BWANA MICHUZI,
NI MIMI MZEE WA BUNJU TENA NOMBA MSAADA WENU NYOTE BILA KUBAGUA. NIMEKUA NATATIZWA SANA NA HAKA KAMTINDO AMBAKO KAMEJIKITA SANA MJINI HASA KWA WATU WA CLASS FLANI, UNAKUTA MTU ANAITWA MAMA LUKAMBA, AU MAMA SWAI, NA HAPO SWAI AU LUKAMBA SIO MTOTO WA YULE MAMA LA! NI MMEWE NDO SWAI AU LUKAMBA!!!! AU UNAKUTA WANAWAKE WAKIAMBIZANA KWA MFANO NAKWENDA UBUNGO KUMPOKEA BABA!!! HAPO ANAMAANISHA MMEWE SIO BABA YAKE MZAZI TOKA ROMBO AU USSOKE!!!!!! HALIKADHALIKA WANAUME UTAKUTA ANASEMA , “ NGOJA NI CHECK NA MAMA TUONE TUTAKUSAIDIAJE!!!!” HAPO HAMAANISHI MAMA AKE TOKA HUKO MABONDE KWINAMA.
ILIWAHI NITOKEA MIAKA YA NYUMA KIDOGO MAMA ANGU ALIKUJA KUTUTEMBELEA TUKAWA NAE KWA MUDA FLANI HAPA KWANGU. SASA SIKU MOJA AKAJA MAMA MMOJA JIRANI YETU AKAULIZA NIMEMKUTA MAMA LUKAMBA?? MAMA ANGU AKATOKA KWA FAHARI AKASEMA “NIPO KARIBU “ YULE MGENI ALISHANGAA SANA NA AKASEMA “SI WEWE NA MTAFUTA MKEWE” KWA KWELI MAMA ANGU ALIFADHAIKA SANA NA ILITUGHARIMU SANA KUMWELEWESHA ,MAANA KWAKE YEYE MAMA NI YEYE NA SI MWINGINE NA YEYE KUITWA BI MKUBWA NI MATUSI MAANA KWETU BI MKUBWA NI MKE MKUBWA KATIKA NDOA MITALA NA YEYE HAWEZI KUA BI MKUBWA KWANGU!!!! SASA JE!
NISAHIHI KUWAITWA WANDANI WETU VYEO STAHILI VYA WAZAZAI WETU ( MAMA AU BABA??)
DINI ZINASEMAJE HUHUSU HILI
MILA ZETU ZINAELEKEZAJE???
NI SAHIHI KUMUITA MAMA AKO BI MKUBWA??
KWA WENYE MITALA WAKE ZAO WAKUBWA WAITWEJE???
SHUKRANI
MZEE WA BUJU
ILIWAHI NITOKEA MIAKA YA NYUMA KIDOGO MAMA ANGU ALIKUJA KUTUTEMBELEA TUKAWA NAE KWA MUDA FLANI HAPA KWANGU. SASA SIKU MOJA AKAJA MAMA MMOJA JIRANI YETU AKAULIZA NIMEMKUTA MAMA LUKAMBA?? MAMA ANGU AKATOKA KWA FAHARI AKASEMA “NIPO KARIBU “ YULE MGENI ALISHANGAA SANA NA AKASEMA “SI WEWE NA MTAFUTA MKEWE” KWA KWELI MAMA ANGU ALIFADHAIKA SANA NA ILITUGHARIMU SANA KUMWELEWESHA ,MAANA KWAKE YEYE MAMA NI YEYE NA SI MWINGINE NA YEYE KUITWA BI MKUBWA NI MATUSI MAANA KWETU BI MKUBWA NI MKE MKUBWA KATIKA NDOA MITALA NA YEYE HAWEZI KUA BI MKUBWA KWANGU!!!! SASA JE!
NISAHIHI KUWAITWA WANDANI WETU VYEO STAHILI VYA WAZAZAI WETU ( MAMA AU BABA??)
DINI ZINASEMAJE HUHUSU HILI
MILA ZETU ZINAELEKEZAJE???
NI SAHIHI KUMUITA MAMA AKO BI MKUBWA??
KWA WENYE MITALA WAKE ZAO WAKUBWA WAITWEJE???
