
Kwanza kabisa napenda kutoa pole zangu kwa msiba ulio tukuta waTanzania, wa dada yetu mpendwa Bi.Mwajuma, huko London, nawapa pole zangu wana ndugu wote.
HOJA YANGU YA LEO NI:
Kuna kipindi cha nyuma ulituma picha za kuonyesha barabara zetu, hasa usalama wake unapo safiri, kutokutingatia mistari, alama za barabarani n.k.
Kuna kipindi cha nyuma ulituma picha za kuonyesha barabara zetu, hasa usalama wake unapo safiri, kutokutingatia mistari, alama za barabarani n.k.
Nilizifuatilia kwa makini sana na niliona usalama wa wasafiri ni kidogo sana, kutokana na kuovateki sehemu ambazo haziruhusu, yaani kwenye kona mbaya ambayo huoni kabisa bele utakutana nanini. Kwekweli ni hatari sana hasa kwa mabasi yanapo kuwa na roho za watu nyingi tu wala sio magunia ya mahindi au mchele n.k.
Nasema hivi kwasababu imeniuma sana kutokana na ajari mbaya iliyo tokea hivi karibuni barabara ya kwenda Dodoma, sijui ni sehemu gani, ilihusisha mabasi 2, moja wapo lilikuwa likiovateki kwenye kona kali kabisa ndipo jingine likatokeza, ikawa balaa. Kuna jamaa yangu alipoteza maisha yake kwenye hiyo ajali, imepita mda kama wa wiki moja nilikuwa nikimtafuta kwenye simu simpati, kumbe kawa marehemu, nimezipata habari jana tu. Ila ajali yenyewe imetokea kama wiki na nusu iliyo pita, na nimesikia walikufa watu wengi tu.
Kuhusu swala hili, hivi kwanini lisichukuliwe hatua kali sana, kwa mwaka watu wengi sana wanapoteza maisha yao na kuwa vilema wa kudumu kwasababu ya uzembe wa madereva? Madreva wanao fanya uzembe huo wachukuliwe hatua kali sana.
Kwa mfano huko: Kuna sheria kali sana kuhusu matukio kama hayo, ajali ikitokea ya uzembe kama huo ni kwamba, kwanza kabisa shirika la basi lililo sababisha ajali linafungiwa kwa mda mrefu, pili wahusika wanawajibika ipasavyo, kwahiyo kabla ya kumwajili dreva lazima wahakikishe kweli dreva yupo safi na udreva wake sio wa kubabaisha, la sivyo ataharibu jina la kampuni.
Pia kwa sasa wameanzisha sheria kali sana ya kupoteza point kwenye leseni, yaani kuna point 20, kila unapofanya kosa kuna point zinatolewa, kutokufunga mkanda tu p.5, ukiovateki kwenye kona p.15, spidi inategemea unaenda ngapi, Ulevi inawezekana usiendeshe tena gari katika maisha yako yote. ukifikisha point 20 lazima upokonywe leseni faini kubwa sana na uanze upya, yaani kwenda shule ya udreva, hawana utani wakikukamata, toka wameanzishe sheria hizi kali, ajari zimepungua sana sana.
Mimi mwenyewe nilikamatwa sehemu ya spidi 70 nilikuwa naenda 120, nilipoteza leseni na faini ya euro 480 = Sh.864,000. Nilienda shule upya, na ghalama ni kubwa za shule. Sasahivi ni mwoga hata kusafiri si mchezo, la sivyo mshahara wa mwaka mzima ni kulipa faini tu, na inawatokea watu.
Na sisi kwetu Tanzania inabidi mambo kama haya yaanze ili kupunguza vifo vya ajari barabarani za uzembe. Ajali zinatokea huwezi kuzuia, lakini zingine zinazuilika jamani.
Na pia shirika la basi lazima liwalipe wana ndugu walio poteza wapendwa wao na walio lemaa, huku wanafanya hivyo kweli hawana utani, utaona watakavyo kuwa makini, kutokuajili watu ovyo kuendesha mabasi. Mimi huwa ninasikitika sana wakati zikitokea ajali za mabasi na kuuwa watu wengi sana bila sababu ya msingi, eti alikuwa anaovateki sehemu ya kona au mlimani ambapo haoni mbele.
Bado tuna shida nyingi sana za magonjwa mbalimbali hayatatuliki, sasa na mambo haya ambayo yanawezekana kabisa kutatulika yaani yaendelee tu kutumaliza?
