Home
Unlabelled
kp leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
KP Tutafsirie kidogo imetubamba
ReplyDeleteUnajua bongo bwana ni bonge la nchi ya aina yake,uliona wapi mfupa ulomshinda fisi mbwa akauweza?kiboko hapa alikuwa Sokoine peke yake,Pinda fanya kazi usipindishe maneno tupe kinachoendelea kuhusu mafisadi ikibidi na picha zao.
ReplyDeleteHuo mkono hapo nyuma naujua ni wa nani,Nilonge nisilonge?Aku Mwaya nisije nikamwagiwa tindikali na mimi bado sijazaa!Cartoon za Kp ni chemsha bongo mwanangu.Shurti kwanza upate bakuli la uji wa ulezi bongo zifunuke au?100%
ReplyDeleteni vizuri kuwa sasa watanzania wanaona kuwa hakuna uongozi tza, kwa lugha nyepesi , hatujapata viongozi ambao wataipeleka mbele nchi yetu.maneno kuwa tunahitaji pesa na kuwa watu hawa watashtakiwa baadaye ni upuuzi mtupu, pesa hizo hazikutupwa sokoni. zililipwa kwa makampuni ambayo wenyenayo wanajulikana. round them put them to trial, thats it. tumpe nchi vladimir putin
ReplyDeleteMichuzi uwe unawashauri pia wenzio wanaoendesha blog. Kuna mwenzio mmoja kabandika katuni hii kwenye bog yake na kuifananisha na kiongozi wa ngazi ya juu ya serikali, tena kamtaja kwa jina kamili! Sasa huyo mkuu akimshitaki huyo mwenye blog kwa kumfananisha na katuni, atajibu nini mahakamani? Kipanya ameweka ujumbe wake, tuliomwelewa tumemwelewa tulivyomwelewa, sasa huyo aliyejipa jukumu la kututajia jina la aliyechorwa kwenye katuni hiyo anatafuta nini? Mkuu Michuzi hebu tumia busara yako uwashauri hao wengine wenye mablog wasiyatumie kujitafutia matatizo yasiyokuwa na sababu, maana yakiwapata ya kuwapata wanaanza kulalamika, kumbe wanajitakia! Nifikishie pia hongera zangu kwa Kipanya, kazi nzuri hii!
ReplyDeleteDuh! Kweli hii ni lugha ya picha. Kwa harakaharaka nimepata tafsiri 19. Eti, kuwa Pinda si 'mtu' bali kitu kinachezeshwa na 'wazee' just kufikisha "blah blah" kwetu! Wadau malizieni hizo 18 na nyingine.
ReplyDeleteBig up Kp. Usiogope tindikali. Sisi yuesieidi, hakiilimu, michudhi n.k tutakupa shavu.
SEV
anon 3:49 umetulia
ReplyDeletenamie naongeza moja: si kwamba si mtu bali ni mtu coz anakichwa pale ila ni mlemavu. mikono na miguu yake ni vidutu,kwahiyo atabaki kuongea tuuu kama kawaida ya ........... tz tz tz
kp big up!!
brrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
ReplyDeleteyanii ni yale yale,ukweli mtupuuuuuuu...
ReplyDeletewatanzania tutafika kweli kwa mwendo wa mchanga machoni?
Ameanza kupyafa pwaya: Ufisadi ni kama "hydra" huwezi kuukamata kichwa! Lakini nayerudisha pesa za EPA (BoT) ni nanai? kama ni kuku, kamata huyo kuku!
ReplyDeleteTanzania inauza reli kwa Mhindi. Wafanyakazi wake wanalilia mishahara iongezwe. Tajiri anashindwa. halafu Tanzania, tajiri wa zamani, anakubali kuwaongeza wafanyakazi mishahara. hapa pia kunanuna ka-samaki!
Richmond wanasema ni kampuni kamili iliyosajiliwa Houston, Texas, Amerika.
Lakini haina ubavu wa kuleta umeme. mara inajigamba kuwa ina uhusianona General Electric ya Amerika. mara ina uhusuiano na Huwett Pachard?
Kwa nini balozi wa zamani wetu wa Amerika, Andrew Daraja, asisaidie kutoa ukweli? Yeye na Alex Massinda walishiriki katika Richmond Development Corporation!
Yaani mwataka kutwambia kuwa ofisi yetu ya ubalozi Washington haikuwa na habari?
Ok Na miye naongezeamo ko kwamba jamaa ni mshkakiz na aanaokwa na miwani yake tarrtiiibu...Sioni mwelekeo tafazalini tusaidiane nji hii inelekea pabaya kuliko kwa ba mkubwa Mu*abez...Ooh kajipu maswali ya papokwapapo.... kama vile bingo za vilongalonga.... ngachoka kapsa...
ReplyDeleteOk Na miye naongezeamo ko kwamba jamaa ni mshkakiz na aanaokwa na miwani yake tarrtiiibu...Sioni mwelekeo tafazalini tusaidiane nji hii inelekea pabaya kuliko kwa ba mkubwa Mu*abez...Ooh kajipu maswali ya papokwapapo.... kama vile bingo za vilongalonga.... ngachoka kapsa...
ReplyDeleteHapa mimi nahisi mafisadi wameshamuwahi huyu mheshiwa mkuu sana na sasa amebaki kutapatapa na punzi ndiyo zinaishia hapo kwa kusema blah blah blah!!.
ReplyDeleteDuh KP kiboko. Usiogope kwani katuni zako zinahamisha utendaji bora. Kimsingi mimi bado nipo pamoja na serikali kwamba hao jamaa warudishe fedha kwanza then mahakamani. Ndugu zangu mifano ipi mingi sana ya watu walioiba, wakashitakiwa na then mahakama zikawasafisha (sitaki kutaja majina ila kama wafuatiliaji mambo Tz mnaweza kuwafahamu baadhi). Kumbukeni ufisadi siyo BoT tu bali hata mahakama zetu haziko safi, polisi ndiyo usiseme na kwa hali hiyo tukianza kuwashitaki hizo pesa zitatumika kuwasafisha, mtashuhudia mafaili yakipotea, ofisi zikichomwa moto n.k. Watu wamejipanga vizuri sana na mtandao wao una kila aina ya wanataaluma na hapa serikali ingefanya kosa kubwa sana kama ingeanza mahakamani. Tumebakisha miezi michache ili tume imalize kazi yake na tuanze kuipa kibano serikali kwa maamuzi yake. Mimi nadhani serikali ikienda kwa staili hii, watu wataogopa kuiba pesa za umma
Michuzi huyo bloga mwenzio aliyetumia jina la mheshimiwa kwenye blog yake na kulifananisha na kikaragosi hiki hebu msaidie ushauri. Yeye anadhani Kipanya alipoacha kuandika majina humo yeye ni mjinga? Mbona ujumbe tumepata? Sasa huyu anamtafsiria nani? Mkuu akimshitaki kuwa kamdhalilisha kwa kumfananisha na kikaragosi atajibu nini? Hebu pitia ukurasa huu hapa halafu umsaidie ushauri mwenzio: http://drfaustine.blogspot.com/2008/04/kipanya-and-mizengo-pinda.html
ReplyDeletewabongo wengine sijui mnakunywaga nini? hakuna mtu atakae rudisha pesa au kupelekwa mahakamani, mambo haya yameanza enzi za nyerere watu wanaiba halafu wanajiuzulu na pesa walizoiba,mnamkumbuka augustine mwingira na wizi wa ATC kwa kununua ndege mbovu halafu wanaambia wananchi ni ndege mpya.
ReplyDelete