najua uko bize, ila hicho asemacho Dr kamanga ni kweli. pamoja na madhafu ya Mugabe kingángánizi lakini bado Harare kumekucha hebu ona jiji hilo linavyopendeza.
Lakini tuache masikhara jamaa uchimi wao umeporomoka ile mbaya, yaani hadi pesa zao zina expiring date! Hata hivyo hii inatokana kwa kiasi kikubwa na hujuma za wakoloni.
Sio wakoloni wanaoshikilia madaraka kwa lazima sasa hivi hata baada ya wananchi kumchagua Tsvangarai!Wakoloni waliondoka zamani sana,ni si sawa kuendelea kuwatumia kama kisingizio cha hali mbaya ya jamii iliyoko sasa huko Zimbabwe.Nyumba za raia zilichomwa moto kwa ruhusa ya Mugabe na sio wakoloni.Wakimbizi wakiZimbabwe wametapakaa kwa maelfu ktk nchi zinazopakana na nchi hiyo na hii na haitokana na wakoloni!!
ReplyDeleteInabidi tuwe wakweli na tumlaumu anaekosea na watu wengine.
MTOWA MAONI WACHA UNAFIKI WAKUSEMA KUWA WAKOLONI NDIO WAMEWAFANYA HAYO HAPO ZIMBAMBWE SASA JIULIZE HIZI NCHI ZA KIAFRIKA KAMA KWELI ZINAPENDANA KWA NINI WASIMSAISIE AU KUSHIRIKIANA NAE KIUCHUMI AU NDIO UNAFUATA MANENO YA TANZANIA KUWA MUGABE NI NDUGU YETU WA DAMU KUKIWA HUKU MAMILIONI YA WATU WANAKUFA NYAA MARADHI NK KAMA NI KWELI NDUGU WAPELEKEENI HICHO KIDOGO MLICHONACHO
ReplyDeleteWaafrica tuwe serious! hakuna hujuma za mkoloni wala nini!
ReplyDeleteWAAFRIKA TUNAJIHUJUMU WENYEWE. Sema tuu we are experts wa kushift blame kwa wengine for our own failures! by this trend we are going no where! We should own up our responsibility for our failures. Ni dhihaka kwa waafrika kwa mtu kama Mugabe kuendeleza unazi wake kwa kisingizio cha imperialism! When shall we get really we Africans? Ukiangalia mambo yanayoendelea Kenya, Zimbabwe na kwingineko, ni rahisi kuwalaumu wazungu, lakini wanaotukaanga na kutuuza ni watawala wetu na wala siyo wazungu. Ofcourse wazungu nao wanamatatizo yao na sisi, lakini they are exploiting our own stupidity. We ukisaini mkataba wa mamilion kwa bei ya bure..unategemea nini? mzungu aliachie hilo deal? My fellow Africans lets get real!
We cant afford a blame game anymore!
Weekend njema kwa wadau wote.
what...!? eti hujuma za wakoloni. uchumi wa zimbabwe unauliwa na wazimbabwe wenyewe, wakiongozwa na kiongozi wao Fashist Mugabe.
ReplyDeleteHaya na wayale hayo majumba sasa, siku hizi hata mkate hawapati, natusipoangalia na sisi tutafika huko, hamuoni shilingi yetu inavyoporomoka kila siku?
Shikamoo tena za nini huku? Ili watu wamuone kwamba ni mdogo au? ....
ReplyDeleteJamani Tukiwacha hujuma za kikoloni Mugabe hafai awaachie wenzake sasa, kwani sio Falme ila ni serikali mpishe mwenzako hata kwenye chama chako. Kibaya Mungu asichopenda kama alivyofanya Sikukuu ya Kuzaliwa kwake Keki Kubwaaaaaaaa, inaoneshwa kwenye TV ya Taifa, Maskini au Watoto wa MAskini inawauma ikishawauma Zambi unapata kwa mwenyezimungu, Ndomana tunaambiwa tutoe "ZAKA" ukifanya hivyo utapata macho ya watu. Wakoloni wanachangia hasa USA na UK. Nchi Kubwa za Wakoloni wanasema Hawatosaidia Nchi Maskini za Africa mpaka Waache Rushwa?. Rushwa inaanzishwa na USA na UK silaha zinafikaje Jeshi za Africa kama sio wao wanachangia mauwaji Libya na Siera Leone. Demokrasia haitoki kwa USA wala UK ni sisi wenyewewe wa Africa.
