
SEKONDARI YA TAMBAZA YAJIANDAA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA KUZALIWA KWAKE
Shule ya Sekondari ya Tambaza inatimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake baadae mwaka huu na inatarajia kufanya sherehe kubwa kusherehekea jubilei hiyo kwa kuwaalika wanafunzi na wafanyakazi wote waliopita hapo.
Tambaza ni shule yenye historia ndefu na ya kusisimua katika rekodi za kitaaluma nchini Tanzania.
Kwa minajili ya kuadhimisha miaka hamsini ya kuanzishwa kwake, Bodi ya shule pamoja na uongozi wa shule umedhamiria kufanya sherehe kubwa ambayo itawashirikisha wanafunzi waliosoma Tambaza na watu waliowahi kufanya kazi Tambaza katika vipindi tofauti.
Madhumuni ya kufanya maadhimisho haya ni pamoja na:
(i)Kusherekea jubilei ya miaka 50 ya shule
(ii) Kuwakutanisha watu mbalimbali waliosoma na kufanya kazi Tambaza katika vipindi tofauti
(iii) Kuhamasisha wanafunzi wa zamani wa Tambaza kuchangia maendeleo ya shule na hivyo kuibua mwamko kwa wananchi kuchangia maendeleo ya shule mbalimbali
Bodi ya shule pamoja na uongozi wa shule utafanya kikao cha maandalizi ya maadhimisho ya jubilei ya miaka 50 tarehe 11/5/2008 saa nane mchana hapo hapo shuleni Tambaza.
Kikao hiki ni cha wazi kwa wanafunzi wote waliowahi kusoma Tambaza. Hivyo kupitia taarifa hii tunawaalika wanafunzi na wafanyakazi wa zamani wa Shule ya sekondari ya Tambaza kushiriki katika kikao hiki.
Historia fupi ya shule ya sekondari Tambaza:
Shule ya Sekondari Tambaza ipo katika wilaya ya Ilala mkoa wa Dar-Es-Salaam. Shule hii ilifunguliwa mwishoni mwa mwaka 1957 na shirika la Elimu la Aga Khan, ambapo Udahili wa kwanza ulifanywa mwaka 1958.
Shule ilifunguliwa rasmi ikiwa na wanafunzi 117 wa ki-Asia wavulana.Baadae shule ilitoa mafunzo ya kidato 1-4 wavulana na kidato cha 5-6 wavulana na wasichana.
Miaka ya 1970 shule ilichukuliwa na serekali na katika kipindi hicho kulikuwa na wanafunzi 273 kidato cha 1-4 wavulana na 5-6 wanafunzi mchanganyiko. Mwaka 1994 shule ilibadilishwa na ikwa inatoa elimu kwa wavulana na wasichana kwa kidato cha 5 na sita tu.
Kwa sasa shule ya sekondari ya Tambaza ina idadi ya wanafunzi 1,000 wavulana kwa wasichana kwenye michepuo minane ya: PCM,PCB,CBG,PGM,EGM,HE,ECA na HKL.
Katika kipindi cha miaka 50 ya kutoa elimu, shule ya sekondari ya Tambaza imefanikiwa kutoa madaktari, mainjinia, marubani, wanasiasa, wahasibu, wachumi, walimu na kada nyingine mbali mbali katika taifa letu.
Wenu katika Maandeleo ya Taaluma
Nicolas James Buretta
Mkuu wa Shule
Da chama letu hilo, makonda walikuwa hawafurukuti kwa vijana waTambazo enzi hizo, wanafunzi wa DSM si wa primary wala sekondari walikuwa wanaona Tambaza mkobozi wao, mara baada ya zali tukahamshwa na kupelekwa mikoani!! baada ya kuwachapa vijana wa Azania waliokuwa wana mchapa mwanafunzi mmoja mmoja,SHULE PEKEE AMBAYO KWA HALI YA SASA YA UFISADI WANGEWEZA KUFANYA JAMBO FULANI!! ama kweli serikali ni sirikali waliliona hilo mapema.
