mwalimu akiwa kazini katika shule ya msingi ya amani iliyoko kigogo, wilaya ya ilala, dar. shule hii ina wanafunzi 2989, madarasa 17 na madawati 287 desks.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. hivi hawa viongozi wetu hawaoni aibu kuiba ikiwa hali ya elimu mpka sasa wtt wanakaa chini tena jijini dar? kweli tutafika?

    ReplyDelete
  2. Ooh Bongo Tambarare na bado huko hujafika huko Kasulu, Mpanda, Tarime, Kwedikwazu nk

    ReplyDelete
  3. Pesa walizokula Mafisadi zingepunguza tatizo hili kwa asilimia 80 nchi nzima kama sio kulimaliza kabisa, ama kweli mafisadi wanamgusa kila mwananchi !!!

    ReplyDelete
  4. can't believe this.Yaani ndani ya dar es salaam kuna shule ya namna hii? sasa huko mikoani itakuaje.

    ReplyDelete
  5. OOOOOOOOOOOOOOH MY GOD!!!BONGO TAMBARARE??????HONGERENI MAFISADI......

    ReplyDelete
  6. Nilidhani Bongo hakuna mwanafunzi anayekaa chini siku hizi! Kweli Bongo Tambarare!

    ReplyDelete
  7. Sio tu kwamba inasikitisha, bali INATISHA. Maswali mengi bila majibu. Maisha bora kwa kila Mtazania yatatoka katika hali hii? Kama hatujaweza kuwapatia watoto wa elimu ya msingi mazingira mazuri, je hizo sekondari za kata za Lowassa na JK zitafundisha watu wa ina gani? Hii picha iwekwe kwenye fremu na atumiwe Rais Kikwete kama zawadi kwa juhudi zake za kuwatetea na kuimarisha ufisadi katika kipindi chake cha miaka miwili ikulu.

    ReplyDelete
  8. Kwa idadi ya wanafunzi na madarasa ina maana kila darasa lina wastani wa wanafunzi 175 halafu CCm wanajidai kusema wanajenga shule.

    Badala ya kuzungumzia techer to student ration wao wanazungumzia majengo na wa-Tanzania munakubali.

    Sijui niwasaidie vipi wa-Tanzania kama wenyewe munakubali haya!!!

    TM

    ReplyDelete
  9. Hii ni makusudi. Kwa kifupi hawa wanafunzi wanakuwa hawana moyo wa kusoma ukifuatilia zaidi uwezo wa kutafakari mambo kwa kina unakosekana, matokeo yake wakija mafisadi na sera mbovu halafu wakawadanganya kwa pilau, kofia na fulana jamaa wanatoa kura.
    Wanatengeneza taifa la mambumbumbu kwa makusudi ili wao wabaki kwenye tabaka la juu pekeyao.
    Michuzi wewe ubane usibane haya maoni utakuwa umeshayapata sababu najua unanibania sana maoni yangu kwa kuwa yanaukweli.

    ReplyDelete
  10. Duuuuuh bora niendelee kubeba mabox watoto wangu wasome shule zinazoeleweka.Bongo tambarare na hapo ni DSM bado hujaingia KIGOMA mwisho wa reli.

    ReplyDelete
  11. Sasa Mwantumu Mahiza hapa atasemaje? Je ni kweli kukariri ndo chanzo cha elimu kuporomoka? Tunaelekea wapi sasa? Je mwalimu anao muda wa kuhakikisha kila mwanafunzi anaelewa kile kinachofundishwa? Je mwalimu anao muda wa kusahihisha madaftari yote ya wanafunzi kwa umakini?

    ReplyDelete
  12. It must be very hard for the teacher to reach and interact with every child in the class. This is a very sad situation kwa kweli, viongozi wetu hawajali kabisa, hawa watoto ndio taifa la kesho. Bless the little kids hearts...my heart is really touched by this kind of brutality...Hawa viongozi ina maana hawaoni haya yote wao kazi yao kula na kufisadi, ama kweli yaarabii nafsi hao viongozi. Wakiwapeleka watoto wao shule nzuri and they give their children excessive comfort that is what matters to them.