ReplyDeleteMdau hebu usianze kuwalaumu wakoloni kwa kila kitu.Wape lawama pale wanapostahili na sio kuwaonea.Sina maana kwamba nawaunga mkono kwa waliyoyafanya,ila kwa case ya Zimbabwe,Mugabe ndio mtu wa kwanza kulaumiwa.Mashinikizo yote ya kimataifa yanasababishwa na ubinafsi wake.Wote tunajua kuwa vinapowekwa vikwazo vya aina yoyote kwa nchi yoyote,wanaoumia ni wananchi na sio viongozi.Sasa kama anawajali wananchi wake kwa nini asiachie ngazi-wengi tuna uhakika kashindwa kwenye uchaguzi na ndio maana hataki kutangaza matokeo.
ReplyDeleteBy the way,nchi kama Zimbabwe na Kenya wapo hapo walipo kiuchumi kutokana na siasa zao.Hawakuwafukuza wakoloni mara tu baada ya kupata uhuru.Sisi tulikimbilia ujamaa tukiamini kuwa wakoloni wote wakiondoka kabisa ndio tutakuwa huru.It was a big transition na ilihadi muda,nadhani kila mtu anaona tuko wapi.
Itachukua muda kupata maendeleo ya kweli hasa ufisadi ukizidi kuendekezwa.
Angalia hawa wakulima wanamsifia huyu mpuuzi eti Harare tambarare,mji umejengwa na hao hao mnaowaita wakoloni na ndio wanauendesha na sheria zao mpaka sasa ndio maana mji ni safi,ingekuwa huyo mkulima mugabe huo mji leo Singida ingekuwa na afadhari,wafrika acheni siasa za kijinga za kina mugabe ndio zinawaletea umaskini...Zimbabwe was better under mkoloni smith kuliko huyo kenge,ni kweli demokrasi ilikuwa chini lakini wangeweza polepole kuweka mambo sawa kama USA weusi walivyofanya,ila kumpa huyu mjinga nchi ilikuwa suicide ya wazimbabwe,angalieni South Africa haina tofauti na resource na Congo lakini uchumi wao ni sawa na nchi nyingi za Europe na sasa weusi wanaendelea kwa sababu wamekubali kushirikiana na hao wazungu,madwanzi kama Mugabe lazima yaondoke maana yanatumia rangi kugawa watu,na hao wazungu kumbuka wote ni wazimbabwe wa kuzaliwa na hiyo ardhi ilikuwa inarudi lakini walikuwa nao wantaka uhakika wa uchumi wao,Zimbabwe was the biggest food exporter in Africa lakini sasa ni kichekesho na jembe la mkono ndio sasa linawaletea njaa
ReplyDeleteHey Mkuu,
ReplyDeleteHee bwana wewee.!!! nimekubali Harare ni babu kubwa,ni moja ya mji wa kujifunia Africa,looks like other western country's cities meeen...!!.
Wadau asanteni sana kwa kumwaga point tupu. Hata mimi nilitaka kushangaa hii biashara ya kuanza kuwalaumu wakoloni.. WAKOLONI!!?? Jamani Africa, lets stop this foolishness. Mpango wa kuwalaumu wakoloni leo hii 2008 ni upuuzi. Yaani Zimbabwe ilivyokuwa miaka ile, leo hii hata Kimanzechana kuna nafuu.. Mugabe kazi imemshinda awapishe wanaume haya ndio yangu machache... Jamaa ni raisi tangu enzi ambazo bongo Rais alikuwa Nyerere!!!!!!!!!
ReplyDeleteMdau - Boston, US
Mugabe ndo mtu safi, acheni ufala nyie, kama Mugabe angekuwa baba yako ungesema kionzi mbaya! au nyie mnataka wazimbabwe wanaendelle kuwa shamba boys wa watasha.
