TUNATOA SHUKURANI NYINGI ZIWAFIKIE WALE WOTE WALIOSAIDIA KWA MISAADA YA AINA MBALI MBALI KWA AJILI YA KUUSAFIRISHA MWILI WA RAFIKI NA NDUGU YETU KADUMA THOMAS MSUKA.
MICHANGO IMEPATIKANA DOLA 24,678.
MWILI UTASAFIRISHWA JUMATATU TAHERE 17 SAA ZA JIONI KUTOKA DALLAS INTERNATIONAL AIRPORT NA KUFIKA TANZANIA JUMATANO.
MICHANGO IMEPATIKANA DOLA 24,678.
MWILI UTASAFIRISHWA JUMATATU TAHERE 17 SAA ZA JIONI KUTOKA DALLAS INTERNATIONAL AIRPORT NA KUFIKA TANZANIA JUMATANO.
MWENYEZI MUNGU ABARIKI KILA MMOJA AMBAYE AMESAIDIA KWA NJIA YOYOTE ILE.
R.I.P BROTHER KADUMA.
Tafadhali tunaomba ieleweke, tulichanga FEDHA ZOTE HIZI $ 24,678 sio kwa kusafirisha mwili wa rafiki yetu tuu !Vilevile tulitoa kwa AJILI YA MTOTO WA KADUMA(ANGEL),gharama za msindikizaji mdogo wake Kaduma(Robert)etc.
ReplyDeleteUdumu udugu wa kitanzania; katika shida na raha, pahala popote, wakati wowote.
ReplyDeleteWatu wanaelewa huna budi ya kufafanunua. Michango yote ya misiba pesa zinabakia huwa wanapewa hao ndugu wa marehemu eg mtoto, mke au girlfriend.au hata kutumwa huko kwa wazazi wa marehemu.
ReplyDeleteMsaada kidogo, poleni wafiwa kwa ujumla, hivi jamani mnao ishi huko Maryland naomba kuuliza swali kuna jamaa mmoja aliondoka Tz siku nyingi sana kwa jina anaitwa Paschal tunsikia anaishi Maryland lakini hatuna uhakika is it true? please let us know.
ReplyDeleteNdugu wa Karibu
Nawapongeza sana watz wa Maryland & DC, kwa kufanikisha shughuli hii ya kaka na mpendwa wetu Kaduma, umoja na upendo niliouna kutoka kwenu umenifariji sana kujua hata kama tuko mbali na nyumbani, we still love & care for each other! True love & Unity will always be our prestige,Mungu awabariki na kuwazidishia ktk yote.
ReplyDeleteMtz kutoka Ohio.
Kumetokea mabadiliko ya tarehe ya kuondoka mwili wa marehemu,hii ni nje uwezo uwezo wetu ,mwili utaondoka j'tano saa 4.45 jioni utafika Dar saa 10.35 a'lhamisi usiku,mdau hapo umeongea kuhusu michango,kama upo hapa DC,MD au VA tafadhali usisite kuiona kamati ama familia usipende kuandika vitu ambavyo havina msingi,kamati ipo chini ya watu waadilifu ambao walifanya kazi moyo mkunjufu hakukuwa na ubabaishaji,andika vitu vyenye kujenga na sio kubomoa.
ReplyDeleteKama una dukuduku la kujua mchanganuo mzima wa pesa zilivyotumika weka jina lako wazi na namna ya kukupata,vingenevyo ndio mwanzo wa majungu,kwa mara ya kwanza tumefahamishwa makusanyo, ni msiba gani hapa DC tuliowahi kufahamishwa makusanyo?ipe hongera kamati,shughuli yote ilifana vizuri,kama ulifika kanisani utapata jibu,hii yote inakuonyesha wabongo DC tumefungua ukurasa mpya msianze kutia madoa,RIP Kaduma
ReplyDeleteMkakile na kamati yako mmefanya kweli,Bwana Malinda nae aliongoza vyema kanisani,wabongo msianze tena ,tunataka mshikamano huu uendeleee.Bwana mpumzishe Kaduma mahala pema .Amen
ReplyDeletemshikaji hapo juu Kaduma hakuwa rafiki yako,mwili haujaondoka umeanza kuongelea mambo ya pesa?
ReplyDeleteRIP kaduma
kwa niaba ya mke wa marehemu na mtoto napenda kuwashukuru kamati, watu wote waliojitolea kwa chochote kile na watu wote walifika kuuaga mwili wa marehemu. I'm sure if Kaduma can say anything it will be the way people came out and dedicated thier time, money and everything else just to make sure he getts where he is supposed to be and for his family.
ReplyDeleteMungu awabariki wote.