    Kwanza ualimu ni kazi moja ngumu sana, so to actaully teach in extreme environmental conditions like this is a big challenge for a teacher. Hawa watoto kwanza utakuta wanatoka kwenye kila aina ya backgrounds - they might have to go to school hungry, hawana madaftari wala kalamu..hii kaka michuzi imenisikitisha sana. HILI NDIO TAIFA LETU LA KESHO...NA HAWA NDIO VIONGOZI WETU WA KESHO...THE GOVERNMENT IS NOT EVEN EQUIPING THE TEACHER OR STUDENTS...IT IS VERY SAD. WALIMU HAWAHESHIMIWI KWA KAZI NGUMU WANAYOIFANYA AND PAID A MINIMUM WAGE.

    MIMI NAFANYA AN EDUCATION MSTERS DEGREE PROGRAM IN USA AND I CAN SEE A BIG DIFFERENCE YA SHULE ZA HUKU NA HUKO - 1. TEACHER AND STUDENT RATIO 2. WHAT THE GOVERNMENT SETS ASIDE FOR THE SCHOOL SYSTEMS - THEY LOOK AT THE PROJECTED INCREASED POPULATION IN THE AREA / COUNTY AND THEY CREATE MORE SCHOOLS AND CREATE MORE JOBS AND INCENTIVES FOR TEACHERS. 3. AN AVERAGE QUALIFICATION OF A TEACHER HERE IS A MASTERS DEGREE. I CAN GO ON AND ON MENTIONING THE DISADVANTAGES OF THE SCHOOLS IN OUR COUNTRY. I THINK GOD JUST HELPED US THROUGH THAT HARDSHIP THAT WE ALSO HAD TO GO THROUGH. I HOPE THAT THINGS WILL CHANGE IN TANZANIA IN THE LONG RUN. I FEEL FOR THE POOR WANANCHI WHO HAVE TO TOLERATE MAFISADI.

    I SALUTE THE TEACHERS FOR THEIR PATIENCE AND TOLERANCE. CONTRATS TO ALL THE TEACHERS IN TANZANIA AND GO ON DOING A GREAT JOB EDUCATION THESE CHILDREN ONE DAY THINGS WILL TURN AROUND FOR THE BETTER.

    MDAU FROM ATLANTA, USA

    ReplyDelete
  13. Ikiwa kila darasa lina wanafunzi atleast 175,je, huyu mwalimu ana msaidizi au ndio kipindo cha peke yake cha kuhakikisha kila mtoto ana pata elimu bora,kwasababu kila mtoto ana uwezo wake wa kufahamu.
    Ni aibu ikiwa mji mkuu bado una shule watoto wana soma katika hali hii.

    ReplyDelete
  14. Dah haya mambo bado yanaendelea?Nakumbuka mara ya mwisho kukaa chini ilikuwa mwishoni mwa 1989 at Mikocheni Primary Sch.Na usishangae kukuta hii shule inawachangisha wazazi michango ya madawati kila mwaka na hakuna kinachobadilika.
    Shule nyingi za bongo huwa zinatengeneza Pesa kupitia "michango ya madawati na michango ya ujenzi" lakini mabadiliko hakuna.

    ReplyDelete
  15. Hayo ndio matokeo ya UFISADI! Kwa kweli inasikitisha kuona watoto wetu wanaendelea kusota sakafu na huku MAFISADI wakiendeleza libeneke la kukwapua fedha na maliasili zetu kwa nguvu ya ajabu! Kwa kweli kwa hali hiyo BONGO si Tambarare. Hatuwezi kusema BONGO tambarare wakati Watanzania wengi wanateseka katika lindi kubwa la umasikini huku WALAFI wachache wakiendelea kupora fedha na utajiri wa nchi hii. Mwenyezi Mungu awalaani MAFISADI WOTE.

    Mzalendo halisi.