Salamu sana kwa wadau wote!
B.CHIBIRITI.
Salamu sana kwa wadau wote!
B.CHIBIRITI.
Chibiriti you are right, serikali ikiamua kufuata taratibu hizi itapunguza ajali ila itabidi ziwekwe camera za kutosha kumonitor nyendo za madereva na trafic, seriakali lazima ione umuimu huo na kuchukua hatua, faini+penalt points=kunyanganywa leseni ukikiuka uende jela.
ReplyDeleteNATOA HOJA, Chibiriti siku hizi ana point sana, arudi nyumbani agombee ubunge.Tatizo moja tu ana mke mzungu !!Na pia mbona kila siku unakataa wewe si Mmakonde sasa wewe ni kabila gani? Mmakua kama Mkapa? au Mmawia?
ReplyDeleteAnyway, unayosema ni kweli kabisa, nakuambuka Mrema alipokuwa waziri alisema Tanzania inasheria nyingi sana na nzuri lakini hazifanyi kazi, utendaji hakuna, kuna kujuana sana. Kama kamanda wa polisi ulisoma naye, au mke wake anaenda saluni moja na mke wako basi hata basi liue watu 40 hamna kitu !!
Chibiriti umeongea pointi sana, lakini kwa sababu umekaa nje umeshaona nature za watu mbalimbali ambazo ni tofauti kabisa na nature za watanzania walio wengi.
ReplyDeleteNature ya watanzania wengi ni kuwa hawathamini uwajibikaji. Mtu kama amesababisha ajali kwa uzembe ukija kutaka kumnyang'anya leseni si ajabu ukute hata leseni hana.
Angalia shughuli mbali mbali za kizembe Tanzania wala hakuna haja ya kuzitaja maana zilikuwa zimejaa kwembe vyombo vya habari, lakini still hakuna mtu anayewajibika wala kuwajibishwa.
Nature yetu bwana ni uzembe uzembe, kutokuambiana directly mtu anapochemsha lakini hodari wa kuponda vitu ambavyo havina hata haja ya kuvifuatilia.
Hatua ya kwanza ni kuwa watu wakajifunze kuendesha magari kwenye driving school na sheria halafu wapewe leseni kiuhalali, lakini sitastaajabu kusikia kamanda wa polisi anayetakiwa kushughulikia hili jambo ndio wa kwanza kumpa jamaa yake leseni mkononi tu mambo mengine mbere kwa mbere.
Jamani tuna safari ndefu mpaka tuanze kubadilika, lakini mawazo haya kama ya Chibiriti yatasaidia taratibu kuelewesha umma.
Chibiliti,
ReplyDeleteKama kutakua na uwezekano rudi nyumbani, na kupumzika kama miezi sita hivi, kwa sababu moja kuu, maelezo yako, vitendo, na obsession zako, inaonyesha tendency za ugonjwa wa akili.
ni hayo tu, kwa msaada wako mwenyewe, jifikirie.
anony wa 9:43 pm, wewe ndiyo una ugonnjwa wa akili. kwa sababu
ReplyDelete1: upo nje ya topik, hatuongelei magonjwa hapa.
2: pinga hoja,usiingilie mambo ya binafsi, chibiriti kasema tunaweza kupunguza ajali nyingi tukiwa na sheria nzuri, unakataa au unakubali? kama unakataa kwa nini,kama unakubali kwa nini.utakuwa kama spika kaabiwa anatumia hela zetu vibaya, yeye anasema watu wanamtafuta !!!jibu swali.
3: chibiriti hahitaji msaada, wewe ndiyo unahitaji msaada.
anon 9:43 wala hujakosea, sema tu umetumia maneno mengi mno, huyu jamaa atakuwa na KCU..Kichaa Cha Ughaibuni,,,na si alishagaonesha picha ana kabinti kakizungu, ndo mana ugonjwa nao umefikia hali mbaya hivi, mana anaproduce pumba tu sijui hata alichokiandika ni nini hapo.
ReplyDeleteMichu,
ReplyDeleteNina mambo fulani naomba msaada bloguni.
1.Kama kuna uwezekano wa kupata bronchaz za utalii za Tanzania ili nizigawe huku ninakobebaga box,labda naweza kuongeza idadi ya watalii kozi sama ndio hiyooo...Wizara husika yaweza kuzituma kwenye barozi zetu,then sie tuwe twaziomba huko na kuzisambaza.
