CAMEROUN WAMEPATA BAO DAKIKA YA 20 YA KIPINDI CHA PILI BAADA YA IVO MAPUNDA KUSHINDWA KUZUIA KROSI YA JUU AMBAYO KATIKA KUDAKA UKAMTOKA NA KUDONDOKA MIGUUNI PA SAMUEL ETO'O AMBAYE AKIWA NDANI YA SITA AKAACHIA MKWAJU KATIKATI YA MSITU WA MABEKI WA STARS NA KUTINGA WAVUNI
Home
Unlabelled
CAMEROUN YAPATA BAO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


haya kayataka Maximo kutuweke kipa bomu.
ReplyDeleteYanga wanajua hawana kipa ndio maana wakamnunua Kaseja kwa milioni 36 na kumfanya kipa ghari kwa afrika mashariki yote.
kwanini Yanga wamgharamie pesa zote wakati Mapunda yupo?
kama angekuwepo Haruna Moshi Boban basi Cameroon wangeipata zaidi.
ndio faida ya kuwa na kocha mbishi ambaye hashauriki na anatudharau sisi wadau wa mpira na wazalendo.
ndio kawaida yetu kuwababaikia wageni.
Tunaomba wanaomkingia debe Maximo wamwambie awarudishe hao wachezaji.
yeye kocha vipi ashindwe kuwafundisha nidhamu wachezaji?
na yeye amekuwa akilalama kuwa amekuja kujenga msingi wa nyumba kwani kiwango chetu kibovu. sasa kama kaja kuweka misingi basi aweke na nidhamu.
mara anasema Boban hamrudishi hadi amuone lakini kamrudisha Mapunda wakati alikuwa nje ya uwanja kwa miezi sita na hakumuona.
kamleta Michael Chuma ambaye hakumuona ila kamsikiliza tu.
Boban alimchagua wiki tatu zilizopita na akamfungia baada ya wiki, Boban akaomba msamaha.
lakini Maximo akasema amemsamehe ila hawezi kumpanga hadi amuone.mtu uliyemchukua wiki tatu kwa kiwango ulichorodhika nacho. baada ya wiki unasema hujui kiwango chake.Maximo acha kutuonea.
Mapunda hajaomba msamaha na anapeta.
serikali ingilieni kati hili tunapoteza pesa nyingi sana na maximo kafuata wallet (pesa) yetu tu.tukiwa hatuna kitu atatukimbia.