    ReplyDelete
  16. INATIA HASIRA BWANA KARNE HII YA 21 TULITAKIWA TUWE TUNAONGELEA STUDENT/TEACHER RATIO,LAKINI INASIKITISHA SANA KUONA TAIFA LA KESHO WATOTO WETU WADOGO WAKIWA WAMEKAA CHINI,JE HAWA WATAJIFUNZA VIPI KUANDIKA VIZURI,JE WATOTO WAHA WATASIKILIZA KWA MAKINI KWELI WAKATI WANAPATA ADHABU YA KUKAA KWENYE FLOW NA KUKUNJA MIGONGO YAO.ALL IN ALL HII KITU KINATAKIWA KUFANYIWA UFUMBUZI WA HARAKA LAKINI KWA TANZANIA NAJUA HUKUNA LOLOTE LITAKOLOFANYIKA KWA SABABU VIONGOZI WETU LEO HII WANAJIANGALIA WAO NA SIO MATATIZO YANAYOWAKABILI WATANZANI.
    WADANGANYIKA AMKENI M-WACHALENGE VIONGOZI WENU

    ReplyDelete
  17. SEMENI NYIE MIMI NIKIONGEA MICHUZI ANAFIKIRI MIMI NI CUF/WATU WAMEIBA DOLLAR MILLION 133 ALAFU LEO UNAAMBIWA KWAMBA HAO WATOTO WANAKAA CHINI SHULENI COMON WATANZANIA WENZANGU SISI NI VIPOFU WA HAINA GANI ? SISI NI VIZIWI WA HAINA GANI? SISI NI MA BUBU WA HAINA GANI? TUKIWASEMA WALE WANAOFUNGUA MASHINA UINGEREZA KWAMBA JE KWA MISINGI GANI UNAWAUNGA MKONO CCM? TUNAAMBIWA SISI WANAFIKI.JE KWANINI HAWA HOJI VIONGOZI WAO WA CHAMA MAMBO KAMA HAYA KAMA KWELI WANA JALI TAIFA LETU? LAANA YA DHULMA NI KUBWA SANA KAMA HAWAJUI.WANAKULA KIAPO KWA MISAAFU NA BIBLIA KWAMBA WATALITUMIKIA TAIFA LETU KWA HUAMINIFU.RICHMOND,EPA,BOT HUAMINIFU HUKO WAPI HAPA.NI FAIDA GANI WANAPATA KAMA WANAFUNZI WANAKAA CHINI MWAKA 2008.WAGONJWA AMANA WALIPANDISHWA JUU YA VITANDA KISA BUSH ANAKUJA,SASA JE TUSIBIRI MPAKA BUSH KUJA TENA HAWA WATOTO~ NDIO WAPEWE MADAWATI?
    CHOZI LA MNYONGE MALIPO KWA MUNGU.
    MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.
    Mdau mzawa na naomba kaka michuzi uliweke dukuduku langu hili manake kidogo presha inaweza kushuka.

    ReplyDelete
  18. JAMANI KILIO KILIO KIKUBWA SAAAANA KATIKA NCHI YA TANZANIA!!!! HIVI HAO VIONGOZI TULIOWACHAGUA WANA FANYA NINI WAKATI WATOTO WADOGO KAMA HAO HAWANA PAKUJIEGEMEZA?????? SASA WAKIFIKIA UMRI MKUBWA SIWATAPATA MATATIZO YA MGONGO JAMANI??? YAAANI HAYA MAMBO NI YA KULIA KWA HUZUNI KUBWA..TANZANIA IMEKUWA SHAGALABAGALA KIASI HICHO JAMANI??? NIMESIKIA UCHUNGU SANA, KUONA KUWA VIONGOZI WA TANZANIA WA NGAZI ZA JUU NA ZA CHINI HAWAJALI WATOTO NA HAWAJALI ELIMU ZAO KABISA. NENO MOJA TU NINALO "AIBU".. UUUUiiiiiiiii...iiii..TANZANIA MAJONZI MAKUBWA SAAAANA.

    ReplyDelete
  19. WHAT A SHAME???????????!!!!!!!!!!!!,halafu utasikia watu wanakwambia bongo imebadilika bwana siyo ile mlioiacha zamani,nyie wabongo na viongozi wenu mnacheza sana,WAKE UP PIPO!!

