Hiki ndo chuo kikuu cha Dodoma. Kwa mwaka wa 2007/2008 kina jumla ya wanachuo 1200, na katika mwaka 2008/2009 kina mpango wa kuchukua wanachuo 5000. Kwa hiyo nawashauri ndugu zangu ku-apply digrii na diploma mbalimbali.
Kuna digrii zaidi ya 40....chaguo ni lako...karibuni sana brothers and sisters.
Thank you.
By Peter Munisi,
Dodoma university student,
my e-mail ni archibody@yahoo.co.uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2008

    wewe uliyetuma hili tangazo inaoneka wewe mwenyewe haujaenda shule ,kwanza unasema chuo kikuu cha dodoma university what do you mean ,umeshasema chuo kikuu cha dodoma sasa hiyo university tena inatoka wapi ,halfu umeshasikia wapi chuo kikuu kinatoa diploma hicho kitakuwa chuo au uchwara kuwa makini na unayoyaleta humu unaweza ukaonekana chizi

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2008

    Ni hatua moja mbele.Hii ni nzuri.
    Kiko mbali na mji?Manake vikianza vikao fulani,ninakuwa na wasiwasi na dada zetu hapo chuoni.Tena mwezi huu tu kuna kikao cha naniiii.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2008

    aisee,i used to be shy to admit that i am from Tanzania here where i live in kentucky,usa but now i am proud to say AM TANZANIAN. kwakweli,mfumuko wa vyuo(kwa kusaidiana na issa michuzi anaetuupdate sisi wa huku ulaya) unatusaidia sana!..naona UDSM,univ of sokoine,dodoma,tumaini,st.john etc yani vyuo sasa ni vingi na mtu anakuwa na choice,pia college zipo nyingi INATIA MOYO kwa sisi ambao enzi zetu there was nothing!!

    BIG UP TANZANIA

    MUNGU IBARIKI TANZANIA,
    MUNGU MBARIKI ISSA MICHUZI

    THE BIG DON!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2008

    MTOA MAONI HAPO JUU AFUATILIE MAMBO VIZURI. ATAJIFUNZA. CHUO KIKUU CHA DAR KINATOA SIO DIPLOMA TU ILA HATA CERTIFICATE(TENA YA SHERIA.) ASI KARIRI KUWA UKIJIUNGA NA CHUO KIKUU BASI UTATOKA NA SHAHADA PEKEE.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2008

    SAFI SANA DOGO, Nimeipenda Blog yako! imetulia hiyo.
    Kuhusu chuo kutoa diploma au Digrii sioni wewe inakuhusu nini we soma bwana achana na huyo ashakosa chuo ni shida tu kwake! kwani we ndio mpanga mitaala?


    --Mchochole, Masikini, Kapuku, Hamnazo The Have Nots
    Aminia Mshkaji imetulia sana blog yako!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2008

    We Anony wa kwanza 6:04 PM hapo juu ni zumbukuku kweli, kwanza unavamia tu hii blog, na wala hujui lugha inayotumika humu unaanza tu kuvamia watu. Kutumia lugha kama Chuo Kikuu cha Dodoma Univesit ndiyo lugha fasaha ya hii blog....Pia inaonyesha ulivyo zumbukuku kuwa eti univesit haitoi diploma....vyuo hata Havard na Oxford na pia hutoa diplomas na hata certificates....
    Usivamie tu gari kwa mbele, jifunze...

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2008

    Wapande miti iote sambamba na ujenzi. Hasa miti ya matunda! Hata kama ni kupanda mizabibu inaweza kukifanya hicho chuo kijitegemee kwa "raisins" (CHEKA) pamoja na kupanda matikiti na "watermelons" kwani wa-Israeli (kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Dunia - miaka ya kumalizikia 1960s) walifanya uchunguzi kwamba maeneo ya Dodoma yanaweza kuzalisha hayo mawotameloni kukidhi mahitaji ya Afrika Mashariki...lakini tulipuuzia utafiti wao!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2008

    Teh teh teh! Nilijua kuna baadhi ya watu ambao huwa hawana sense of humour watakurupuka baada ya kusoma kichwa cha habari!! Dang people, loosen up:-)

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2008

    Anon wa kwanza; You lose your sense of humour...! Please save your breath, huyo jama huyo alo post hiyo habari, nna hakika anajuwa hicho unachojaribu kukmkosia, lakini hiyo ni lugha ya blog tu ndo kaamuwa kuchanganya chuo kikuu na university.
    Inakubalika endapo anaeleweka kwa jamii husika, na nna hakika wengi wetu (isipokuwa wewe) humu tunaielewa hiyo lugha ya blog yetu "kiswa-english"

    Pili chuo kikuu kutoa diploma na degree ni jambo la kawaida duniani,hata UDSM wanatoa diploma kwa kozi za computer!Pia kuna mpaka post garaduate kozi (diploma) ualimu!
    Kwa hili naomba jifunze uelimika zaidi!

