meneja wa kilaji cha kesto mpeli nsekela 'kiongozi' hana mbavu baada ya kutaniwa na mapaparazi juu ya mkataba wa kuwa wadhamini wakuu wa kombe la kagame cup 2008 wa shilingi milioni 80 uliotiwa saini katika hoteli ya moevenpick usiku huu hapa jijini dar na bosi wa masoko wa kampuni ya bia (tbl), david minja, na rais wa cecafa na tff, sir leodehar chilla tenga, huku katibu mkuu wa cecafa nicholaus musonye akishuhudia wingi ya kulia.
kampuni ya bia kupitia kilaji chake cha castle lager wamefungua ukurasa mpya wa kuendeleza soka eneo la ist afrika mashariki na kati ambapo kuanzia julai 12 hadi julai 27 mwaka huu mashindano ya kombe la kagame yatarindima neshno na kuoneshwa moja kwa moja na tbc ambao wamenunua haki ya kufanya hivyo kwa dau la shilingi milioni 60.
klabu zitazoshiriki ni yanga na simba (bara), miembeni (zenj), apr na rayon sport (rwanda), benadir (somalia), cid (djibouti), ten ten (eritrea), tusker (kenya a.k.a watani wa jadi), ura (uganda a.k.a ukweni), vital'o (burundi) na awassa ya ethiopia.
pazia litafunguliwa kwa mchezo kati ya simba na tusker hiyo julai 12, 2008. meneja wa kesto 'kiongozi' mpeli nsekela amesema wadau wa soka wa dar, morogoro, arusha, mwanza, mbeya na a-taun wakae mkao wa kula kwani kutakuwa na burudani safi kuanzia wiki hii ambapo promosheni za castle lager zifanyika huko.
pia tbl imeandaa vituo kibao kila sehemu nchini ambavyo kutakuwa na luninga la wadau kujionea laivu mashindano hayo kupitia tbc. kazi kwenu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2008

    david nakuona mtu mzima,shavu dodo!!!
    bonjo kuna hara yake jamani,big up!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2008

    THAT DAVID MINJA IS HOT...
    KAKA MICHUZI NAOMBA CONTACT YAKE PLIZ USIBANE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...