Kaka Michuzi,
Naomba msaada wako na wadau wote kuhusiana na hili suala la Mirungi.


Kwa ufahamu wangu ni kwamba Mirungi ni kilevi ambacho si halali kutumika ndani ya mipaka ya Tanzania. Jirani zetu Kenya na Ethiopia pamoja na Somalia hili ni zao la biashara.


Sasa kaka mimi tatizo langu ni jinsi hii mirungi ilivyokuwa common hapa Arusha, yaani hakuna dereva na kondakta wa daladala ambaye hatafuni mirungi (kama wapo wasitumia ni wachache sana) na hata inavyouzwa ni wazi kabisa hata huo mtaa baadhi ya watu huuita ni mtaa wa mirungi.


Kwa kweli hii hali haifurahishi kwa sababu wanausalama wanapita hapo na huzungumza na hao wanaokula hiyo mirungi ambao wengi wao ni vijana wadogo sana na nina wasiwasi kwamba labda wengine wa hao wanausalama pia wanatumia hiyo hiyo mirungi.


Naomba kaka na wadau mniambie kama serikali ilisha ruhusu matumizi ya mirungi ili na wale tusiotumia tuanze kujifunza.... Lakini inakera, njoo Arusha ujionee mwenyewe!!


Mdau Arusha!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2008

    wewe inakuhusu nini umbeya umbeya tu?? eti kilevi?? bora mirungi au pombe... pombe inaweza kusababisha ajali,fujo n.k lakini mirungi/miraa/gat inasaidia sana ndo mana madereva wengi huitumia kwasababu inakufanya u-concetrate na ukitaka kukesha basi mirungi inakusaidia kukaa macho...hii pia inawasaidia walinzi(nightwatchers).. pia inakusaidia kitandani kama una mke/mchumba (nafkiri utakuwa umenielewa hapa)... pia ni nzuri kwa wenye kisukari...hebu niambie sasa, hapa uingereza penyewe ni LEGAL(HALALI).. sasa hebu niambie nchi kubwa duniani kama hii ihalalishe mirungi kwani hawana akili ama?? mirungi haina ubaya wowote...ni MREMA ndo aliekataza mirungi kwa sababu zake mwenyewe... MIRUNGI kitu safi bwana! wadau msimsikilize huyu...!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2008

    ndugu mpendwa unayouliza juu ya uhalalishaji mirungi Arusha au popote pale Tanzania, kwani wewe umeona mirungi tu ndio kitu kinachouzwa hadharani kisichoalali? kuna bangi, dawa za kulevya na vingine vingi, lakini mimi ninaona tusizubalie mirungi wakati kuna watu wanao kaa na njaa wasio jua hata jioni watalalia nini?? kuna mambo mengi sana yanayoikumba Tanzania na mikoa yake yote ambayo yanahitaji kipao mbele, kama barabara,umeme, dawa za matibabu na kadhalika..Tanzania bado tupo nyumaa sana kimaisha inasikitisha sana. Asanta sana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2008

    BESTE NIAJE, HAINA YOTE HIO YA VILEVI UMEONA MIRUNGI NDIO INAKUKERA SANA?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2008

    Gomba,Miraa ni majina maarufu ya kuweza kuinogesha na kuipamba Mirungi.Kama ilivyo bangi na majina yake mengi.Mirungi ina aina zake kama kangeta ,giza na hutofautiana kwa bei kutokana na majina yake.Gomba husagwa na pipi nyeupe,Big G,Coca cola,au sigara.
    uwezo wa kutengeneza Taksima huweza kuleta handasi kwa haraka sana.kwa wakazi wa Arusha Mirungi ni kitu cha kawaida sana kwa miaka mingi sana na imetumika zaidi kama sehemu ya kumfanya mtu akae macho kwa kukosa usingizi huku akiendesha gari au kufanya bishara zinazohitaji masaa dhaifu.
    Kadri muda ulivyozidi kwenda na watu kuzoea matumizi ya mirungi,haijawa swala la kutisha na kuchukuliwa kama swala la utumiaji wa miharadati katika Jiji wa Arusha.Imekuwa kama vile watu wanavyokunywa kahawa sehemu za Pwani,kunywa Togwa,kula Ngisi.
    Sababu za jiografia na ukaribu wa mji wetu na maeneo yanayozalisha Mirungi,tumejikuta katika wimbi la utumiaji wa Mirungi.Kama mtoa mada alivyoeleza ya kwamba Mirungi ni biashara,basi biashara hiyo inafanywa na watu na watu wamehama nayo toka huko wanakoilima na kuileta mjini kwetu.Je nitakuwa siko sahihi nikisema ya kwamba Mirungi ni moja ya biashara maarufu mjini Arusha?Unawezaje kulitenganisha Jiji la Arusha na Mirungi?Nini athari za mirungi kwa jamii ya kiarusha?je Mirungi ni kero kwa jamii?Ni nini mtazamo wa Jiji dhidi ya Mirungi?watu wa usalama ni sehemu ya jiji la Arusha,je Mirungi imekuwa sehemu ya maisha yao?Usiniruhe handasi
    Baba Ngondi

