Je unajua kuwa ukijua siri ya viganja unaweza kujua jambo lolote katika maisha yako litakutokea lini na nani atahusika au litakuathiri vipi?.


Pia utaweza kujua kama utaoa au kuolewa au la! na hayo yote yatatokea lini, Je ndoa utafunga ua la?, je, ndoa itadumu au haitadumu, je mtapata watoto au hamtapata, je mtapata watoto wangapi? na je wangapi wataishi maisha marefu na wangapi hawataishi maisha marefu.


Katika sehemu hii nitawaeleza Siri za ndani kabisa ambazo zipo katika viganja vya kila mtu. Je unajua kuwa mambo yatakayokutokea maishani mwako pamoja na maajaliwa yako yote yameandikwa katika viganja vyako?.


Je unajua kuwa ukijua siri ya viganja unaweza kujua jambo lolote katika maisha yako litakutokea lini na nani atahusika au litakuathiri vipi?. Pia utaweza kujua kama utaoa au kuolewa au la! na hayo yote yatatokea lini, Je ndoa utafunga ua la?, je, ndoa itadumu au haitadumu, je mtapata watoto au hamtapata, je mtapata watoto wangapi? na je wangapi wataishi maisha marefu na wangapi hawataishi maisha marefu.


Kwa muda wa miaka mingi sana nimekuwa nikiwasaidia watu kujua maisha yao ya mbele kwa kusoma viganja vyao na kuwapa ushauri wa nini kifanyike ili waweze kufanikiwa maishani kutokana na Majaliwa yao yalivyoandikwa kwenye viganja vyao.


Na sasa nimeamua kuwapa hii elimu watu wengi zaidi ili muweze kujua siri za dunia na ili muweze kuelewa ni nini cha kufanya katika maisha yenu ili muweze kufanikiwa zaidi.


Kwa kuwa Elimu yenyewe ya Viganja ni pana sana, itanibidi niwe ninawaeleza siri za mikono yenu hatua kwa hatua ili muweze kuelewa elimu hii ya ajabu.

Ahsante,
Sheikh Yahya Hussein.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2008

    Si mchezo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2008

    huyu mzee ni mganga au nini??maana naona sheikh,ila je ni mganga pia!?NI HAYO TU

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2008

    Dini ya kiislamu hairuhusu usomaji wa viganja na kutazama nyota kwani sheikh Yahya ni Sheikh wa dini gani?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2008

    katika tovuti zote TZ sijaona tovuti iliyotulia kama ya Sheikh.imetengenezwa kisomi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2008

    Sasa Sheikh Yahya kama wewe ni mjuzi wakutabari yale ya ghaib (ya siri) kwa kuangalia viganja, mbona ulishindwa kujitabiria mwenyewe kwamba utatapeliwa gari hivi majuzi?! Au ulisahau kuangalia kiganja cako? Au ndo mganga hajigangi?

    Anaejua siri ni Allah tu (huwa ladhy aghalamu sirra wa akhfaa) binaadamu twadanganyana.

    Ajabu binadamu kutaka kujivika joho la mungu!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 27, 2008

    Astrologers claim the stars influence your future; psychics claim to know your future. All such things are condemned in the Bible (Isaiah 47:13). Which says

    "Keep on, then, with your magic spells and with your many sorceries, which you have labored at since childhood. Perhaps you will succeed, perhaps you will cause terror. All the counsel you have received has only worn you out! Let your astrologers come forward, those star-gazers who make predictions month by month, let them save you from what is coming upon you. Surely they are like stubble; the fire will burn them up. They cannot even save themselves from the power of the flame. Here are no coals to warm anyone; here is no fire to sit by. That is all they can do for you - these you have labored with and trafficked with since childhood. Each of them goes on in his error; there is not one that can save you."

