Home
Unlabelled
jongwe laendeleza libeneke
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
MUGABE oyeee!! Achana na Bush, Blair na watu wengine wanaodhani kwamba wazungu ndiyo bora kuliko waafrika. Na ukitoka hapo jambo la kwanza ni kurudisha mashamba yaliyobaki mikononi mwa wazungu wachache. Chapa kazi na usikatishwa na vibaraka kwani wao kula yao inategemea michango ya wazungu hivyo ni haki yao kupiga kelele ili nao waonekane wapo upande wao
ReplyDeleteWadau naomba kuuliza hili neno "libeneke" maana yake nini?
ReplyDeletehuyu bwana alimfukuza Ian Smith kusudi aje yeye kuwaonea watu weusi alijifanya anataka kuwakomboa kutoka katika makucha ya wakoloni matokeo yake amekuwa balaa kuliko wakoloni cha ajabu kwa nini viongozi wa africa hawamfahamishi ukweli anaona kutawala zimbabwe haki yake amesahau kwamba nchi ina watu zaidi ya milioni kumi na kwamba kila mtu ana haki ya kuwa kiongozi it time wa africa wakemee tabia chafu kama hizi
ReplyDeleteAibu aibu aibu tena aibu kubwa!!!!Huyo Mugabe anatia aibu na viongozi wa nchi za kiafrika waliompongeza kwa ushindi usio halali hawana hata heshima kwa raia wa Zimbabwe waliopeteza maisha na hadhi zao kwa ajali ya ulafi wa madaraka uliomjaa!
ReplyDeletehakuna atakaempongeza huyo. hapo anasalimiana na jiani yake sio kupongzwa. apongezwe kwa lili kubwa? kupiga watu kuutumia mkono wa chuma katika kutawala?
ReplyDeletehuyu hana maana kabisa ni wa kupiga risasi tu
unajua ujinga kama huu ndio unaotufanya tubaki nyuma kila siku unashindwa uchaguzi halafu hutaki kutoa matokeo watu wako wenyewe wamekataa kukuchagua na dunia nzima inajua halafu unalazimisha uchaguzi mwingine na unajaribu kulaumu watu wengine nchi umeishaiua ni lazima hawa watu waelewe kwamba utawala siyo haki yao wananchi wakiamua wanataka mtu mwingine lazima iheshimike amekuwa jambazi kuliko wakoloni wazimbabwe wanapata shida kuliko wakati wa ukoloni
ReplyDeleteHongera sana komredi Mugabe kwa kuchaguliwa tena kuendeleza libeneke. Nashangaa wanaomponda, wakati amechaguliwa kidemokrasia! Hivi ni lini Waafrika tutakua na uhuru wa kweli?? Ina maana usipopendwa na Bush au Blair, unageuka kua dikteta?? Mbona kina Museveni, Khadafi, Omar Bongo,Meles Zenawi,.....hawasemwi?? Kwa wasiojua ukweli wa Zimbabwe, wala hakuna fujo zozote, bbc na CNN wanakuza mambo ili kumpaka matope Mugabe. Long Live Komredi, ukoloni tumeshauzika; huwezi kukabidhi nchi kwa watu ambao hawana uchungu na nchi, vibaraka wa wakoloni.
ReplyDeleteMdau aliyetaka kujua maana ya libeneke ni kifupi cha maneno nane ya kizaramo.
ReplyDeletewewe anon wa kwanza kabisa unaonekana jinsi gani ulivyo na fikra za kizamani watu wanateseka unashangilia,chakula shida na kila kitu shida unasema mugabe oyee,africa inashindwa kuendelea kwa kuwa na majuaa kama wewe amabo mnafurahia udikteta na sio swala la mzungu ni swala la kutumia akili na sio wazungu wanaakili pekee hata waafrika baadhi tuna akili sasa wewe kama unaona hali ya zimbabwe shwari basi unabudi kwenda mirembe kutibiwa,mtu anamiaka 84 anasubiri nini kujiuzulu?Juzi watu wamesherehekea sikuku ya mandela ya kuzaliwa na wamepishana miaka sita na huyu jongwe na mwenzie anakula maisha ya kustaafu mwaka wa ngapi sasa?na utabakia kuwa kuona wazungu ndio wanataka mambo mazuri hata waafrica tunapenda maisha mazuri kwa kila mmoja wetu
ReplyDeleteMichuzi nadhani Africa tunataka midume kama hawa ili heshima yetu irudi. kwani nimechoshwa na viongozi vibaraka amabao wanajipendekeza kwa wazungu then baadae wanajisainisha mikataba ambayo hatuwezi kuivunja.
