rais wa Msumbiji mh. Armand Guebuza akiwa na waziri mkuu mh. mizengo pinda jijini maputo leo ambako anahudhuria mkutano wa umoja wa maendeleo ya elimu barani Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2008

    Hivi Chissano sio Rais tena Msumbiji?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2008

    Swali gani hilo. kama huna chakuliza nyamaza.Kwani wewe upo kwenye island usituboe.Alafu unabahati ningekuchambua!
    Mulox

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2008

    Mulox-naona pombe za bure zimekufanya uwe kichwa cha panzi.Mtu(anon wa 1)kauliza swali la maana,unamjibu kunya.Watu wengi tunaoingia hapa tupo nje ya Africa hatupati kila kitu kinachotokea huko home kama nyie.Mimi binafsi sikujuwa kuwa Chissano keshatoka madarakani na nina uhakika kuna mamia walikuwa hawana habari hii.Tunashukuru Michuzi kwa kutuletea info za home na africa kwa jumla.Big up michuzi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2008

    Kaka Michuzi naomba uwe makini zaidi unapotaja majina ya watu. Jina la kwanza la rais wa Msumbiji ni Armando na sio Armand kama ulivyoandika.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2008

    hivi jamani kwa watafiti wa mambo ya elimu barani africa, naomba kufahamishwa kama kweli nchi nyingine za africa viwango vyake vya elimu ni bora kuliko tanzania au nako niyaleyale ya funika kombe mwanaharamu apite? msinimeze jamani nacho maanisha ni msingi wa elimu yao ukosawa au ndio kama kwetu?maana kwetu taaluma ya ualimu wanao pelekwa kuisomea ni wengi wao ni wale ambayo ama credit zime gonga ukuta,au life limekwama anga nyingine zote hivyo inakuwa last altenative.
    nakumbuka kipindi nilipo maliza kidato cha sita,sikumoja ktk pitapita zangu nilifia pale BAPTIST center magomeni kipindi hicho tuition ikifundishwa pale[sijui sikuhizi maana ninamiaka mingi nje ya africa] sasa jamani nikakuta kijana mmoja niliye fahamishwa kuwa naye kamaliza form six anafundisha tuition.sijui combination yake ilikuwa ni ipi,lakini nilicho kuta akifundisha ilibidi NICHEKE HADI NIKAWA MBAVU SINA,pamoja nakuwa mmi nilikuwa nimechukuwa PCB.
    kichekesho ni hiki:-
    aliandika neno "LO!" kisha akauliza mnajuwa hilineno ktk sarufi linaitwaje?wanafunzi wakasita kidogo walikuwa nadhani form TWO, akajibu mwenyewe hiki kinaitwa KISHTUSHI! jamani nilibakiwa mbavu sina ikabidi niondoke pale, kwa ninavyo juwa mimi hicho ni KIHISISHI,kama sarufi ya kidato cha nne haikunitoka tangu miaka yote kumi na zaidi!
    haya waheshimiwa na mengineyo mengi tu ambayo hata walimu waliofuzu walikuwa wakichemsha shuleni hasa kiingereza,mmoja wapo akiwa ni second master wetu 'o'level [sitaji shule] alikuwa akitaka kumrusha mtu kichura utasikia anaanza "YOU!DO THIS huku anaonyesha kwa vitendo,then dent akijifanya haelewi NAMWAMBIA JUMP GROG FROG! lakini sikumoja akifundisha historia ndipo aliniacha hoi akielezea jinsi watumwa walivyokuwa wanakamatwa akaewa anasema[hapa natumia lafudhi yake] ZEI COULD GO STAND IN THE BUSH, ZEI WAIT! ZEI WAIT! WHEN ZE PEOPLE COME ZEI WAIT ZEI PASS ZEI PASS ZEN ZEI JUMP LIKE THIS[anaonyesha kwa vitendo] and catch zem!
    haya wangwana nasubiri majibu

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2008

    Nani aliyemshinda mwenzie kwa Tabasamu la Nguvu? Hivi tabasamu linaweza kuashiria nini? Na je Tabasamu linaficha nini? naomba waganga na waganguzi wanichambulie hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...