    Waswahili wanasema "..ujanja mwingi mbele kiza...!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2008

    OOOOOOOOOOOOOPS!! Sorry anony. june 04,06.04pm.Next time be careful or rather think before you act.What a shame!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2008

    wewe wa kwanza hapo juu mwenyewew nenda shule hivi unajua maana ya diploma kwanza au hata degree huna...usiongee tu...tafuta dictionary uangalie diploma ni nini? acha hizo...nenda shule wewe kwanza msiwasimange wenzenu kwa makosa ya kijinga lakini diploma hajakosea chochote...kwa taarifa yako a diploma is a document certifying the successful completion of a course of study. Sasa usikurupuke tu na kujifanya much know


    By the way chuo kinaonekana kimetulia sana hicho....kazi nzuri sana ....

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 05, 2008

    daa kweli kuna mzumbukuku mengi watanzania,liangalie hili nalo anon.6.04 pm anajifanya anajua kumbe hata darasa moja halina,chuo kikuu cha dar es salaam kuna hadi certificate hata hiyo diploma.nenda kasome kabla haujaanza kupinga watu,mwangalie mimacho yake,

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2008

    mi wasiwasi wangu ni kuwa hawa UDOM wanatangaza watachukua watoto wengi ili watu wafurike kuapply kama mwaka jana. Kisha wanachukua wachache. Huu ni wizi. wanatuibia sana sisi wazazi.

    Mbaya zaidi, wanapokea kila cheti wakati application. sio kama UDSM ambako kama mtu hana sifa hapewi fomu hivyo hela yake inapoma, dodoma hata ukiwa hufai unauziwa form. Wajirekebishe haraka.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 05, 2008

    Wewe anony wa kwanza mshamba kweli kweli.Nani alikwambia Universities hazitoi Certificates au Diploma??.Usichangie vitu ambavyo huvijui.Hiyo Form six yako usiilete humu kwenye blog yetu tukufu.
    Hicho kichwa cha habari ni lugha yetu ya Blog,ndo maana michuzi huwa hagusi(ha-edit?) hata herufi moja.
    ZIPO NYINGI TU LUGHA ZETU.KUNA GREEN VEST YA KIJANI,BARABARA YA..KAWAWA...ROAD,MTAA WA CONGO STREET n.k.
    Tulia uliza Blog ni nini mshamba wewe,umetuchefua.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2008

    WEWE ULIYETOA COMMENT HAPO JUU UMESOMA KWELI AU UNAKURUPUKA TU HUJUI CHUO KIKUU KINATOA DIPLOMA NA CERTIFICATE PIA AU UMEKARIRI CHUO KIKUU NI DEGREE TU POLE SANA

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2008

    kaka michuzi hongera blog yako inafanya kazi sana. nakushukuru sana kaka uliyotoa huu ujumbe mi nashida sana ya kwenda hicho chuo naomba msaada wako kulikoni mi nije dodoma naomba tuwasiliane email yangu ni Proditram@gmail.com
    natanguliza shukurani za dhati.
    sweet,
    Arusha.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2008

    ukweli ni kwamba kwa dodoma udom mpo lose sana..wanafunzi kutwa nzima wanazunguka mjini na ucku wapo 84..shall we make it? nimefuatilia utakuta wiki nzima mtu ana vipindi viwili..ndo maana wanapata muda wa kuzurura,kuweni busy kama chuo cha st.john's..in such a way ukimaliza chuo unakuwa mtu wa reasoning kiukweli ukweli..coz unakuwa umesoma vitu vingi..ni hayo 2..chunda mkazi wa dom nipo bcom ud..2po likizo ndeeefu mpaka sept..