ReplyDeleteKila siku wanakula kwetu nasisi tunachekea, siku ukipata solution unaambiwa mkataba huu umesainiwa kwasheria ya kimataifa hauvunjwi,,, huu ni utumwa tu.
Kifupi wanaoona mugabe hafai then wasiulaumu mikataba ya madini, richmond na wala ile misitu ambayo serikali ya finland imeinunulia kampuni ya kwao. hayo ndio masuala ya international business na hao mabalozi ambao wapo humo nchini kazi yao ni kupulizia hiyo mikataba na makampuni ya nchi zao yaje humo mwetu.
Michuzi naomba email yako kwani ninahoja nataka kutoa kwenye blogu yako: inahusu utalii na historia. kifupi nachukia kuwapeleka wazungu kuwaonesha maoneo ambayo babu zao waliwadhalilisha babu zetu kama bagamoyo... mbona wayahudi wamepinga historia ya wanazi na hakuna anayeonesha?? yaani unamwambia mtu hapa ndipo babu yako alipomkata makofi babu yangu!!! hiyo heshi or kujidhalilisha?? njaa zisituuwe jamaniiiiiiiii.
Mukikuwa mutajuwa niyasemayo!!
G7
UK
Wazungu tumewazoea kwa kutetea maslahi yao kwa njia yeyote. Mfano mzuri ni huyo mnayesema amesherehekea siku yake ya kuzaliwa (Mzee MANDELA) mpaka leo sheria za Marekani zinamtambua kuwa ni GAIDI mpaka hapo zitakapo badilishwa hivyo sishangai maoni ya watu wanaotukuza propaganda za magharibi mpaka leo. Hivi ni haki kwa mtu kama Mandela kuitwa gaidi mpaka kutambulika kwenye sheria za Amerika kama gaidi wakati alikuwa anatetea maslahi ya weusi. Juzi tu Bush na blair waliudanganya umma kwamba SADAM ana silaha za maangamizi na wengi waliamini lakini hii leo tunashuhudia vifo vya maelfu ya watu na wala siyo silaha za maangamizi. Waafrika tujadili matatizo yetu wenyewe na siyo kukimbilia magharibi kwani hawa watu wanafanya kwa maslahi yao. Zipo sehemu nyingi zina matatizo lakini hao mnaowafagilia hawana maslahi kwani kazi yao ni kulinda maslahi. SOMENI historia ya ukoloni pamoja na harakati za kujikomboa. Hivi vyombo vya habari vya magharibi (CNN, BBC) siyo kwa kuamini kila kitu wasemacho kwani vipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya nchi zao.
ReplyDeletePamberi na Chimurenga = A luta contnua = VIva la Revulicion - the Struggle Continues = Mapambano Yanaendelea!
ReplyDeleteMbeki upo? Aridhi, aridhi, aridhi ya itarudishwa kwa wananchi!
Brown Gordon, warudishie wananchi wa Diego Garcia aridhi yao, upesi!
George Bush, aridhi ya wazawa wa Amerika, irudishe!
New Zealand, rudisha aridhi ya wazawa wa-Maori na wewe Australia!
Afrika inaweza kujikomboa kwa kukataa vikwazo dhidi ya Jongwe la Zimbabwe! Nchi 52 zinaweza kuikomboa Zimbabwe, kulingana na utamaduni wetu wa jadi...kila nchi ya Afrika ikubali kuisaidia tarafa moja ya Zimbabwe!
Kumtenga Mugabe sio "panacea" (dawa) ya matatizo ya Zimbabwe! Msaidieni Jongwe, asaidike! Kumsusa ni kuongeza unyonge wa Afrika...
Eti, "Afrika ya leo"! AMKENI na fahamuni kwa makini historia ya Mugabe kuwa alivyo leo, acheni ulimbukeni wa "ignorance"!
