
KUNDI la mwanamuziki Bozi Boziana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo linatarajia kusindikiza uzinduzi wa albamu ya Impact ya bendi ya Akudo Impact.
Msemaji wa Akudo amesema leo kuwa kundi la Bozi Boziana linatarajia kuwasili Mei 13 likiwa na wasanii takribani 17.
Uzinduzi wa albamu hiyo umepangwa kufanyika Mei 16 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee ambao utafanyika kwa ushirikiano wa Kampuni za Qssp Group Ltd na NY Production.
Mratibu wa tamasha hilo Bahati Singh alisema : " Akudo wao wako kwa ajili ya vijana, lakini tukaona ni heri tuwape burudani ya watu wa aina mbalimbali na ndio maana tukaamua kuwaleta Bozi Boziana kwa ajili ya watu wazima na Jahazi Modern Taarabu kwa wapenzi wa muziki wa mwambao," alisema.
Habari zaidi na picha nenda: lukwangule.blogspot.com
Duu!!! mmmm!!!wazairwa wanatumaindisha.Abiria chunga mzigo wako,wazaire on a mission to take our women.Jamani mawindo haya,mimi akifika tu jamaa mke wangu nafungia kwenye clozeti nishachoka mara wazambia,wasouth,Koffi,khah!!! Bozi naye
ReplyDeleteOkey!Mzee Aboubakar Bozi Boziana,
ReplyDeleteni vema kuwa umeguata mila na desturi za blog ya jamii kuwa Fulanaziiiiii!uliyovaa ni ya aina ya MKUU WA TAGETA mheshimiwa Kaka
Michuzi hapa hakuna cha Usupa staa
bali ni kufuata mila na desturi za baraza la jamii
Hana lolote huyo kuwashinda wazee wa kutwanga na kupepeta.
ReplyDeleteVena , arusha