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2008

    Yaani mijitu bwana mtu ameuulza swali hakuna hata mmoja aliyempatia jibu.kweli mtaacha kufisadiwa na wachache wenye akili kama Akili zenyewe ndio hivi na shule kweli mlisoma nyie I doubt nakama ulisoma basi elimu ya bongo itakuwa duni sana.kwa upande wangu mimi sinajibu ndugu yangu maana sijawahi kuishi kwenye makundi ya watu wengi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2008

    duuu nimeimiss sana hiyo gomba!! tena hilo kangeta hapo juuu sio type yangu mimi ni giza tena ukute ile laini kama maini na coca au pespi na big g duuuu full ahandassss. naona bongo inatakiwa kuhalalisha tuuu ili wananchi wapate ajira maana kenya ila limwa na hapo bongo lushoto inasitawi na hedaru inaweza kuwapa watu ajira, sasa nini bora konyagi au gomba?maana nyagi ni kama gongo tuuu haina tofauti

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2008

    WEWE NI NANI MPAKA UUNE JAMBO LIMEKUKERA? TULIA WEWE?MIRUNGI NI KTU SAFI NA KIZURI NCHI NYINGI WANATUMIA SO WACHA KELELE!!!UUUUSSSS

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2008

    Duh! kweli hii ni blog ya jamii. kaziii kweli kweliii!!
    Mirungi ni haramu kama yalivyo madawa ya kulevya. kinachoonekana hapo Arusha mzunguko wa pesa unaotokana na mirungi ni mkubwa na ndiyo maana hata hao askari wameamua kukaa kimya ili wawe na sehemu ya kupata rushwa. Inaonyesha hao wauza mirungi wanaufahamu vizuri mtandao wa polisi na wanafahamu nani wa kumfuata ili mambo yawe mswano. Ndugu yangu ujumbe wako umeshafika lakini kilichopo sasa ni utekelezaji wa ule msemo ''Mbuzi hula urefu wa kamba yake'' ndicho wanachofanya askari kwa kulifumbia mambo hili suala.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2008

    Inaonyesha jinsi nchi ilivyooa ndio maana tunaliwa hela na mafisadi wakati tuko macho kumbe ubongo umejaa Mirungi.

    Yaani kila mmoja anamkandia huyu kama vile kaleta jambo baya sana...Mirungi inamadhara sana. Mtu asikwambie kitu...Mnaosema bora Konyagi au mirungi sijui vipi. Ugonjwa ni ugonjwa hamna cha bora ugonjwa huu au huu. Hao madereva wakila mirungi basi mnaenjoy wakiwaendesha huko. Mungu atunusuru tu. Ndio maana ajali haziishi njiani.

    Kama Kenya wanafanya waachie wao kwani huwaoni akili zao silivyo fyatu?