Mugabe alipaswa atoe mfano bora kwa Vijana watakao rithi Mikoba ya Wazazi wao katika safu ya Uongozi barani Afrika katika siku za karibuni.Hata akipewa miaka mingine MIA MOJA ya kuiongoza Zimbabwe Mugabe hawezi kubadilisha lolote nchini Zimbabwe kwa akili za kizee alizo nazo hivi sasa labda afanyiwe BRAIN TRANSPLANT.Huu ndiyo ukweli wenyewe.Bainadamu ana ukomo wake kifikra,kiakili na kiutendaji.Mgogoro wake na Tony Blair au Gordon Brown asiubebeshe kwa wana Zimbabwe ambao hawana kosa lolote.Alipo ingia msituni ili kumwondoa Ian Smith ni kwa sababu aliuchukia utawala wa kikandamizaji na kibaguzi wa Watu Wachache kwa Maslahi ya watu wachache!Aliuchukia Udikteta.Alipoingia madarakani wana Zimbabwe walitarajia kwamba Mugabe angekuwa mtetezi mkubwa wa Utawala wa Kidemokrasia kwa Maslahi ya Wengi.Katawala kwa kipindi cha miaka 28 akiwa na umri usiopungua miaka 84!Kama ni Kiongozi aliyekuwa anaona mbali na alikuwa akiongoza kwa malengo maalum kipindi hicho kirefu cha uongozi(ambacho kuwezi kukiita utawala wa demokrasia)angeweza kutekeleza na kufanikisha malengo yake yote au sehemu kubwa sana ya malengo hayo.Na angekuwa kesha jitayarisha kuachia madaraka kwa Mtu Mwingine hata kama ni kutoka chama chake cha siasa.Lakini bado Mugabe anaonekana kama hakujitayarisha bado kuachia madaraka hata baada ya utawala wa miaka 28 na katika umri wa miaka 84!Hata kama pasingekuwepo mfarakano wowote baina ya Mugabe na Uingereza bado Mugabe atakuwa kesha poteza sifa zote za kuendelea kuwa kiongozi halali wa wana Zimbabwe katika mfumo wa utawala wa Demokrasia ya Vyama Vingi Vya Siasa.Wote wale wanaomtetea Mugabe ningewashauri wajiulize kwamba iwapo pasingekuwepo na mgogoro wowote baina ya Mugabe na Utawala wa Uingereza,je,Mugabe bado alikuwa na sifa za kuendelea kuwa Rais wa Zimbabwe katika Demokrasia ya Vyama Vingi Vya Siasa?Kama jibu ni Ndiyo,Bado tuna Matatizo makubwa sana Barani Afrika.Na tutarajie kuendelea kutawaliwa na Mataifa ya Nje kwa kipindi kingine cha miaka 200 ijayo!Why?Because Independent Rational Thinking is totally lacking among our 'intellectuals'!It is the BALLOT not the BULLET stupid!
ReplyDeletehuo mkutano sidhani kama una umuhimu wowote kwani inaonyesha umejaa wehu watupu, kwani kama sivyo iweje wamruhusu huwe mweu kuudhuria, hii ni homework yako michuzi tuone kama utaiweka hii comment.
ReplyDeleteDuh jamani!!!basi mie nasema hongera mzee Mugabe...sio kwamba umechaguliwa kiharamu,bali mauaji uliyoyafanya dhidi ya raia wako...na sio wazungu bali weusi wenzako...
ReplyDeleteKweli ujinga wetu weusi hadi siku ya kiama na labda baada ya kiama pia!!!
bpkrmsgWatu wanaomshangilia mugabe mimi siwalaumu kwani sijajuwa huenda hawajaona kwa macho yao mambo anayofanya mugabe,au ni kwa kinyume chake au wanamatatizo ya hakili kama alivyo Thabo mbeki au nao ni wauwaji hatuwezi juwa.
ReplyDeletenaamini mtu yeyote anaejuwa mambo ya mugabe hawezi mtetea!!
JAMANI, TUJIULIZE HIVI: WAZIMBABWE WANAUMIA SABABU YA ROBERT MUGABE AU SABABU YA VYOMBO VYA KIMATAIFA NA NCHI ZA KIBABE ZINAZOWEKA MASHARTI YAO KAMA USA, UK NK? JIULIZENI, RAIS ROBERT MUGABE KAFANYA NINI CHA KUWAUMIZA WAZIMBABWE ZAIDI TU TA FITNA ZA WAZUNGU KUIWEKEA MASHARTI NCHI, AMBAPO WANAOUMIA NI RAIA.
