mdau katutumia hii kutuonesha kwamba kuikuwa na treni huko zenj miaka hiyo kwa mujibu wa stuido maarufu lyapicha ya mc. gomez ambazo zinapatikana http://www.zanzibarhistory.org/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hayati Karume alikuwa mpenda maendeleo , alitaka kuifanya Zanzibar iwe kama London... Unajua mzee alikuwa .. baharia hivyo .. alikuwa anaona mbali..unajua Zanzibar ndio nchi kwanza Afrika kuwa na TV ya station ya rangi .. wakati sisi BARA. .. tulikuwa hatujui .. hata TV ni nini..

    ReplyDelete
  2. Tena alikuwa si mbaguzi kama wanavyobaguana sasa, alihimiza wachanganyike kwa kuowana na kila mtu, kwa msisitizo yeye alimuoa bi fatma na kuwaelewesha wananchi wake kuwa tuondoe ukabila na matabaka, Mungu amhrahamu alikuwa na mabaya yake na mazuri mwengi aliwaachia ndugu zake wa unguja na pemba

    ReplyDelete
  3. Jamani habari ya hii treni ya Zanzibar inahusiana vipi na Marehemu Karume?Hii treni ilikuwepo mwanzoni mwa miaka ya 1900 hata huyo Mzee Karume alikuwa hajazaliwa.Mnaandika vitu kana kwamba yeye ndie aliyeleta treni Zanzibar,jamani acheni umbumbumbu,muwe mnauliza kwanza.
    Michuzi wafahamishe watu vizuri wengi wanaona hiyo treni ililetwa na Marehamu Karume.
    Watu wengine bwana!

    ReplyDelete
  4. Msisahau kwamba wakati ule wa enzi za biashara ya utumwa,Zanzibar ilipewa hadhi ya makao makuu ya Afrika ya Mashariki na Kati.Kwa hiyo matajiri wote makao yao makuu yalikuwa Zanzibar.Maisha yote ya kifahari na anasa yalipatikana pale.Hata mahusiano ya nje baina ya bandari ya Zanzibar na bandari za Marekani ni ya zamani zaidi kuliko bandari zingine zote katika mwambao wa Afrika ya Mashariki.Mtambo wa kwanza kabisa wa kuchapishia magazeti uliletwa Zanzibar na Seyyid Bargash na gazeti la kwanza hapa nchini lilichapishwa Zanzibar.Harakati za kuukataa ukoloni zilianzia Zanzibar katika mapambano baina ya watumwa na waarabu walio endesha biashara ya utumwa.Kwa hiyo Zanzibar ina historia ndefu sana.Mali kila aina ilikuwa ikichukuliwa toka bara na kupelekwa Zanzibar tayari kwa kusafirishwa na majahazi kupelekwa ng'ambo zaidi.Dar es salaam imekuja anza juzi tu baada ya purukushani baina ya wajerumani na waarabu katika kugawana maeneo ya kuyamiliki wakati huo.Jambo moja tu namsifu Mzee Karume ni kwamba alikuwa na EXPOSURE kubwa sana iliyo mfanya awe mjanja na muelewa wa mambo mengi sana ya Dunia kuliko viongozi wengi sana ambao walimzidi elimu ya darasani.Lakini yeye aliwazidi elimu dunia.Aakadiriki kufanya mambo makubwa sana kuliko hata wenzake waliokuwa na madigrii kibao.Ubaharia ulichangia sana katika kumfanya Mzee Karume awe na ueledi mkubwa kiasi kile cha kuweza kufanya mambo makubwa.Lakini mafanikio yake Mzee Karume yasihusishwe na upuuzi unaofanyika hivi sasa.Viongozi waliopo sasa hawamkaribii hata kwa chembe.Si mtoto wake na si hao wengine.Lakini katika ulimwengu wa sasa ni ujinga ulioje kuyakataa mageuzi yanayo letwa na nyakati.Yasihusishwe kamwe na mambo ya kale yaliopita.Vinginevyo hapatakuwepo na maendeleo yoyote asilani.Zanzibar hivi sasa ni Demokrasia tena ya vyama vingi.Huu wimbo wa Mapinduzi utakwisha lini?Mapinduzi sawa yalishafanyika yakaondoa utawala wa dhulma na ukandamizaji.Lakini watu hivi sasa wanataka maendeleo.Na isitoshe zaidi ya robo tatu ya wakazi wa Zanzibar hivi sasa ni vijana waliozaliwa baada ya mapinduzi ya 1964.Hawayajui manyanyaso ya utawala wa Kisultani.Vipi leo uliondolewa usultani wa waarabu urejeshwe usultani wa waswahili kwa kisingizio cha kulinda mapinduzi?Kuna mapinduzi yasiyo na mwisho?Wazanzibari hivi sasa watatakiwa washikamane kwelikweli ili kuviendeleza visiwa vya Zanzibar.Kubaguana kwa misingi ya huyu hakuwemo katika mapinduzi na huyu alikuwemo nafikiri siyo jambo la busara hata kidogo.Hakuna aliyependa kujikuta akizaliwa hivyo alivyozaliwa.Lakini tayari umeshazaliwa hivi sasa.Huwezi tena kumrejea Mungu na kumlalamikia kwamba hivi sivo nilivotaka mie nizaliwe,nilitaka nizaliwe vile!Hapana hiyo itakuwa ni kumkufuru Mungu.Wazanzibari wote mnapaswa kuwa familia moja msibaguane.Kila mzanzibari anayo haki ya kikatiba ya Kuongoza na Kuongozwa.Madhali anazo sifa za kuwa kiongozi bora na raia mwema.Wapo viongozi bara ambao wamekuwa wakinufaika na mgawanyiko uliopo baina ya wazanzibari wenye asili ya Pemba na wale wa Unguja.Kwa bahati nzuri Bara pia wapo ndugu wa damdam ambao wangependa kuona Wazanzibari wanakuwa kitu kimoja na mwenye sifa na kukubalika zaidi na awe Kiongozi.Lakini utawala wa kibabe hapana.Kura ya wazanzibari iachiwe iwe mwamuzi.