2.Hiviinawezekana kuanzisha kategoriz humu bloguni ili kuweza kupunguza mambo fulani fulani?
Haswa hii kero ya "Natafuta mwenza" mi naona kama ingekuwa na mahali sei pameandikwa "watafutao wapenzi" au "unyumba" halafu post hizo za uchafuzi wa hewa zote zikaenda huko,tena weka na eji ristrikshen kuaksesi kipande hicho.Hili laweza saidia kupunguza uchafuzi wa mazingira kozi kama hupendi mambo hayo,huko utafuata nini??!!
3.Enibode gloguni ajua kuinstolu brauza ya sony DCR-DVD109?Yaani mie sasa yakaribia kunliza.Je nahitaji software zozote?Niko na DirectX tayari lakini kamkoda na tarakishi zakataa kuoana.Msaada tafadhali
Bro Chibiriti wewe nae umeanza ku-supervise misosi kama yule jamaa wa Spain au?
ReplyDeleteYou're more reactive than proactive... Nilifikiri kuwa Italy kungekusaidia kuwa na fikra endelevu... preventive and proactive thinking than curative and reactive ones kama hizo zako...
Nashangaa unaanza kubwabwaja kisa ndugu yako kafa... Michuzi alipotoa time zile huku-respond ila sasa hv ndo unajidai kuwa more concerned kisa nduguyo amekufa... Acha ubinafsi....
mdau unaeuliza
ReplyDeletekuhusu issue namba moja nenda tz embassy au tumia tovuti ya embassy kuwasiliana nao, brochures za utalii zipo za kumwaga ni wewe tu. mi nimejipendele kibao na sasa hivi naitangaza bongo kama sina akili nzuri. ahsante
hacha mambo yako chibiriti wewe una gari kwanza?
ReplyDeletehizo issue wanaongeaga watu ambao ndio wameingia ulaya..kapumzike bwana nachingwea inonekana maboksi bwana yanakuchosha sana...
Kweli elimu Tanzania ina tatizo, hivi wewe Chibiriti uliishoa darasa la ngapi? Yaani hata kujieleza kwa lugha fasaha huwezi?
ReplyDeleteHivi chibiliti ukiwasha computer yako unasubiri muda gani ili iweze kufungua files zote na kuanza kuitumia?
ReplyDeleteNafurahia sana kuona kuna watu wanatunza vitu vya zamani, sbb bila nyie mazingira yangeharibika, Computer unareuse, gari ya gas, na sasa unapiga vita ajali za barabarani
Hivi huyu ndiye yule yule Chibiriti ? Basi Chibiriti unaongea vitu vya maana. keep it up !
ReplyDeletewelldone chibiriti, na hayo ndyo baadhi ya matatizo ya usafiri wa nchi yetu.
ReplyDeletekwanza me naomba nesemee haya mabasi ukweli haya mabasi sio mabasi kweli ila ni malori ambayo yananunuliwa yakiwa used huko ulaya then yanakuja hapa na wanatengenezewa body ya basi huko nyerere road hapa tanzania hakuna tajiri wa kununua mabasi mapya wengi hutumia usanii huo na kwao wanapata faida kubwa kuliko angeagiza basi jipya
sasa haya mabasi malori hata me hupanda sana kama nasafiri mbeya, dodoma arusha n.k. vipuli vyake vimetengeneza madhubutu kwa gari ya mizigo kwahiyo sio flexble kwa kukwepa ajari kama uko speed hata kumudu kama kuna itilafu imetokea
mwaka jana ajari za mabasi zilikuwa nyingi sana kupita kawaida kwahiyo serikali ikaingia kwa nguvu zote kukagua mabasi kabla ya kuondoka na eti wakajifanya wamegundua mabasi yote kumbe ni maroly sio special bus wakazuia basi hizo kwahiyo ikawa shida ya usafiri karibu mikoa yote ukweli ilikuwa vigumu kwani basi zote ni lory ndipo ikalegeza kamba na kutoa waraka kuwa mwisho wa mabasiroly ni june,2008 lakini mpaka sasa sijaona jitihada zozote za matajiri kuanza kuingiza mabasi halisi kwahiyo matajiri wa mabasi wa bongo wengi ni njaa tu
USHAHURI
Serikali ya tanzania ikitaka iongoke katika ajari hizi za mabasi kwanza yenyewe ijikite zaidi katika kusimamia mabasi kwani sumtra wameshinwa zaidi wanasimamia nauli
serikali ifute kodi au kusamehe kodi kwa mabasi mapya yatakayoingia tanzania hii matajiri ndiyo watamudu biashara hii ya mabasi bila hivyo matajiri wataendelea kuagiza malory ambayo wamesamehewa kodi na kujengea body nyerere road pale ali yusuph bus body
NAOMBA KUTOA HOJA
Asante sana Chibiliti kwa hoja yako nzuri. Inasikitisha sana kuona watu wanakufa kwa ajali zinazotokea kijinga ambazo serikali ingeweza kuzizuia.
