Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Majaar (kulia)akizungumza na aliyekuwa mwakilishi wa Angola katika shindano la BigBrother Africa, Tatiana Durao alipotembelea ubalozi wiki iliyopita.Tatiana anatarajiwa kuwasili nchini Jumanne ijayo kwa mwaliko wa kampuniza Beyond the Lines Mobile Service na New Habari (2006) Limited.KAMPUNI ya Clouds Entertainment wamiliki wa kituo cha redio cha Clouds FM na jarida la Kita Ngoma pamoja na kampuni ya CXC wamejitokeza kudhamini ziara ya Tatiana Durao ambaye alikuwa mwakilishi wa Angola katika shindanola Big Brother Africa 2 lililomalizika mwishoni mwa mwaka jana.
Mratibu wa ziara hiyo, nchini Petter Mwendapole alisema leo hapa Dar kwamba wamezungumza na Clouds pamoja na CXC ambao wamekubalikudhamini ziara hiyo.
Tatiana anatarajiwa kuwasili nchini Aprili 22 na kufanya onyesho la kwanza mjini Arusha katika hoteli ya Naura Springs inayiomilikiwa na kampuni ya Impala na Ngurdoto ya Arusha.
"Tumezungumza na Clouds ambao wamekubali kutudhamini na matangazo na taarifa mbalimbali za ujio wa mwanadada huyo ambaye pia ni mwanamitindo zitakuwa zikipatikana kupitia kwenye redio yao kwenye vipindi vyaombalimbali," alisema.
Alisema CXC pia wamekubali kusaidia kudhamini ziara hiyo na kwamba wameahidi kutoa mchango wao wa hali na mali kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa.
"Mkurugenzi wa CXC, Charles Hamka amesema atatusaidia na atashirikiana nasi, bado tunaomba wadhamini zaidi kujitokeza katika kufanikisha ziarahiyo, ambapo itakuwa ni nafasi ya watanzania kumshukuru Tatiana kwakusaidia ushindi wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa2,"alisema.
Mbali na kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa hoteli hiyo, Tatiana pia atashiriki katika onyesho la mavazi ambalo litafanyika kwenye hoteli yaMovenpick, Dar es Salaam siku ya Aprili 26 ambayo itakuwa sikukuu ya Muungano.
Ziara ya Tatiana ambaye juzi alikutana na balozi wa Tanzania nchini Uingereza, imeandaliwa na kampuni ya Beyond the Lines Arts Mobile Service kwa kushirikiana na New Habari 2006 Limited, Ubalozi wa Angola na kudhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chao cha Redd's,
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), hoteli za Impala na Ngurdoto, CXC na Clouds Entertainment.
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), hoteli za Impala na Ngurdoto, CXC na Clouds Entertainment.


I don't like this
ReplyDeleteCan someone educate me. What is the impotance of this girl and what does she add to TZ? I feel the sponsorship should have been given to our girls. I am sure we have our own girls who have what this girl has plus more!
ReplyDeleteHuyu Tatiana mbona anajibadilisha kuwa mzungu!?
ReplyDeleteNinachoshindwa kuelewa, huyu Tatiana ni Muangola au kabadili uraia? Ubalozini kenda kufanya nini hadi kapata hadhi ya kupokelewa na balozi?
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteme too I don't like this.
ReplyDeletemungu wangu papa la angola limeingia dar mke wa richard mtilie mumeo kufuli na ufunguo ukae nao mwenyewe hata kipanya usimuamini maana ni rafiki wa richard.tatiyana katia nywele rangi ashindana na mke wa richard.kanogewa na jana dume la tanzania anakuja kuchukua karatasi kwa rich kipanya kazi kwako.
ReplyDeleteHivi huyu Tatiana kakosa kazi? Richard katulia na mkewe, sasa yeye na kujishaua kwake anakwenda Tanzania kufanya nini? asiotafuta mwanaume wake pekee naye akatulia. Hivi kwanini waTanzania tunapenda kuentertain ujinga?
ReplyDeleteMe too, I don't like the sound of this.. Sijaelewa mantiki ya huyu binti kuingia ubalozi wetu na kuja hapa Dar ati 'itakuwa ni nafasi ya watanzania kumshukuru Tatiana kwa kusaidia ushindi wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa2'. This is GROOSSSSSSSSS!
ReplyDeletemdhamini anasema nukuu(alimsaidia richard kupata ushindi) kwa hiyo hao wadhamini wanamlipa fadhila kwa kumwalika tanzania.te te te te te heh,kazi kweli kweli
ReplyDeletetatiana anawapenda watanzania hiyo haina ubishi
ReplyDeleteUnajua nini...wabongo wana mzuka wa ngono na mabinti maarufu, kuna mdau flani ana ushawishi mkubwa kwa wadhamini ndo ameshinikiza ujio wa huyu binti, ziara yake itakuwa na manufaa gani hatujui lkn mahela yatatoka kibao.
ReplyDeleteMnamkumbuka Aby wa BBA? alialikwa ivivi na wadau wamemmega na samantha kakolea ameoa kabisaaa...tusubiri nani atajitoa muhanga kwa tatiana.