    ReplyDelete
  20. Afisaelimu wa Ilala na timu yako unafanya nini hapo ofisini? upo tu na vikao vya kila siku bila utendaji? Uafisaelimu ni kufanya wanafunzi wajifunze, na sio wakariri. Sasa hapo wanasoma kweli au wanahudhuria shule? halafu mnakataza twishen! unategemea huyo mtoto wa watu hapa ataelewa nin na msongamano huo. Kwani fedha za MMEM ulipeleka wapi mzee watu. Naona likitoka kule litaingia kwa maafisa elimu wazembe kama wewe. au nanyi ni mafisadi wataaluma wetu? Fedha za MMEM kazi yake ilikuwa kupunguza matatizo kama hayo. Au unataka kutudanganya kuwa ndizo ulijengea hayo madarasa 17?? Halafu ripoti zenu mbona mnaandika uongo? Si mlisema kuwa hakuna mwanafunzi anayekaa chini Dar nyie?? Mbona alipokuja kutembelea mama Sitta wakati wa uwaziri wake hamkumpeleka huko. Namshukuru sana huyu mdau aliyeleta habari hii. Lakini alisahau kutuambia idadi ya walim. Dogo naomba umalizie na idadi ya walimu kabisa ili tujue teacher students ratio ni ngapi. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
    sijui kama kwa mtindo huu watoto wetu walala hoi kama watapata elimu bora. wanapata bora elimu maskini. ndio EFA inasema hivyo? what I know is that according to Universal Educaion For All,we need Quality basic Education for all. and not quantity!!

    ReplyDelete
  21. Kamanda Manyota:
    "Jamani mbona kira mutu ni mkaaari? turizeni vipago bana mambo hayendi hivyo, hiyo shure ndipo walipotoka wakina chidi beeenz na faraji wa ilala ambae ameondoka na degree A+++, pamoja na kuwa wanakaa chini na wingi wao ila panatoka vichwa hapo kwa magunia. musijari bana mbona kusota ni kawaida tuu. pigeni shure watoto na nyinyi warimu toto rikiwa harifahamu chapa makonzi tuu wataerewa.

    Ni hayo tu:-)

    ReplyDelete
  22. That is pathetic! Yaani siamini hali hii ipo! tena Dar!!!!!! Jamani matabaka yaliyopo sasa hivi Tanzania yataendelea for generations kwani hao watoto will never break the circle of poverty they are in, kwani wanashindana na watoto wa watu wengi wenye uwezo walio kwenye shule nzuri sana za private......God Bless Tanzania and please God open the eyes of our leaders to see this.....naamini wengi wao wala hawajui au kujali yanayoendelea.

    JJK - Toronto

    ReplyDelete
  23. Acheni kulaumu tu. Acheni kufanya kazi za kudhalilishwa huko nje na badalala yake nendeni bongo mkajenge nchi yenu