    Here God was particularly judging the Babylonians who were strongly involved in this.
    God is saying that they are going to be so consumed by the fire that they won't even be worth a coal to warm over. They are going to go up fast in smoke. That's God's attitude toward astrology, star gazing, monthly predictions. That's fairly clear! No Christian has any business in any sense, under any circumstance fooling around with that. It simply opens your mind to demonic suggestions. And if you listen to that suggestion, it isn't that the horoscopes will tell you what you're like, they will simply make you into what they want you to be. People who listen to astrologists begin to pattern their life after what he/she says and, literally, they become transformed into their horoscope.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2008

    As I know as a Muslim mimi,mambo ya utabiri ni HARAM in Islam meaning this is forbidden and it is one of the worse sins that one can do. Sasa sijui huyu Yahya Hussein kwa nini anajiita Sheikh wakati ana fanya SHIRK ya kutabiri. Na yeye anajifanya anajua DINI. SHIRK is one of the MAJOR SINS in Islam and one is not supposed to associate God with anything or say that they can predict people's lives...huu ni ushirikina completely. DHAMBI KUBWA MBELE YA MWENYEZI MUNGU. MWENYEZI MUNGU NDIO MWENYE KUPANGA KILA JAMBO NA KILA JAMBO LIMESHAANDIKWA NA MWENYEZI MUNGU LITOKEE, KWENDA KWA WATU KAMA HAWA WAKUPE USHAURI NI WASTE OF TIME, HE CAN NOT EVEN PREDICT HIS OWN LIFE...

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 27, 2008

    Kinachofanyika mtu akikufuata msoma viganja ni kumtabiria mtu kuwa utakuwa hivi na hivi halafu anapoondoka unamuwangia ili awe vile ulivyosema vimtokee ili awe mteja wako wa kudumu na unamgeuza kuwa chuma ulete ndondocha wa kukuletea pesa.Kila wakati atakuwa akikufuata na matatizo na kukuletea pesa.Wengi wamegeuzwa chuma ulete kwa kujipeleka wenyewe kwa wanajimu na waganga wa kienyeji.

    Wapenda njia za mkato karibuni kwenye ulimwengu wa kugeuzwa chuma ulete wa watabiri na wasoma nyota.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 27, 2008

    Hongera sana Sheikh

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 27, 2008

    Kama aliwahi kutapeliwa gari kama huyo jamaa mmoja wa juu alivyoandika. Mimi nakumbuka aliwahi kamatwa wakati wa msukosuko wa bucha za nguruwe. Kama anajua yaliyo mbeleni angewatoroka Askari. Kupiga Ramli, kutazamia kwa waganga kwa kutumia nyota, mfano mtu anapotaka oa anaenda kutazamia vyote ni HARAM ndani ya Uislamu. Na Mungu kasema "Ma Ya'alamuna l-ghaibu", hakuna afahamuye litakalomtokea muda ufuatao, sasa huyu Sheikh anajua wapi. Pia mkae mkijua Sheikh si maana yake kiongozi wa dini, Sheikh ni mtu hasahasa mzee ama mtu mzima anayeheshimika. Hivyo kuwa Sheikh haimaanishi ni muislamu. Muislamu hupimwa kwa matendo na imani yake sio kwa kuitwa Sheikh, ama Abdallah. Siku zote "Uislamu waweza kuwa waislamu, lakini waislamu si lazima kuwa Uislamu"

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 27, 2008

    Shekh Yahya atamtwangia albadilu huyo aliemtapeli gari na kumshusha mshipa asiweze tanua na hilo gari la wizi

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 27, 2008

    Nikiwa mdogo mimi nakumbuka alikitabiri ni watu wangapi funga zao zimekubaliwa baada ya Ramadhani. Mara nyingi ilikuwa watu watatu au wawili tu Afrika ya Mashariki nzima. Sijamsikia tena kutabiri hayo lakini wakati wa uchanguzi wa 1995 alitabiri kuwa atashinda mtu mwenye nywele kidogo - what a hedge kama angeshinda Mrema (TRUE) and even Mkapa (TRUE). Haram, thumma haram.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 27, 2008

    Nakubaliana na wadau wa May 27, 2008 3:48 PM na May 27, 2008 3:57 PM na May 27, 2008 4:05 PM,na msimamo wangu naamini ya kwamba mafanikio yanaletwa na bidii ya katika kile unachojishughulisha nacho,pamoja na ucha Mungu,lakini tatizo binadamu hatuna subira na imani,pindi tunapomwomba mola.
    Hii hupelekea kufata njia za mkato ambazo ni kufuru kwani hazikubaliki katika imani zetu.
    Kila binadamu ana utashi wake,hivyo uamuzi ni wake mwenyewe.
    gEoRGe