Michu usiibanie maana miongoni mwa wadhamini ni ww mzee wa kita ngoma
...'labda' alikwenda kuomba Viza ya kuingia Tanzania, na kwa 'role' yake hao sponsors wake wali-organise akutane na Mh. Balozi!
ReplyDeleteJamani naweza nikawa sielewi lakini sioni sababu ya huyu dada kuja hapa na kupewa kipaumbele, kwanza si mfano wa kuigwa na pili anakuja tu kumkera wifi yetu kwa kweli WE HAVE TO STOP HER asije kabisa
ReplyDeleteWith due respect I beg to differ from most of you.Huyu Tatiana ni entertainer,some of us were watching BBA2 because of her and Richard.Ukiachilia mbali jinamizi la mapenzi ambalo hata nyie mnaojifanya maaskofu limeshawahi kuwakumba kwa namna moja au nyigine,ni msichana strong,mtanashati,mwenye kipaji na upendo wa kweli.That woman fell in love with Richard,we all sometimes fell/fall in love with the wrong person hapo msibishe!Na japo walikua na strong feelings towards each other,walijitahidi ku-behave,uzalendo haukuwashinda live kama Abby na Gaetano.Mnauliza kwa nini apokelewe kwa mbwembwe zote..well she is a star,ana fans wa kumwaga na zaidi ya yote he loved our brother,our country!She most of the times was wearing our Tanzanian flag in the BBA2 house...Kwa kifupi nyie msiompenda msije kumuangalia(how could you,wengi wenu karatasi haziruhusu anyway) sisi wengine tuko nae...
ReplyDeleteTatiana nenda kamuone rais, mawaziri, wabunge, wakubwa wote wa TZ. lakini unachokitaka hukipati.
ReplyDeleteweweee anonymous wa kumi na tano wewe wacha unafiki hayo ni maradhi mnayoletewa tiba hamna kama wewe umezoea kupenda na kula urada hovyo nakuomba angalia sana hii inamaana kuwa huyo dada ni hatari anakula uroda kila sehemu na kila mtu tumshukuru mungu kaka etu mzima kwani huyo dada si mzima ukiangalia jinsi alivyo ndugu watanzania hasa kaka zetu mabibi kama hao wako tele hapa home msibabaike na huyo papa la angola limechokwa kwao sasa lina kuja kumaliza kaka zetu ulizeni historia zake kabla hamjatokwa na mate kwani hata yeye anatafuta nchi ya kuhamia angola hana maket mwachieni kipanya akampime amekuja kuwamaliza kaka zetu.
ReplyDeleteAnony wa 17 pole sana...hiyo research yako uliyofanya Angola na kugundua kuwa Tati kachokwa kwao naomba urudi field,umechemsha.Na kuhusu upapa wake trust me that woman can be even better than you.Sikujui ila kuna uwezekano mkubwa kuwa uyafanyayo mafichoni ni uozo kuliko aliyoyafanya Tati (falling in love with Rich) kwenye camera.Who are you to judge her...nyie wote mnaomuita dada wa watu fuska,i bet nyie sio mafuska kwa kuwa huwa mnajistiri chini ya meza za mabosi wenu lol...Hivi hao stars wote mnaojaaga majukwaani kuwaangalia iwe bongo au huko mlikozamia huwa mmepeleleza kwanza na kugundua kuwa wao ni watakatifu?Acheni unafiki wenu u find other reasons to dis her lakini sio eti alikuwa fuska bla bla bla...mtakatifu na awe wa kwanza kumrushia jiwe!
ReplyDeleteKama kuna kitu ambacho WaTZ tunastahili kukikemea au kukigomea at large ni huu 'ujio' wa huyu Demu.
ReplyDeleteMimi naona ni kuchanganya mambo ambayo hayajengi hata kidogo. Huyu demu alikuwa na drama kibao ambazo sio somo lolote kwa waTZ (hususan mabinti wa kiTZ), sioni sababu ya yeye kuja na kupolewa kwa shangwe. kama vile hao 'mapromota' wake wanavyotaka iwe
kuna watu walizungumzia ku-boycot ziara ya mwenge wa olimpick, mimi nasema Ziara ilikuwa na faida na heshima kwa nchi yetu na bara kwa ujumla - japo siasa na umashuhuri usiokuwa na maana vilitawala. Kwa hii 'ziara' ya huyu Demu (najisikia hata kichefuchefu kutaja jina lake) SIKUBALIANI NAYO HATA KIDOGO.
Nadhani kuna watu walinufaika na drama kati ya Richard na Mkewe, hii 'ziara' nahisi ina nia ya kutonesha kidonda ili watu wapate kuuza habari.
Ombi langu kwa DSTv/Multichoice au wadhamini wengine, kipindi ambacho huyu demu atakuwa nchini, Richard apewe ZIARA ya kikazi nje ya nchi ili asikutane na haka ka-demu.
Mnasemaje wadau khs hili???
Kwenye hiyo picha yupi ni Tatiana?
ReplyDeleteYani Tanzania imekuwa jalala la kila msanii wa nje.. jamani nyie clouds tumechoka .. kila siku tunachangia hela zetu watu wasinii wa nje .lini na sisi wasanii wetu watachangiwa huku...
ReplyDelete