Kalunde kupamba Tuzo ya Kalamu

Na Mwandishi Wetu

BENDI ya Kalunde inatarajia kupamba hafla ya utoaji wa Tuzo ya Kalamu inayotolewa leo na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni Tanzania (CAJAtz).

Hafla hiyo imepangwa kufanyika Ijumaa hii kwenye Hoteli ya Peacock Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaa.

Katibu Mkuu wa CAJAtz Hassan Bumbuli, alisema washindi hao waliopatikana baada ya jopo la wataalamu kupitia kazi zilizowasirishwa watatunukiwa tuzo zao.

Alisema washindi watapewa tuzo, vyeti na fedha taslimu Sh 150,000 kila mmoja ikiwa ni kuthamini mchango wao katika sanaa.

Alisema kwa mwaka huu, CAJAtz imepangwa kutoa tuzo katika vipengele vinne kwa upande wa waandishi wa habari baada ya vipengele vingine kukosa washiriki.

“ Pamoja na tuzo na vyeti, mwaka huu washindi watapatiwa fedha taslimu kila mmoja ikiwa ni tofauti na mwaka jana ambapo chama kilitoa tuzo na vyeti,” alisema Bumbuli na kuongeza kuwa zawadi hiyo imeongezeka kutokana na kupata ufadhili.

Bumbuli alisema kuwa tuzo hiyo inafanyika kwa udhamini wa Benki M, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Sengerema Engineering Group, Serengeti Breweries, Afrika Sana na Kampuni ya Lips.

Alisema kuwa mbali na kutoa tuzo kwa waandishi pia CAJAtz itatoa tuzo kwa taasisi zilizotoa mchango mzuri katika kuendeleza fani za sanaa na Utamaduni hapa nchini.

“ Pia tutaoa tuzo kwa vyombo kadhaa vya habari ambavyo vimetoa mchango mkubwa katika kuandika na kutangaza habari za sanaa na Utamaduni kwa mwaka 2007, na pia taasisi mbalimbali ambazo kwa namana moja au nyingine zimeshiriki katika kuendeleza sekta ya Utamaduni hapa Tanzania,” alisema.

Hii ni mara ya pili kwa CAJAtz kutoa tuzo kwa waandishi, katika tuzo ya mwaka jana waandishi wa habari wanne na taasisi tatu zilitunukiwa tuzo hiyo yenye heshima kubwa na y a juu kwa Chama hicho ambayo imelenga kutambua na kuthamini mchango wa waandishi na vyombo vya habari na taasisi mbalimbali katika kuleta maendeleo ya sanaa na Utamaduni.

Pia tuzo hiyo inalenga kutoa changamoto kwa waandishi wa habari kupenda kuandika habari za kina Sanaa na Utamaduni ikiwa ni sehemu na njia muafaka ya kuutangaza Utamaduni wa nchi yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...