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 27, 2008

    Naona Mzee kaamua kwenda commercial siku za hapa karibuni utamwona kwenye CNN,hayo mambo hua sio kweli

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 28, 2008

    mungu anasema kuwa: Hakika ya pombe, kamari, kupiga ramli au kuabudia sanamu ni HARAMU na ni katika njia za shetani. jiepusheni nazo ili mpate kufaulu.
    Je huyo anayejiita SHEIKH Yahaya Hussein ameisoma hii aya kwenye kitabu cha mungu au yeye dini gani?
    aache ushirikina mwanga mkubwa huyo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 28, 2008

    Michuzi Ittaqi Allah (Muogope Allah),Unajimu na Ramli ni Haramu na shiriki kwa Allah.. naamini wewe ni kati ya waliotoa shahada. Huna haja ya Kupost Hii... kwani ni ujumbe kwako.. na kama unaona kuna faida ya kuwafaidisha wengine basi ipost.. Mtume s.a.w anasema man Ata Kaahin faqad kafara bimaa unzila allaa muhammad..atakayemuendeea mpiga ramli basi kakufuru alichoshishiwa Muhammad, sasa kama kumuendea ni kufuru vipi kumsikiliza na kufata afanyanyo.. Allah peke yake ndio Allaamu Alghuyuub.. Mwenye kujua yaliyofichika.. MUOGOPE ALLAH, BLOG YAKO ITAKUFIKISHA USIPOPENDA NA SIPOPENDA YEYOTE MWENYE AKILI KUFIKA.
    Maa Salaam

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 28, 2008

    HUHITAJI KUWA PROFESA KUJUA UONGO WA WANAJIMU NA WAPIGA RAMLI, KILA GAZETI LINATOA NYOTA TOFAUTI, NA KILA MTABIRI ANASEMA TOFAUTI NA MUNGINE. DINI ISHATUKATAZA NA NI SHIRKI KUWAFWATA NA INAPELEKEA KUFURU. MUOGOPENI ALLAH. .. DALILI ZIPO WAZI WAZI KATIKA KITABU TUKUFU NA HADITHI SAHIHI. HAMNA HJA YA KUSHINDANA NA ALIYOANDIKA NA KUPANGA ALLAH YEYE NDIO MWENYE KUJUA YALIYOFICHIKA NA SI MUNGINE...YAHAYA HUSENI NA WENGINEO TUBUNI KWA ALLAH KABLA HAMJAFA/HATUJAFA MANAAKE MAUTI HUTUJIA BAGHTA (GHAFLA), NA UKIFA NA SHIRKI HUSAMEHEWI KWA KAULI YA ALLAH INNA ALLAH LA YAGHFIRU AN YUSHRAKA BIH WA YAGHFIRU MAA DUUNA DHAALIK LIMAN YASHAA...TUNAKUBALIANA KWAMBA KILA ALIYETOA SHAHADA ATAINGIA PEPONI.. KAULI YA KUTOSAMEHEWA MAANA YAKE UTAADHIBIWA NA MOTO KWANZA NDIO LATER UTASAINGIZWA PEPONI BAADA YA KUTUMIKIA ADHABU UNAYOSTAHIKI KWA KUMSHIRIKISHA ALLAH. JAALANA ALLAH WA IYAAKUM FIL FIRDAUSI AL AAALA.
    NB SOMENI DINI YENU JAMANI... HAKIKA WAMCHAO ALLAH KATI YA WAJA WAKE NI MAULAMAA.. (QURAN), WE R TOO DOWN TO EARTH... JAMANI

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 28, 2008

    mbona hiyo tovuti ni bomu haifanyi kazi?????????????????????

