Pamoja na mambo mengine, Mh. Pinda aliwaambia washiriki wa semina kwamba ripoti ya wataalamu ya uchunguzi wa wahusika wa kashfa ya Richmond atakabidhiwa wiki ijayo na atatoa mapendekezo ya nini kifanyika kwa JK. habari zaidi juu ya hilo bofya hapa na soma sehemu ya hotuba aliyotoa leo hapa chini...
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali itaendelea kulisaidia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ili liimarike kiutendaji na kibiashara na lijiendeshe bila ya kuitegemea serikali.
Alikuwa akifungua semina ya Wabunge kuhusu miswada ya sheria za umeme na biashara ya mafuta kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo (Jumatano Machi 19, 2008),
Waziri Mkuu pia alisema kwamba kuna mpango wa kuliwezesha Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) lifanye biashara ya mafuta ili kutathimini na kuisawazisha (checks and balances) biashara hiyo nchini inayofanywa pia na mashirika na makampuni mengine.
"Napenda kuwashauri Waheshimiwa Wabunge kujadili na kuipa nafasi ya kutekelezwa kikamilifu mipango na mikakati ya kuendeleza sekta za umeme na mafuta ya petroli kwa kasi," alisema.
Semina hiyo ilianzia Dodoma mapema mwaka huu, lakini haikumalizika vizuri. Madhumuni ya semina ni kutoa nafasi kwa Wabunge kuipitia na kujadili miswada kabla ya kufikishwa Bungeni.
Waziri Mkuu PInda alisema katika kuiimarisha TANESCO serikali pia inaazimia kuondoa ukiritimba wa Shirika hilo "siyo kwa maana ya kuiua TANESCO, lakini kwa kuweka mazingira ambapo huduma itatolewa kwa ushindani hivyo kumnufaisha mteja".
Kuhusu TPDC Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa Shirika hilo litasaidia kuifanya serikali itathimini na kuiweka sawa biashara ya mafuta kwa sababu ni rahisi kupitia hesabu za Shirika hilo na kuweza kubaini udanganyifu wowote katika biashara hiyo.

Mie nafikiri wazo la kuondoa ukiritimba (monopoly) wa TANESCO itakuwa nzuri, kwani kukiwa na companies nyingine zitazotoa huduma ya umeme itasaidia sana wateja kwani kutakuwa na competition hivyo umeme utashuka bei na hata huduma kwa mteja itakuwa ni ya haraka tofauti na sasa. Mteja akitaka umeme yapasa asubirie muda mrefu ndio umeme uvutwe nyumbani kwake.
ReplyDeleteJamani kumbe Makinda bado yuko kwenye ulingo wa siasa.
Mama Malaika
UK
Mimi binafsi sioni kama ni wakati muafaka wa kuruhusu makampuni binafsi ya kigeni kuanza kuuza umeme Tanzania kwani bado tuna matatizo mengi ya mikataba yanayohusiana na umeme kitu ambacho ndicho chanzo cha bei kubwa. Nadhani ni vema serikali ikamaliza matatizo ya mikataba mibovu iliyoingiwa na Tanesco na IPTL, AGREKO, SONGAS kabla ya kuanza kuwaruhusu hawa jamaa otherwise itakuwa maafa kwa taifa. Pia sindhani kama tukiruhusu makampuni binafsi bei ya umeme itashuka kwani gharama za uzalishaji umeme ni kubwa na kwa kampuni binafsi mteja atalipa 100% +faida tofauti na sasa ambapo serikali ichangia kupitia tanesco. Mfano mzuri ni bei za mafuta jinsi zilivyo unstable hapo nyumbani kwa sababu ya makampuni binafsi kupandisha bei kila siku kwa kingizio cha bei ya dunia. Wanachi inabidi tujifunze kutokana na makosa na si kila kitu ambacho serikali inafanya kina matokeo mazuri (mifano mnayo mingi). Kumbukeni wafanya biashara siyo rafiki wa masikini, hivyo maeneo yaliyo vijijini yatachelewa kupata umeme kama tusipoipa nguvu tanesco.
ReplyDeleteHongereni wabunge kwa kuukataa huu mswada, wakati ukifika utapitishwa lakini siyo sasa. Pia nashauri ikiwezekana tanesco iuze hisa kwa kampuni ya uwekezaji ya wazawa, NICO ili ijiongezee mtaji na pia itapunguza wizi wa umeme kwani wenye hisa watakuwa walinzi wazuri wa transfoma pamoja na wezi wa umeme. NCHI HUJENGWA NA MWENYE NCHI.