ReplyDeleteShule Bomba, tatizo kuu kipndi hiki ni ukosefu wa walimu Commited na mazingira mabaya ya kujifunza. Inasikitisha kuona Waalimu wazuri na wachapa kazi wamekuwa wakibaguliwa, kudhalilishwa na wengine hata kuhamishwa kwa FITNA za Mkuu wa shule na kusogeza walimu wake wa VODA FASTA na kusababisha shule kupoteza muelekeo wake kielimu kama ilivyokuwa kwa wakuu wengine waliopita KUMBUKENI: TAMBAZA MNAYOISHABIKIA SIYO HII TULIYONAYO YA MATOKEO MABOVU. Tusaidieni nasi tusome na kufaidi kama nanyi.Form six mtarajiwa Tambaza 2008
ReplyDeleteDiii! hii mwake mwanangu, enzi hizo bwana Father K, mwl.Shija, Mishako Andre, Mwl. Mdemu, mwl. Damas, mama Singano, mama Kilembe (mkali wa namba) mwl. Abiud, Mwl. Gupoloma n.k ah! simchezo. Akina Shetani, Okello, Kichele, Billy Singano, Dr.Edmund Ndalama, Benno Evance, Amandus Manda. Ni watu wazito mno kwenye mfumo wa sasa ni lazima ikumbukwe hiyo. Ni muhimu kuandaa mkakati wa maksudi ili kuhakikisha sherehe inafanikiwa na kunakuwa na mafanikio endelevu.
ReplyDeleteTambaza tunaibeba Mioyoni mwetu
ReplyDeleteNaomba niungane na wenzangu wote wenye nia njema ktk maazimisho hayo ya miaka 50 ya Tambaza.
Kwa wale tulio ughaibuni tunajisikia furaha kubwa kuona mkakati huu ukiendelea na tunaomba liwe ni jambo la kudumu na tuko tayari kushirikiana bega kwa bega.
Pamoja na umbali tuliokuwapo, bado tunaibeba Tambaza na Tanzania kwa ujumla mioyoni mwetu na tunajihisi fahari kuitwa Wanatambaza na Watanzania.
Tambaza imetulea na ikatupa chachu ya kusonga mbele zaidi na tunaiwakilisha vyema.
Bado tunaikumbuka ile motto; 'TAMBAZA- Tazama Mbali Zaidi'
Kila la kheri wadau wote katika kufanikisha siku hii adhimu.
Waziri Kindamba- Former Head-boy
wewe Anonymous wa 8:56 AM utakuwa umetoka Tambaza mwaka 1989, na ulisoma na Akina Kikoti, Paulo Kaigarula, Kwipojera, Arthur Ganai, Kichele, Isack Jeremia, Eugen Mollel,
ReplyDeleteSamwel Mkumbo na wengine wengi. Jamani Tambaza ilikuwa shule nzuri sana, kwa wale mliosoma hapo mnajua ukweli huu.
Katika shule ambazo zilikuwa tishio. Tambaza walikuwa kama mtoto wa baba mmoja. Miaka hiyo kulikuwa na zile kaptura za Grey mimi nilifika enzi zile H/Master akiwa anaitwa Moshi. Mtu yoyote ambaye amepitia Tambaza lazima awe mjanja. Wako wengine walioharibikiwa lakini bado Tambaza ni familia moja. SAMBUKILE ............TAMBAZA
ReplyDeleteTAMBAZAAAAAAAAAAAAAAA ENZI ZETU BWANA UKIPITA WATOTO WA JANGWANI NA ZANAKI WALIKUWA WANATUOGOPA KWA VIPONDO! YAANI MPAKA WANAFUNZI WAKAGAWANYISHWA MIMI MWENYEWE NIKIWA MMOJA WAO NILIPELEKWA KANTALAMBA! NATAMANI SANA NIONANE NA WANAFUNZI WENZANGU WA TAMBAZA: (Tazama Mbali Zaidi')
ReplyDeleteDENTI
VIpi Kindamba upo mpenzi uko wapi siku hizi bado london au tunawasiliane basi mimi nipo northampton sasa najua unaelewa ni nani
ReplyDeleteHongera sana Tambaza! Publicity mbaya miaka ya 90 lakini vichwa vizuri!
