Michuzi,
kwanza naomba jina langu lisirushwe hewani wala address ila huu mchango tu.
kwanza niliposoma kuwa kuna mwislamu (mke ) na mkristo (Mme) wamekaa pasipo ndoa kwa miaka 14. na wamezaa, ila kwa sasa kwa kufupisha story wanataka kutoa uahamuzi wa kutengana.
kwa kweli huo uhamuzi mimi siuhafiki kwa sababu kuu zifuatazo.
1. wamezaa watoto, watakuja kupata tatizo mfano:- wakielemea upande moja, na upande huo baada ya kutenngana na kuoa au kuolewa watapata mateso kama unavyo jua mateso ya mama wa kambo au baba wakambo, inabidi wafikirie kwa makini kabla ya kutengana.
2. kumbuka ndoa haichwi kwa namna ingine zaidi yoyote ya zinaa tu, kwani unaweza kuacha ukaingia pabaya:- kwalugha ingine ukaruka majivu ukakanya moto na wakati unarudi kuomba msamaha ukaonekana mjinga kwani wapo watu wengine wanatamani utajiri au uwezo wao waliochuma hao (mke) na (Mme) walio ishi bila ndoa kwa 14 watumie huo uchumi kwa manufaa yao na kujirusha pembeni na either vimwana au vidume na kuacha watoto wakitaabika na lawama kuwarudia wengine.
mfano mzuri kuna mama mmoja analia kuachwa na mwanamme alikuwa na tatizo hili ingawa mama alikuwa na uwezo mzuri alikimbia ughaibuni (UK) kwenda kusoma at least kupoteza mawazo, akiacha watoto wanataabika na mama wa kambo dogo dogo aliyeolewa na mmewe, watoto wanalia wanataka kurudi kwa mama na mama yuko ughaibuni na Baba hataki kuwaachia, sasa nani alaumiwe kazi kwako kujenga au kubomoa hiyo nawaachia wenyewe.
3. mwisho: kitu hicho janga au gonjwa la kisasa linanyemelea iwapo kuna mistake itakapo tokea mara baada ya kutengana na je huko nje mtakaa hivi hivi?
kazi kwenu kuska au kunyoa.
Mdau nanihii...


we nawe,wangapi wameachana hamjasema kitu.au leo kwasababu ni mkristo na muislamu..miaka 14 nini bwana,watu wamekaa miaka 50 kisha wameachana.mambo ya ndani waachieni wawili.mi niko divorced,i know what am talking about.nyie mnaona ya nje,ya ndani hamyajui.hata kama wananyanyasika au nk abaki tu,eti ili mradi alinde heshima,na kulea watoto.sometimes wazazi wanagombana mpaka kero kwa watoto,wao wenyewe wanaomba wazazi waachane ili makelele yaishe.kwanza mazingira hayo siyo mazuri kulelea watoto..nasemaje..ACHANENI if its not working..
ReplyDeleteMdau ulichoeleza ni kweli. Watoto kweli wanahitaji malezi ya baba na mama. Watu wajitahidi kupenda mahusiano yao hata pale dini inakuwa kikwazo. Naamini Mungu sio binadamu, na ataelewa huko mbele kwa mbele. La muhimu ni kuheshimiana.
ReplyDeleteInasikitisha sana jamani. mwanamke anakuja kulala kwenye kitanda ulichokilalia kwa miaka. Wanawake wengine hawana aibu. sijui wakoje na wanakubali vipi kuingia mahali wanajua kuna wife tayari.
if they are not happy waachane there is no need ya watu kulazimishana kuwa pamoja-unhappy hayo ni mambo ya kizamani
ReplyDeletekama wameamua kuachana vizuri tu
ReplyDeleteMICHUZI, ZINAA NI ZINAA TU, NA HAYO NDIO MADHILA YA ZINAA. MIMI NAWASHAURI WAACHANE MAANA HATA HAO WATOTO SI WA BABA KWA MUJIBU WA SHERIA YA DINI YANGU, ILA BABA ANAWAJIBIKA KUENDELEA KUWATUNZA MAANA YEYE NDIO SABABBU YA WAO KUZALIWA. MAMA ACHANA NA MWANAUME HUYO ATAKUINGIZA JEHANAM UTAMUELEZA NINI MOLA WAKO KWAMBA UMEISHI NA MWANUME MIAKA KEDE BILA KUFUNGGA NDOA?? MALI NA ELIMU KITU GANI AKHERA?? KWANI SIKU YA KIFO MALI NA ELIMU YAKO VITAKUSAIDIA NINI??? KAMA WAMESOMA WATAENDELEA KU WA KEA WATOTO HATA KAMA WAMETENGANA MBONA MAYATIMA WANAISHI??? AU WATOTO WAMASIKINI HAWAISHI??? MREJEENI MOLA WENU ACHENI UZINZI WA KUDUMU. KAMA KWELI WEWE BABA WAMPENDA HUYO UNAEMWITA MKEO!!!! BADILI DINI UWE MUISLAM
ReplyDeleteNAJUA MTAKASIRIKA NAJUA LAKINI MESAAGE DELIVERED
MZEE WA BUNJU
ee bwana wewe mzee wa bunju vipi mbona upo so selfish,kwanini huyo mwananmke asibadili dini na kuwa mkristu??what the big deal? watu wengine bwana stop being so negative.