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 05, 2008

    Mr.Munisi Kwa faida ya wanablog ambao hatujawahi kufika chuoni hapo hilo jengo ni la nini?.nadarasa,mabweni,utawala,maktaba n.k.Ni kizuri.
    Michuzi mruhusu bwana munisi aongeze picha zingine mbili tu za chuo (Matangazo ya elimu bure mr.Issa Michuzi si ndiyo mzee wa kazi?au?)

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 05, 2008

    dah mbona anon wa kwanza kashambuliwa hivyo,msameheni!

    miss keys

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 05, 2008

    Haya siyo mafanikio haba ndugu zangu watanzania.Tjis is a Monumental Landmark achievement!Big Up to the Authors of the Idea.Tunataka tuone kila kijana aliyemaliza Kidato cha Sita(FormSix) hapa nchini anapata nafasi ya kuendelea na masomo yake Chuo Kikuu.Na mambo yatapendeza zaidi iwapo Vyuo Vikuu hivyo vitakaribisha wanafunzi kutoka hata nchi zingine duniani.Multicultural Training Centre ina utamu wake.Chuo kiwe more Internationalised than Localised to make it Richer academically!Tunasubiri kuona Chuo Kikuu maalum cha PolyTechnics!Hapo sasa.Dodoma sasa itachangamka zaidi.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 05, 2008

    ninyi wazushi sana mliokuwa mnanipiga madongo kuhus maoni yangu niliyota kuhusu chuo kutoka diploma ,tatizo lenu nyie ni mabox hayo mnayobeba ndiyo yanawatia wazimu mameamua kukimbilia ulaya kusoma lakini matokeo yake mnakuwa wehu mlichokitegemea sicho hicho mlichokikuta mimi sikuamanisha chuo kukuu wapuuzi wakubwa nyie nilimanisha chuo kikuu cha dodoma kuwa hakina dploma kama mnadhani kuwa mimi sijasoma kwa taarifa yenu mimi ni mwamlimu nafundisha hapahapa dodoma ,rudini nyumbani ache ni kuwa watumwa na hivyo vidiploma vyenu mnavyovipigia debe na mkija huku hakuna kazi ya kuwapa shule ni ud ,mzumbe sua na dodoma lakini mkija na hivyo videgree vyenu vya mabox lazima tuwaweke benchi wapuuzi wakubwa nyie

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 05, 2008

    naungana na mdau hapo juu mm ni denti wa udom wale wadau wa nje namaanisha university of dodoma,ni kweli kabisa tupo lose hata mauggo na nancy wanajua hilo.sup zipo za kumwaga hatujui tatizo ni letu au lecturers.
    mdogo wangu munisi blog yako ni nzuri ila tunahitaji picha ulizotafuta mwenyewe na sio kuchukua za internet kama vp sema tukutumie.
    udom hatusomi watu ni kulala na kuangalia muvi 2 hapa kisasa.digree yetu itakuwa ya muvi 2.na mwaka wa pili nitarudi mm 2 wengine wote watadisco!! coz mm nilikuwa nasoma.msema kweli ni mpenzi wa mungu na huo ndo ukweli tusifiche maovu.kesho tunamaliza mitihani,nawatakia likizo njema
    ciou!!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 05, 2008

    haya bwana na shule yenu isiyokuwa na ubusy wa shule...anagalieni senema na kwenda kwwenye michuzi(supu) asubuhhi mpaka jioni mkidhani ni ujanja...manake kumbukeni mkimaliza mnataka kazi na kazi siku hizi mmmh ndo ivo manake itaonekana hamna kitu...shauri zenu

    nyaningedere

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 05, 2008

    Kama kweli wewe mwalimu na ukaandika upumbavu hapo juu basi tumekwisha ndio maana wanafunzi wanatoka hata hawawezi kupata kazi kwenye soko la dunia . Kabla hatujakanyaga bongo tunapewa kazi mnaanza kutafuta juju...eti mutuweke bench nakuja soon na nitakutafuta nikuonyeshe kazi niliyopata tayani na bado hata sijakanyaga ardhi....looser

