jk akikabidhi mwenge wa sullivan kwa rais paul kagame wa rwanda ambaye nchi yake itaandaa mkutano wa tisa wa sullivan huko kigali miaka miwili ijayo. pili shoto ni mwenyekiti mwenza wa mkutano wa sullivan balozi andrew young na pili kulia ni balozi carl masters ambaye ni mwenyekiti wa mikutano ya taasisi ya sullivan
jk akikabidhi mwenge wa sullivan kwa rais paul kagame wa rwanda ambaye nchi yake itaandaa mkutano wa tisa wa sullivan huko kigali miaka miwili ijayo. pili shoto ni mwenyekiti mwenza wa mkutano wa sullivan balozi andrew young na pili kulia ni balozi carl masters ambaye ni mwenyekiti wa mikutano ya taasisi ya sullivan

msaada nauliza,
ReplyDeleteeti JK alipoenda kupewa mwenge alipenda nini katika haya mambo?
je alipoyaleta huku alikusudia nini?
je amepata?
Kagame anategemea nini?
Inawezekana ni kujuana na hawa watu personaly? kudevelopurafiki? kuanzisha biashara ndogondogo za kueexport cbm 3 za vinyago?
Hii nadhani ilikuwa iende wizara ya utalii, biashara ya nje wamejishusha, wanatakiwa wasimamie biashara kubwa za kujenga uchumi wa nchi. (my opinion, stand to be corrected)
Kwa mtu anayeona mbali tukio kama hilo la Sullivan kuwakutanisha Wamarekani wenye asili ya Afrika na Waafrika wenzao wanao ishi katika bara la Afrika na ikibidi hata wale wanao ishi katika nchi zingine ulimwenguni angalau mara moja kila baada ya miaka miwili au mitatu ni jambo la kupongezwa sana.Achilia mbali masuala ya fedha au kukuza biashara baina ya washiriki.Muhimu zaidi ni kule kuthamini utu na udugu wa jadi na wa asili baina ya makundi ya watu wa familia moja waliotenganishwa na historia na kujikuta wakiishi katika mazingira mawili tofauti kabisa.Na wakilifanya hilo kwa faida ya vizazi vijavyo.Tuwe wakweli na tusiruhusu chuki zikatawala busara zetu.Kwa hilo nampongeza Kikwete kwa sana tu na ikiwezekana afanye maandalizi mengine ya kuwa wenyeji wa Sullivan Summit nyingine baada ya hiyo ya Kigali mwaka 2010.Tutakuwa tumejiandaa zaidi na itatupa msukumo wa kufanikisha maazimio fulani fulani kwa manufaa ya watu wetu wenyewe.Maendeleo yana gharama zake.Lile tukio tu la Obama kupata ushindi wa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democrat wakati Mkutano wa Sullivan Eight ukiwa unafanyika nchini Tanzania wakina Jesse Jackson na Andrew Young pamoja na kina Sullivan Masters tukiwa nao hapa hapa nyumbani Tanzania ni tukio la kihistoria sana na litakumbukwa daima.Mambo haya hayatokei bure bila ya baraka zake Mwenyezi Mungu!Watanzania wamenufaika sana na mkutano huo wa Sullivan kwa namna nyingi lakini itawachukua muda kulitambua hilo.Sasa hivi daraja limesha jengwa kati ya Watanzania na Wamarekani Weusi.Tulitumie daraja hilo na kulilinda lisije likabomolewa na wasiotutakia mema.Tusitarajie kulishwa midomoni jamani.Lazima tujitumikishe na kwa kushirikiana na ndugu zetu tutapiga hatua mbele.Viva African Solidarity for the Liberation of the African Mind!
ReplyDelete