ReplyDeleteUamuzi wa ama watoto wateseke au waendelee kuishi nao vizuri wanao mke na mume,ni mume amfuate mke kwenye dini yake ama mke amfuate mume kwenye dini yake uamuzi mgumu lakini ni bora sana kw ustawi wa familia.Kama kukosea wote wameshakosea ila ni jukumu lao kuhakikisha watoto hawapati mateso kutokana na makosa yao.
ReplyDeleteHao watu si kwamba hawapendani bali mapenzi yamepungua nguvu,muhimu upande mmoja umfuate mwingine na mapenzi yatazaliwa upya
MMMh Michuzi na wewe huwa unakaagaaaaa halafu ukiona watu tumetulia tunamind business zetu then vuuuup unalizusha kama kawa yako.....sasa tusubiri waosha vinywa tuone watasema nini maana hii topic very very sensitive inagusa wengi katika jamii zetu !! Ila tukumbuke tuu Muislamu ukisia mtu amekufa huwa tunasema ......."Inna Lillahi Wa Inna Ilayhi Rajiun"...maana yake ni kwamba " Hakika SISI soote ni waja wa Mwenyezi mungu na HAKIKA kwake TUTAREJEA" ....Kwa wanaojua kutafakari maana wataelewa kwa nini nimeweka maneno matatu hayo katika herufi kubwa ili kujapa msiitizo na yana uzito gani !!....Kwa Bwana na Bibi wahusika wa hili swala kaeni MTAFAKARI HATMA zenu !!!
ReplyDeleteKABLA YA KUISHI NA KUZAA,BABA ULITAKIWA KUFIKIRIA HAYA,WEWE NI MKRISTU NA UMELELEWA KATIKA MAADILI YA KIKRISTU,NA MWANAMKE KALELEWA KATIKA MAADILI YA DINI YAKE,AMBAYO NITOFAUTI NA HAYALINGANI ATA CHEMBE,DHAMBI MLIO CHUMA NI KUWACHANGANYA WATOTO,SIJU WALIENDA CHUO KUSOMA KURAANI AU KANISANI KUPATA MAFUNDISHO YA KUMUNIO NA KIPAIMARA,(HATUJUI)ATA KAMA WANGEOWANA LAZIMA MBELE NDOA INGEVUNJIKA,KUTOKANA NA KILA MTU KULELEWA NA MAADILI TOFAUTI YA DINI,ATA URAFIKI WA MKRISTU NA MUISLAMU SIKUZOTE NI WAMASHAKA,KUTAKUA NA SABABU INAYO WAFANYE WAWE MARAFIKI NA KAMA HIZO SABABU HAZIPO TENA URAFIKI UNAKUFA,KIKRISTO WATOTO NI WA BABA,NI MAJUKUMU YAKE KUAKIKISHA ANAWAJENGEA,MSINGI BORA WA MAISHA(ELIMU).MAMA WA KAMBO KABLA YA KUINGIA NDANI LAZIMA AJUE UNA WATOTO WAKO NA LAZIMA AWAPENDE KULIKO WEWE ILO NDIO LIWE SHARTI LAKO NA ULISIMAMIE.KOSA MOJA LA MAMANYANYASO KWA WATOTO WAKO UKIGUNDUA,ATA KAMA UMESHA MTIA MIMBA MUONDOSHE KAMPANGIE,MBALI SANA NAWEWE,UNA WEZA KULEA WATOTO WAKO MWENYEWE,UKO NYUMBANI MNA UWEZO WA KUWEKA MFANYAKAZI WANDANI,UTAPATA TU MFANYAKAZI MZURI KATI YA WENGI WATAKAO PITA,SWALA LAKUZINI HAO WANAO UBIRI HILO NDIO WAZINIFU WA KUBWA,TUSIHUKUMIANE DUNIANI,WE ARE ALL SAILING IN THE SAME BOAT.
ReplyDeleteNimesoma neno "uahamuzi" nikafikiri ni kosa la bahati mbaya. Baadaye chini nikaona tena "uhamuzi" nikasema siendelei kusoma nisije nikajichanganya akili na lugha nisiyoijua nikaondoka...
ReplyDeleteal musoma nimesema before,dont jifanya msomi sana..sio vizuri mzee..hata wewe ulitokea huko huko!
ReplyDeleteNafikiri ni jambo jema sana watu tujue kusoma na kuandika kiswahili fasaha. Haya mambo ya kujidai eti si nimeeleweka hayakubaliki. Wenzetu wanafuata na kutii sana lugha zao hasa katika suala la kuzungumza au kuandika katika mpangilio unaokubalika. Uma si sawa na huma. Tujifunze kiswahili wadau. Ukipata bahati ya kukosolewa shukuru si kulalama.
ReplyDeletengwengwe na wewe kama unafata sheria mbona sijaona comma kwenye sentensi hata moja hapo.
ReplyDeleteMimi ninavyojua ni kwamba kwa wakristo (wakatoliki) kuna ndoa za mseto. Haijalishi anayeoa au kuolewa ni dini gani. wanafungishwa ndoa ya kidini halafu wanabaki kwenye dini zao na sijaona tatizo lolote hapo. Ushauri mwanamke akubali kufungishwa ndoa ya kikristo halafu aendelee kuswali katika dini yake. Mungu ni mmoja tu na ni wa wote wakristo na waislamu. kama yeye hatubagui kwa kutupa uzima je sisi kwa nini tubaguane?
ReplyDelete