    Inabidi sheria iingilie. Na kama mapolice wanakula mirungi pia basi kazi waachie. Kuna watu wengi wanatafuta kazi wenye kutaka kula mirungi waachie wengine.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 05, 2008

    Wakilipiga marufuku gomba si tutaenda hapo namnaga..kuingia upande wa Kenya..kusaga gomba na kujirudia zako upande wa bongo likishanasa!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 05, 2008

    mirungi inapunguza nguvu za kiume,mwammme anaetumia mirungi na asietumia wako tofauti kabisa,asietumia ana nguvu sana kwenye majamboz kuliko anaetumia.nina uhakika na ninachosema.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 05, 2008

    Kwakweli huyu mdau kaandika kitu cha maana sana. Kwakweli ni kero sana hii MIRUNGI, lakini mie nadhani hii kitu sio hairuhusiwi kutumiwa nadhani inaruhusiwa sana tu. Hao wana usalama wenyewe wanaitumia sana tu, nadhani hata kituo wanainga nayo. Wakiwa kwenye hizo DIFENDA zao nao hula hiyo MIRUNGI kama kawa. Na ni askari wengi sana hula mirungi.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 05, 2008

    MIRUNGI NI POA, MNAO IKANDIA NI WANAFIKI TU MNATAKA KUSEMA KENYA AMA UINGEREZA NI WAPUMBAVU SANA KUIRUHUSU MIRUNGI, AND TAKE INTO CONSIDERATION THAT THOSE TO COUNTRIES ARE UP AHEAD ECONOMIC WISE THAN US. WEWE HUJIULIZI KWANINI MKAZO WA KUWASHIKA WAUZAJI HAUWEKWI SANA, PROMINENT PEOPLE WANAKULA SANA HII MIRUNGI AND THEY GO ABOUT THEIR DAILY BUSINESS PERFECTLY. TATIZO MIRUNGI KURUHUSIWA NI KIVUMBI, NAHISI WAKUBWA WENGI WANATAKA IRUHUSIWE ILA HAKUNA MWENYE UJASIRI WAKUANZISHA MADA. KILA KILEVI KINA SIDE EFFECTS, LAKINI SIONI KAMA MIRUNGI NI MIBAYA KIASI HICHO.

    KUNA ALIESEMA KUHUSU UFASADI SIDHANI KAMA HII TOPIC INAHUSIANA NA UFISADI. HISTORIA PIA INATUAMBIA ZAMANI KENYA PIA KULIKUWA NA WANAFIKI KAMA HAPA BONGO, NA MIRUNGI ILIKATAZWA LAKINI WATU WALILALAMIKA MPAKA KWA RAIS NA MIRUNGI ILIRUHUSIWA NA KENYATTA INFRONT OF A CROWD.

    SIONI KUWA MIRUNGI NI KILEVI NOMA, NA NASHANGAA KINACHOKUKERA NA NINI HASWA HAUPENDI WAKILA AMA NI NINI BOSS, UCHAWI UNAANZA HIVI HIVI KUKERWA NA VITU VIDOGO VIDOGO TU

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 05, 2008

    we kaka umeongea lamaana sana jama langu mi niko Arusha kweli hili jambo limekuwa kero sana na hawa wanaokula mirungi wanatafuna mpk huku pembeni ya midomo yao kuna kuwa na vitu vimegandia mmmm wanatia kinyaa sana alafu sijui kuna stail yakutafuna kwani wanatafuna vibaya kweli mmmmmm wanakinaisha sana hao watu wajirekebishe kwani wamejisahau kabisa.

    sweet
    Arusha.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 05, 2008

    hata misupu anakula mirungi hamumuoni mdomo wake

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 05, 2008

    Mirungi haina madhara yeyote kwa jamii na ni kweli ni zao la kichumi Arusha mimi nawajua watu wamesomeshwa na hela za mirungi.Kama ni mgeni Arusha we zuka karibu na msikiti mkuu wa ijuma ni bidhaa inauzwa nje kama bidha zingine,kwa mtazamo wangu serikali haina so na hili zao letu la machalii wa A.City.mzee RPC Matei analikubali hili zao lenye kuleta rizim ya aina yake

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 14, 2008

    sweet/sour wa arusha, kama mirungi inakukinaisha wewe sasa kwa nini watu wengine wasitumie? you have a choice to control your life not of others, it is like watching tv if you dont like the channel you change it, right? leo unalalamika kuhusu mirungi kesho utalalamika jirani zako wakipika vyakula vyao vinanuka!!! typical wabongo ,wengi hawaelewi haki zao zinaanza na kuishia wapi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...