ReplyDeleteWAAFRIKA TUJIFUNZE KUNG'AMUA NANI ADUI WA HAKI, NA SIYO WAZUNGU WANASEMAJE KUHUSU HAKI ZETU. KINACHOFANYIKA ZIMBABWE NDICHO KINACHOFANYIKA NCHI KARIBU ZOTE ZA AFRIKA, ILA TU SEMA NCHI ZINGINE TUMEKUWA MAFALA KWA KUKUBALI MATAKWA YAO. NAKUBALIANA NA G7 -UK HAPO JUU. NDIYO MAANA MADINI NK. VINACHUKULIWA NA MATAKWA YAO WAWEKEZAJI, NA SI SISI. HIYO NDIYO WAZUNGU WANAITA UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA.
ACHA MUGABE AWAONYESHE JAPO WATU WATAUMIA. NAJUA HUU HAUTAKUWA MWISHO WA DUNIA ZIMBABWE.
Ha ha ha mlie tu na roho zenu mbaya! Ndo hivyo tena JONGWE karudi ikulu kwa mbwembwe...who cares?!
ReplyDeleteVibaraka wa magharibi hawana nafasi ikulu ya Zimbabwe.
Mombasa wasema "wamize wembe"
Na mie nasema wasiopenda Mugabe atawale Zimbabwe wahame kwenye sayari hii (earth) waende sayari nyengine (zimebaki 8.i.e. mercury venus, mars, jupiter, saturn, uranus, neptune and pluto) wakaishi! Mkiona mtabanana hata kwenye mwezi kawekeni kambi!
"Always fortune fevers the braves"
we ano 1.20 pm acha upumbavu wako umesikia wapi uchaguzi ameshinda kidemokrasi ya wapi ? hata sadac obsever wamesema uchaguzi ulikuwa si fair watu walikuwa wanalazimwisha kumpigia huyo kichwa ngumu wako MUGABE uchaguzi wa mtu mmoja ithink umoja wa africa ungemtoa mbio huko egpt na kama unamuona ni komredi wako aliyeua uchumi na bado unamkumbatia ndio nyie watu uliozoe kutukuza watu hata akiharibu ndio mzee nenda na wakati MUGABE wako kaua nchi
ReplyDeleteHongera Mugabe for standing up to our former colonial masters,who are still rulling us via IMF and World Bank policies. It is not easy , it take a strong leader like you to do that, remember they are still out there to get you thereby the fight is not over. If you win this battle, you will be my hero. Hell to those want to be slaves of the west, you got my support gangster!
ReplyDeletekwa wale wasio na upeo wa kuona yanayotokea zimbabwe na kudhani kuwa tuhuma zote ni majungu ya us na uk nawaambieni amkeni fumbueni macho muone ukweli, hamko mbali na zim nendeni mkaone wenyewe yanayotendeka, mimi nimefika mwezi uliopita kweli mjini si rahisi kuona udhalimu wa hawa wanaojiita war veteran; nasema wanajiita maana wengi ni wadogo haiwezekani kabisa kama walihusika wakati wa mapambano ya uhuru. watu wanateswa ile mbaya na narejea tena yeyote yule anaedhani ni uongo na afunge safari aende zim kujionea mwenyewe.
ReplyDeleteNa yule alosema eti akina gadafi hawasemwi namuuliza suali moja tu, unaishi ulimwengu gani wewe?
wewe g7 unaandika hayo kumbe uko uk kwa wazungu unatafuta nini huko
ReplyDeleteNawashangaa wanaompongeza mugabe, nchi zote za SADC zinamabalozi wao zimbabwe na wanashuhudia live kinachotokea zimbabwe hawategemei cnn wala bbc na kwa kuwa viongozi wa SADC ni watu safi walioingia madarakani kidemokrasia ndio maana hawapati kigugumizi kukemea yanayotokea zimbabwe, nyie mnaopongeza hebe fikirieni nyinyi ndio mngekuwa wazimbabwe, hali ile ya uchumi iliyokuwa Tanzania miaka ya themanini ndio waliyonayo zimbabwe. tusifanye mambo kishabiki tuwahurumie wazimbabwe
ReplyDeleteaibu sanaaaaana na sielewi Africa inamwogopa nini huyo...