ReplyDeletehapo umenena chibiriti lakini tatizo kwa hapa bongo na ndugu zetu hawa wenye fomu nyeupe wana njaa sana, yaani nakwambia rushwa itazidi mara 2 yake. kwanza tutilie mkazo swala la rushwa ndio hizo sheria zifuate.
ReplyDeletelengine chibiriti hongera sana kumbe una miliki kausafiri mitaa ya watu? kweli unatisha
CHIRIBITI, UKITAKA KUENDELEA KUWA SUPER STAR, INABIDI USUBIRI ANGALAY MIEZI MIWILI KABLA HUJAPOST ISSUE MPYA, WATU WAMESHAANZA KUKUZOEA, SI UNAONA HATA HUJAPATA COMMENTS NYINGI, KWA HIYO CHA KUFANYA NI KWAMBA, USIPOST ISSUE KILA MARA - huu ni ushauri wangu.
ReplyDeleteHayo aliyoongea Chibiriti ni kweli kabisa, kama kuna sheria na sheria hazifuatiliwi kwa adhabu kali, madereva hawawezi kuogopa.
ReplyDeleteSiku moja nikiwa Ujerumani, nilijaribu kuvuka barabara kabla taa hazijaniruhusu kwani kulikuwa kweupe,hakuna gari mbele wala nyuma, jamaa yangu aliniwahi akanishika mkono kabla sijasogea hatua moja mbele.
Jamaa yangu alinieleza kuwa sheria za hapo ni kali ukifanya kosa unaweza ukauza gari ili kulipia faini yake.Si mchezo manake!
Hapa kwetu nchini, sheria zipo kama kiini macho, sheria nyingi ni za kuwabana walalahoi! Magari mengi hasa ya daladala yanamilikiwa na matrafiki au mabosi fulani. Na wenyewe wanajuana kuwa gari lile ni la afande fulani, au ni la bosi fulani.
Chukulia mfano mabasi ya Gongolamboto au Mbagala, yanajaza watu kama magunia. Ikifika jioni au asubuhi ambapo abiria ni wengi wanaowahi kazini au majumbani mwao magari hayo yanakatisha `ruti' kama vile hayana kibali maalumu. Ukitaka usafiri mpaka upande mtindo uitwao `geuza nalo'(ulipie nauli mara mbili. Na matrafiki kwasababu wanajua hayo, wanakuwa hawapo kuangalia nini kinachoendelea. Wanasubiri amri itolewe, au ajali kubwa itokee ndipo wanajidau kukamatakamata
Ili sheria zifuatwe, adhabu kali zitolewe bila kujali huyu ni nani. Lakini hata hivyo, barabara zetu nazo ni mitihani. Angalia mvua zinazoendela sasa hivi ndipo utakapogundua kuwa sisi bado tupo karine ya 47.
Labda tusubiri tena Bushi atutembelee, huenda kukawa na mabadiliko.
mimi
emu-three
Mdau Uliyetaka msaada Tarehe April 09, 2008 12:05 AM, Unataka kuinstall kwenye Pc au mac? Kama Ni PC basi angalia kwanza video card yako ina MB kiasi gani.. vifaa vingi vya sony vinataka atleast VGA 128MB au zaidi yapo.. kama una chini ya Hiyo utakesha mdau kwa kuinstall kitu ambacho sio compatible.. Ushauri mungine unaponunua kitu angalia kwanza kama machine yako itaweza.. i've had many guys asking me Pc games haziplay kwenye PC zao...na nikija kuangalia tatizo ni machine haiko compatible kufanya kazi hiyo.. Kwa msaada zaidi unaweza kupitia kwa wataalamu hawa mara kwa mara www.pcadvisor.co.uk nadhani nimekusaidia.
ReplyDeleteMdau UK.
Chibiriti nakushauri uanzishe blogu yako kwa kuomba msaada kutoka kwa braza michuzi...
ReplyDeleteMimi nitakuwa mdau wako..