Kwako Kaka na Wadau wengine.
Nchi zetu zina makabila mengi yenye lugha tofauti na lafidhi tofauti pia. Lakini pia kumekuwa na Kiswahili tofauti na wakati mwingine kulingana na tafsiri za moja kwa moja toka katika lugha tulizozoea.
Na hili sasa nalizungumzia kwa upana wake kuanzaia Kiswahili cha Pwani mpaka cha Visiwani na kile cha Bara (kwa Tanzania ambacho sidhani pia kama chafanana baina ya mikoa) na kile cha Kenya, Uganda, Kenya, Rwanda, Kongo na hata Burundi.
Sasa msaada kwangu ni kutaka kujua kuwa NI SEHEMU GANI WAZUNGUMZAPO KISWAHILI FASAHA?
Nawakilisha
Bandio M.T


Nafikiri nionavyo mimi wahaya ndiyo wenye kiswahili fasaha kwa hapa Tanzania.....au??
ReplyDeleteWazenji na watu wa lamu mombasa ndo wenye kiswahili chao bwana, hawa wengine tunaiga tu.
ReplyDeleteWewe huwez kulinganisha Mzawa na mjaleo.. kwa hiyo usiweke Kenya Uganda Rwanda na Burund Congo katika List ya kiswahili fasaha.. Ni sawa na kuiweka Tanzania au Nigeria katika kulinganisha Kiingereza na England...
ReplyDeleteLabda Useme ulinganishe Pwani na Bara..
Na kiswahii fasaha ni Cha PWANI na sipendinginepo...
kumbuka kabla ya nchi kuanzishwa na wakoloni nchi ulizotaja kwawengi ni Wabantu. Pwani Wabantu wali mix na waarabu kuishi na biashara, kwa hiyo kiswahili cha pwani kina kiaarabu kingi. Jinsi unavokwenda west ndio kiswahili original unakipata. Conclusion yangu kiswahili cha kongo ndio 'Fasaha' kwasababu waarabu hawakufika kule kwa sana. Nakuachia na hili, identity yako kwanza iwe kabila yako, pili Ubantu,( kwa mimi naishia hapo) kwa wengine, Dini, alfu nchi au vice versa. Waafrika nirahisi kuwa 'brainwash' mambo mengi tuyayofanya sasa ni kufata na kuiga utamaduni wa watu, ukifata asilia zetu unaonekana mshamba hatuna pride at all.
ReplyDeletewewe na Anoy wa kwanza najua ni mhaya kama kawaida yenu mnajisikia nakujivuna acha uongo kwanza wahaya lafudhi yenu haipendezi kwenye kiswahili labda wazaramu wa jijini Dar wanaweza wakasema wanakiswahili m fasaha kisicho athiriwa na lafudhi yeyote.
ReplyDeletewewe ndo unazungumuza kiswahili fasaha na familia yako. maswali haya peleka bakita acha kupoza muda wa watu itakusaidia ukijua hilo.
ReplyDeleteNilitoa comment pale kwa Haki-ngowi kuhusiana na Standard Dialect ya Kiswahili...
ReplyDeleteKuongezea tuu ni kwamba:Lahaja Rasmi ya Kiswahili yaonekana imechukuliwa kutoka kwenye Dhana ya KISWAHILI NI KIARABU; ambayo yapaswa kutupiliwa mbali...na Badala yake twende na Dhana ya Kiswahili ni KIBANTU na hivyo Lahaja Rasmi kuwa Kiswahili Cha Dar aS it contains mchanganyiko wa Makabila yote
MWISHO:JIBU ZURI LATOKA KWA EIDHA WALIMU WA KISWAHILI AU WANAFUNZI WA FORM ONE KWANI NI TOPIC YA KWANZA YA SOMO LA KISWAHILI SEKONDARI
Hapo wadau inabidi kuelewa maana ya wanaozungumza kiswahili fasaha na wanaoongea kiswahili cha pwani ya afrika mashariki.
ReplyDeleteWanaoongea kiswahili cha pwani ni Waunguja,WaTanga(waja/leo/waondoka leo), Mombasa, Malindi, Lamu. watu wengine kama Wazaramo,Wamatumbi, watu wa Lindi, Mtwara kiswahili chao kinaingiliwa sana na lafudhi za kabila zao mfano Kidengeleko, Kimakonde n.k.