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 06, 2008

    Nyie mnaosema Dodoma University inachukua watu wa kila aina na sio kama UDSM mnakosea sana. Sio kila chuo kitalingana na chuo kingine kwa vigezo fulani vya kuchukua wanafunzi. Kumbuka maana ya kuchukua wanafunzi wenye vigezo fulani ni kukuza umuhimu wa chuo na kwa wakati huo huo wakijua fika kwamba wale wasiowataka watachukuliwa na vyuo vingine pia.
    Havard ina vigezo vyake hata kama una GPA ya 4.0 bado kuna vigezo vinginevyo lakini ukishindwa kupata nafasi hapo utakwenda vyuo vingine vinavyoweza kuwa vinakuhitaji. Ikumbukwe kwamba hata aliyepata Division four ni PASS hivyo kama UDSM haimchukui kuna vyuo vinaweza mchukua kama amefanikiwa kupata vigezo vingine kama mika miwili kazini au kuwa na PASS ya division three, two au one form Four.
    Halafu hawa wanaoanza kusema watu fulani wana chuki na vyuo vya TZ kwa kuwa ni wabeba maboksi wanaonyesha uwezo wao wa kimasomo hawautumii vizuri. Kama kweli wewe umesoma na kutumia akili/elimu yako vizuri na una-degree ya UDSM, Mzumbe, Tumaini au OPEN university huwezi msema mwenzio kwa sababu wote mna degree inayotambulika kama degree. watu wengi unaowaita wabeba maboksi waliondoka TZ kuja kusoma hapa USA, UK, Canada kwa kuwa vyuo vingi vilikuwa haviwapi nafasi ya kusoma hapo Nyumbani na kama walipatanafasi basi migomo ilikuwa mingi sana kiasi cha mtu hamalizi chuo. Pia miaka hiyo ukumbuke vyuo vikuu vilikuwa vichache sana hapo TZ sio kama leo hii. Na najua watu wengi unaosena ni wabeba maboksi sasa wanafurahi sana kuona kwamba dada zao na kaka zao wanasoma katika vyuo vikuu hapo nyumbani na kumaliza degre zao na idadi ya wasomi inaongezeka sasa. Kwa mimi niliyesoma nje ya nchi (ulaya) shule ya msingi,halafu nikasoma sekondari nyumbani (Tanzania), halafu sekondari ya kati(high school)nikasoma nje ya nchi (marekani), halafu nikarudi nyumbani TZ kujiunga na jeshi la kujenga Taifa (JKT)na kuanza kusoma Tanzania chuo kikuu kishiriki cha Muhimbili hadi migomo ilipoanza na kuja kumalizia degree yangu hapa marekani , na pia kumaliza degree yangu ya pili hapa marekani ninashindwa kukuelewa. Hasa mnaposema tukija tutakuta kazi hakuna wakati kila siku tunakuja na tunakuta hizo kazi zipo hapo nyumbani na tunaomba wasomi wetu wa nyumbani wazipate , maana mimi ninao uwezo wa kufanya kazi popote kwa elimu yangu na hati yangu ya ukazi wa marekani huku nikiwa bado raia wa Tanzania. Ninachoomba ni wasomi waongezeke na watoke ili tuwe na wasomi wengi huku na kule.Wewe kama mwalimu unapokuwa na roho mbaya za kuona ndugu zako walio nje ni wabeba maboksi unaonyesha chuki binafsi.
    Hili la "reasoning" la kusoma nje lina utofauti na huwa halina ubishi- kwa kuwa hata wewe utakapomaliza chuo hapo TZ bado utahitaji kuona vitenda kazi vya vitu ulivyosoma katika vitabu, na namna ya kuviona ni kutoka nje iwe Kenya, Uganda , South Africa, Urabuni, Ulaya na hata Amerika.
    Kumbuka msomi anapomdharau msomi mwenzie badala ya kuunganisha nguvu za elimu - ujuzi(Education - experience), elimu - ufahamu( Education - knowledge), na elimu -uraia (Education - culture) - basi ana matatizo makubwa.
    Hili la watu kuwa huku na hawana mpango ni la kupita tu na pindi watakapoweka mambo yao sawa na kwa elimu yao walionayo watafika wanakotaka kufika.
    Tuijenge nci na wala sio kusema au kuandika kwa dharau kama vile hujasoma, waache wasiosoma waandike alkini pia usiwadharau maana watafika wanapopataka siku moja.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 06, 2008