SHUKRANI
MZEE WA BUJU


Mzee wa Bunju hicho nacho ni kiswahili.
ReplyDeleteMzee wa Buju, hoja imetulia kweli hii... Huku kukua kwa lugha yetu naona kumekuwa kukua kiupande upande..
ReplyDeleteSteveD.
MZEE WA BUNJU wewe vipi?leo umepatia spelling ila umechemsha,sasa unauliza DINI zinasemaje kuhusu hili we unachekesha wewe... mtu anaitwa kwa jina lake..naitwa amina,ntaitwa amina sijasikia cha kuitwa mama flani au flani,izo mila za kibongo.nchi zingine watu wanaitwa majina yao,unless kama ni mama yako au baba yako ndio unaita mother or father...UPO HAPO?
ReplyDeleteAMINA YUSUF
GIRL POWER
Mzee wa Bunju, katika kujibu maswali yako kuna vitu 3 vyakuzingatia. 1 Lugha 2 Mazingira 3 Nafasi ya mwandani wako kwako.
ReplyDelete1 Kuhusu lugha lazima ufahamu kwamba lugha yoyote inasifa kama kiumbe hai, kwa maana huzaliwa, hukuwa na hufa! Kwa hiyo kutumika kwa maneno hayo siku hizi ni sehemu ya kuzaliwa na ukuwaji wa lugha! Ambao kimantiki unakubalika
2 Mazingira, ndio yanayoweza kuhalalisha kufanyika au kutokafanyika kwa jambo, kukubalika au kutokukubalika kwa jambo. Mfano Kama wewe kwenu mke mkubwa mnaita bimkubwa, kwetu haitwi bimkubwa, kwa hiyo haizuii mama kumuita bimkubwa. Pia inategemea unamuita mke mamaa au mume baba kwa kumaanisha nini, Unachomaanisha ndicho kinacho halalisha au kuharamisha. Kwani ukimwita mkeo "honey" unamaanisha ni asali kweli? au ukimwita "nyongo mkalia ini" au barafu wa moyo, wengine huwaita, " Habibty chocolate" kwani wanamaanisha ni vitu hivyo?! Ni kujaribu tu kumuenzi mpenzi wako kwa majina mazuri na yenye hadhi katika jamii!
3 Nafasi ya mwandani wako kwako, kila mtu anategemea yupoje na yule ampae usingizi (mkewe au mumewe), kama kweli mkeo anakuthamini na anakulea kama alivyokulea mama yako mzazi (kwa mapenzi ya dhati),sasa kwanini asiwe mama wa pili (ni kama cheo unamtunuku) Ngoja ni mnukuu Omar Kopa wimbo wake "ebwana ndio" anasema "...wewe ni mama wa pili kunilea unaweza, nami kwako nitayari chochote kukuliwaza.."
Nakama mumeo anakujali, anakutunza na anakuthamini kama alivyokuthamini baba yako, kwanini usimtunuku hiki cheo (kwa heshima ukamwita baba).
Jamami kwani hamjui kunampaka degree za kutunukiwa, mfano PhD za kutunukiwa kwa heshima,bila kukaa darasani!
Wengine mama zao wanawaita haloo, na bibi zao wanawaita mama, au wengine mama zao wanawaita dada!
Yote kwa yote, nafasi ya mama katika uhalisia wake itabaki pale pale! Sio kila neno linamaanisha!
kaka michue nimekosea coment yangu nimeitumakwenye habari isiyo yenyewe..fanya makalatee ipeleke kwenye ile ya mzee wa bunju..badala ya hiyo ya shaaban robert
ReplyDeleteasante
nyaningedere
Mzee wa Bunju swali lako ni lenye Hekima, 100%, nadhani maswali kama haya yangekuwa yanaingia hapa bloguni, wala hali ya hewa isingechafuliwa. Bado natayarisha jibu, nitaposti ila swali limenikuna!