Baada ya hapo sasa wazungumzao kiswahili fasaha ni wale wote waliosoma shule zenye kutumia kiswahili ktk kufundishia shuleni na pia wale waliosoma lugha ya kiswahili kama somo(subject). Hapo utapata wamasai, wahaya,wamakonde,
wadigo, waluhya, wabaganda,waluo, wa-lubumbashi, waingereza,n.k.
Si ajabu kumkuta mmatumbi anaongea kiingereza fasaha kuliko wazaliwa wa Uingereza, mfano hai ni Raisi mstaafu Ben Mkapa wa Tanzania na hata kuna watanzania wanafundisha waingereza kiingereza fasaha ktk vyuo vya Marekani na Uingereza.
Mdau
Rocky
London.
Unatafuta kitu ambacho hakipo. Hakuna kitu kinaitwa kiswahili fasaha kulingana na makabila au hata nchi. Kiswahili ni kugha na kwa kawaida ligha inakua.
ReplyDeleteUfasaha au usahihi wa lugha unatokana na makubaliano ya namna ya ktumia misamiati na miundo yake kwa watumiaji wa lugha hiyo. Baada ya kukubaliana ndipo swala la ufasaha na usahihi linakuja kwa yule anayetumia lugha hiyo nje ya makubaliano kuambiw akuwa hazungumzi lugha fasaha.
Kwa hiyo ndugu yangu ukitaka kiswahili fasaha nenda BAKITA au Chuo kikuu watakupatia njia sahihi ya kutumia maneno ya kiswahili.
Hakuna kitu kama kiswahili au hata akiingereza fasah kulinganana makabila au nchi. Labda uulize asili ya kiswahili au kiingereza si ufasaha wake.
Ndio maana kuna kitu kinaitwa lugha za mitaani katika kila nchi. Ni za mitaani kwa kuwa hazijakubaliwa kuwa rasmi.
tanga bwana, asikudanganye mtu, tanga ndo kwao kwa kiswahili, pangani, kasoro lushoto tuu kwa kina shelukiondo ndo wanakoharibu lugha,
ReplyDeleteSwali ni kwa kuwa nililogundua ni kwamba wanaojifanya kuwa na Kiswahili fasaha ni wale wasiokijua vema. Wenye kuongea saaana na kuweka "kiswahili katuni". Wenye kiswahili halisi ndio wachekwao wazungumzapo, waonekanao "waporipori" na watu wakuja. Nadhani kuna tofauti kati ya "Kiswahili Halisi" na kile kitwacho "Kiswahili cha Kisasa" na hapo ndipo wengi wachanganyapo na hata wale wenye kiswahili halisi wanakipoteza kwa kutaka kuonekana "wa kisasa".
ReplyDeleteKwa hiyo tuchangiapo (kwa wale mjuao) tuelezeni "dialect" halisi ya kiswahili iko ama inapatikana sehemu gani? Na ni Ipi LAFIDHI HALISI ya KISWAHILI isiyoathiriwa na laafidhi ya lugha asilia? Hivi kwani wanaosema kuwa hawana lugha asilia walikuwa wakiongea nini kabla ya ujio wa walioleta Kiswahili?
Bandio M.T
kusema kweli, lamu, mombasa wala zenj hawana kiswahili fasaha. Mtu wa lamu badala ya kusema mchuzi anasema nchudhi, mzenj nae badala ya kusema 'hicho' anasema 'hiko' au badala ya kusema umenielewa? anasema 'umenifahamu'. kiswahilli fasaha si sauti ya kuremba ila ni matamshi makini yanaoendana na maana halisi.
ReplyDeleteKiswahili fasaha kipo Tabora kule anapotoka Mheshimiwa Spika SS. Ni hayo tu
Nyie wote pamoja na mtoa mada naona hamjui maana ya Kswahili fasaha.
ReplyDeleteKiswahili fasaha ni kile kilichomo katika vitavu vya kufundishia au kinachotumika katika usomaji wa taarifa za habari katika TV na Radio zamani kilitumika pia katika kuandika habari za magazeti.Hiki kiswahili Fasaha hakina maneno ya mitaani.
Kiswahili wanachoongea watu huko mitaani ni kiswahili fasihi yaani kina mchanganyiko wa lugha za mitaani na lahaja mbalimbali.