    Hii ya kuwaruhusu watu wenye CPA, CSP kufanya Masters inanipa utata mkubwa kabisa.
    Wengi wa watu hawa waliosoma zamani kwa mfumo wa form four, halafu DSA(ya zamani-kurasini), wakichukua NABOCE/NAD, au NSC/NDMM huku wakifanya mitihani ya bodi ya NBAA au NBMM na kufaulu hadi CPA au CSP. Inabidi watu kama hawa pamoja na CPA/CSP zao au madaraka yao warudi kufanya baadhi ya madarasa/masomo ya Undergraduate kama manne au matano ndio wakubaliwe kujiunga na Masters programs (MBA)
    au
    wakubaliwe kujiunga na Masters program lakini credits zao ziongezwe masomo manne zaidi kama CPA/CSP zao kabla ya kuzipata hawakupitia vyuo vya high learning vyenye utaratibu wa mtaala wa wizara ya elimu ya juu na sio Wizara ya Fedha kwa wakati huo,vyuo kama UDSM, MZUMBE, NYEGEZI vilikuwa chini ya mtaala wa wizara ya elimu ya juu etc
    sababu ni kwamba ukimchukua mtu aliyesoma DSA(ya zamani)- NABOCE,NAD 1, NAD 11 na CPA kwa mtindo wa bodi ya Uhasibu hadi kupata CPA atakuwa amesoma kama masomo kumi na nane jumla. Wakati aliyesoma MZUMBE, NYEGEZI, ARUSHA na UDSM au kwa sasa NIA( DSA ya zamani) na kupata CPA jumla huwa wamesoma masomo thelathini na sita(36). Hivyo hawa ni sawa kusoma masters bila matatizo.
    Rekebisheni hii japo CPA/CSP zote ni moja bali lazima uangalie ulingano wa wote na ubora wa elimu. Hii inafanyika sana hapa USA.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 06, 2008

    Kusoma tu bila international Exposure ni ujinga wa hali ya juu.
    University of Dodoma is a growing secondary school. full stop.

    kama Chuo kikuu cha DSM ni kiboko vipi kazi zinachukuliwa na wakenya?
    mkifika UDOM AU UDSM mijadala yote kwa kiswahili na wote wazalendo watupu.

    majuu unasoma kitabu kilichotungwa na lecturer wako anakufundisha.
    wanaoweza kusoma nje waende.wakiwa hawana uwezo wa kusoma nje basi waende UDSM AU DODOMA.

    NI SAWA NA MTU KUILINGANISHA YANGA AFRICA NA MANCHESTER AU LIVERPOOL YA MICHUZI.

    VYUO VYETU BADO NI MBINGU NA ARDHI.
    TUNAVIPENDA LAKINI IKIPATIPATIKA FURSA YA NJE, NJE NI BORA.

    INTERVIEW ZA KAZI WATOTO WA UDSM WANSHINDWA KU PERFORM.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 06, 2008

    ushauri wa bure..acheni kuandika ujumbe mreeeefu,sisi sio madenti wako kusema unatupa lectures.toa comment zako jikatae unatupa darasa la nini? kuwa brief nenda straight to the point..we need short and clear messages.atlanta

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 07, 2008

    siyo UDSM tu inayotowa Diploma au Certificate hata vyuo vya USA, UK, CANADA, kote duniani vinatoa Diploma na Certificate, hata HARVARD UNIVERSITY inatoa Certificate, na kuna course zingine hata cheti hupati, kwa hiyo si ajabu kwa CHUO CHA DODOMA KUTOA CHETI AU DIPLOMA.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 07, 2008

    Ndugu zangu wazalendo wa TANZANIA ninawashukuru kunipata nafasi ya kujieleza kidogo. Mimi ni shabiki wa siku nyingi wa KAKA MICHUZI na kazi anaoyfanya ni great! Tataizo langu mimi ni kuhus lugha ya KISWAHILI anavyoitumia naona KAKA MICHUZI anatumia SLANG NYINGI SANA hasa kwenye headline zake maneno amabayo sio kiswahili fasaha ( Sisi wazalendo wa KItanzania tunaelewa) lakini watu wa mataifa mengine ambao wako katika harakati za kujifunza lugha hii yetu wana kuwa kufused HASA pale anapochukua neno la kiingereza kama NATIONAL STADIUM na kusema uwanja wa NESHINO !!!! hii kwangu mimi naona ni kuidhoofisha hii lungha hasa katika blog kama hii ambayo inasomwa dunia nzima. Ninaomba maoni yenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...