jk akisalimiana na carl masters, mwenyekiti wa mikutano ya sullivan
jk akisalimiana na mkurugenzi mtendaji wa leon sullivan foundation mama hope masters ambaye ni binti wa hayati mchungaji leon h. sullivan mwasisi wa taasisi ya sullivan. pia ni mke wa balozi carl masters ambaye ni mwenyekiti wa mikutano ya sullivan


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2008

    Picha ya juu mbona inamuonyesha JK kama anashangaa vile lakini ya china inamonyesha akiwa mchangamfu sana na kama anataka kudadisi jambo fulani vile. tehee!!! teheee!!! teeeheeee!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2008

    Ah kumbe taasisi yenyewe ni ya kiukoo namna hiyo. aise wazungu hawa bwana wakija afrika wanasema nepotism kumbe kwao baba mmiliki, binti mkurugenzi, mkwe mwenyekiti nanhiii basi endelea mwenyewe. hapo sio nepostism na watakuambia ni kujitolea. MMMMMMmmmmmmm

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2008

    MAALIM ISSA TUNASHUKURU SANA KWA KUTUPATIA HABARI “..MUHIMU NA NYETI..” KAMA HIZI . HUU MKUTANO UNA “..FAIDA NA MANUFAA..” MAKUBWA, (#1) “..KITAIFA..” NA BILA KUSAHAU (#2) “..VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI..”

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2008

    yani huyu president wa sullivan hope masters,nilipomuona kwenye TV akiongea utadhani ni binti wa miaka 26 hivi na ka mwili kake kadogo dogo,kumbe baada ya kugoggle ndo nikagundua amezaliwa august 21,1963. ama kweli ndipo niliposema kweli unene sio dili na inafanya mtu aonekane mzee kuliko umri wake.lol

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2008

    huyu hope masters nimezimika na ka mwili kake, 45 yrs kwa mama wa kitanzania angekuwa bonge la mtu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2008

    Michuzi,
    Ahsante kwa kunifungua macho... Kwa hizo caption za picha yako, ninaanza kukosa imani na hii taasisi ya Sullivan sambamba na matakwa ya huu mkutano.
    Kama serikali inaupigia debe mkutano huu wa 'kindugu', basi uchunguzi wa Ajira za watoto wa vigogo BOT nao usitishwe, kwani ni jambo lilelile tu.
    Ni mapema mno kuwa na wasiwasi sana, lakini ninachoweza kuseam kwa sasa level yangu ya mashaka imeongezeka kuhusu nini hasa ni nia ya huu mkutano na tasisi ya Sullivan kwa ujumla.
    Sijapata nafasi ya kuchungulia luninga za kimataifa (CNN, BBC & Aljazeera) wanaonyesha habari za huu mkutano? au waandaaji hawakuwapa 'bahasha'?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2008

    Nilipata bahati ya kusikiliza Hotuba yake ya Ufunguzi wa Sullivan Eight Summit juzi usiku katika AICC Simba Hall kwa kweli Mama Hope Masters bintiye Leon Sullivan mwenyewe alinivutia sana kwa kipaji na uwezo mkubwa alionao wa kuzungumza mbele ya halaiki ya watu.Ni mzungumzaji mzuri,aliyedhihirisha wazi kwamba ni mwerevu na mwenye elimu ya kutosha,mfano bora kabisa kwa kina mama zetu,mwanamke shupavu na jasiri aliyeamua kusimama kidete kutetea yote aliyopigania marehemu baba yake Mzee Leon Sullivan wakati wa uhai wake,yale ya kuhakikisha kwamba bara la afrika linasimama kidete na kupigania maslahi yake katika jumuia ya kimataifa kwa kujenga mashirikiano ya kidugu zaidi baina ya nchi na nchi ulimwenguni kote.Lakini muhimu zaidi ni kwa kuhakikisha kwamba Wamarekani weusi wanahamasika zaidi katika kutambua wajibu wao katika kulisaidia bara zima la afrika liondokane na aibu hii iliyopo sasa ya umaskini uliokithiri,umaskini wa mali na hali,elimu duni,utegemezi uliotopea,ufisadi na ukandamizaji wa haki za raia na binadamu kwa ujumla na mengine mengi.Kwa hilo nampongeza sana sana dada HOPE MASTERS,mkurugenzi mtendaji wa Sullivan Foundation,waandaaji wakubwa wa Sullivan Summit.Watanzania tumepata Faraja Kubwa kwa ujio huo wa Watu mashuhuri duniani wakiwemo Andrew Young,Jesse Jackson na Olusegun Obasanjo.Tunawakaribisha tena na tena nchini Tanzania.Hapa ni kwenu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2008

    ukibahati kupeana mkono na MC huyo lazima uimbe kimoyo moyo...."ule wimbo wa akina..nani .vile...(samahani nimesahau) ila una chorus inasema "unanitega*"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...