TAIFA STAAAZ IMEFANIKIWA KUVUKA KIGINNGI CHA KUSAKA TIKETI YA KUSHIRIKI FAINALI ZA KWANZA ZA MATAIFA YA AFRIKA KWA WACHEZAJI WANAOCHEZA LIGI ZA NYUMBANI MAARUFU KAMA CHAN BAADA YA KUILAZIMISHA SARE YA 1-1 TIMU YA UGANDA CRANES UWANJA WA NAKIVUBO HUKO UKWENI.
GOLI LA STAA LIMEPATIKANA DAKIKA YA 44 MFUNGAJI AKIWA ATHUMANI IDDI 'CHUJI'
HII NDO KUSEMA STAAZ INAPETA KWA MABAO 3-1 BAADA YA USHINDI WA 1-0 ILIYOPATA IKIWA NYUMBANI WIKI MBILI ZILIZOPITA. SASA TUNAMNGOJA MSHINDI KATI YA SUDAN NA RWANDA AMBAPO TUKIMSHINDA TUNAINGIA FAINALI YA KOMBE HILO ZITAZOFANYIKA IVORY COAST MAPEMA MWAKANI.


1+1=3? numbers bob.
ReplyDeleteNatubu kwa maximo na taifa stars sasa tunaelekea kunako.congatulation all
ReplyDeleteMagoli ya ugenini yanaanza kuhesabika mawili iwapo tu timu zitakuwa zimelingana kwa idadi ya magoli. Kwa mfano kama Stars wangetoka sara Dar ya 1-1 halafu watoke tena sare Kampala ya 2-2 hapo ndipo magoli ya ugenini yanaanza kuhesabika mawili na stars ingeshinda kwa mabao 5-4.
ReplyDeleteHayo mahesabu mwachie yeye na mwalimu wake wa hesabu sijui Bunge au wapi. Mimi naomba tu nifahamishwe kwa nini Uganda kuitwe ukweni? Naomba msaada kwenye tutazzz...
ReplyDeleteHesabu, hizo mwachie mwenyewe rafiki yangu mmoja alizoea kusema "hesabu tabu sana kujua...bora kuruwani".
Mwanzo mzuri kwa Stars. Inatia moyo. Nadhani ya matunda ya Maximo yanaanza kuonekana.
ReplyDeleteMdau
http://drfaustine.blogspot.com/
Sudan vs Taifa Stars. Hureee JK boyz ,sasa subiria "misifa wine" itakavyowalewesha jamaa zako.Utaniambia jinsi kina Mwakalebela watakavyozingatia kujaza uwanja badala kuhamasisha timu ishinde.Ningependa mchezo huo ufanyike Mwanza hapo Code D'vour kutaendeka kwani haya mashindano hakika ni rika letu kabisa.
ReplyDeleteGeoRge
kasheshe ipo kwa m sudan
ReplyDeleteGOLI LA UGENINI HALIWEZI KUWA APPLICABLE HAPO.
ReplyDelete125th. ST. HARLEM,NY,NY.
sasa mkaze but maana bongo fainali hiyooo muache mambo yenu ya kwenda bungeni kabla hata hamja pata tiketi yenyewe hamchelewi kwenda kuchangiwa pesa na huyo maxsimo aache maneno mengi mara kidogo anakwenda kuongea na raisi akuze kiwango cha soka kwanza la sivyo ataiona inchi mbaya hii
ReplyDeletedalali
Yeah kama kawaida wajitahidi tu watafika mbali sana maana kocha na yeye ni mzuri.Lakini mkuu Michuzi hapo sijaelewa mara ya kwanza walishinda 2 au 1 na kama walishinda 2 na ugenini wameshinda moja basi ni tatu na kama walishinda moja na away moja basi itakuwa ni 2 kwa 1 sio tatu kwa moja.Ok anyway wajitahidi tu kwa sana.
