAIMA

-MICHUZI


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. fulanazzzzzzzz
    michuzi yaani mie hujanitaja, poa tu! nimekumind!
    sikukaribishi tena supu ya utumbo!
    tunashukuru kwa salamu za sikukuu, sijui mwenzetu utakuwa wapi, kama vipi karibu kitaa.
    maoni yangu kuhusu kumpata mdau wa mil4, apatikane kwa kutuma chochote kwenye hii blog huku akiambatanisha namba ya simu, wewe ndio utahifadhi hizo namba maana ukiziexpose na namba hapa ni kukaribisha usumbufu, si unajua tena...
    ni hayo tu!

    ReplyDelete
  2. AKISENTE KAKA MICHU SIKU KUKU NJEMA IWE NA WEWE PAMOJA NA FAMILIA YAKO AMANI YA MUNGU IWAFUNIKE NAKUWAHIFADHI.

    ReplyDelete
  3. Brother Michuzi, na mimi pia nakutakia maulidi na pasaka njema naa kukushukuru kwa kuendeleza libeneke kataika blog yako maarufu.

    Mimi nafikiri njia rahisi na ambayo iko reliable ni kwa mtu atakayedai kuwa wa milioni 4 kukutumia screenshot ya wakati akivisit blog ambayo itaonyesha hit counter kwa chini, kuthibithisha madai yake.

    ReplyDelete
  4. Mkuu asante Katshirt hako hakaishi ama unavyo vingi, ni long long time nakuona nako unadunda tu hahahah

    Masanilo

    ReplyDelete
  5. tiintii..sms imepokelewa.

    Mimi pipa nakutakia Pasaka njema na Maulidi njema kaka MISUPU.


    tupo pamoJAH..

    ReplyDelete
  6. jamani kaka michuzi asante sana kwa salamu hizi. Je na wewe unauza sura?by the way you look handsome....je una mke? kama unaye je unampango wa kuongeza mke mwingine?maana sijui wenzangu huwa wanafanye hadi wanaolewa....nimeamua tu nijilete kwako hata kama nitakuwa mke wa tatu haina neno. Niko tayari kubadili dini.

    ReplyDelete
  7. Nashukuru sana kwa kunikumbuka, sina mengi zaidi ya kukushukuru sana Bro.Michuzi. Pia na wewe kila lakheri sana katika sikukuu hizi takatifu. Ubarikiwe pamoja na Familia yako yote. Asante sana!
    CHIBIRITI.

    ReplyDelete
  8. hahahahaahaaaaaaaaaa!mzee wa fulanaz tunashukuru kwa salaam zako na wewe pia pasaka njema na maulidi pamoja na familia yako bro!ila hiyo fulana itkujua wewe ni nani manake mmh,au umekuwa mhindi na wewe nini kwa kuabudu mambo tofauti na wengine?fulanaziiiiiiii,

    ReplyDelete
  9. Kaka Michuzi nikushukuru kwa salam zako za heri ya sikukuu! Nawe ninakuombea heri.

    Wana 'globu ya jamii' ninakutakieni heri, baraka na fanaka katika sikukuu hizi na pia katika siku nyingi zijazo kadiri atakavyokujalieni Manani.

    Idumu 'Globu ya jamii'!
    Zidumu fikra endelevu za wana-'Globu'

    Subi'
    nukta77.com
    & nukta77.blogspot.com

    ReplyDelete
  10. Tuko pamoja.... Sikukuu njema huko Bongo Michu... Na wadau wote popote tulipo ktk kuzisaka noti.... sikukuu maboksi yanalipa zaidi.... teheteheteheteheeeeee...

    ReplyDelete
  11. SLIME YAKO NZURI NA YA KWELI KAKA YANGU KWA SABABU HAIBADILIKI.....SIO ZILE FEKI ZA WENZETU...UKIGEUKA NYUMA TU IMEONDOKA USONI. IDUMU SMILE YA MICHU!!!!!! IDUMU!!!!

