profesa faustin kamuzora, ambaye ni makamu mkuu wa chuo cha mzumbe, leo ametema cheche kwenye mkutano wa kimataifa wa utalii na safari jijini a-taun kwa kusema bongo inabidi wafunge mikanda katika teknohama ama sivyo wataachwa solemba na wengine duniani. ametoa mifano kadhaa lakini kubwa na la ukweli ni kushindwa kwa taaisi kuwa na website na kama wanazo hawazi up-date kila siku na kdhalika. kasema bongo inapitwa na wengine kwa kuwa kila mtu nimbumbu kwenye mtandao.wadau mnaizungumziaje mada hii?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2008

    Kama kuna watu naowaaminia Tz ni pamoja na Prof kamuzora. Ni mmoja wa watu wakini sana na wmenye kujitolea katika kuleta maendeleo ya Mzumbe na hata wanafunzi wake. ni urasimu na ubinafsi ndio unaokwamisha juhudi zake lakini ni mfano wa kuigwa. TCRA walishaelezwa miaka miwili iliyopita wapitishe sheria ya kuchukulia hatua na kuwabana taasisi na website za serikali zitakazo kuwa zimekufa au hazina habari mpya (updated) sijui kama wamelifanyia kazi mpaka na kamuzora tena ankuja kusema this is not serious! halafu tukiachwa nyuma na kudharauliwa tuna lalamika tumake jamani usingizi wa pono tuliolala unatosha

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2008

    Mkubwa huyu anaongea nini hapa tena?? mbona anacheza faulo? taasisi yake mwenyewe ukiangalia baadhi ya mambo hayajawa updated toka website ya chuo imeanzishwa. Namshauri aweke mambo sawa kwanza nyumbani/ kwenye taasisi yake ndipo apate nguvu ya kuongea hivi vitu. Pia kusema kwamba wote ni ma mbumbumbu sidhani pia kwamba ni kiasi hicho, tuache ku exaggerate mambo. Wapo wa TZ wazuri sana kwenye mambo ya mtandao... nadhani anatakiwa tu kusema kwamba juhudi ziongezwe zaidi. Professor angalia...credibility disposability!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2008

    Fungua www.udsm.ac.tz
    au
    www.udom.ac.tz

    Website inachukua masaa kibao kufungua even though ninatumia the fastest broadband connection around.
    University of Dar es Salaam, kwanini hamna website ya maana?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2008

    Ni ukweli mtupu alicho kisema.tuko nyuma sana sana na sio kwamba vijana hawapo wa kuchapa kazi,wapo wengi tu sema ndio hivyo bado makampuni hayaja elimishwa umuhimu wa teknohama.
    Napia tuhajili watu wenye qualification sio ndugu zetu tu mambo ya kumpa kazi mtoto wa mjomba kisa kamaliza form 4 tuache jama.maisha hayaendi hivyo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2008

    Kaka Michuzi napenda kuungana na Prof. ni kweli katika Teknohama twaweza kuwa nyuma ingawa kuna initiatives nyingi zinafanywa kuhakikisha Tanzania inakuwa kiuchumi kupitia Teknohama, moja ya initiative hizo ni kuanzishwa kwa wizara ambayo imepewa rungu la kusimamia ICT nchini, kama utakumbuka Mhe. Rais aliunda wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia hapo ikawekwa component ya ICT kuwa chini ya wizara hiyo.
    Jukumu kubwa mi naona ni kuwepo kwa "awareness" juu teknohama" kwa kuanzishwa "Telecentres", "Teleeducation", "E-libray" na nyingine nyingi tu ambazo zitasaidia kupatikana kwa information kwa uraisi zaidi.
    Kuhusu taasisi kuwa na "Website" ambazo mara chache zimekuwa zikiupdatiwa hii inatokana na taasisi hizo kutokuwa na Webmasters katika taasisi zao isipokuwa wanawapa tender website designers na kutengezewa website tu na kuzihost basi, taasisi chache zimekuwa na Idara ya IT(Information Technology)ambapo wangeweza kusimamia website hizo na kuziupdate mara kwa mara pindi contents zinapopatikana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2008

