Peter Gachuma,Thomson Msigwa Wafariki Dunia.
Wanajumuiya wa UK tumepokea habari Ya kusikitisha za kifo cha Wenzetu Peter Gachuma na Thomson Msigwa kilichotokea leo huko Tanzania kwa ajali ya gari wakitokea Tarime (mara) kuelekea Mwanza.
Marehemu Peter Gashuma alikua akisoma university of Birmingham na kuishi Reading,vilevile Marehemu Thomson Msigwa alikua anaishi Reading Uingereza, Marehemu walikwenda nyumbani (Tanzania) wiki iliyopita kwa likizo fupi.Marehemu Thomson Msigwa ameacha mke na watoto.
Mwenyezi mungu azilaze Roho za Marehemu Mahali pema peponi Amen.
Tutaendelea kuwajulisha habari zaidi kadri zinavyotufikia..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. R.I.P Peter na Thomson!Poleni sana ndugu na jamaa za marehemu

    ReplyDelete
  2. No comments.BWANA ALITOA NA BWANA AMECHUKUA.POLENI WAFIWA WOTE WALIOKUWA ,NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU HAWA WAWILI.

    ReplyDelete
  3. Ni huzuni kubwa lakini sisi wote ni wasafiri wa kwenda mbinguni. Wametangulia tutafuata Amen.

    Naomba kufahamu kama Thompson Msigwa ni yule aliyemaliza Form IV Minaki 1992. Asante

    ReplyDelete
  4. Pole sana familia na wapendwa wa Peter na Thomson... Mungu awapumzishe kwa amani. Mapenzi yake mungu yatimie. Tuliwapenda lakini mungu amewapenda zaidi.

    RIP brothers.

    Mkwajuni

    ReplyDelete
  5. IT IS GREATER FORTUNE TO DIE HOME . THEY ARE VERY LUCKY OUTSIDERS

    ReplyDelete
  6. Jamani poleni sana Eliza Gachuma (sijui yuko wapi), Gati Gachuma (DC, USA), Edda Gachuma (DC, USA), wengine wote ambao siwakumbuku. Mwenyezi Mungu awalinde na kuwafariji.

    ReplyDelete
  7. My deepest condolences to all two families.
    And for all of us who still overseas,remember to hire a Tanzanian driver when your in vacation.Just because we've adopted different rules how we drive.So far we've lost more than 20 Tanzanians that i know,who died in car crashes while in vacations.This can be prevented.
    Rest in peace Peter and Thomson

    ReplyDelete
  8. Pole sana wafiwa,kaka yangu Frank Msingwa wa Houston naomba ukumbuke kuwa pamoja na kuwa kaka yako mpenzi amekutoka,jipe moyo na mweza wa yote atakufariji.Tunakuombea poleni sana.

    ReplyDelete
  9. Kifo cha Bw. Thomson Msigwa kitakuwa pigo kubwa kwa wananchi wa Makete na Njombe. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehema mahali pema peponi. Amina

    ReplyDelete
  10. Poleni sana wafiwa mimi ni rafiki wa karibu sana wa familia ya Gachuma familia hii imepata pigo sana ukizinitia Peter alikuwa ndio kijana wa kiume mkubwa,na huyu baba alishawahi poteza motot wake mkubwa wa kiume wa kwanza kwa ajali miaka ya juma na kwasasa amebakiwa na mtoto mmoja wa kiume kitinda mimba chake Emmanuel Gachuma, mdau aliyeuliza Eliza yupo wapi, Eliza yupo UK, Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, AMINA

    ReplyDelete
  11. Lucas KahungwaDecember 13, 2011

    Poleni sana familia ya Mzee Gachuma, na fammilia ya Msigwa. Hii ni huzuni sana ndugu zangu. Mwenyezi Mungu awafariji. Mungu aziweke roho za ndugu zetu waliotutoka mahali pema peponi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...