Kuongea kiswahili fasaha maana yake ni kutotumia hizo lugha za miataani sasa ni wapi katika nchi za wazungumzao kiswahili hawatumii lugha za mitaani?.
Hakuna sehemu yoyote wanayoongea kiswahili fasaha zaidi ya vitabu vya jufundishia masomo mbalimbali vilivyoandikwa kwa kiswahili na usomaji wa taarifa za habari Radioni na katika TV au magazetini(yale yanayofuata uandishi bora)
Napenda kuunga mkono baadhi ya wadau na kupingana na baadhi ya wadau pia. Kiswahili fasaha ukitaka kukijua fatilia historia ya wabantu na waarabu kwani kiswahili ni mchanganyiko wa lugha za kiafrika (kibantu)na kiarabu na pia baadhi ya maneno ya kireno na kingereza, na hii ilitokana na watawala (wareno,waingereza)na wafanya biashara (waarabu)kujaribu kutafuta lugha ya kuweza kuwasiliana na wenyeji(waafrika). Sasa kwa minajili hiyo ndipo kiswahili kilipozaliwa. Kwa lugha ya kiswahili inaitwa 'lingua franca'-yaani lugha kwa yenye malengo ya kukidhi haja ya mawasiliano baina ya makundi mawili (waafrika na waarabu au wazungu). Angalia pia misamiati kama 'creole' na 'pidgin' kule jamaica na sieraleone. Utaweza kutafautisha baina ya hizo lugha na kiswahili.
ReplyDeleteKuhusu kiswahili fasaha utakipata zile sehemu za pwani ambapo waarabu walikua na nyendo zao za kibiashara, nazo ni Zanzibar na Mombasa. Hizo sehemu nyengine nyendo hizo zilikua hafifu ndo mana pia kiswahili chao ni hafifu kimisamiati. Watu wa bara wanalugha zao za asili kwa hiyo hawawezi kua na kiswahili fasaha, kidogo watu wa Tanga (ile ya zamani). Kwa mfano neno 'lugha' lina asili ya kiarabu sasa mtu ambae hajasoma Kurani au kuzaliwa sehem za mwambao 'gha' inamshinda na badala yake anatumia 'ga', kwahiyo 'lugha' atasema 'luga'. Huyu kweli atasema anazungumza kiswahili fasaha? Mfano mwengine utumiaji wa 'l' na 'r'. Kuna makabila mengi tanzania bara wanachanganya hapa sehemu ya l wanaweka r au kinyume chake hii ni kutokana na lafudhi za lugha zao za asili.Hawa hawawezi kusema kwamba wanazungumza kiswahili fasaha.
Achana na hicho kiswahili fasaha lugha always inaexpand na kuevolve according to mazingira bin environment na especially na these globolaizenesheni times and all that makorombwezo siku hizi mambo yote ni KISWANGLISHI tuu........... soo wewe tell me hapa mimi hujaniundestand zaidi kuliko hao wenye roots zao ama vipi ??
ReplyDeleteBaadhi ya watanzania walio wengi na hao waganda,wakenya wanaongea lugha mbili mfano kichaga na kiswahili,kihaya na kiswahili,kijaluo na kiswahili kisukuma na kiswahili jibu lako litakuwa ni wazanzibari ambao hawana lugha nyengine ni hicho hicho kiswahili na kiswahili chao ni fasaha.
ReplyDeleteLamu Kenya na Kama sikosei kuna sehemu visiwa vya Unguja na Pemba wanaongoza kwa kuongea Kiswahili fasaha.
