rais wa zanzibar mh. amani karume akifunga rasmi mkutano wa siku nne wa sullivan hoteli ya ngurdoto mountain usiku huu, na kuwakaribisha wageni toka marekani visiwani leo ijumaa kwa hafla maalumu ambayo amewaandalia kwenye hoteli ya zamani kempinski
gavana wa a-taun mh. isidore shirima (mwenye miwani) na balozi wetu marekani mh. ombeni sefue walikuwapo katika hafla ya kufunga mkutano wa nane wa sullivan
chris tucker akiwa na baadhi ya wageni wenzie toka marekani usiku huu ngurdoto
hema kubwa ambamo shughuli za tafrija za mkutano wa sullivan zilifanyika. juu ni muonekano wa hema hilo kubwa kwa nje na chini ni kwa ndani


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2008

    sasa hapo red bull za nini kwenye dinner? Duuh!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2008

    kama Tanzania tumeweza kupamba kiasi hiki na kuwalisha wageni wote hao, kumbe tunahela? Ina maana mafisadi wamechukua nyingi zaidi ya hizi, basi shughuli!!!

    Misupu nichunguzie kama kiasi gani hivi kimetumika kwenye shughuli nzima kwa hesabu za chapchap.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2008

    Mazingira mazuri nimekubali na natumai wote wanaosema waliopo marekani hawana mpango wamejua umuhimu wao. Hawa ni watu weusi waliopo huku wenye elimu na nafasi zao za fedha au biashara walioamua nao kupata kidogo kutoka kwa wenzao wa-Afrika. Ambacho wazungu wanaendelea kukitafuna bila jasho.
    Suala la aliyeko huku USA sie mwenzako, epuka kuwa mnaandika maneno ya wabeba maboksi kila siku maana kama huelewi kitu kaa hivyo hivyo. Wachahche wenye elimu zao wanakula nchi kama wako TZ bila rushwa wala bughudha.
    kwa usanii kidogo- Chriss Tucker kama hajalewa basi mhh, maana naona glass anayokunywa ina Coca-cola au hamuelewi Mheshimiwa Karume kii-ngereza chake.(Jokes not serios guys)

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2008

    Karume kawakaribisha wageni Zanzibar ningeomba wabaki mpaka usiku waone hali halisi ya umeme, tusifiche matatizo labda tutasaidiwa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2008

    kilichonifurahisha kingine ni kuona baadhi ya wamarekani weusi wanawake kuvaa nguo za utamaduni wa kiafrika kama mabazee na vitenge.wameonyesha kuipenda asili yao kweli.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2008

    Kumbe keshatoka Italy.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2008

    Michu! sometime hawa viongozi wetu wawe wanashauriwa, znz hakuna umeme siku ya 20 leo...huo ugeni wa sullivan wa nini japo kempinski wana jenereta? au ndio misifa ya viongozi wetu wa kibongo?
    Zanzibar Bila umeme inawezekana.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 06, 2008

    Nani mpambaji?? NI Monica?? Kweli pamependeza tunaomba kujua mpambaji kaka Michu

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 06, 2008

    yani wabongo kwa kupamba kiboko,maandalizi yalikuwa si mchezo naamini wageni wamejifunza mengi kupitia sullivan hii Arusha, watakuwa mabalozi wazuri kuwapasha wenzao uzuri wa TZ na ukarimu walioupata kwa jamaa zao huko US.
    hongera sana JK kwa kuwezesha kuitangaza TZ, kwa sekta ya utalii na michezo hiyo umejitahidi sana na watz tunaona mabadiliko siku hadi siku,sasa sullivan imeisha shughulika na mafisadi.
    Ms Bennett

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 06, 2008

    afadhali karume amerudi na kuwakaribisha wageni zanzibar japo wapate upepo wa kisiwani na marashi ya karafuu lol.isingependeza kama wangeondoka bila mwenyeji wao raisi karume kutokuwepo na kuwakaribisha wajionee ya zanzibar nayo.hongera Karume umefanya vizur kuwepo ingawa dk ya mwishoni.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2008

    jamani bongo tambarare wanaoibeza nchi yetu pole yao,lakini wenyewe wamejionea mambo mazuri watu wamependeza si kitoto.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2008

    nimependa mbunifu wa hii hema,anastahili pongezi kwa kweli.bongo tambarare duh

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 06, 2008

    michuzi huchelewi, kupata news hivi sefue amehamishwa kutoka canada kwenda washington.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 06, 2008

    Michu,
    Shukrani kwa kutuwakilishia hii ngoma 'live'.
    Hiyo hafla ya kufunga kongamano babu ni funika bovu, ilikuwa JUU.

    Mdau wa NY.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 06, 2008

    watawasha kibatari!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...