ReplyDeleteKwa maoni yangu matumizi ya haya maneno yanakubalika ila wakati unawaambia watoto wako. mfano mtoto anakuomba kitu fulani na wewe unataka kuwasiliana na mkeo kuhusu hicho kitu hapo unaweza kumwambia ngoja niwasiliane na mama ukimaanisha mama yake huyo mtoto wako. Mara nyingi utamsikia mtu akimwambia mtoto wake ngoja niongee na baba/mama akimaanisha baba/mama wa huyo mtoto. Hapa huwa hawapendi kusema baba yako/mama yako. katika matumizi ya nje ya hayo nadhani ni makosa kwani mama ni mama na mke ni mke. Nadhani hapa wametafsiri maneno ya kizungu, MR, MRs sasa hapa nadhani wataalam wa kishwahili watusaidie tafsiri sahhii ya haya maneno
ReplyDeleteMdau umeiwazaje hii?Mmhh kwa kuchangia kidogo tu,wale wakristu hasa R.C kabla ya kufunga ndoa huwa wanakwenda kupata mafundisho kwenye vigango e.t.c(Mimi nilishahudhuria).Moja ya vitu nilivyofundishwa ni hiyo topiki unayoizungumzia hapo mdau.Wanasema hivi(watu wa saikolojia?).Inakuwa vigumu sana kwa watu kutamka neno MME WANGU AU MKE WANGU ndiyo maana hayo maneno yanaibuka.lakini jina zuri kwakweli ni kutamka neno naenda kumpokea MME WANGU AU MKE WANGU.Haya mambo ya mama watoto,baba watoto,mamsapu n.k ni uhuni.Sijui dini zingine zinaslisemaje hili.
ReplyDeletehii mada nzuri sana mi nashukuru kwa kabila letu wagogo mtu anaitwa kwa jina lake,kama anaitwa rose basi ataitwa rose mpaka azeeke, na kama mtoto anaambiwa kitu na baba yake yule baba atamwambia nenda kwa mama yako mwambie kitu flani na sio nenda kwa mama.
ReplyDeletehalikadhalika kwa madada na makaka,kama dada anaitwa mwendwa hata kama ana watoto 10 huwa hatubadili jina na kumwita jina la mmoja wa watoto wake bali ataendelea kuitwa dada mwendwa,hivyo hivyo kwa makaka pia.
mimi nimezoea kuitana na mume wangu majina yetu na tukibadili sweet au honey kutokana na yeye utamaduni aliokulia sio wa kuniita mie mama na yeye kumuita baba. watoto nao hivyo hivyo baba yao wanamwita dad na mimi mummy nikiwatuma kwa baba yao nasema aende kwa baba yake akamwambie jambo flani na sio aende kwa baba.
kazi ipo kwa mzazi aliezoea kuitwa mama na mkwewe alafu mwanae aoe au aolewe na taifa jingine inakuwa ngumu kidogo wazazi wetu kuelewa.maana mkwe anamuita kwa jina lake.
huyu mkatoliki hapo amenichekesha sana. ila ameongea kweli tupu.. neno mume/mke wangu ni gumu kwa wengi. mnaweza kuitana wenyewe mkiwa wawili ila katika mkusanyiko tena hasa wa ndugu inakuwa soo.
ReplyDeleteila mi nadhani ni vizuri watu waitwe kwa majina yao (hii ndio kidini zaidi) mi naamini hata mbinguni tunatambuliwa kwa majina yetu,...nk. haya mambo ya mama fulani ni uswahili. i.e ubantu
nyaningedere naomba nikuulize swali, je wewe ni bwana Danstan? maana hilo neno 'makalatee' naamini alilianzisha yeye,kama ni wewe,PLIZ TUWASILIANE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteMAMA SOME FUD
mimi nafikiri,mume na mke kuitana baba au mama,japokuwa inawapendeza watumiaji,lakini bila kujua kwa kiasi fulani huwa ina athari zake.
ReplyDeleteMaana utakuta sasa ule uhusiano wa mke na mume unakuwa (formal)sio wa ukaribu sana kama wapenzi bali kwa ajili ya vyeo vyao na kwamba kama wanandoa.
Hivi vijineno kama mpenzi,mume wangu,hny na mengineyo mengi huwa yanaongeza mapenzi na kuwaweka karibu zaidi.Yakikosekana hapo halafu ikatokea mmoja wao ameteleza na kule akaitwa honey,sweety,mpenzi n.k basi itakuwa shughuli.
