Jumuiya ya watanzania Washington-Dc inayofuraha kuwatangazia kuwa kutakuwa na mkutano wa hazara utakaofanyika siku ya jumatano, tarehe 05/14/08.saa 6.00pm ambapo Rais wa Zanzibar mheshimwa Amani Abeid Karume atahutubia.
Watu wote ambao wangependa kuhudhuria mkutano huu wanaombwa kujiandikisha majina yao na namba za simu kwa kupitia anuani ya Barua pepe Tanzaniadc@gmail.com kabla ya siku ya ijumaa 05/09/08 ili kuweza kuandaa mkutano na sehemu ambayo mkutano utafanyika.Kwa wale ambao hawatojiandikisha hawataruhusiwa kuingia.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na
Rais wa jumuiya Stephano Mhina 443-278-6119
Katibu Mkuu Khalfani Lyimo 202-468-8312
Mweka hazinaKenyatta mayanga 240-565-8289
Asante!
Association of Tanzania Washington-Dc
Itumieni fursa hiyo kumwuliza Karume kinacho mfanya ashikwe na kigugumizi linapokuja suala la kuunda serikali ya mseto visiwani zanzibar baina ya CCM na CUF ni kitu gani,ikitiliwa maanani kwamba Pemba nzima inamilikiwa na CUF na Unguja nayo inamilikiwa na CCM japo kiasi fulani cha CUF kipo pia Unguja?Hili jina la serikali ya mapinduzi litakwisha lini?Hayo mapinduzi bado hayajaisha katika mfumo wa sasa wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa? Msisahau kutupasha jinsi alivyo yajibu maswali hayo mawili.
ReplyDeleteJifunzeni Kiswahili sahihi nyinyi watu wa DC, sio Mkutano wa Hazara bali ni Mkutano wa Hadhara. Lugha yetu ya Kiswahili ni nzuri mno na inayomfanya mzungumzaji awe na lafudhi ya kuvutia lakini nyinyi wakuja kutoka milimani ndio mnaiharibu.
ReplyDeleteJamani jamani mbona watu mnatuharibia lugha yetu kila kukicha? sasa hazara ndio nini? ni mkutano wa hadhara! halafu kuna cha kuchekesha pia, huu umeitwa mkutano wa hadhara sasa kwa nini atakae kuhudhuria ni lazima ajiandikishe? Hiyo sio maana ya Hadhara, angalieni kamusi na utaona kuwa huu mkutani unatakiwa kwa yeyote atakaye, sio kwa mwaliko au kujiandikisha unatakiwa kuwa open to anyone, yeyote apitae akauona anaweza kukaa na kusikiliza! Tusivuruge lugha yetu jamani!
ReplyDeleteWatu wa Washington DC mie nawasifu MKO JUU, pamoja na makosa madogo madogo lakini angalau nyie mmetumia Kiswahili safi sana. Hayo makosa madogo madogo yanarekebishika hongereni sana kwa hilo asiwadanganye mtu 'titi la mama litamu' na 'mdharau kwao mtumwa'. Endeleeni na moyo huo huo wa kutumia kiswahili kwa mawasiliano waacheni hao wazungu weusi wasiotaka kiswahili. Hongereni sana Tanzania Association of Washington DC kwa kutumia lugha yetu tamu na mwanana ya Kiswahili.
ReplyDeletejamani hata kama kunamakosa lakini naona ujumbe tumepata. Maana sidhani kama kuna binadamu ambaye anajua kila neno katika lugha yake au wakati mwingine ni makosa tu katika uchapishaji.Mfano mzuri ni huyo jamaa mtoa maoni wa tatu, amewakosoa wenzake'tusivuruge lugha yetu' wakati hata kuandika mkutano hawezi(mkutani)sikulaumu ila jaribu kuwa positive.ili tuweza kufika kwenye maendeleo.
ReplyDeletejamani tutumie fursa hii kufika na kuuliza maswali na ili tujue mambo yanaendelea vipi huko visiwani. Asanteni wanajumuiya kwa kutufikishia ujumbe!
ReplyDeleteKwa kweli fursa hii ni nzuri sana lakini swali linarudi palepale yaani mpaka ujiandikishe?kama ni michango simtuambie tu maana watu wa dc mizinga mingi sana madai umoja hauna pesa maana ya mkutano wa hadhara ni nini?
ReplyDeleteSababu ya kujiandikisha ni kwa ajili ya kuandaa ukumbi ambao utaweza kutesheleza watu, na kuandaa vinywaji na vikorombombwezo vingine lakini hakuna mchango wowote unaohitajika.
ReplyDeletefungueni website ya umoja wenu mnatia aibu wabongo wa dc
ReplyDelete