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 28, 2008

    mimi nitamwita yahya hussein kwani tittle ya shekhe kwa kiswahili ni mtu mwenye elimu ya dini ya kiislam na kiarabu ni mzee, sasa yahya hussein mwisho wake unaonekana mbaya, ku practise uchawi ni kufuata nyayo za shetani na ni kukufuru, kama ALLAH ANA VYOSEMA SURA YA 2: 102("Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi").sasa yahya mimi naona wewe upo ofisi moja na mashetani kwa mujibu wa aya hii. na kama aya hii yahya hussein unajifanya uijui basi unaangukia kwenye kundi la kukubali baadhi ya aya na kuzipuuza nyingine kama allah ana vyosema sura ya2 : 85("Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayo yatenda")
    so yahya hussein kama hutofanya toba kabla kifo unaenda pabaya

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 28, 2008

    Biblia inasema na alaaniwe yeye amtegemeaye mwanadamu kuwa kinga yake na ngao yake, wajameni haya mambo hayafai ni kufuru kwanza kwa Mungu.bidii zetu katika maisha na kumuomba Mungu ndio inatufanya tufanikiwe na si vinginevyo.
    Ms Bennett

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 28, 2008

    Dah!! nakumbuka miaka ya nyuma enzi hizo tunaambiwa TV/ Video ANASA..Huyo mzee nadhani alikuwa mtanzania wa kwanza kuwa na video .. bsi shuhudia siku atakapotangaza kuitoa nje kaTV ka nchi 21 ,tulikuwa tunakanyagana kwa jinsi watu walivyofurika mbele ya nyumba yake pale Magomeni mikumi ..kuangalia mpira na miziki ya Luambo..Akhasente sna sheik ulitufungua macho .. jamani tumetoka mbali kweli .. hivi siamini kama ilikuwa kweli ....

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 28, 2008

    Huyu bwana Yahaya ni tapeli kweli. Simuiti Sheikh, maana ingawa hiki si cheo cha kidini, ni neno la kiarabu linaloashiria heshima. Huyu hahitaji heshima, bali karipio. Anatumia jina la Mwenyezi Mungu kujipatia ujira mdogo!! Hakika atapata ujira unaofanana na matendo yake siku ya masiku. Mwenyezi Mungu anasema, Yeye anasamehe madhambi zote isipokuwa shirk - yaani kujipa, au kumpatia asiyekuwa Allah sifa za Allah.
    Matukio ya hivi karibuni ya imani za kichawi hapa nchini yanachangiwa na wapotofu kama hawa, na wanayefanana naye katika madhehebu mengine. Wanawatisha watanzania kwamba karibu wote tuna majini au mashetani au mapepo na wao wana uwezo wa kuyatoa.
    Michuzi, kwa kuweka tovuti yake, sijui utaambulia nini. Ama itasaidia watu kuelewa kwamba Yahaya ni mshiriki wa dhambi kuu, au utakuwa promota wake. Mungu akusaidie. Amin.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 28, 2008

    Shirk ikishakuingia husambaa kama sarakani na bila kutaka kinga ya Allah ambukizo lake ni mara moja. Kwa wanaomjua Yahya Hussein huogopewa na watu wengi na pengine hata Michuzi anagwaya kuitoa hii tovuti. Lakini pengine ni bora kwamba sijaona sifa alopewa hapa bali makaripio na ishallah kwa kuwekwa hapa ataonywa aonyeke. Hapana asojua kuwa ramli ni haram na thumma haram.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 28, 2008

    Shehe Yahya hutauza 'details' zetu tutakazo kupatia ktk webusaiti yako kwa vyombo vya 'sirikali'? maana historia yako inautatanishi.

    Nimesoma kisa cha kusisimua ulipokuwa unafanza vitu vyako Swaziland, stori ya mambo yako makubwa ni kama vile agenti wa KGB,Mosaad n.k rejea webusaiti ya [[http; www.zanzinet.org/files/darkside.txt]].

    Shehe tuondoe hofu ya 'Darkside' sie wapenda 'nyota', ili tuwasiliane nawe tuje bhakti na dhahama zitakazotukabili ktk mihangaiko hapa duniani.

