
Mimi ni Mdau wa Gieta, ningependa kuwasilisha mada hii kwa niamba ya wadau wenzangu.
Ni kipindi kirefu sasa tumekuwa tukipata tatizo la umeme hapa Geita na sababu ya msingi hatuijui. Kila siku lazima umeme ukatike na ikifika mwisho wa mwezi bill inakuja kubwa mno.
Tunashindwa kuelewa hawa watumishi wa Tanesco wanatumia vigezo gani kutoa bill za umeme kwa wadau. Inaonesha wazi kuwa ufisadi bado unaendelea kwani sababu za kukatika kwa umeme hatuzijui nabado bill haibadiliki.
Je Meneja wa Tanesco Geita yuko hai au amerest in peace??????????????? Huu siyo uungwana na wala siyo UTU.
Tunaomba Tanesco - Geita wajirekebishe.
Mdau Geita.
MDAU WA GEITA POLE SANA, NDIO UTAMBARARE WA BONGO HUO! TATIZO SI LA KWENU PEKE YENU, NI NCHI NZIMA.
ReplyDeleteNYUMBANI, TUNA TATIZO LA LEADERSHIP, UONGOZI NI MBAYA KILA MAHALI, MTU AKIPATA KAZI YA UMENEJA ANAJIONA YUKO ENTITLED KUHESHIMIWA NA KUITWA BOSI, LAKINI HAJIONI KUWA ANA RESPONSIBILITY KUTOA SERVICE KWA JAMII. YAANI WABONGO HATUNA UWEZO WA KUFIKIRIA CRITICALLY... SASA MANAGER KILA SIKU BILLS ZINALALAMIKIWA,LAKINI AAH, HANA HABARI, UMEME UNAKATIKA KILA WAKATI, WAGONJWA WANAKUFA MAHOSPITALINI KWA KUKATIKIWA UMEME WAKIWA WAMEPASULIWA, LAKINI NDIO KWANZAAA, WANA RICHMONDULI KUANZIA NGAZI YA JUU KABISA..., SASA HUONI TUNA MAMATIZO YA LEADERSHIP?
POLE, LAKINI HAITKUWA HIVYO FOREVER.
Mi Pia nlishachokhagha na hiyo hali, Wewe, wazungu wanasema IF U CAN'T BEAT EM JOIN EM! Njooni Dar, najua ni temporal solution for a permanent problem ila si unakua ushajitoa matatizoni, Tujaghe wote huku nyie shaurienu! Msaada sina maana naelekea Bar kunywa na huyo meneja mnayedhani amerest in peace, hapana yupo Dar!
ReplyDeleteahaha!!! kwa habari zaidi mapate hapa: www.mkandamizajipushelizisadomangiwasheduzesnake.shinyanga.vijijini
Siyo Geita peke yake kuhusu tatizo la Umeme.Tanesco hebu zindukeni kutoka usingizini na mfanye biashara kwa faida.Kuna maeneo ya Wachimbaji wadogo wadogo wa Dhahabu ya Nyarugusu kilometa chache tu kutoka Geita hawana umeme kabisa kwa kipindi kurefu sana.Hili ni eneo ambalo linahitaji umeme sana na linazalisha dhahabu kwa wingi.Lipo eneo la Rwamagasa kilometa chache tu kutoka Katoro au Buckreef Gold.Hili nalo ni eneo ambalo linazlisha Dhahabu kwa wingi sana.Wachimbaji wadogo wadogo wanakatishwa tamaa na vikwazo mbalimbali likiwemo ukosefu wa umeme kwa ajili ya uchimbaji.Kila mashine katika uchimbaji wa dhahabu itahitaji nguvu za umeme.Lakini Tanesco haina mpango kabisa kuhusu maeneo hayo.Yamebakia maneno matupu kila kukicha.Lipo eneo lingine la Nyakagwe kilometa chache tu kutoka Bulyankulu Kahama.Nalo matatizo ni yaleyale.Maeneo mengine ambayo yapo katika ukanda huo huo ni pamoja na Mgusu,Ushirombo,Nyamtondo na Ipalamasa.Kwa kweli Tanzania tunachezea Utajiri tulionao hata watu wa nje wanatuona HATUNA AKILI KABISA.Hayo