ReplyDeleteYaani picha za watu waliopigwa ili wakapige kura ukiziona ndio utajua kweli huyu si mtu....
Acheni kusema bush wala blair huyu mtu anaudhaifu mkubwa saaaaaaana tu. Africa isingeitambua uongozi wake kabisa...
Sio uchaguzi wa halalai....Ilikuaje matokeo ya awali yachukue miezi miwili kuhesabiwa lakini huu uchaguzi hata siku moja nzima haikuisha matokeo yakatoka?
Unajua ni wangapi waliosema NO? Hata kama hakuwa na mpizani this time lakini kura za watu waliomkataa zimehesabiwa?
Na alipata hiyo 50% aliyokua wanaitafuta????let be realistic huyu mtu hapana....
Ndio maana dipolomatics wao wamekataliwa kuingia USA...Wao ndio wanamsupport huyu babab na weng i wamejilimbikizia mahela huko USA sasa wanataka kwenda kujilia kiulaini wakaambiwa hamna kuspend nje ya nci yenu...Sasa tuwaone hao mafisadi wa Zimbabewe sijui wataenda Manyara tu kula hela yao....
ReplyDeleteWanaomsifia huyu hawana upeo wa macho kabisa...mtasema sijui US na UK lakini mwenye macho haambiwi tazama .Iweje asishinde mara ya kwanza?
Yaani nawashangaa watu ambao wanampinga mugabe,, unajuwa hawana point zaidi ya kutaja vitu havina msingi. fuatilia uchumi wa zimbabwe mpaka 1995 ulikuwa zaidi ya bongo. sasa why ushuke ghafla?? kama watafiti wa kweli mutaona ni baada ya zimbabwe kuanza kuvutana kuhusu ardhi. SASA upeo munaotaka nyinyi ni upi????????
ReplyDeletebaada ya hapo wale wazee wenu wakataka wamuoneshe mugabe kwakumteua tchangarai. So unawezasema Tchangarai ndio sababu ya yote zimbabwe kwani yeye ndiye kawa kichefuchefu na ndio maana kakimbilia ubalozi wa holand. yaani nchi zote hizi Y akimbilie kwa walioporwa mashamba????UPEO MUNAUJUA NYInYI??
Kuhusu kuwacharaza bakora walioasi ni kawaida. Tena walitakiwa wapelekwe lupango haswa kwani hawajakuwa na wala pesa walizosomeshwa history ya wakoloni haikuwasaidia na zimepotea.
Kuna mpuuzi kauliza nafanya nini Uk? nipo nasoma then narudi kwetu mimi sio mtumwa wa mawazo kama wewe. Kimsingi sio kosa kusoma or kutembelea or kuishi UK or USA but kupelekwa kama ling'ombe ndio proble.
Mukikuwa mutajuwa dunia inaendaje watoto!!!
G7
UK
mtu asiye na dhambi yeye na serikali yake awe wa kwanza kumlaumu Mugabe, mambo yanayoendelea nchi nyingi za africa ikiwemo TANZANIA NI MABAYA KULIKO YA ZIMBABWE.
ReplyDeleteKinachonikera mimi si huyu Mugabe na ishu zake, jamaa yuko poa tu kama unafuatilia mambo ya dunia hii. Shida yangu mimi kufanyia mkutano Misri. Hawa watu wanajiita watu wa Mashariki ya Kati na unaweza kupigana nao ukisema Misri ni Afrika. Tunawakumbatia nini sasa? Mubarak ameshakuwa Mwenyekiti wa Afrika zaidi ya mara moja na bado tunamkumbatia, wa nini? Hawa Wamisri wapuuzi na ndio maana huwa wanatufunga Yanga magoli kibao!
ReplyDeleteHuyu mzee ana kichaa. Bora tu wamdondoshee bomu afe.
ReplyDeleteG7 we meet again...certainly a pleasure! Mtoto aliyesoma hapa
ReplyDelete!