    Mdau
    Rocky
    London

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 28, 2008

    nyie mnaomkandia mnajiamini nini?atawageuza majini,hamuonagi anaonyesha majini yananyonyesha mara sijui nini..sasa zile picha sijui anazitoa wapi au za sinema?hatari

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 28, 2008

    Dawa ni kutoangalia lolote kumhusu huyu. Maana ukianza tu unakuwa mtumwa wake!! Hujiamini wala hutamuamini Mwenyezi Mungu bila kufuata yale yaliyosemwa na WATABIRI kwenye nyota.

    Mimi hujiepusha na mambo ya watabiri maana kuna wakati nilianza kufatilia nyota za magezetini nikawa nakosa raha pale unapoona jambo baya. Baadae nikarudi nyuma na kugundua nimeathirika na hizo nyota hizo, SO NAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU NIMEACHA KABISA KUANGALIA WALA KUFUATA CHOCHOTE. Ninasubiri maajaliwa yangu kutoka kwa MUUMBA.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 29, 2008

    Namuomba Mwenyezi Mungu atukinge na vitimbi vya mashetani na washirikina. Katika uislam hakuna kitu kama kutazama nyota wala nini, unatakiwa umtumainie Mwenyezi Mungu kwa kila kitu

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 30, 2008

    Usilolijua ni Usiku wa Giza!Daima Litakusumbua.Wale walio ifuata Nyota hadi Mtoto Yesu alipozaliwa tutawaitaje,washirikina au wasoma nyota?Astrology ni moja ya Fani au Taaluma za Zamani sana hapa Ulimwenguni.Kalenda unayoijua na kuifuata hii leo ni matokeo ya Kazi kubwa ya Miaka Mingi sana ya Usomaji wa Nyota!Shk.Yahya asihukumiwe tokana na Ujinga wetu!Yeye mwenyewe pamoja na kuwa stadi wa kusoma nyota hawezi kutabiri lini ataiaga dunia kwa mapenzi ya Mola!Kwa hiyo watu wasichanganye mambo wasiyo yajua asili yake na hatima yake.Asalaam Aleikhum WaBarakatu!

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 30, 2008

    Nyota waliyotumia mamajusi kumwona Yesu hawakuonyeshwa na sheikh au mganga wa kienyeji aliyewadai pesa. Mwenyezi Mungu ndiye aliwaonyesha na kuwaongoza.

    Kinachokataliwa ni hizi nyota za viganjani za Akina Sheikh yahya ambao wanakuangalia kiganja badala ya Juu aliko mwenyezi Mungu halafu wanaanza kukutabiria mambo!

    Hizo nyota za viganjani ambazo Mwenyezi Mungu haonyeshi watu bali watu ndio wanaonyesha watu hizo ndizo tunaziita ushirikina.

    Mwanadamu kuibuka na kukuambia nyota yako hii ndiyo ya kukuongoza huo ni ushirikina.Mtu haongozwi na nyota huongozwa na mwenyezi mungu tu peke yake.Kuendekeza watu kuamini kuongozwa na nyota ni ushetani mkubwa.

    ReplyDelete
  30. Mimi naona utabiri wa Sheikh Yahya ni mzuri kwani unatofauti kubwa kati yake na wanaopiga ramli kwa waganga. Kwa ufupi elimu hiyo ya Astrology hata na Nastradamous kwenye kitabu chake ametabiri mambo mengi na yakaja kutokea duniani. Hivyo basi maswala ya utabiri ni muhimu kuwepo kwani yanasaidia kuongeza chachu katika ushindani na uvumbuzi

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 25, 2009

    Sheik naomba uwasaidie watanzania jinsi ya kuchukua mali zilizofichwa na Wagerumani ndani ya nchi yetu. Pia naomba utuambie ni ujanja gani waliotumia kuzificha. Nijibu kupitia Fabimanyonyi@yahoo.com

    ReplyDelete
  32. jamani nimejaribu kufungua website ya sheikh yahya mbona haipatikani toka mwaka huu unze kwenye mwezi wa nne. je kuna mabadiliko yoyote yametokea au tovuti imefungwa

    ReplyDelete
  33. mbona tovuti ya sheikh haipatikaniki inakuja mabo mengine kunani twaomba mtujibu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...