    ReplyDelete
  24. NANI ARUDI KAMA HALI NDIYO HYO. KWA NINI PICHA KAMA HIZI HAZIPATIKANI KWENYE BLOG YA JM KIKWETE NA SHEIN?
    KWA NINI. KWA NINI KWA NINI KWA NINI KWA NINI?
    KWA NINI TUNATEGEMEA KILA KITU KIFANYWE NA SERIKALI? KWA NINI TUSIWE NA MSIMAMO KAMA ULE KWA KENYA WA KUANZISHA HARAMBEE KWA KUSAIDIA SHULE BADALA YA MAMBO YA HARUSI NA KITCHEN PARTY. KWA NINI, KWA NINI?
    HIVI KUNA PARTY NGAPI ZA AJABU AJABU ZINAZOPITA BONGO AMBAZO HAKUNA HATA MOJA INAYOLENGA KUSAIDIA TAASISI YA ELIMU? KWA NINI, KWA NINI?
    HIVI HAO WENYE PESA ZA KUWAITA WANAMUZIKI HAWAKUSOMA KWENYE SHULE HIZO HAPO ZAMANI ZILIPOKUWA NA MADAWATI, VITABU, MADARASA NA WALIMU WA KUTOSHA HUKU MCHANGO WA UPE UKIWA SH 20? NA MCHANGO WAO NI NINI. KWA NINI WASISADIE KUINUA SHULE HIZI ZA MSINGI?
    KWA NINI KILA MKUU WA WILAYA ASIWE NA UWEZO WA KUONGEZA KODI YA MAFUTA SHILINGI 100 AU 200 KWA KILA LITA MOJA KWA ILI KUSAIDIA MAENDELEO YA SHULE ZA WILAYA YAKE. KWA NINI KWA NINI?
    IANSHANGAZA SANA KUONA MBAO HUKO ZIPO. KUNA SHULE ZA UFUNDI KIBAO. KUNA MAGEREZA YALIYOJAA WAFUNGWA WENYE UJUZI WA USEREMALA.
    KWA NINI JITIHADA ZISIFANYIKE KUHAKIKISHA WANATUMIA SEKTA HIZO KUISAIDIA SERIKALI KWANI WAFUNGWA WENGI WANAISHIA KURUDI HATIANI KWANI WATOKAPO JELA WANAKUWA HAWANA UJUZI WOWOTE ZAIDI YA KUTENDA TENA MAOVU.
    KWA NINI SERIKALI ISIWATUMIE KUTENGENEZA MADAWATI NA KUPAKA RANGI SHULE? KWA NINI. KWANI WENGI WANAKULA BURE NA KULALA BURE!
    SIYO LAZIMA KILA MTU AFUNGWE JELA HATA KAMA KWA KOSA LA KUMPIGA MWENZIE. KWA NINI WASIPEWE ADHABU ZA KUFUNDISHWA ADABU KAMA VILE KUFAGIA BARABARA, KUPAKA RANGI KUTA ZA MADARASA.
    WANAPOFUNGWA WANAISHIA KUTIA GHARAMA SERIKALI NA WALIPA KODI KUWALISHA NA KULALA BURE. KWA NINI. KWA NINI?
    KUNA MAGARI MANGAPI YANAYOLIPA KODI BARABARANI KWA AJILI YA SERIKALI YA WILAYA FULANI NA KODI ZINASAIDIA NINI NA WAPI. KWA NINI ZISITUMIKE KWENYE SEKTA NA NYANJA KAMA HIZO. KWA NINI, KWA NINI?
    LINGINE LA MUHIMU KWETU SOTE PAMOJA NA MICHUZI;
    KWA NINI TUNATOA RUSHWA BADALA YA KULIPA KODI HALISI KWA KILA UNACHOTAKIWA KULIPIA KODI.
    KWA NINI TUSILIPE KODI KAMILI BILA RUSHWA ILI JAMBO LITAKAPOONEKANA BAYA KAMA HILI, MTU UNAKUWA NA SAUTI YA KUZUNGUMZIA NA HATA KUIPELEKA SERIKALI YA MITAA MAHAKAMANI KWA KUSHINDWA KUTIMIZA MOJA YA MAJUKUMU MUHIMU KAMA HAYA.
    VINGINEVYO NENO "KWA NINI" LITAKOSA JIBU HATA KAMA LITAENDA BUNGENI. MTADAI MAMBO YA BUZWAGI, BOT LAKINI CHANZO KIPO WAPI?
    CHANZO KIPO NYANJA YA CHINI KWA SABABU WENGI WETU HATUPATI ELIMU BORA ITAKAYOFUNGUA MACHO NA KUJUA CHANZO CHA KUDHULUMIWA HAKI ZETU BILA KUJUA...KWA NINI?


    KAMA KWELI MICHUZI UNAJALI NA KUTHAMINI MICHANGO MUHIMU, NADHANI HOJA HII INGEENDELEZWA HADI SUALA HILI LITAKAPOPATIWA UFUMBUZI.
    NIMEONA KUNA MAMBO YASIYO NA UMUHIMU KAMA MPIRA, YAKICHUKUA SURA KUBWA HUMU NDANI KULIKO MASUALA MUHIMU KAMA HAYA. HAYA NDIYO YANAYOSTAHILI LIBENEKE NA SIYO MPIRA TENA WA ULAYA!

    ReplyDelete
  25. Jamani msishangae,hayo ndio maisha bora kwa kila Mtanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...