Inaelekea una hasira na wazungu sana sijui walikufanya nini!! Swali langu ni moja...hao wazungu wanaoishi Africa kwa mfano Afrika ya Kusini na hao walionyang'anywa mashamba zim ni wa nchi gani? Uholanzi, Uingereza au ni wa Zim? Hata kama historia inaonyesha ni wametokea huko Uholanzi...hii ni generation ya ngapi kuishi huko. Wanatambua Zim kama nchi yao na wanaipenda kama Mzim Mweusi apendavyo. Huwezi kuwakatalia nchi yao. Swala la ardhi ni nchi karibia zote. Hata ukiangalia Kenya...nayo ilikuwa moja ya issue.
Lazima uweze kutofautisha vibaraka na insane leaders. Sisi wenyewe tume-prove many times over kuwa kujisaidia wenyewe ni ngumu. Sisi binafsi udhaifu wetu ndo unatufanya tujisaidie wachache. Wewe kama kiongozi umesoma...ukaenda ku-sign mikataba kama ya Richmond...hufai! Na nani alisema kuwa haiwezi kuvunjwa? Unajua kujifanya mbabe mara nyingi inaishia kujiumiza mwenyewe. Lakini hiyo ni off topic. Mugabe ameshapita wakati wake...la maana ni kujitoa taratibu. Tchangarai mwenyewe alimpa heshima ya kujiuzulu mwenyewe bila ya kumshtaki...lakini wapi! Hana uwezo wa kuongoza nchi tena...akae kando.
mugambe ni mtemi wa afrika yule ni kidume cha kweli mtasema ila ukweli utabaki yule ni mtemi wa wazungu
ReplyDeleteMtoto Uliesoma karibu sana.
ReplyDeletewell mimi sinachuki na wazungu mbali ninachuki na waswahili wenzangu wanaosikiza kila mzungu asemacho. kujalizia hapo nikwamba nilisomeshwa undergraduate na mzungu-Mama ambaye pia nilifanya naye kazi na bado she is very special person to me. Masters yangu pia nimelipiwa na scholarship ya wazungu pia, mpenzi wangu wa moyo hasa ni mzungu, familly yangu pia inaconnection nao wengi sana. na nimewasaidia wengi sana.
But when it comes to kuamua na kushirikiana bado wote wananiheshimu pamoja na familly yetu kwamba sio watu wa kupelekwa kama mang'ombe. mfano walitaka kununua sehemu kubwa ya beach kule home but mzee wangu pekee ndiye kikwazo kwani hatukukubali kuwaondoa wanavijiji kadhaa just coz wazungu wanataka that area. Nadhani mtu kwao ndio dignity--otherwise ni mtumwa.
hao wazungu waliokule sio wazimbabwe wala wasouth na ndio maana wanakuwa na tabia za kibaguzi. mashambani wanawatumikisha jamaa kama watumwa wao. so mimi binafsi nasema heri ya lawama kuliko fedheha.
Ningekuwa kibaraka sasa ningekuwa naishi US kwani deal moja la kununua that land nikwamba mimi niende nikasome na kuishi kule na mke wangu but nooo. sio ring'ombe mimi.
nadhani binti(mtoto umenipata)
enjoy being african. nawasikitikia baadhi ya watu wanadiriki hata kusema wazungu wanaakili zaidi ya wabongo.. mmeliwa sana.
G7
UK
Wewe, Tarehe June 30, 2008 11:04 PM, mtoa Maoni: Anonymous, unajua mambo kweli ama ni kupanua domo tu?
ReplyDeleteKwanza, "dipolomatics" ni watu wa namna gani, kabla sijasoma maoni yako?
jamani,u ol are tokn abt wazungu ths mugabe tht bt if u hav seen wat the zimbwabwean pple are goin thru hata kuhav tht heart of supporting him(mugabe)disappears completely...pple are dying like flies and the survivors,God help them they luk mesd up kabisaaaa,very bad condition,its like anawatoa for sacrifice,kuna wengine mmesema ati cnn,bbc wanaongeza maneno poa bt r u tryn to tel me hata wen they show the Zimbabwe pple waliopigwa wanafekisha?!!wat the zimbambweans are goin thru sio fair,the man is dispeakable
ReplyDeleteKwenye mkutano wa Africa wa kuzungumzia masuala ya maji na usafi (sanitation) uliokiendelea katka mji wa kitalii wa Sharm el-Sheikh, Bahari ya Shamu, Misri, msemaji wa Rais Mugabe, George Charamba, aliwajibu waandishi wa habari kuhusu swali la eti Rais Mugabe kujiuzulu wadhifa wake:
ReplyDelete"Isn't that an odd question. He's a few days into office and you expect him to retire, do you? ... Five days have expired, not even a week after. ... Why is the issue of the retirement of the president of Zimbabwe such an obsession for the West?"