Hivyo ni vizuri hata kama ni wana ndoa tuitane kama tulivyoitana tangu mlipoanza uhusiano,na sio kuzeeshana na kupunguza ladha ndani ya mapenzi.Hatima yake siyo nzuri.
Acha watoto wawaite kwa vyeo vyenu halisi na si vinginevyo.Kwanza watoto wangu ikitokea baba yao aniite mama watamuuliza "kwani na wewe ni mama yako?"
ni swali la maana sana. Kama walivyochangia wa juu hapo kuwa inatokana na mazingira uliyokulia.
ReplyDeleteMakabila- Kwa mfano kabila la wangoni na wagogo huwa nasikai watu wanaitwa majina yao hata awe na mvi kichwa kizima tela na wajukuuu 100. Na kama ni dada ndo watatanguliza dada fulani, ama kaka au shangazi mjomba n.k tena nawasikia wakijitambulisha
kwa majina yao, wataongezea tu jina la mume ama la ukoo wao kwa kutaka kukuelewesha uhusiano ulopo ama kujitambulisha zaidi. Hii ya kusema mrs fulani yaani jina la mume ni pale wakiwepo mjini, ama uswahili wanapotumia majina kusema mama fulani.
Na huwa navutiwa sana nikisikia mume anamwita mkewe jina lake ama mume wake, huw aunamvuto fulaniii.
Kwa sisi Waislam kumuita mumeo BABA au mkeo MAMA ni dhambi, kwani amekuzaa???
ReplyDeleteSi mjuzi sanaaaa wa dini kiundani lakini najua kuna muslims humu wanajua, tafadhali watufafanulie
ScArEcRoW
Ahsante mzee wa Bunju kwa mada nzuri yenye kuhitaji taaluma na faida tele. Kuhusiana na suala lako, dini tukufu ya Kiislamu inakataza kabisa suala la kumuita mke kwa jina la mama, inamaanisha kwa Muislamu hata baada ya kuolewa mwanamke ataendelea kutumia jina la baba yake na si la mumewe, mfano mie kama jina langu Asha Hassan basi hata baada ya kuolewa na Yusuph Ali basi nitaedelea kuitwa Bi. Asha Hassan na sio Bi. Asha Ali au Bi. Asha Yusuph ambao ni utamaduni wa kizungu wa kurithishwa majina ya waume baada ya kuolewa. Suala hilo linatiliwa mkazo na Quran pale inaposema kuwa.."waiteni (ikimaanisha wanawake) kwa maajina ya baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu..."..Qur'ani 33:05. Kwa hivyo suala la kumuita mke mama ni makosa na mume baba ni makosa pia. Tukienda ndani zaidi katika sheria za Kiisilamu zinazojulikana kama FIKIH.. hata kumfananisha mkeo na mama yako ni kosa kubwa ambalo mtu alofanya hivyo kama ni mume anatakiwa kutoa kafara ili kulipiza suala hilo. kwa hiyo mke ni mke na sio mama, na mama ni mama na sio mke, halikadhalika kwa upande wa mama.. kinyume cha hapo ni makosa. Ingawa mume kumuita mkewe mama wakati anapozungumza na watoto wake, inaweza kukubalika na viceversa. hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi.
ReplyDeleteNawakilisha
Mdau Uajemi
Nadhani kiswahili kimekuwa na kuvunja ungo kabla hakijafikia umri unaistahili. Nimesikia mengi sana na tunaenda mbali sana kwani siku hizi hata kifimbocheza kaacha majukumu yake pia.
ReplyDeleteMfano:
1. Mimaji 2.. Mvua ananyesha 3. mjomba wake na fulani(badala ya mjomba wake fulani) 4. mikaka na midada nk
nikwamba tunapotea na mihimili yetu inakufa kuanzia home. how come mkeo umuite MAMA? mumeo BABA?
nawajuwa niwatani wangu wangoni na wazaramo ndio wanaleta balaa hizi!