yote ni maeneo ya uzalishaji wa dhahabu amabayo nishati ya Umeme ni nyenzo muhimu na ya msingi sana.Hakuna mbadala 'alternative energy'.Waziri wa sasa wa Madini na Nishati,anatoka maeneo hayo hayo.Aliwahi kupita katika maeneo hayo hivi karibuni bado akiwa Naibu Waziri wa Madini na Nishati katika mikutano yake ya hadhara kwa wachimbaji ilikuwa ni maneno matupu tu yasiyo na kichwa wala miguu.Barabara ya huko ni aibu tupu licha ya Dhahabu nyingi inayotoka huko.Kama vile Serikali yetu imekodishwa kwa mamluki wanaopanga priorities wao wenyewe bila kushirikisha wenyeji wa maeneo hayo.NI AIBU KUBWA.Barabara ya Geita hadi Mwanza ni vumbi tupu!Jamani kama Kazi imewashinda si mseme?Tutaendelea kufuga huu UJINGA hadi lini na hali zetu zinazidi kuharibika na utajiri tunao?Je,hii siyo aina nyingine ya UFISADI?Kutukwamisha kimaendeleo?
ReplyDeleteEeeey kumbe ni katanesco ndio wanaotufuata hadi ughaibuni kutuzimia kaumeme? mi nirifikiri ka si si emu eti?
ReplyDeleteMana kira kaumeme ukizimwa mimi nawarani tu kwa vile ni joto sana na huku kammbu kananing'ata.
Ama kweri utu si mavazi bana, pore sana mdau mwenzangu ndio afurika hiyo.
by KAMANDA MANYOTA
Pole sana mdau,najua unaongelea ukataji wa mwezi uliopita!Unapigwa mgao siku tatu.Kuna siku moja nilienda kulipa bill tanesco Geita nikakuta na wao hawana umeme!!!(Believe me).Ngoma inapigwa kutoka Mwanza!!Msiwahukumu Geita.Jamani wanadai nguzo zinaanguka kwenye'majaruba' ya mpunga katikati ya sengerema na Geita!!Wanatumia njia za mwaka 1947 kugawa umeme.
ReplyDeleteNi kweli suala la uwajibikaji kwa wafanyakazi wa serikalini na wa kwenye mashirika ya serikali bado ni mdogo sana na unahitaji kupigiwa kelele na sisi wananchi wenyewe ili wabadilike. Haya mambo yapo kila mahala katika utendaji wa kazi waajiriwa wa serikali. Lakini pamoja na hayo inabidi pia sisi tunaolalamika tujiangalie pia kama tunatimiza wajibu wetu kwani wakati unailamikia Tanesco nawe pia unahusika kuwaumiza wanachi ktk eneo lako la kazi. Jambo lingine ni hujuma zinazofanywa na wananchi wenyewe iwe kuiba nyaya za umeme, kukata mabomba ya maji, kuiba vifaa vya serikali kwa manufaa yao nk, haya yote inabidi tuyajadili pia badala ya kulamika kwani bila kuonyesha uzalendo hatutofika mbali na tutakuwa watu wa kulalamika kila siku. Tanesco acheni kutuumiza walalahoi badala yake zibitini mapato yenu kwa kuwabana wafanyakazi wenu wanoihujumu Tanesco
ReplyDeleteJAMANI KUNA UFISADI WA KIPEKEE GEITA JAPO MNALINGANISHA NA KWINGINE
ReplyDeleteUMEME HUKATWA KILA KUNAPOKUWA NA EVENT YOYOTE MUHIMU KTK TV yaani dk ya kwanza ya kila mechi ya ligi za uingereza ?? yaani filimbi ikilia tu na umeme unatimka
jamaa(meneja ) anazunguka tu na prado yake mpya jamani sio bili tunazozidishiwa hizo??????????????
siku yake ipo tumemwekea we ngoja tu tutakaiba hako kaprado kake