ReplyDeleteWako wapi kina; Salma, Kuhunga, Puja, Kulinga, Bashir, D-Kilato, Said Dongo, sister Lucy, Ajuza, wana Tambazana lol na wengineo?
PCB - 1993
Tuwasiliane,
dr Imani Kyaruzi - Bham
Dah mheshimiwa issa michuzi aaah!! umetuletea shule ya wachumba zetu Tambaza, ama kwa hakika kwanza walikuwa vibonde wetu, namkumbuka kijana Ally bitebo aliwabeba mwaka wetu akawatoa nao wakaonekana wapo ndani ya ulimwengu wa elimu. kwa kifupi mheshimiwa J K Kaaaya headmaster ambaye yuko minaki ndiye chanzo cha kuiharibu shule hiyo na sasa anaiharibu minaki.
ReplyDeleteStephen Nyagonde,
University of Dar es salaam,
Dar es salaam.
Tambaza!?
ReplyDeleteShule hii nayo imetoa vigogo wengi
katika fani ya siasa,michezo n.k
wakiwemo marehem Kaka!Brother Ukiwaona Ramadhani Mwishehe wa Ditopile Muzuzuri,Marehemu John Garang (SPLA) wa Sudan!!?naye alisoma hapo.Lakini wengi hawajui kwa nini jina shule hii hilipewa jina la Tambaza?! jina hili ni la mojawapo ya wazee maarufu jijini,Marehem Tambaza ambaye ndiye aliokuwa akimiliki shamba au eneo hiliopo shule hii,na alilitoa ijengwe shule ya H.H AGA KHAN Sec ambayo Shule ya Msingi Muhimbili,na upande wa pili ni Shule ya Tambaza
Kulikuwa na teacher mmoja anaitwa Oluoch alikuwa noma kweli. Watu tumekwenda kujirusha Bilicanas, yeye anapita kukagua wasiokuwepo vitandani.
ReplyDeleteTAMBAZA HONGERA KWA KIFIKISHA MIAKA 50. UJANJA WOTE ULE WA MIAKA YA 90. KUMBE TATIZO LILIKUWA MNAPATA MIFADHAIKO KWA UHABA WA WASICHANA; JAPO WA KUSAFISHA MACHO..KAMA AZANIA…!! TANGU SHULE IMEKUWA YA MCHANGANYIKO, TAMBAZA WAMEKUWA MABISHOO SANA.
ReplyDeleteBIG UP AZANIA.
Duh kuna jamaa kanikumbusha mbali, Mwalimu Abihudi. Huyu alinichapa akanichana mkono, alikuwa akifundisha sasa akakasirika kwa lililotokea, akatoka nje akaokota gongo na kutuchapa wote. Da namkumbuka Mwalimu wangu wa Historia, sijui yu wapi sasa.
ReplyDeleteKheri Mtanga, Charles Mwishema, James Tuvana, Samwel Manase, Salim Wasia, Ramadhan Juma, Nzagi Nyakirang'anyi, Mabuli Kahwa, Edmnund Lawrence wa Form 4 M 1992 mpo?
we uliyepelekwa kantalamba unanishtua nani wewe!! nilipelekwa umbwe mkuunilikuawa group2 ,lebo za kijani, SAMBUKILE TAMBAAAAAAAAAAZA. GOOD MEMORY , MISS YOU GUYS.Mwalimu nyau yuko wapi??
ReplyDeletemdau
Canada
Michuzi naona una lako.Miaka yote unaweka shule mbalimbali isipokuwa AZANIA tu.Hii ni mara ya pili au Tatu unaweka hawa wanywela wetu.Vipi michu,ulisoma Tambaza ama kuna mtoto wako alisoma Tambaza nini?Tuwekee Picha ya mababa wa kazi jijini Dar,Azania.tujikumbushe tulipotoka.
