vifaa vilivyoagizwa kwa bei mbaya na serikali kwa ajili ya mazoezi ya viungo hasa kwa maafisa wa taasisi mbalimbali zinakula vumbi uwanja wa ndani wa neshno na haonekani mtu akila tizi hata siku moja mahali hapo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Tatizo la nchi yetu ni 'motive'. Ukichunguza hapo utagunduwa kwamba pesa iliyotumika kununuwa vifaa hivyo utakuta ni kubwa mno kulinganisha na bei halisi. Kinachokuwepo hapa ni kwamba watu wanasuka 'dili', wakishakula pesa basi! Hakuna tena mtu anayekumbuka kwamba kuna kitu fulani kilinunuliwa kwa kazi fulani.
    Hivi hujaziona zile mashine za tiketi pale kwenye vituo vya Feri ya Kigamboni? Ni fedheha tupu!

    Kununuwa vifaa vya mazoezi kwa ajili ya vingozi wa taasisi za umma na kuviweka nesho wakati watu wenyewe wanakaa Masaki unategemea nini? Kwani wana kambi yao ya mazoezi?...huu ufisadi unatupeleka pabaya

    ReplyDelete
  2. lazima vipate vumbe hivyo vifaa na badao.Maana wapo busy kui-FISADI nchi...

    Hapo wangekuwa wameletewa mikataba kusign wangekuwa wamemaliza kusign na kuvuta cha juu

    ReplyDelete
  3. Oooops!, thats so bad!, serikali inatakiwa kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kila siku! Ndio maana life expectancy ni ndogo TZ na afrika kwa ujumla, kila kukicha watu wanakufa kwa heart attack! simply due to the ignorance of such activities (GYM)

    ReplyDelete
  4. Kwa nini hiyo Gym iwe ya viongozi pekee wakati wenyewe wenye haki hawapewi nafasi (wananchi) hapo wangeweka Gym ya watu wote kwa bei nafuu kuliko gym private ili kila mwananchi afaidike na wangejiingizia hela nakuendeleza afya za wananchi.haki ya mungu daaa kweli maisha sio sawa nashauri kila mwananchi akifa aombe kuzikwa na sila yake ili ukifika huko kama kweli kuna dunia nyingine unawasha tu mafisadi

    ReplyDelete
  5. Mbona sielewi hapa??Hivi kabla ya kununua vifaa kuna alifanya research kujua hawa jamaa hawafanyi mazoezi kwa nini??Mijitu hii haifanyi mazoezi kwa kuwa haitaki mazoezi na si kwa sababu hawana vifaa.Huu ni ubadhirifu wa mali ya umma.Namuambo Mkuu wa wilaya ya Tegeta aitishe cooper Test kama ile ya marefa kwa watumishi wa umma wote.Au Bar zote zifungue Gym jirani labda?

    Mdau wa Mayfair Plaza

    ReplyDelete
  6. Aliyenunua hana na kuviweka neshno ndio wa kulaumiwa. Kwanini usiweke kwenye ofice zao au kwenye maeneo wanayoishi hao watumishi? Tenga chumba kimoja kwenye building kiwe gym. Huko neshno ni saa ngapi mtu ataenda huko?


    Kuna mtu alipata tenda wana hakuwaza kwanza akatengeneza hela yake haraka haraka. Huyo aliyeagiza hivyo vitu ndio wakujibu mashitaka. Mafisadi kila kona

    ReplyDelete
  7. Sasa siunajua jamaa wanaona sifa kuwa na mitambi hile.hawajui umuhimu wa kufanya mazoezi na hio gym kama hawatumii wafungulie raia pia watumie watu wote wana haki ya kufanya mazoezi hapo washakula hela nyingi sana haina maana kuwanyima raia watumie hapo kwani hela yao ya kodi ndio imetumika kununulia vifaa.
    Mdau mzawa

    ReplyDelete
  8. Do people have time to go for a gym???Life la bongo tizi tosha, why u need a gym for????? hehehehehe

    ReplyDelete
  9. hapo kuna mtu kashatia ndani cha kwake! hivi nchi yetu ina nini?

    ReplyDelete
  10. Siamini kama tatizo la hivyo vifaa kutotumika ni watu kutokuthamini mazoezi tu, bali kuna mbinu za kiufisadi zilitumika kuvinunua, na bado kuna restrictions kuvitumia. Si bure! Watu wanaenda gym za kulipia, iweje wasitumia hivyo vya bure?

    >> Wadau,kuna bonge la HOTELI katikati ya Kampala na Entebe, linafanyiwa finishing kwa sasa ni la MKAPA na MUSEVENI. Jamani ni soo! Kama michuzi hatanibania, nitaweka mapicha yake hewani. Ufisadi?

    ReplyDelete
  11. Hao vigogo wenyewe wana vifaa vya gym kwenye majumba yao, sasa serikali ilivyoagiza ilitegemea nani atoke Masaki kwenda Temeke - Neshno. Hahaaaaaa
    Hiyo pesa ingetumika kujenga visima na kununua madawati.

    ReplyDelete
  12. sasa mnataka wapunguze unene muambie wameshakanyaga mawaya?Wenyewe mnajuwa bongo unene ni dili,sio kama huku majuu ambapo unene ni gonjwa kubwa.Hivi vitu havipo kwenye utamaduni wetu bana.

    ReplyDelete
  13. Tatizo sio aliyenunua vifaa jamani.
    Hivi vilikuwa katika mkataba wa kujenga uwanja mpya wa taifa na lazima vingenunuliwa kwamni hiyo ni Package.
    Tatizo hapa ni Umeme, hivi vifaa vyote vinatumia umeme na kama hakuna umeme au kuna mgao wa umeme unaotolewa usiku wa manane maeneo ya kurasini na Chang'ombe basi hivi vifaa ni kama zero "kazi bure".
    Ni sawa na kuwa na big screen uwanja wa taifa mpya au projector, na hata Air-condition chuo kikuu chang'ombe wakati unajua wazi bila umeme hivyo vitendea kazi vitakuwa kama mapambo maana havitafanya kazi.

    ReplyDelete
  14. It should be a law for them to go to the gym.Eeehh! alafu tuone wataiba saa ngapi,wapige vyuma mpaka wanyong'onyee,mission zitakuwa impossible.Aaaaahhhh!!!!

    ReplyDelete
  15. watumishi wa umma wengi baada ya kazi wao nikupita bar full kupombeka na nyama choma hiyo ndo starehe yao,ndo maana vitambi kibao,mazoezi kwao sio dili.

    ReplyDelete
  16. salama kaka machu mimi ninaomba huyo mdau anaetaka kutuletea habari za kampala mpe nafasi aseme aliyoyaona kwani mambo kama hayo ndio tunayotaka kuyasikia na ninawaomba watanzania wanzangu tuyazidi kuyafichua haya mabaya yanaoendelezwa na wakubwa zetu ndani ya nchi na nje ya nchi wabongo wako kila kipembe cha dunia kuwafichua waizi wanao iba katika serikalini aibu jamani kaka wewe lete picha za hoteli hiyo ya kampala ya mkapa ya rafiki yake wanayoiteremsha kampala michuzi wacha kubania hii comment yangu ni kweli tunayoongea mpe huyo kaka nafasi aseme aliyoyaona asante .

    ReplyDelete
  17. Vigogo wa Bongo akili finyu. Hata mwendo nusu kilometa wanataka waende na gari. Kutembea kwa miguu wanaona inawashushia hadhi. Hakuna sababu yoyote ya kununua vifaa hivi. Wangeweza kushiriki kabumbu au ngoma ya sindimba, ni mazoezi tosha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...