G7
UK
Mimi ni Mume wangu huwa ananiita Mama kwa kweli SIPENDI.Na nimemwambia, mara nyingi huwa anasema sorry lakini nadhani ameshazoea vibaya ,NA wanaume wengi wana tabia hiyo, na nimegundua wanawake wengi hawaifurahii hii tabia, sikilizeni HATUTAKI MTUITE MAMA.FIND OTHER NAMES FOR US PLEASE. BTW THANKS BUNJUMAN.
ReplyDeleteNASHANGAA SANA, watoto wenu wa Kike mnawaita MAMA,Wake zenu/rafiki wa kike mnawaita MAMA, MAMA mnamuita MAMA,MNATUCHANGANYA.MNAONDOA MAANA NZITO YA MAMA!!!!!.
ReplyDeletewewe mzee wa bunju yaani umeyaacha majina yote ambayo ungeweza kuyatolea mfano ukachagua SWAI,hili jina sio la kulifanyina mchezo.popote unapolisikia hili jina ujue kinaeleweka.kwahiyo uwe makini sana unapochagua majina ya kuyahusisha na mambo yenu ya kiswahili.Tunakusamehe lakini usirudie tena. kuna majina ya kienyeji kibao ambayo ungeweza kuyatumia kama, kamugisha, mapunda, shemdolwa,nk
ReplyDeleteWENU MBEGA MWEUPE
Kumuita mkeo 'mama' au mumeo 'baba' imezoeleka sana ingawa nasikia kwa waislamu hiyo haitakiwi, mkeo hawezi kuwa mama yako.
ReplyDeleteMara nyingi wanandoa huita wake zao mama na waume zao baba kwasababu ya watoto. Mfano mimi na mume wangu tunaitana tofauti sana yeye huniita mimi mama mdogo na mimi humuita yeye baba mdogo, hii ilitokana na kuwa na watoto wa dada zangu wengi wanaotuzunguka ambao walikuwa wanamuita yeye babamdogo na mimi mamamdogo tukawaiga. Ila akiongea na watu kuhusu mimi ananiita BIMKUBWA na sio mamdogo, sijui kuna bimdogo mahali au? (he he) na mimi nikiongea na watu kuhusu yeye kama wanamjua ntamtaja jina lake kama hawamjui ntasema mume wangu na sio baba.
Mada nzuri sana hii. Katika mwendelezo wa mada hii hii, neno "mamaa" nalo linamaanisha nini?
ReplyDeletekidini sisi waislam ukimwita mkeo mama ni haram na huwezi kulala nae sijui wenzetu wakristo kwao imekaa vipi,pili hii kuita mama musa kwa maana ya mke wa musa haijakaa sawa ila ndio vile ipo tutafanyaje mfano nakumbuka shule tulikua na mwalim mussa kisa mke wa mussa,wenzetu wazungu wanatumia mr/mrs sasa kiswahili hakina hizo pronouns,kwa upande mwingine wapenzi kuitana mamaa/babaa its funny...........by usinijue
ReplyDeleteKumbe Bablii huwa unaweza kuongea point hivyo!!!!. Kuna mdau mmoja hapo juu kasema kuwa wanawake huwa hatupendi kuitwa mama. Mdau napenda kukufahamisha kwamba sio wote! Kama wewe hupendi usijumuishe na wenzio. Kwa upande wangu, mpenzi wangu akiniita MAMA huwa nafurahi sana! yaani huwa nahisi kuthaminiwa!
ReplyDeleteMi nafurahi tu kuwa na kwetu kunajulikana hehehee USSOKE. Mzee wa Bunju umekujuaje jamani? Tena mpaka spellings umezipatia....
ReplyDeleteShukrani za dhati kwa mdau kutoka Uajemi, naona ameliweka hili swala kwa undani sana na limeeleweka vizuri kwelikweli...Mola akuzidishie amani.
ReplyDeleteWadau wenzangu mungu azidishe neema zake humu ndani na baraka zijae tele kila siku.
Shukrani sana.
Mzee wa bunju hiyo ni misemo tu itakuja na kupita
ReplyDeleteHuku niliko watu wanawaita wake au waume zao kwa majina yao kabisa hata wawe na watoto kumi hamna cha baba fulani...jina lake ni steve ataitwa steve na mkewe mpaka afe...Jina la mke ni sophia ataitwa na mumewe Sophia hata akiwa na wajukuu...