    ReplyDelete
  12. ahsante sana kaka michuzi kwa salam zako za sikuu na wewe pia tunakutakia heri,kuhusu mshindi wa milioni 4,nitafurahikia apate ushindi huu kaka chibiliti kwani ni shujaa wa blog yetu.

    ReplyDelete
  13. Eid-e-Miladun Nabi...Mashaalah

    ReplyDelete
  14. ZE fulanazzzz...naivizia tuu kwani mishemishe zako mh m.i.m nazijua siku ukifua tuuuuu..nimeibaaa! ntaona unaapia na mvao gani!...samahani

    ReplyDelete
  15. MOSTI WANTEDI!

    KWA ATAKAYEFANIKIWA KUMUIBIA MICHUZI FLANAAZ HII NTAINUNUA KWA DOLA 800/= PAPO KWA PAPO....mail ya kampeni hii ni ibaukamatwe@michuzi.blogspot.com...SORRY

    ReplyDelete
  16. Tufanye hivi waliooa/olewa humu ndani wanyooshe vidole waliobaki waelewane. lakini Issa kesha oa si aliwaambiaga? anao watatu tayari. Good luck anon hapo juu

    ReplyDelete
  17. Asante sana kaka Michuzi. Nakutakia sikuu njema wewe na family yako

    Mama Malaika

    ReplyDelete
  18. ASANTE KAKA MICHUZI KWA SALAMU ZA SIKUKUU SEMA UNGEONGEZEA TU TANGAZO LA GRAND SLAM SUNDAY LA LIGI YA UINGEREZA AU UNAMUOGOPA MAN UNITED? MIE UTABIRI WANGU HUU HAPA NAKUWEKEA
    MAN UNITED~ 1 LIVERPOOL 1
    CHELSEA 1 ARSENAL 2

    ReplyDelete
  19. ASANTE SANA KWA SALAMU ZAKO BWANA MICHUZI MUNGU AKUZIDISHIE AFYA NJEMA

    MANKA S MUSHI

    ReplyDelete
  20. Asante sana Michuzi kwa kututakia heri ya Pasaka (na Maulidi).

    Muonye Rafiki yako Mjengwa aliyetuwekea picha ya demu mwenye mimba aliyetundikwa msalabani kama Yesu.
    Ajue sisi tumeshakisoma na kukitafsiri kitabu cha Salman Rushdie 'The Satanic Verses'. Tunakaa kimya tu, Uislamu tunaufahamu vizuri pamoja na mapungufu yake yote.

    ReplyDelete
  21. hivi Michuzi huna nguo nyingine? Una bore sasa , au huwa unaazima kwa marafiki.
    Zuwena

    ReplyDelete
  22. Hongera Misupu kutuleta karibu. Mwenyezi Mungu akubariki. Nami nakutakia sikukuu njema wewe na familia yako

    ReplyDelete
  23. WEWE ZUWENA NGUO YA MICHUZI INAKUKERA NINI AU NDIO UNAMTAKA KIJANJA SIO MAANA KUNA NJIA NYINGI ZA KUMTONGOZA MTU PILI MKE WAKI YEYE SIJASIKIA AKISEMA INAMKERA SASA WEWE INAKUWAJE .SORRY MICHUZI IS NOT REACHABLE IS WELL MARRIED

    ReplyDelete
  24. BRO MICHUZI,

    NAKUTAKIA HERI ZA SIKUKUU NA WEWE PIA.

    AHSANTE

    ReplyDelete
  25. Hakyamungu.... Annon aliyesajesti wenye doa wa humu kijijini wanyooshe mikono, na waliobaki waelewani >>nimenyoosha, ila sijapata jibu!

    Au ulimaanisha tunyooshe 'mkono' gani mzee. Wanaume tunanyoosha kwingi ujue...
    SEV

    ReplyDelete
  26. Hao sponsor ARISE BEAUTY SUPPLY NDIO AKINA NANI? AU NDIO LILE DUKA JIPYA LA PAFUM NA VIPODZI SINZA? LINA VITU VIZURI NA WENYE DUKA KUMBE WAMEOKOKA bwana!!

    ReplyDelete
  27. Kadumu ka-tisheti ketu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...