    Ni kweli kabisa alichosema, baadhi ya tasisi zinafikiri ukishazindua website kwa mbwembwe nyingi basi umemaliza kazi! Ndo maana hata baadhi ya balozi zetu za TZ huku ng'ambo unakuta zina website lakini information zilizopo ni za toka website ilipozinduliwa! Ukija suala la wabongo na mtandao hilo nafikiri bwana Michuzi kuna kipindi ulitoa ranking ya nchi za Afrika zinazoongoza kwa kutumia mtandao, sikuiona bongo! Mimi kuna baadhi ya rafiki zangu tulimaliza nao mlimani, huwa nawaandikia e-mail zinakaa hata miezi 3 bila majibu, naamua kuwapigia simu, wanachonieleza eti kwamba muda wote huo alikuwa hajaenda net kwa sababu ya kutingwa na mihangaiko! Kweli mtu uko Dar, unakaa miezi mitatu hujafungua internet?? Wa vijijini wasemeje sasa? Ukimuuliza kwa nini, anakwambia mobile phone inatosha! Duh! Inashangaza sana!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2008

    Hakuna kumponda ameongea ukweli haklisi ingawa hata taasisi yake hawa update mambo lakini amesena ukweli halisi, taasisi nyingi ikiwemo yake hasa za serikale even za watu binafsi website zao toka walinyo update mwaka 2001 hadi leo unakuta informatios ni zile zile,tatizo ni kwamba umbu-mbumbumbu kwenye matumizi ya technology ya computer kwa tz tuko nyuma kwa eastafrica ni wa mwisho.angalia watani wanatumia sana technology ya computer kuliko sisi, mtu yupo chuo kikuu usdm hata kufungua email hawezi kwa maana hawajapewa changamoto jinsi ya kutumia computer katika mambo mbalimbali.



    Mdau na mtaalam wa Tech- South Korea AKA Benlango-kilungule

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 19, 2008

    taasisi zisizo na tovuti nzuri igeni toka SUA..http://www.suanet.ac.tz

    ...simply the Best!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 19, 2008

    Eti mnasema "teknohama"! Mna maana gani?

    Mafiga yetu (sisi walalahoi vijijini) ya kupikia ni yale yale tangu tuvumbue moto na vyungu vya kupikia!

    Tunavundika mihogo kupata udaga wa muhogo wa kutwangwa na kusagwa kwenye jiwe la kusagia ni tekno ile ya jadi tangu tuchukue mfumo wa kibinadamu!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 19, 2008

    Samahani Bro Mithupu, kuuliza si ujinga, ni nini maana ya Teknohama, maana akili yangu inanambia may be ni teknolojia, hebu yang'aze bro

    Wako
    KIHIYO

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 20, 2008

    Kweli alichokisema Prof Kamuzora, mfano mzuri ni website ya wananchi iliyozinduliwa kwa mbwembwe lakini sasa iwapi hovyoo, haina lolote la maana na ni kama imekufa vile wakati wizara husika wala haioni kama ni tatizo hilo. Jamani hiyo website ya wananchi ni e-goverment, wewe waziri wa habari hulijui hilo na tena ingekuwa kiunganishi kikubwa cha wizara na taasisi mbali mbali. 'Kusema mbali kutenda mbali!'

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 20, 2008

    aibu ni kuwa hata www.jakayakikwete.com or kikweteshein haiko updated tokea December 12, 2007. Au ndio washachukua kula?