ReplyDeleteMI NAULIZA ATC ITAKUWEPO BAADA YA KIKAO? MAANA HII ILIKUA NDEGE YETU MAALUM KABLA YA TIME KAMILI YA KUTOKA. WALE WA MIAKA YA 84,85 MPAKA 89 NAFIKIRI MNAIKUMBUKA HII NDEGE.
ReplyDeleteyuko wapi Mwalim Nkya?
ReplyDeleteWee Anonymous wa saa 10.34 am yuko wapi Sam Mkumbo jamaa alikuwa mkali sana Darasani, alikuwa na ndugu yake Arnold Nzali nae alikuwa mbaya wa Chemistry, Juma Karia, John Gacha, Juma Karia wako wapi? walikuwa namshikaji wao Asimwe Kabunga hawa jamaa walitesa sana Bilicans ana kijwe chao Mkwepu Street, wako wapi hawa watu?? please nijulishe.
ReplyDeleteMdau,
Denmark.
Jamaa hapo umenikumbusha SAM Mkumbo alikuwa Mchafu darasani, jamaa poa sana,Kama unafahamu yuko wapi tunaweza kupata contacts zake, hey GACHA, NZALI mko wapi Juma Karia.Nimekumbuka Mbali saaaaaaaaana.
ReplyDeleteAhaa TAMBAZA weeee! Hii shule imebeba sehemu kubwa ya maisha yangu! Nimesoma hapo toka form one mpaka six! Nayakumbuka sana maisha ya pale kuanzia kielimu, kimichezo na burudani zingine. Ile mixture ya wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali ilinifanya nijifunze mambo mengi sana. Ningekuwa bongo, ningehudhuria, nawatakia kila la heri katika hiyo jubilei. Michuzi tutakuomba tena picha za hiyo sherehe, at least I will be able to see some of my friends.
ReplyDeleteMdau,
Gothenburg, Sweden.
Yuko wapi Mwl. Warioba wa Physics A level? Kuna siku assembly ya Jumamosi aliamrisha Mguu Upande watu wakacheka (People were not use to magwaride)
ReplyDeleteThen kulikuwa na Mwl. Marmo (Ukome...)nasikia alihamishiwa Pugu..
Then alikuwepo 2nd Master wakati wa Father Kalu kwa jina Mwaipopo a.k.a Willy Gamba...Mnamkumbuka?
Then kulikuwa na Mwl jina nimesahau (a.k.a Mwl Mzuzu) alileta mtafaruku mpaka akina Marehemu Big Papa wakasimamishwa shule!
Sijui So much simple yuko wapi kwa sasa
Hivi Mzuzu Club ipo? Na wanachama Wapo?
Tambaza imetoa various products including akina Papa Musofe! Tunategemea kumuona kwenye mkutano on 11th May 2008!
Do you remember lile gari (I think ilikuwa Datsun pickup) la supplier alikuwa analeta ndizi mbivu then zogo linaanza lilikuwa limeandikwa kwa nyuma "Mzimu wa Mhyao"? Lilikuwa very popular!
Enzi hizo Tambaza ilikuwa Tambaza I do not know what is happening now!
Tuwekee wanamume wa kazi Pugu boyz michu usituwekee matozi haya,weka shule zenye akili bwana ala!
ReplyDeleteEx-Pugu boy,Philadelphia
Mheshimiwa Michuzi tunashukuru sana kwa kuiweka hii habari , imenikumbusha enzi hizo safu ya walimu iliongozwa na Brother Felix Kalumuna, Professor Mwaipopo, Khan Mzee, Khan M...e, Mrs 'african pride' Mdemu, Iron Lady Shija,Dictator Mzuzu, Colonel Sindato,Miss Juma, Mama 'strict' Singano, Mrs 'calculus' Kilembe (tutafurahi kuona picha zao)
ReplyDeleteKwenye wanafunzi alikuwapo marehemu big papa na marehemu nyau, shetani, so much simple, dennis mdoe,
Vyama vya ATC (air tambaza) na TISA bado vipo???
Kuna alumni kibao wametapakaa tanzania na dunia nzima mmoja ni mheshimiwa waziri dk Mwinyi.