ReplyDelete40% ya Budget ya Tanzania inategemea wafadhili. Hiyo ndio inalipa mishahara ya serikali wakikata tu Tz nayo itakuwa Zimbabwe.
ReplyDeleteHaya Bongo asilimia kubwa ya kuendesha serikali mnapewa na mkoloni.Rais Omar Bongo yuko madarakani kwa miaka 38, Gadaffi 40 Paul Biya 25, na wengineo. Pale wakoloni walipokuwa wanaendelea kuhodhi ardhi waliyopora kwa akina Karumanzila, Jongwe hakuwa na problem. Pale tu wakoloni walipoambiwa ku-share na akina Karumanzila ndipo mzee Jongwe akaanza kuonekana ni mbaya na kupakwa choo.Chavez angekuwa hana mafuta, leo angekuwa ni Jongwe wa pili. Korea ya Kaskazini anaambiwa asiwe na silaha fulani lakini wakoloni wana haki ya kuwa nazo. Fungukeni Macho!
ReplyDeletehakika cha kusikitisha sisi waafrika weusi ni majitu mapumbavu kushinda hata wanyama sijui kutokuwa na elimu kazi yetu kulaumu wakoloni ndiyo mwimbo tunaojua.
ReplyDeletenchi ngapi za kiafrika zenye uhuru na wakoloni hawapo lakini angalia wananchi wanavyoteseka kazi ujambazi tu. angalia nchi za kiarabu zilizoko afriaka na maendeleo huweza kuamini nchi zenyewe jangwa tupu lakini sijasikia misri inaomba msaada wa chakula. lakini tanzania leo ina zawadi zote toka MUNGU maji ya kunywa mwanza hamna sasa jamani hapa mkoloni kafanya nini haya UFISADI wa pesa makoloni kafanya nini. tuache majungu tufanye kazi na tupendane viongozi watawale kwa maslahi ya taifa na siyo matumbo na familia yao.
leo inaglikuwa wazungu hawapo hata dawa ya aids basi tusingalipata tungalikufa kama wanyama msituni na maiti kuoza mitaani.
mimi nimezaliwa wakati wa mkoloni na kuona faida zake hamna anayeweza kunidanganya wakoloni waliicha tanzania na zimbabwe katika kheri kubwa lakini viongozi wetu wametunyanyasa.
leo bara la afrika katika sehemu wanazoishi waaafrika weusi na vita, majambazi na kudhulimiana na pia kutegemea misaada kama yatima.
ni aibu kubwa kulalamika wakoloni kila siku tusafishe nyumba zetu kabla ya kulaumu wengine.
na kenya mkoloni sijui kafanya nini haya kongo, uganda na nigeria jamani. kila mkoloni haya zanzibar sijui mkoloni naye. MUNGU TUBARIKI TUWE WATU WA KUSHUKURU NA KUJUA BAYA NA ZURI PIA HAKI AMINI
Mugabe ana nia nzuri ya kuwakomboa wazimbabwe. Kitendo chake cha kuchukua mashamba ya wazungu na kuyagawa kwa waafrika ni kukamilisha harakati zake za kuwakomboa wazimbabwe. Tatitizo la sasa ni wazungu ndiyo waliyosababisha kwa sababu ya chuki binafsi dhidi ya mugabe na wanafanya hivyo ili kumuondoa madarakani. Morgani ni kibaraka wa wazungu na hafai kuingoza zimbabwe ktk wakati huu ambao watu wanataka uhuru wao kamili. Hivi mbona sisi waafrika tunakuwa wajinga kiasi hiki kwa kuona kila lisemwalo na wazungu ni sahihi bali na sisi wenyewe siyo sahihi? Hivi ni kwa nini hawa jamaa hata wakiishi kwenye nchi zetu tunawapa zile sehemu nzuri na wakati huo huo sisi weusi ni marufuku kufika maeneo hayo? Ni wapi weusi tunaweza kujiona tunathamani kama siyo kwenye nchi zetu? Tunabaguliwa kila kona ya dunia. Sasa kitendo cha wazungu kunyang'anywa mashamba ni kinyume cha haki za binadamu ila kitendo cha wao kuwanyima ardhi wazimbabwe weusi siyo kinyume kwa sababu sisi siyo binadamu!!! Waafrika hamjui kwamba wazungu wametubagua hata kwenye hicho kitabu wanachokiita cha mungu. MUGABE chapa kazi, matatizo yataisha na nchi itarudi kwenye mstari. Propaganda za magharibi tumezizoea kwani hata Bush alitudanganya kwamba Sadamm alikuwa na silaha za maangamizi badala yake kaenda kusabibsha maafa.