Msemaji huyo alipozidi kudadisiwa, alitamka kuhusu nchi za Magharibi:
“They can go hang. They can go and hang a thousand times."
Kauli ya ki-JONGWEISM = Pamberi na Chimurenga = Mapambano Yanaendelea = A Luta Continua = Viva le Liberación!
Maneno ya wakubwa,
Maneno ya wazee
Yote sawa
Kwa kumaliza ukoloni uliotokea
Tunawapa heko
Na tufe njaa
Sisi wote twakubali yote
Ni afadhali kuwa huru na masikini
Kuliko kuwa tajiri na mtumwa!
Madini yetu yanasombwa na matajiri wageni wakishirikian na mafisadi wenye kuunda kampuni nje ya Tanzania kuogopa kulipa kodi au kushitakiwa popote ili wanufaike na “vjisenti”!
Wakina Museveni (Uganda) na wWakina Raila Odinga (Kenya)na wakina Membe (Tanzania)nao wanajidai kumkosoa Mugabe na huku wanataka kuendelea kutawala Uganda milele kwa kushinikizwa na wakina Muamar Kaddafy (Libya); mikono yao imetapakaa damu (Kenya); na kushindwa kutatua “muafaka” (Tanzania)!
Wenye kumtakia mabaya Rais Mugabe: “They can go hang. They can go and hang a thousand times."
Tunachangaya mambo.Tunaweza tukamsifia Mugabwe kwa kuwadindia Wazungu katika masuala ya ardhi, ok.
ReplyDeletelakini kwa nini alikumbuka kuwagaia
ardhi watu wake miaka miwili/mitatu
kabla ya uchaguzi?? Alikuwa wapi miaka yote?? Hili si ndio lilipaswa
kuwa suala la kwanza kabisa kulifanyia kazi aliposhika madaraka
mwaka 1980?? Alikwina??
Kuonyesha kuwa hili lilikuwa ni suala la kukurupuka tu angalia uchumi wa nchi ulivyo sasa. Mkate shilingi alfu 10!! Kama angekuwa amejiandaa basi angeweza kuwanyang'anya wazungu ardhi na asingetetereka!
Ni kweli tunafurahi anapojitokeza kiongozi wa kiafrika anayeweza kusimama against Bush and Co. lakini kwa hili la Mugabe, at what cost!!
Sisi sote ni waafrika. Tunajua wazee wetu wanavyokuwa kadri umri unavyosonga mbele. Kwa hakika, hii sio karne ya kuongozwa na raisi mwenye miaka Themanini na Kitu, awe amewadindia wazungu ama la!!!
G7 naona matusi yanaendelea tu na sasa waniita binti...hehehe. Mimi haiwezi kuniuma. Kama nilivyosema angalau bado umeniita binadamu kuliko kuniita mnyama! Watu kama wewe ndo nawapenda...Kama umesoma ivyo hukufundishwa kuingiza kashfa katika mazungumzo haisaidi?!
ReplyDeleteFrankly...i dont care kama una mke mzungu, mtoto mzungu, baba mzungu, Mungu mzungu...yote hayo mimi sijali! Hamna mtu anawaabudu wazungu hapa. The issue is "Is Mugabe really helping his country?"