Kila lakheri na tutumieni picha, na basi uongozi utumie fursa hii angalau kuanzisha website ya alumni, kuchanga pesa za kusaidia vifaa na rangi ya shule, i hope kamzizi cha ufisadi hakitakuwepo au itakuwa kama alivyosema anony wa kwanza.....
Mdau Middle East
Bennedict Ndomba,Joe Tungaraza,Kalokola,Daniel Kighuha Chacha, David Kihiyo,Iddy Nzaro,Paul Besha,Godfrey Makalla,Raymond Charles,Salehe Marijani, Chacha Marwa, Kasinde Umelle, Victor Akili,Bro KITTO,Prosper Mambo,Makulilo Kasela,Bakari Jamal,Deogratius Mathias,Steve Maonyesho,Brozameni Jeremiah wa Tabata, James Ruge,Allan Mphuru,
ReplyDeleteSudi Ali,John Massawe,Simmon Mengere,Emmanuel Mfundo, Kasambula,
Wooote wako wapi?
Kama Kamanda hapo juu ulivyonena....Bro Misupu tuwekee Azaboyz mkuu. Watoto wenyewe wa Kwayu. Tambaza mnakumbuka mechi za airwing?..lazima mpigwe bao halafu mtembee kwa mguu hadi uwanja wa ndege kupanda chai maharage! hamkuwa na hela ya kukodi kosta!! Hahahaha.....
ReplyDeleteJamani Bro tunashukuru kwa hii taarifa ni ya kufurahisha sana, Kuja mwalimu wa Biology Mama Mbele alikua anatunyanyasa sana wanafunzi wa CBG lakini poa tuu tulifaulu karibu darasa zima si kwa shukurani yake hata kidigi kila siku alikukua anatubebsha viti tukasome darasani kwake PCB badala ya kwetu alikua anatuita MAPARASITE lakini tumefika mbali sana wengi OYA CBG ya 1998-2000
ReplyDeletelazima tuone imefika wapi shule yetu. nA MWALIMU KABIKI wa Geo alikua anapenda sana wanafunzi wote........... VIVA WU-TAMBA BOYZ MPO........NAJUA WENGI MKO MAJUU
Hii bomba Michuzi ' umenikumbusha mbali sana na ni kweli nilipita karibuni hapo TAMBAZA nusunilie ningekuwa nauwezo ningepiga rangi shule yote NASHUKURU UONGOZI KUTUKUTANISHA SOTE TENA??? hELLO WANA KISAMBUKILE TUJUMUIKE KUENZI SHULE YETU KUFANANA NA HESHIMA YA SASA TULIYOKUWA NAYO SASA
ReplyDeletetAMBAZA HOYEEEEEEEE??? KILA ANALIKUBALI CHAMA
hey Tarehe May 08, 2008 12:56 AM, Mtoa Maoni: Anonymous,
ReplyDeleteNasikia Anorld yuko Bongo, Sam Mkumbo yeye yuko Houston Taxes, siku nyingi, alikwenda alipomaliza chuo India
Asimwe Kabunga anaishi Australia Miaka Mingi, Huwa anakwenda sana USA , uki m google anakampuni yake eiq.net.au.
Peter Kintu nasikia yuko Rwanda
Sema Mshikaji wao yule Nelson John(AKA kwatu, Easy E) alifariki mwaka huu dar, Yeah Jamaa walitesa sana wakati hule pale Billican.
Je tukitraka kutoa donation kwenda tambaza tukutumie wewe Michu au tumpelekee mwalimu wa tamnbaza?
ReplyDeleteAsante
Sijui kwa zali gani nimesoma leo kuhusu JUBILEI ya TAMBAZA!!!!!!tangu mwaka 2008!!!!wala habari nilikuwa sina; Anyway nilikuwa nataka tu kumjibu huyo "anonymous" ambaye anaulizia habari zetu halafu yeye anajiweka "anonymous"!!!!si ajabu hii, jee tutampaje habari?
ReplyDeleteKama anataka habari zangu mie ni juma KARIA, lazima atakuwa ni mtu aliyemaliza mwaka 89 au?