mazishi ya katibu mkuu wa shirikisho la ndondi marehemu gaston mlay jioni hii makaburi ya kinondoni
bondia nassoro michael akiweka shada la maua kwa niaba ya mabondia wa timu ya taifa. shoto mwenye suti nyeusi ni naibu waziri wa habari, utamaduni na michezo, mh. joel bendera
juu toka shoto ni iraqi hudu, joseph michael, willy isangura, mdau, rashidi matumla, isaac mabushi na timothy kingu. chini ni mmiliki wa hoteli ya friends corner, mzee masawe (pili shoto) akiwa na mabondia nyota wa zamani akiwemo koba kimanga 'assossa' (magongo) na wengineo
leo tumemlaza kwenye nyumba yake ya milele bingwa wa ngumi uzito wa juu na katibu mkuu wa shirikisho la ndondi (tbf) gaston mlay kwenye makaburi ya kinondoni katika mazishi yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa mabondia mbalimbali, wadau wa ndondi, ndugu, jamaa na marafiki wakiongozwa na naibu waziri wa habari, utamaduni na michezo, mh. joel bendera.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. RIP - GASTON MLAY,
    Hey Michizi,nimeona kuna msiba mwingine wa Capt.Lema wa JKT RUVU??Anyway Mola awalaze mahali pema peponi,AMIN.

    ReplyDelete
  2. Bwana alitoa na Bwana ametwaa; Jina la Bwana libarikiwe. Amen.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...