ReplyDeleteKuna tofauti mbili hapa lafudhi na maneno yanyewe
ReplyDelete1-kwa lafudhi wenzetu wengi wa mikoa ya bara mwa tz wanachemsha kwenye kiswahili sina haja ya kutaja mikoa nikisema bara inaeleweka kidogo tanga wanajitahidi pili wa zenji kwakua wana mix sana na uarabu basi kunabadhi ya maneno yalio mixna kiarabu wao wanayatamka fasaha sasa lafudhi zuri wandugu penda msi pende ni sisi wazaramo wa dar haswa tuliotokea msasani,mbweni kunduchi ndio tuna lafudhi fasaha ya kiswahili pili ukija kwenye maneno ndio kabisa wamikoani wanaharibu sana huwa natamani kuwachapa mfano kunawenzetu jamani wao wanasema wajemeni na mengi tu,ukija zenj wao kuna tofauti kubwa ya maneno mfano bomba la maji kwao mfereji sokoni wao marikiti ila wao piaukiondoa hilo la toufauti ya maneno basi wanakiswalili fasaha pia,hizo nchi nyingine ah zimo tu kwenyelist lakini kiswahili mwenyewe mtz........acha nirudi zangu hyena squeare maana huyu sist ananichekesha mara ananihuzunisha,kuna dem anasema watu wanauza nyu####kamahawana akili nzuri,mwisho huyu sist kanifanya nijione mwenye bahati kua hapa nilipo na hakuna cha ajabu nilicho fanya kwamungu kunilipa neema hizi na yule dada kua pale alipo ni mamlaka yake tu..binadam tuwewenyekushukuru na kuoneana huruma maana hukuna kati yetu mwenye haki yakupata shida wala mwenyehaki ya kuneemeka ila ni mapenzi ya mungu, tusijisahau waungwana
We Anonymous wa Kwanza lazima utakuwa Muhaya tu .... tena yule wa Muleba
ReplyDeleteWakuu wangu heshima mbele kama kawa, ninaomba kuweka mpya kutoka Dodoma:-
ReplyDelete1. Leo asubuhi Mbunge Chenge, alichukuliwa na polisi na kuepelekwa kituo cha
polisi Dodoma mjini, kwa mahojiano ya muda wa karibu masaaa matatu kuhusiana na
kitendo alichokifanya majuzi cha kujaribu kuweka "Uchawi" kwa baadhi
ya wabunge wenziwe ndani ya bunge, kitendo ambacho kilikamatwa na vinasa picha
vya jengo vilivyomo ndani ya jengo la bunge, Dodoma.
2. Mheshimiwa Mkapa, kwa mara ya kwanza leo amehudhuria kikao cha siri cha NEC,
kinachoendelea toka jana usiku, mjini Dodoma, ameonekana akiwa hoi na amechoka
sana, wachunguzi wa siasa hawaelewi ni kwa nini baada ya Mkapa kukataa kwa
makusudi kuhudhuria vikao mbali mbali vya cc na NEC vilivyopita, safari hii
ametokea bila ya taaarifa kuhudhuria kikao hiki, ambacho kimeitwa ghafla sana.
3. Gavana wa Benki kuuu Bwana Ndulu, kwa mara nyingine aliiitwa mbele ya kikao
hiki kutoa maelezo mazito sana, kuhusiana na ishu za EPA, na zingine za
ufisadi, according to the dataz ni kwamba alishambuliwa sana kwa maswali ya
wajumbe huko ndani.
4. Hali ya Mbunge Shujaaa Mwakyembe, sio mbaya sana lakini sio nzuri pia, sasa
hvii ninapooandika yumo njiani kuepelekwa Dar, kwenda kuangaliwa zaidi kiafya
na wataaalamu wa juu wa afya nchini, inasemekana kuwa chanzo ni sangoma ya
Chenge.
5. Kwa niaba ya wananchi wengi hapa, tumewasiliana na Mbunge Kimaro, ili aweze
kuja na kutupa yanayojiri kulingana na haitma yake kiuongozi na all the ishus
za siasa za taifa kwa ujumla, tunategmea kupata jibu rasmi baadaye kuhusu
kupatikana kwake na siku, then tutawasilaina na wakulu wengine hapa na hasa
mkulu MMMJ.
Ahsante Wakuu, na Mods naomba ikisha expire iepelekwe popote, ni kuhabarishana
tu kinachoendelea kwenye siasa za taifa letu!!