ReplyDeleteBro..michu...tunajua shemeji anatoko huko ndio maana ..unapunguza magoli...tulishinda 2-0.hahahaha
ReplyDeletehesabu bwana mwalimu wa hesabu anaanza mwanzo kingia class, kamahujawahi ku copy daftari la mwenzako matokeo ndio hayo mwanzo 1-0 leo 1-1 jumla 3-1 hahaahah! mwanzo ni 2-0 leo ni 1-1 sawa zote 3-1 hesabu za mpira hizo lakini, na wewe annon uliyesema 1+1=3 HUJAELEWA MICHUZI KAKOSEA VIPI POLE NA WEWE. taifa oyeeeeeee. wa pemba wanasema sie twapara samaki wao uganda waparamiwaaaa. kule MIWA mingi sana uganda.
ReplyDeleteMichuzi leo hakuna nanihii toka kwa my wife wako!!! mwenzio anasikitika wewe unafurahia, utakiona cha moto, hapo ni mzungu wa nne tu!! tehetehe
ReplyDeleteKaka Michuzi nahisi ni furaha ya ushindi iliyokusahaulisha mechi ya kwanza matokeo yalikuwa Stars 2 Cranes 0
ReplyDeleteHi Bro Michu,
ReplyDeleteHivi mzee mbona namba zinakukataa sana mkuu,kila siku wachanga habari ya matokeo hasa ya "Mguu wa kwanza"/First leg...!!!!.Ni kweli kuwa Taifa Stars iliifunga the Cranes 1-0 kwenye mtanange wa kwanza....??????!!!!!!.
Safi sana,na hongera sana wachezaji, viongozi na watanzania wote kwa mafanikio haya, na huu uwe ni mwanzo kwa mafanikio endelevu!
ReplyDeleteBwana michu hapo hesabu mbona haziendi vema?
ReplyDeleteanyway bora tumepita HONGERENI sana, labda hii tutacheza
kila la kheri taifa stars
Mungu ibariki Tanzania....
Nyaningedere
Starz wamesonga mbele kwa jumla ya magoli 2-1 maana cranes hawakutufunga goli tulipocheza ndani ya bongo.Timu zinapokuwa sawa sawa kimagoli ktk michezo yote miwili ndipo goli la nyongeza linapohesabiwa kwa timu iliyofunga goli ugenini.
ReplyDeleteMfano mechi ya kwanza ingekuwa suluhu ya 0-0 na hii ya pili 1-1 tungeongezewa goli na kuwa 2-1.
Ama mechi ya kwanza ingekuwa 1-1 na ya pili ingekuwa 2-2 kwa kila goli tulilofunga ugenini lingeopewa nyongeza na kuwa 4-2.
Heko Taifa Stars. Wadau hii timu inaitwa Taifa Stars. Haya mambo ya JK Boyz, JK Eleven, JK blah blah blah yanafanya timu ionekane kama vile ni timu ya kisiasa, ukizingatia inaitwa hivyo ikishinda tu, ikifungwa "Taifa Stars yachabangwa". Chonde chonde hii timu ilikuwepo toka enzi na enzi, tulio na mapenzi nayo hatungependa kuona inatekwa nyara.
ReplyDeleteSi mnakumbuka maswaibu yanayozipata sekondari zilizopewa majina ya wanasiasa?
HEKO TAIFA STARS!!! YEBA!
Mbigiri na wengineo ambao hamjui.
ReplyDeleteSheria hii inaitwa 'away goal rule' na sio 'away goals rule'. Sheria hii inatumika endapo timu zitakua na idadi sawa ya points na magoli.Hapo sasa atatafutwa aliyefunga goli nyingi zaidi ugenini ndie atakayesonga mbele!
Kwa mfano Tanzania 1 Uganda 1( Tanzania) marudiano Uganda 2 Tanzania 2 (Uganda).Matokeo ya jumla yangekua Tanzania 3 Uganda 3,Tanzania ingesonga mbele kwa faida ya goli 1 la ziada ililofunga ugenini( ugenini ilifunga 2 nyumbani ilifungwa 1,hivyo tofauti ni (2-1=1!). Pia kama ingekua Tanzania 4 Uganda 3 kisha marudiano Uganda ikawa Uganda 3-2 Tanzania,matokeo ya jumla yangekua 6-6,na Uganda ingesonga mbele kwa kua ilifunga goli 3 ugenini na kufungwa 2 nyumbani (3-2=1! i.e goli moja la ziada itahesabiwa mawili.
gEoRgE
Hii Comment kwa Al-Musoma Kuhusu Ukweni, Issa Michuzi anatumia neno Ukweni sababu ameowa huko Uganda kama sijakosea muulize michuzi, kama umepata msg utaelewa.