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 20, 2008

    Kwa kweli inatia-ahibu sana, embu fungua website ya Rais Kikwete. http://www.kikweteshein.com/tanzania/
    kwa kweli hii Website inatia ahibu sana, kwani kwa muda mrefu aijafanyiwa update na mpaka leo inasomeka kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ni Bw. Lowassa.
    kumbuka kuna watu wengi wanaokuwa wanatafuta taarifa muhimu kama za nchi. na hii Website inaonyesha ni moja ya sehemu unayoweza kupa Taarifa za kiserikali. kwa mtu usiyejua unaweza kuchukua taarifa zilizoko na kuzifanyia kazi bila kujua, ni taarifa potofu.
    Hivyo wadau wenzangu embu tujaribu kuwastua hawa watu wa Ikulu, nilijaribu kuwaandikia email lakini hakuna mabadiliko.
    embu Bigwa Michuzi Tafadhali liweke hili jambo hewani.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 20, 2008

    Tekelinalokujia na teke linalokuhama huku kwetu makunduchi bado twatutusa maji kwa utosi vino mwatwambili kuna maenjeleo maenjeleo ya jajee? twapigana malungu twaumizana kuno makunduchi mwatwambili twajitakia.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 20, 2008

    Juu ya nini hamuwatafuti wale jhamaa waliotengeneza www.harusiyangu.com?

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 20, 2008

    well Najuwa kwamba watu hasa mchangiaji wa mwanza munamsikia kamuzora from distance. Nawaomba muulize watu wa mzumbe watawaambia who he is.. contrally na munayosema humu ndani.

    pia e-business na e-governance sio kama munavyosikia na yeye anavyodhani, hivi vitu vinasaidiwa na policy za nchi. ukienda nchi za wenzetu utaona act zao zzipo wazi kuhsu privacy, security trails na pia infrastructure. Mfano leo kuwe na user-centric site TZ unadhani ukinunua kitu utaletewa wapi kama unaishi mbagala? or kama unatuma vielezo vyako nani atasecure kwani nimeona mara kadhaa makampuni ya simu yanatoa taarifa za nani kapiga kwanani kirahisi sana. huku duniani hata police kusikiza simu ya mtu inataka sheria.

    so kamuzora anatakiwa aongee kama professor (awe critical thinker) sio aishie website haijawa updated.

    kunamtu hapo juu kasema hatuna webmasters: inafurahisha- unasite moja ambayo inachange twice a year then unataka webmaster ambaye kila mwenzi utamlipa 500,000/= zaidi?? akili matope.
    Narudia suala la update linategemea aina, purpose na information ya site na who are the users of the site.. unajuwa watu wanakurupuka kuwa na site bila kimsingi kuwa na sababu ,, na ndio maana unakuta site inapicha za familly and ukimuuliza unamuonesha nani na kwanini hana sababu.

    so for a critical thinker angeshauri watu wame na site pale wanapohitaji na wajue sites zinakuwa na intended audiences and from their utakuta unapata chaku update.. ukiangalia site ya kamuzora last update ni september 2007. and ukiiona ilivyo naturally hatakuwa na sababu ya kuapdate kila siku.. http://www.kamuzora.co.tz/

    All the best najuwa tutafika hatakama slowly.

    g7
    UK

    g7
    uk

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 20, 2008

    Nadhani Tanzania kwa hotuba tumezidi.

    Sasa kama hata Profesa anaongelea tatizo sasa Tanzania nani anayetakiwa atoe ufumbuzi wa matatizo?

    Maana wasomi wanalalamikia matatizo yaliyoko nchini,wasiosoma na wao wanalalamikia matatizo yaliyoko nchni sasa nani atoe ufumbuzi wa matatizo ya nchi?

    Yaani nasikia kuchoka kabisa.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  18. Alichosema Profesa ni kweli kabisa..ila kwa neno moja angesema makampuni na taasisi nyingi sana na viwanda havina kitu kinachoitwa Corporate Identity System. Ambayo ni Mind Identity, Behaviour Identity na visual identity. Wanaotaka kujua hii CIS inafanyaje kazi zaidi wasome paper yangu http://www.paper.edu.cn/en/downloadpaper.php?serial_number=200704-577&type=1
    hapa nafikiri Tanzania inatakiwa kuiga na kuweza kuangalia mafanikio

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...