Kwa hiyo mi naona ni heshima tu kubwa kumwita mume baba na mke mama kwa vile watoto humo ndani nao wanaita baba na mama....
Na huku nilipo huyo mama mkwe wako akija atashangaa...Huku mkwe haiti mama au baba hata siku moja mama ni mama yako tu lakini mama wa mumeo au mama wa mkeo huku wanawaita kwa majina yao...Sana sana amekuheshimu ndio atakuita MRS au MR so and so ... otherwise unasikia mume wako anamuita mama yako kwa jina lake la kwanza Marie
Na mwambie mama asifadhaike ....You know what I have learn heshima ni rohoni ...kama mtu anakuheshimu hata asipokuita mama au baba ...kama anakuheshimu jina halina maana yeyote...Kuna wengine wanaitwa mpaka waheshimiwa lakini heshima yao iko wapi? Hamna anayewaheshimu kabisa.Bora mtu asiniii te jina lolote lakini heshima yangu anipe
WEWE MBEGA MWEUPE,ACHA PUMBA ZAKO.
ReplyDeleteHow about Sweetheart, Honey,Baby,Sweet,Darling, kwa kiswahili tumia, La Azizi,Mpenzi, Sabuni ya moyo, Waridi,Swahiba,jicho na Majina mengine mengi ambayo yanaweza kwendana na Wakati na Mahali kati ya wapenzi wawili. Acheni Mama na Baba. thanks.
ReplyDeleteUmesema Kweli mdau Usinijue, kwa waislam ukimwita mkeo mama au ukisema nakuona kama mama yangu sikutamani, ujue hapo hamna ndoa tena inabidi murudiane kwa kuwepo mashahidi kuwa mmerudiana mlikua hamna ndoa tena.
ReplyDeleteMzee BUnju yaelekea wewe umetoka Zenjy au umekulia huko ndiko kwenye busara hizo za kutokumuita mke mama. ukweli huko ni mwendo wa kuita jina kamili tu m.f bi Bahati Bi kidawa bi hidaya n.k hukuti wanaitana mama na baba kwa mke na mme, wakimaanisha mama ni yule aliyekuzaa tu na baba ni yule aliyekuzaa, au kama amekupandisha daraja atakwika biti (binti), makame au biti Pandu au biti Ali.na kwamke utaskia Bwa( bwana) masudi bwa au kama atakwita kwa huba atarembesha jina lako mf bwa-Mha (Moh'd, bwan Saidi n.k, au akitaka kutumia neno mama atasema mamakeee flaniiii,na mara nyingi hawana kugugumizi au kujishaurishauri utawasikia mtu anamwita mwenziwe mkewanguuu au mumewanguu hata awepo nani haoni vibaya, naweza kusema huona fahari hasa wakitunia neno mkewangu/mumewangu. inapendeza sana inaleta raha na inaleta maana ya utambuzi, ingawa wengi wanaona labda ushamba au kuonekana hukusoma,au hivi na vile. Cheo cha mama ni kikubwa na kina heshima zake na miiko yake pia.
we Mbega Mweupe..kweli wee lofa.
ReplyDeletetena mpumbavu mkubwa sana. Yaani kama kuna ubaya kutumia jina la Swai kwanini atumie hayo mengine?
Tumia akili sio mavi, shenzi kwelikweli wewe.
Jamaa katolea mfano haimaanishi kuwa Swai ndio tabia zao ama vipi.
Inaonesha hujaenda shule wewe...na angalia usije ukaua mtaji wako wa genge kwani unaonesha hutumii akili za kuzaliwa na busara.
Pumbavu.
Mdau mwenye hasira na washenzi wa Tabia.
BOFYA eastafricatube.com tafuta wimbo huu MTAZAMO-GODFREY GREGORY ft BANANA utapatajibu.
ReplyDeletewewe mdau mwenye hasira na washenzi wa tabia inaonyesha kuwa jina lako liko kati ya majina ya kienyeji yalio tajwa hapo. Hakuna ubaya ukiwa na jina la kienyeji
ReplyDeleteMzee wa Bunju i can only say one thing, it depend with the roots of ur family. Meaning, mmelelewa vipi.
ReplyDeleteMdau T-dot