Ninatoa shukrani zangu za dhati kwa nafasi mlizonipatia katika blogu zenu ili kuweza kufikisha ombi langu la kupatiwa msaada kwa ndugu yangu (binamu) aliyekumbwa na tatizo la mdawa ya kulevya.
Wakati nikituma ombi hili nilidhani walionitangulia kiumri na mawazo katika familia wangenishambulia kuwa nimeaibisha familia kwa kulitangaza tatizo, lakini kumbe sivyo.
Familia imepokea kwa moyo wote maoni yaliyoandikwa kwenye blogu zenu.
Nimekusanya na kuorodhesha maoni endelevu kunako wakati nitayabandika katika tovuti ya nukta77.com ili iwe rahisi kurejea na msaada kwa wengine wenye tatizo kama hili.Ndugu zangu, kazi mnayoifanya si ya kuburudisha na kuhabarisha tu jamii, bali mnaokoa pia familia.
Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema na baraka akupeni maisha mema na kukufanikisheni katika kazi zenu!
Pokeeni shukrani zangu za dhati tafadhali Kaka Michuzi, Mjengwa, Ngowi na Dada Chemi!
Inshaallah,
Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye kutoa baraka,
asiwapungukie!
Subi
Kwa kweli hata mimi nakusadia kuwashukuru watoa ushauri, mungu awabariki. Cha maana kilicho nifurahisha hakukuwa na wapondaji safari hii, ushauri wao umetusaidia wengi, sio wewe peke yako, wengi tulikuwa hatujui cha kufanya kwa ndugu zetu ambao wame athirika na madawa, lakini labda tulikuwa tunaongopa tujitokeza hadharani na kuomba msaada asante kaka.
ReplyDeleteMKUBWA WANGU MIMI NILIONA TU ISSUE YAKO LAKINI SIJAITOLEA MAONI KWANI NAJUA KIASI GANI MAMBO HAYO YA MADAWA MATATIZO YAKE...SIJAWAHI KUVUTA LAKINI NIMEWAHI KUWA KARIBU SANA NA WATU WALIKUMBANA NA MATATIZO HAYO...NA NAJUA AINA ZOTE ZA MADAWA DUNIANI....NAKUPA POINT MOJA KUNA MADAWA AMBAYO UNAWEZA KUWA NA HOPE YA KWAMBA NDUGU YAKO ATAACHA SIKUMOJA,NA KUNA MADAWA AMBAYO UKIGUSA TU KUACHIKA KAZI,,,,KUNA DAWA AU UNGA UNAITWA MWEUPE UNATOKA SANA SOUTH AMERCA,AMBAO MATAJILI WENGI NA MARAISI KAMA KINA BUSH WANAUTUMIA AU AKINA MARADONA...HUO SIO KAZI KUACHA,,,NA KUNA UNGA UNAITWA EROINE UNATOKA PAKISTAN,HUO UNATUMIWA SANA NA WATU WA DUNIA YA TATU KWANI BEI YAKE SAWA NA KUNYWA BIA AU GONGO,,,HUO PIA LABDA LABDA KAMA KIFO AKIJAPITA KARIBU ANAWEZA KUWACHA....SASA NAKUPA UNGA UNAOVUTWA BONGO SASA HIVI...UNAITWA NUSU MZUNGU...MEANS SIO MWEUPE SANA WALA BROWN SANA,,,HIYO NDIYO INAVUTWA NA VIJANA HAPO NYUMBANI,,,,MKUBWA KAMA MDOGO WAKO KAANZIA NA HIYO BASI KAZI UNAYO...KWANI HUO UNGA UNAVUTWA SANA MAREKANI YAHANI UNAITWA NI BAADA YA UNGA WOTE MKALI DUNIANI NDIYO HUO....NA ANAYEGUSA UNGA HUO KUACHA NI KIHAMA...HIVYO FANYA UCHUNGUZI NDUGU YAKO ANAKULA KIMONDO GANI...KAMA NUSU MZUNGU TOKA TAHILAND KAZI UNAYO NA UTAMAILIZA HOSPITALI KAMA NYEUPE YA BRAZIL LABDA AFADHALI...MDAU 00316
ReplyDeletePole sana wakwatu, tatizo hilo ni baya na linaathiri sana vijana. Nashindwa kuelewa kwanini lisifanywe janga la kidunia, na hatua madhubuti zikachukuliwa, ikiwemo kuondoa kabisa uzalishaji wake! Kama wanaweza kupambana na ugaidi kwanini washindwe hili?
ReplyDeletem3