ReplyDeleteBado kabisa kutoka sare na Uganda ni upumbavu tu,huyo maximo anaendlea kutuletea hadithi tu sare na kufngwa...haya tusubiri tuone...
ReplyDeleteHongera taifa stars na michuzi..kazi nzuri
ReplyDeleteWabongo tuna matatizo ya kurithi; Kwa taarifa yako itakuwa jambo la kihistoria kupita awamu inayokuja!!! Mara nyingi tunashindwa awamu hiyo yenye tension... ulimi huo unatoka... kwa kuwa tunacheza wakati tunafikiria mijisifa tutakayopata baada ya mechi kutoka kwa Mh. Rais na Mabibi zetu wa mtaani....
ReplyDeleteHizo awamu huwa siku zote tuna-chachawa... na kushindwa
mechi ya Kwanza (Dar es Salaam) Matokeo: Tanzania 2 Uganda 0
ReplyDeleteMechi ya Pili (Kampala)
Matokeo: Tanzania 1 Uganda 1
Matokeo ya Jumla: Tanzania 3 Uganda 1
Kocha huyu Maximo naona bomu sana. anamtaka kipa ambaye hana uwezo IVO MAPUNDA.
ReplyDeleteTIMU HII INASHINDA KWA KUDRA ZA MWENYEZI MUNGU.
MAXIMO SIO KOCHA NI BOMU ALISEMA HAWEZI KUCHUKUA MCHEZAJI TIMU YA TAIFA MWENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 24. SASA TUKITIZAMA WACHEZAJI KAMA DROGBA ANA MIAKA 30, KOLE TOURE,GALLAS ANA 30.
LAMPARD 29,BALLACK MICHAEL 30,MAKELELE 34,HENRY ANA 31,KANU 30s,john TERRY 27,GERRARD 27.BECK HAM DAVID 32.ANELKA, HUKO BRAZIL KWENYEWE GILBERTO ANA 30. ROBERT CARLOS, CAFU ALIKUWA NA 33,GATUSO,ZAMBROTA N.K
HUYU SI KOCHA KILA SIKU ANABADILI WACHEZAJI.
HATUFAI
Misupu.huyo anony wa 2:48A.M aangalie hasije akajinyonga sababu ya chuki kwa maximo zisizo na msingi.Pia naomba nimsaidie kwamba ni bora kuwa na huyo golikipa anaemsema hana uwezo lakn ni mwenye nidhamu kuliko kuwa na yule mwenye uwezo hasiye na nidhamu (Huyo golikipa wanaemtaka ni kweli alishangilia sana siku Senegal ipoifunga Taifa stars kule Senegal) na ripoti yake ilifika TFF na ndio maana anaonekana kama msaliti na asie na uzalendo.Ila akikiri makosa yake na kuomba msamaha kwa watanzania anapaswa kurudishwa lakn akiendelea kufuata maneno ya washabiki wake tutamsahau.
ReplyDeleteSuala la umri wa wachezaji halina ubishi kwamba kila kocha anaangalia future ya timu yake.kutupangia list ya wachezaji na umri wao haisaidii sana kwani hao wote anaowataja wanaelekea kustaafu na kibaya zaidi ni kwamba uwezo wao umefifia ukilinganisha wakti walipokuwa na miaka 22 kurudi chini.
HIVI HAWA NI TAIFA STARS AU DAR YOUNG AFRICAN?? MAANA NAONA MAVITUZ YOOTE YANAONYESHWA NA VIJANA WA JANGWANI DAH YANGA BWANA RAHA TUPU.....
ReplyDeleteNGOJA WADAU WAOSHA VINYWA WA SIMBA WAAMKE HUKO