    ReplyDelete
  5. Hapana!sio kwamba habari hizi azimuhusu Marehemu Rais Karume!zinamuhusu kwani!kwani aliyeleta Picha hiyo alikuwa na maana ya kuwa Treni hiyo!hiliondolewa kimakosa!na utawala wa SMZ si bora kuliko wa utawala wa Sultani,ambaye mmiliki wa wa mtandao aliyeleta hii picha ni mjuu
    wa Sultani!
    wakati wa Enzi ya Sultani watu wengi wa visiwani walinyanyaswa

    ReplyDelete
  6. Trein hakuileta Karume ila ni trein ya kwanza afrika mashariki nzima. na ni kweli Zanzibar walikua na kituo cha TV ya rangi wakati nchi kibao za afrika hawana ya black and white

    ReplyDelete
  7. zanzibar ni nchi ya mwanzo katika afrika mashariki kuwa na mtambo wa tv ya rangi na vile vile serikali iliweza kuwakopesha wananchi wake tv kwa mkopo nafuu.

    ReplyDelete
  8. Michuzi hawa ma-anon wanaohusisha hii picha na Karume wameenda shule kweli? Jamani hii picha inahusu HISTORIA YA ZANZIBAR muelewe msiosoma nakuelewa.

    Namshukuru Mdau kwa kuleta hii picha nikiwa shule nilisoma kitabu kinahusu hii shule ya MTAKUJA. Nimesoma hii historia kwa makini nanimepanga kwenda kutembelea
    Zanzibar. Namuunga mkono mdau aliyesema kwamba Karume pia alikuwa anaona mbali. Inawezekana Historia ya Zanzibar ikitangazwa vizuri ikaleta pato kubwa kwani HATA LONDON haina historia kama hiyo wao wana QUEEN VICTORIA na CHURCHILL wao tu.
    Mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...