haiwezekani ukasema mhaya ndo anajua kiswahili kwani ukiachilia dar unapokwenda mikoani kiswahili kinakuwa influenced na lugha (mother Tongue) ya kabila katika mkoa husika mfano ukienda mwanza kiswahili chao kinakuwa na lafudhi ya kisukuma,wapare vivyo hivyo, hivyo siyo kiswahili pure na mikoa mingine kadhalika mimi nasema watu waishio dar (sijui tuseme kabila gani) ndio wasemao kiswahili safi hakina lafudhi ya lugha nyingine
ReplyDeleteKwanza tungerejea nyuma kabisa tulikotoka kwa kuangalia muundo wa kiswahili na matumizi yake na hii ndo itatupa maana ya zaidi ya kiswahili fasaha. Kuna kanuni, sheria na taratibu ambazo huendesha mfumo mzima wa lugha na hivyo vipengele vikifuatwa katika lugha yoyote basi mzungumzaji ama mwandishi wa lugha hiyo twaweza kumuita mtumiaji wa lugha husika kwa ufasaha. Lafudhi katika lugha yoyote ni kitu cha kawaida maana tulio wengi tunatawaliwa sana na lugha mama. Ngoja nitoe mfano mmoja wa lugha ya kiingereza Ãnayozungumzwa Uingereza (England). Ukimsikiliza mwingereza wa London, na mwingereza wa Liverpool au Manchester utagundua ya kuwa wanaongea lugha ile ile kwa kufuata misingi na matumizi sahihi ya lugha yenyewe ya kiingereza lakini matamshi yao yatakuwa tofauti kabisa hii inatokana na kanda tofauti wanazotoka. Kiswahili ni vile vile, Ukimsikiliza mkongoman, mtanzania, mganda, mkenya, n.k. utagundua tofauti zao dhahiri kabisa. Sasa tukirudi ni kwa nani anaongea kiswahili fasaha jibu lake haliwezi likapatikana mara moja, maana kiswahili wakati mwingine kinaongewa kama dialect kwa maana ya kwamba kuna maneno yanayotoholewa kwenye lugha mama kutoka kwenye eneo husika. Wataalam wa Kiswahili wameliweka hili bayana wametunga vitabu mbali mbali ambavyo vinatumiwa na vyuo mbalimbali katika kuendeleza kiswahili fasaha na katika mitaala hiyo ndimo tunamoweza kupata jibu sahihi ya swali lililo ulizwa. Imani.
ReplyDeletenashkuru ndugu yangu kwa kutaka ufahamu zaidi juu ya hili suala la,kwa urahisi zaidi ni kukutaka kukujulisha kua, neno swahili limetokana na lugha ya kiarabu SAHEIL(watu wa pwani)sasa utakuta moja kwa moja waswahili ni watu wa pwani mashariki mwa afrika,na ndio maana napenda ujue kua kabla mombasa haijauzwa na sultan wa zanzibar kwa wangereza(wakoloni)ilikua yote hiyo inaitwa zanzibar hadi visiwa vya kismayu(somalia)zaidi nitafute mkombozi@hotmail.co.uk
ReplyDeletekiswahili sanifu kiko mikoa mitatu tu hapo bongo,mara,kagera na kilimanjaro wengine wote bado wanajifunza
ReplyDeleteMbega
MTOA MAONI NAMBA MOJA NIMEKUFAGILIA SANA,TAALUMA YAKO IKO JUU NA SANAA ULIYOTUMIA IKO JUU,WATU AMBAO HAWAKUWA NA UELEWA WA HARAKA WAMEDHANI WEWE NI MHAYA!!!NA KUANZA KUKUPONDA.NA MIMI NAONGEZEA SANAA.'KISWAHILI FASAHA NI KILE KINACHOZUNGUMZWA NA WATANZANIA WENYE ASILI YA KIASIA(WAHINDI)'.NIHITENI NA MIMI MDOSI BASI,MSIKURUPUKE TENA TUMIENI AKILI.
ReplyDeleteyou people,achana na sisi bwana,me muhaya,nitajua wapi swahili.LUGHA ya kwanza kujua ni kihaya,alaafu najua english,baadae ndiyo najifunza kiswahili.hiyo kiswahili ni ya zaramo na hata wachagga,sisi NO
ReplyDeletekiswahili original ni cha kibantu hakina kiaarabu east Kongo ndio wanakiongea. kiswahili mnacho shauriwe ukisome kwenye vitabu sio authentic bado kina kiaarabu.
ReplyDeleteSuala la kusema kipi ni kiswahili fasaha siyo rahisi kujibiwa, kwasababu hauwezi kulinganisha kiswahili cha dar na unguja, au unguja na mombasa, dar na bara, hebu nenda sehemu kama konde (pemba) sikiliza wanavyo ongea harafu niambie ni kiswahili ulicho zoe au ni lugha asilia ya pemba?
