Tangazo la Msiba kwa wanafunzi wote wa Kazima Secondary school toka 1997 mpaka 2000
Kwa niaba ya familia ya marehemu ndugu yetu, kaka yetu, mwanafunzi mwenzetu enzi hizo za mwishoni mwa miaka ya 90 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2000.
Nasikitika kutangaza kifo cha kaka yetu mpendwa HUSSEIN JUMA MATOVOLWA kilichotokea kwa ajali ya pikipiki.
Mazishi yamekwisha fanyika tarehe 27.04.2008.
Habari ziwafikie wanafunzi wote wa Kazima Secondary School na wale wote walio soma nae katika shule ya Msingi Itetemia Tabora, Na ndugu na jamaa wote walio kuwa wakimfahamu kaka Hussein mahali popote pale walipo watakaposoma Ujumbe huu!!
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!!
Ipyana Ambele
Poleni sana wafiwa. Mungu amlaze marehemu mahali pema peoponi.
ReplyDeleteMie pia nimesoma kazima lakini miaka hiyo ya 80.
Mdau
UK
oh poleni sana wafiwa,jamaa na marafiki.nimesoma kazima from 1999-2002.chini ya uongozi wa makonda.
ReplyDeletepoleni sana ktk kipindi hiki kigumu,bwana ametoa na ametwaa
mdau