Wanafunzi wote ambao walisoma Ljs Morogoro Mnaalikwa kuudhuria katika kikao muhimu cha kujadili changamoto mbalimbali juu ya umoja wetu.
MAHARI: ROSE GARDEN
DAR ES SALAAM
MUDA:SAA TISA MCHANA
TAREHE: 1 MAY 2008
Watakaofika watapata kuonana na marafiki ambao hawakutegemea kuwaona tena na kukumbushana maisha ya Seminary

-- MR.Godwill Philip Matayi
Kamati ya maandalizi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Ndugu Godwil.
    kiswahili kigumu, sema Mahali ni Rose Garden sio Mahari ni Rose Garden. mdau UK

    ReplyDelete
  2. wee anony wa kwanza vipi?watu wengine mnapenda tu kutafuta kasoro.kwani ujumbe hujauelewa??kwanza huwezi kuwa mwana ljs.

    ReplyDelete
  3. Kuna watu ambao kazi yao ni kutafuta makosa tu!! hata kama ni mambo yasiyomuhusu yeye atatafuta kosa na kulieleza ili kwanza yule aliyefanya hilo kosa ajisikie vibaya halafu yeye apate umaarufu na kujisikia ametoa dukuduku lake...watu hawa mara nyingi wakikosolewa huwa wanakuwa kama Mugabe...ni wakali mno!!

    ReplyDelete
  4. Tatizo la kiswahili sanifu kwa Bw. Matayi ni la Kiasilia hivyo hamna haja ya kumlahumu cha muhimu ni ujumbe kufikia walengwa na kueleweka. hata hivyo kujifunza kiswahili sanifu ni muhimu Mzee Matayi- wazee wa Kuji Motel (bweni la Kujitegemea)

    ReplyDelete
  5. Jamani si kila mtu anajua hapo Bustani ya Waridi (Rose Garden) ebu wekeni hata huku chemba ya maoni namba au email ya mdau mmoja Mwandaaji, so Please Matayi weka email kwa ajili ya shughuli hii au email ya umoja ka ipo, ili wengine tujue tunafikaje na wengine nje ya Dar tunaweza book guest ya fasta na kuja hapo, hatari kitu gani...Tushalizwa mjini hapa wengine hatupo tayari kumuuliza yeyote swali barabarani! Dar Yenyewe hii ya wachawi wala watu Mhh

    ReplyDelete
  6. Duh kama vigozi na hanjumati za mama K zitakuwepo basi hiyo italeta kumbukumbu zaidi lakini mbaya ni sisi wanaljs tulioko huku ughaibuni tumeikosa hiyo.Tunatamani tungejumuika nanyi lakini ndo hivyo tena.
    Mdau wa Mapinduzi no 10

    ReplyDelete
  7. Jamani mdau wa UK yuko sahihi kuilinda maana ya MAHALI NA MAHARI
    unaposema mahari ni kitu tofauti na unaweza kuharibu au kubadili maana ya sentensi nzima na ukatoa ujumbe ambao unamaana nyengine na ulilokusudia kuwakilisha miongoni mwa watu.

    Anon Apr. 29 8:25 acha kumlaumu mdau hapo juu kwa kumkosoa Mr Matayi kwani kumwambia hivyo anajaribu kumsaidia ili afikishe ujumbe wake kwa walengwa kwa ufasaha(kwa kufahamika)sio kujitafutia umaarufu au kumuudhi mzee Matayi kama ulivyodhania.

    Tudumishe kiswahili sanifu na fasaha.

    ReplyDelete
  8. Nashuru kwa Comments zenu sorry mimi ni mkurya r na l siwezi kutofautisha.Simu ni 0784456343 na email ni matayigo@gmail.com

    ReplyDelete
  9. Kaaaazi Kwelikweli! Hao wanaoafiki mwenzao kukosolewa wanachekesha,maana wao wenyewe kiswahili chao kimepinda!
    Anony wa saa 9:06am hatusemi KUMLAHUMU bali KUMLAUMU. Nawe anony wa saa 10:37am hatusemi MAANA NYENGINE bali MAANA NYINGINE. Toa boriti lako kwanza kabla ya kibanzi kwenye jicho la mwenzako. Nawasilisha.

    ReplyDelete
  10. Ombi langu kwamba mgeni wa heshima awe Merisali a.k.a "Jaja" akisaidiwa na fundi mabomba wetu mzee Kirigila na nesi wetu maarufu Ndandala kwa ajili ya wale watakaozidiwa na vinywaji na mlo!
    Mdau DK

    ReplyDelete
  11. Nakubaliana kabisa na mdau aliyesema Jaja of Opobo awe mgeni rasmi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...