ReplyDeleteMkombozi ametupa maana ya swahili kuwa ni watu wa pwani, je hiyo pwani ni ya afrika mashariki au pwani yeyote ya duniani? je kunatofauti kati ya pwani na visiwani? Je nini maana ya pwani?
je waarabu walipokuja kufanya biashara waliishia unguja tu? tazama takwimu ya watu wa waunguja kwa sasa na rudi nyuma miaaka 100 je unadhani kulikuwa kuna watu wanagapi unguja? amabao walikuja magharibi na kuwafanya watu waongee kiswahili? wengi walio kuwa sio kama walikuwa nao ni wafanyabiashara walikuwa wakulima na waligeuzwa watumwa na wapagazi! hivyo sio kusema kuwa wao ndio wajua kiswahili fasaha, inakubarika kuwa kiswahili kina maneno mengi ya kiarabu kiliko lugha yeyote ya mkoloni lakini huwezi kusema kuwa mwarabu nae anajua kiswahili, hivyo watu wa zenji kusema kuwa wao kwa sabuu baadhi yao wanaongea kiarabu ndiyokuwa kuwa na wanakiswahili fasaha, hilo halipo akilini ,
Kwa mtazamo wangu ni kuwa kiswahili hakina mwenyewe na kama mwarabu alipita kutoka bagamoyo, tabora, ujiji mpaka kongo ambako tip tip aliishi kwa muda kote humo kulikuwa na wabantu wengi tu hivyo mwarabu au mkoloni yeyote yule alihitaji kiswahili kuwasiliana na wazawa.
Hivyo hakuna kusema kuwa kiswahili fasaha ni cha pwani au bara au kongo cha muhimu ni kuelewa ukisema maharage, mahalage, maharange,karibu, kalibu, fanta, fanda, malkiti, sokoni vyote sawa ilikhali amaana ipo palepale.
Zanzibar na wala hili halina mjadala.
ReplyDeletekiswahii fasaha bwana cha kimasai au kisukuma si mnaona masanja anavyokiwezea
ReplyDeletekiswahili fasaha kinaongewa ZANZIBAR hili wala halina mjadala, na huyo mdau alosema kuwa zanzibar wanasema kiko baada ya hicho inaonesha hajawahi kufika zanzibar, kiswahili cha zanzibar ni kile kilochoandikwa kwenye vitabu, yaloandikwa kwenye kitabu na matamshi ya kiswahili ya zanzibar ni sawa sawa, wala sio watu wa bara au lamu au mombasa wanaongea kiswahili fasaha, mtu wa bara utamsikia anasema sungula baada ya sungura, na mtu wa lamu na mombasa utamsikia anasema naamka kuchelewa baada ya nimechelewa kuamka, kiufupi kiswahili fasaha ni ZANZIBAR hili mutake musitake
ReplyDeleteMNAKUMBUKA KABLA YA MWALIMU KUWA KIONGOZI WA NCHI WAKTI ULE TANGANYIKA KISWAHILI KILIKUWA SIO WENGI WANAOKIZUNGUMZA NA BAADA YA MWALIMU KUWA KIONGOZI WA TANGANYIKA KWA WAKATI ULE NDIO AKATANGAZA RASMI KUWA SASA KISWAHILI KIWE NDIO LUGHA YA TAIFA NA WENGI WAKALAZIMIKA KUKISOMA NA KUJIFUNZA NA NDIO MPAKA LEO KUNA WENGI KINAWAPA MASHAKA KUKIZUNGUMZA
ReplyDeleteLahaja Rasmi ya Kiswahili inaitwa KITUMBATU!!!Hayo ndiyo maamuzi ya BAKITA ila nahisi wakati umefika wa kusema Kiaswahili ni KIBANTU na Kufanya Dilaect inayozungumzwa DAR Es SALLAM ndiyo LAHAJA RASMI YA KISWAHILI.
ReplyDeleteEti mtu wa Kwanza kuona Mlima KILIMANJARO ALIKUWA MZUNGU!!!
Hatupendi kujivunia Vyetu.
Kiswahili ni chetu
Mngoni2
Lugha hukua na kubadilika. Zaidi yapo makosa ya grama mengi yanayokubalika na yasiyokubalika - kutegemea unamuuliza nani. Kwa mfano Mbasa hapo juu katumia neno "hauwezi" kitu ambacho mwalimu wangu wa kiswahili aliwahi kunipiga sana na kuniambia natakiwa niseme "huwezi". Hivi karibuni nimesoma mdau mmoja akiandika "...hivi hawa hawanaga mtu wa kuwashauri..." - naamini ni ndugu au jirani yangu huyo. La muhimu ni kwamba hata hao wazenji mnaowasifu kwa kiswahili wana grama mbaya sana wakati mwingine. Kusomesha ni kufundisha wakati Mbasa (naamini mbariadi huyo) angeelewa kumlipia mtu gharama za shule (tena zenji skuli).