ReplyDeleteanayemsifu mugabe basi aende huko siyo unapiga kelele wakati unakala raha bongo.
ReplyDeletewacha wananchi waamue nani wakuweza kuwatawala na uchaguzi uwe wa haki.
ni rahisi kuzungumza kwenye internet hebu ndugu niwaulize wale majambazi wa kuvamia mabasi na kuwavua watu nguo bila ya wazazi na watoto hao ni wakoloni. ingalikuwa mkoloni kafanya kosa kama hilo basi sisi waafrika tungalilamika dunia yote kuwa tunanyanyaswa.
haya ndugu mie NSHUKURU nimejaliwa kutembea leo ukienda uinmgereza mfano seheme wanaozoishi waafrika utakuta kuta zote zimechorwa kwa maneno machafu sasa jamani hapo wakoloni.
chukulia raisi wa mbeki wa afrika ya kusini wakati wananchi wake wanataka wapatiwe dawa za ukimwi jibu lilikuwa afrika kusini hakuna ukimwi nani anayekufa mwafrika na nani asiyejali watu wake mwafrika sasa hapa mkoloni kafanya nini.
haya mbeki huyo huyo wakati wa kupigania uhuru alitaka msaada dunia yote leo zimbabwe kuna hatari ya kutokea mauaji ya wenyewe kwa wenyewe anasema zimbabwe wasiingiliwe watamaliza matatizo yao wenyewe jamani huyo na mkoloni?
leo wazungu wakisaidia sehemu ooooooooooo maslahi na wasiposadia ooo hawana maslahi.
jamani maslahi kila kiumbe anayo ikiwa mtu atapewa mwanga atatumia.
mfano mzuri wa kwetu tanzania ufisadi kwanini wakati wa baba wa taifa ulikuwa hamna na leo ndio ibada ya viongozi kupata kazi ili kujitajirisha na familia yake.
watanzania naimani singalikuwa wazungu kuleta balance basi viongozi wetu wa nchi 3 na siyo afrika tu hata chakula tusingalipata ingalikuwa na viongozi na familia zao.
Tukumbuke Zimbabwe ilipata uhuru mwaka 1980 na hivyo iliridhi 'system of governance" iliyoachwa na Uingereza. Uchumi wa Zimbabwe umeharibiwa na Mugabe mwenyewe kwa kujaribu kupata support ya wananchi wake kipindi cha 1998/1999 - ilikuwa karibu na uchaguzi na watu walikuwa wameanza kumchoka. Nchi hiyo ilikuwa na uchumi mzuri sana na Zim dollar yao ilikuwa very strong and stable (in 1997, the exchange rate of Zim $ to US$ was 10:1 !!).
ReplyDeleteMugabe angekuwa na subira, Uingereza ilikuwa iwasaidie kuhamisha mashamba kwa indiginous Zimbabweans kwenye utaratibu ambao ungekuwa wa mpangilio mzuri and also to compensate the white farmers (kumbukeni hao white farmers were Zimbabwe citizens and had been there for generations. Mugabe ili ashinde uchaguzi kipindi hicho akaamua kuwanyang'anya white farmers hayo mashamba kipindi hicho kiholela na hivyo kufanya kuanguka kwa uchumi big time. Mashamba ninayoyazungumzia hapa ni mashamba kama yaliyo huku Marekani / Canada that are well mechanized with irrigation systems in place......in thousands of hectares....not peasants business ambayo tunayo nyumbani Tanzania (sina maana ya kuwasaga wakulima wetu kwani my parents are peasants: heka 15 - 60). Mugabe akagawa mashamba hayo ambayo na kuwapa wazawa na kugawanya the farms of that caliber to little plots for people to construct their huts!!