Katika kuendeleza nchi lazima uangalie viable short-term na long-term solutions za kusaidia wananchi wako na uchumi vile vile! Ishu ile ya ardhi haijaisaidia Zim hata kidogo...thats the conclusion! Na ni kama nilivyoshasema mara nyingi...he could have gone about it in a different manner lakini he chose the one that benefited him (kushinda uchaguzi)
Yeye alikuwa na agenda tofauti kabisa kichwani mwake. Mnataka kuleta mambo ya ya kutaifisha tena haya jamani? Watu kama nyie ndo mtadai watu kama Stalin walikuwa great leaders maana they stood up against the West...lakini u have to ask urself at what cost? Urusi ukitoka hapo Moscow...ni nchi iliyochoka sana! during the iron curtain era and the berlin wall...people were risking being shot just to cross the boarders! Unajua unapoona kuwa umeshindwa...kubali bwana. No need ya kujifanya mbabe. In the end angalia nchi zote zilizokuwa communists sasa zinagombea kuingia EU. Natumia hizi kama mfano wa ubabe na fikra duni zilizotumika (na wazungu)...ambazo tusipoangalia mwisho zitatuadhri na sisi pia. Wewe umeona Wazimbabwe wamefanyiwa nini SA. Sasa mtu kweli ukirudi kwako upigwe, ukienda kwa wengine upigwe...where is home?!
Sisi sio kwamba tunaabudu wazungu na kusema everything they have done has been right. They have failed...a million times, but they learnt from it. There will never be another Hitler because they have learnt...and hopefully there shld never be another Mugabe anywhere in Africa because we shld learn from this. Na for TZ...hopefully there will never be another Richmond!
alafu kuna mahali nilisoma ukasema kuwa Wayahudi(Jews) hawataki watu kutembelea sehemu zinazowakumbusha kuhusu mauaji yao kipindi cha WW2? Ulikuwa unaongelea mambo ya Bagamoyo. Kama nimekumis-quote...samahani...lakini ningependa kukufahamisha kuwa Auschwitch (the biggest concentration camp) is a museam and a World Heritage Site. (nadhani unaelewa maana ya sehemu kufanywa a World Heritage Site kama hujui uliza tu...maana kuuliza si ujinga) Sijui wewe ultioa wapi hiyo akili kuwa watu hawaruhusiwi kuziona.
Mtoto aliyeenda shule....to G7
halafu nimejibu kwenye ile nyingine (the cartoon)...sijui utaweza kuipata. Nenda kwenye kumbukumbu...then June. Utaiona katika articles za June!
BUSHI ALIIBA URAISI KUTOKA KWA AL GOR NA WATU KIMYA,KAMAKUSAFA KWA WANANCHI? BASI ULIZA REKODI YA BUSHI KUHUSU KATRINA!!!TURUDI ZENJI NA "KAFU" NK...WATU WALISHALALA JELA NA SIKU ZA KURA MLIONA WENYEWE BAKORA ZILIZOTEMBEA, JE HAPO DAR MWEMBE CHAI SI INASTORI ZAKE PIA....WATU WAZINGATIE MATOKEO NA ATHARI ZINAZOWAKUMBA WANANCHI,NA KUTAFUTA "IMIDIET SOLUSHEN"WANANCHI HAWANA CHAKULA, WANAPIGWA MAPANGA WANAPOKIMBILIA SAUZI NK HILO NDIO MUHIMU, HALAFU KUDILI NA HUYU MZEE INABIDI WANAODILI NAE WASAFISHE THEIR OWN CLOSETS HALAFU WAWEZE KUMYOSHEA MTU KIDOLE
ReplyDeleteAGAIN "MUNGU IBARIKI AFRIKA"
tatizo watu wanapoteza maana nzima ya ubishi huu hapa hakuna mzungu anayeumia wanaoumia ni wananchi wa zimbabwe na kwa bahati mbaya anayewaumiza ni mtu ambaye hapo zamani walimuamini awaongoze kalewa madaraka anaona ni haki yake kutawala mugabe hana jeuri yoyote kwa wazungu isitoshe wazungu hao hao wanawapigia kelele wazimbabwe kwa sababu amini usiamini kama akijaribu kupiga wazungu huo ndio utakuwa mwisho wake watamfanya kitu mbaya sana siku zote ukiangalia watu wanaopigwa niwatu weusi yeye anajaribu kulaumu wazungu kama mbinu yake ya kupata sympathy kwa waafrika obviously wafrika wote bado wana hasira za kihistoria kwa wazungu lakini wazungu sio wanaoua watu zimbabwe ingekuwa wazungu wanaua watu zim sote tungejiunga kwenda kupigana nao lakini sasa huyu mugabe basi hatuwezi kwenda kupigana naye kwa sababu sio adui lakini basi japo tumwambie ukweli kwamba eeh bwana unaharibu
ReplyDelete