ReplyDeleteMatatizo haya yapo katika lugha zote. Ni kingereza kipi kizuri? Msikilize Ally McCoist au Sir Alex Ferguson akiongea. Ukiwa kaskazini mwa uingereza dinner huliwa mchana wakati ukiwa kusini watakushangaa.
Huyo alieuliza swali labda angeanza kwa kutafuta ainisho la kiswahili fasaha - angetuweka busy kujadili hilo kwanza kabla ya kuamua ni wapi wazungmzao kiswahili kizuri. Labda masihi angetukuta hatujamaliza hilo akatusaidia...
Hivi mnajuwa historia inasemaje juu ya kiswahili, sasa niwadokeseeni kidogo tu kwamba ni WAJERUMANI NDIO WATU WA KWANZA KUENEZA KISWAHILI Tanganyika wakati wanatutawala, walisisitiza elimu ifundishwa kwa kiswahili masuleni hadi chuo kikuu, kwa bahati mbaya hatukuwa na chuo kikuu wakati wa utawala wao lakini shule zote masomo yote yalikuwa yana fundihwa kwa kiswahili, mambo yalibadilika baada ya vita kuu ya kwanza baada ya kushindwa vita na kunyang'anywa koloni na kupewa waiingereza ambao wasisitiza kutumika kwa kiingerreza ili wapate wafanyakazi wa kada za chini ili wawasaidie kutawala, watu kama matarishi hivi. Kiswahili kinachozungumzwa Tanzania kote ni fasaha bali hutofautiana lafudhi/accent kama vile waiingereza wa London wanavyotofautiana na wa say Liverpool, Newcastle, Glasgow watu wanazungumza kiingereza lakini ni accent tofauti kabisa kiasi kwamba kama ni mtu wa Africa huwezi kujuwa kama wanachuzungumza ni English, na kwa kuongezea tu mtu anayeweza kuzungumza lugha yoyote ile kifasaha ni yule ambaye ameisomea hata kama ni kiswahili watu wengi wa mitaani hatuzungumzi lugha fasaha kama inavyotakiwa.
ReplyDeleteHuyu bwana hajakosea kuuliza, na jibu lake ni watu wa pwani au kwa kiswahili fasha tunawaita watu wa mwambao ndio wenye kuzungumza kiswahili fasaha, huwezi kuniambia kuwa kila unapoelekea coast ndio wanazungumza kiswahili fasaha hiyo sio kweli, hao wanaotoka west ndio wanaochanganya kiswahili na maneno ya lugha za makabila yao ambapo kiswahili hicho kinatumika kwa baina yao tu. Lakini mtu wa pwani anaeleweka popote pale panapozungumzwa kiswahili.
ReplyDeletelugha ya pwani iliyosambaa kuelekea bara baada ya serikali kulazimisha kuwa lugha ya taifa ndio maana watu wa bara hawataki kuamini kwamba kiswahili asilimia kubwa kuna kiarabu kwasababu zao binafsi.kiswahili lugha ya mwambao kuna jamaa hapo juu amasema kiswahili fasaha ni cha congo nadhani si kweli,kiswahili asili yake pwani kimetokana na mchanganyiko wa kabila za pwani na kiarabu.huo ndio ukweli hakuna cha kupotosha hapo
ReplyDeleteWadau wengi naona wamezungumza kwa jazba na pengine kejeli na mzaha mwingi.Majibu ya wengi nilioyasoma kwa makini naona waliojibu hawakutafakari kwa makini kwani kinachopaswa kueleweka hapa ni kwamba, kuna tofauti baina ya asili ya kiswahili ni wapi na wanaozungumza kiswahili fasaha ni akina nani.Kiswahili asili yake Pwani kwa kuzingatia kwamba, pwani wakazi wake wengi ni Waislamu, basi Waislamu ndiuo wanaozungumza kiswahili fasaha na mchango wao katika kiswahili haukanushiki wasiojua hayo wafahamu.
ReplyDeletenjooni nyaluland (iringa)tuwafundishe kiswahili fasaha..
ReplyDelete