Wawekezaji wote wakaanza kuondoka Zimbabwe na wasomi wengi wakaanza pia kuondoka (brain drain) kwani kulikuwa hakuna stabillity tena na hela yao ikaanza kuanguka vibaya sana. Sasa hivi nafikiri exchange rate in Zim $ : US$ ni 400,000:1
Hivyo jamani sio wakoloni au Uingereza for this matter but Mugabe ambaye ana uchu mkubwa wa madaraka na uporaji wa chochote kilichombele yake na mke wake Grace.
Hapa sina maana kuwa black Zimbabweans wasingepewa mashamba, not at all, all that was needed was a proper planned transition and to ensure the farms continued to function. Tukumbuke South Africa pia mashamba yao are run by white farmers and from Zimbabwe mistakes, South Africa will never commit the same mistake.
Mugabe will not let go of leadership of Zimbabwe as he has no where to go....once he is out may be we will see in the Hauge infront of the Human Rights tribune kwani amewauwa sana Zimbabweans of Matebele tribe (wana ukabila sana nao hawa) na wapinzani wengi kwa ujumla. All I can tell you guys is Zimbabwe was a paradise prior to year 2000 and was the country which had a "system" in place.
Poor Zimbabweans, their country is damages beyond repair...it will take 20 years or more to be where it was before.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
JK - T.O.
jamani naomba mnisaidie nani aliandika how EUROPE UNDERDEVELOP AFRICA???? kama yuko hai nadhani aNajuta. hatuna haja ya kuwalaumu wazungu kwa lolote sisi wenyewe ndio mazoba, waongo wanafiki ,majungu, wavivu,MAFISADI, ISHU YA KIBAKI, MUGABE UTASEMA WAZUNGU???? NA HIZI FEDHA ZA CHEBGE DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI MOJA , CHENGE MZUNGU???? RICHMOND, IPTL,EPA&???? TUTAWALAUMU WAZUNGU????
ReplyDeleteNYIE MNAOMSIFIA MUGABE KUHUSU MASHAMBA, HAMJUI MKO GIZANI.
ReplyDeleteNILIKUWA PALE , MASHAMBA WAZUNGU WALOPORWA BILA CHEMBE YA UTU, VIONGOZI WASERIKALINI NA WANAJESHI WAKAGAWANA, MWANANCHI WA KAWAIDA ALIYEPATA ARDHI AIDHA ALIPIGIWA KIFUA, NA WENGI WAMEPATA ARDHI SEHEMEU AMBAZO HAZINA RUTUBA.
ACHENI UJINGA WA KUSIFIA VITU MSIVYOVIJUA.
HAYA SASA HIVI KAMA ANAJIAMINI KWA NINI ANASHIKIRIA MATOKEO, KWA NINI??
WAKATI RAIA WA ZIMBABWE WANAMPINGA NA KUMTUSI HUYU JAMA, KUNA RAIA WA TANZANI MANZESE KWA MFUGA MBWA ANAMSIFIA MUGABE!!!!!!!!
Njooni hapa South muone wazimbabwe wanavyohangaika na kukimbizana na polisi na kulala mitaani wanakimbia kwao???
Mdau-South Africa.
Nyinyi mnaosema huko nje hamjui chochote. Mimi niko hapa Mutare toka 2001. Ni kweli maisha ni magumu lakini yana mwisho. Mkoloni ndiye mwenye haki ya kila kitu duniani; Mweusi ni mtwana. Watanzania wenzangu wanaosema uhalifu uko Africa, nilipotoka USA 1998 ndiyo nchi iliyokuwa ikongoza kwa wafungwa wengi duniani wa uhalifu! Watanzania waoombea kwamba mashamba waachiwe wakoloni poleni. Mzee Jongwe chapa kazi.
ReplyDelete