Michuzi na Wadau, naomba msaada wenu.
Rafiki yangu na mkewe ambao wote wapo kwenye miaka arobaini hivi wameishi pamoja kwa miaka 14 sasa bila ndoa rasmi.Bwana ni mkristo(mkatoliki) na mkewe ni muislam mzuri tuu.
Wamefika mahali kwamba kwa sasa wanataka kuweka mambo yao sawa kwa maana ya kufunga ndoa, lakini kikwazo ni dini zao.Wawili hawa wana maisha mazuri sana.
Baba ana kampuni yake binafsi ambayo ni bomba sana, na mama ni afisa mkubwa katika shirika moja kubwa hapa nchini. Pesa kwao sio tatizo kabisa. Kila mtu ana chanzo kizuri cha income.
Baba nanihii anapenda sana ukatoliki wake, na mama nanihii anaupenda sana uislamu wake.
Wawili hao wanapendana sana na wamejaliwa watoto wawili wazuri mno, msichana na mvulana.Baba hayupo tayari kuwa muislamu, na mama pia hayupo tayari kuwa mkatoliki.
Solution wanayoitafakari sasa ni kutengana/kuachana kwa sababu ya ki-imani, japo miaka ya mwanzo mama alishapromisi kuwa mkatoliki, lakini akaghairi baadaye.
Je wadau,uamuzi wanaoutaka kuutoa wa kutengana?
NAWASILISHA.
MDAU A-TAUN


hao labda kama wanataka kutengana kwa sababu zingine na sio za kufunga ndoa. Mimi ni mkatoliki na ninazifahamu sana taratibu za kanisa katoliki zinavyosema kuhusu masuala ya ndoa. sisi katika kanisa katoliki hatuzuii ndoa mseto, yaani watu wawili wa imani tofauti ikiwa mmoja wao sio mkatoliki. ni ndoa inayoruhusiwa katika kanisa katoliki, hivyo kama kweli wanataka kuhalalisha ndoa hilo sio tatizo, wawaone viongozi wao wa kanisa watawaambia, sisi kwetu ni ruksa kwa sharti kwamba hiyo ndoa ni lazima ifungwe kwa madhehebu ya kikatoliki. hivyo binafsi sioni kikwazo kama kweli wanataka kuhalalisha kuishi kwao pamoja kama mke wa mume wa ndoa. nawatakia maamuzi mema ya yenye busara zaidi ila kutengana kama sababu ni kila mmoja kushika imani yake sio busara!!
ReplyDeletesi wakafunge ndoa mahakamani! Kama hakieleweki kwenye dini basi nenda mahakamani! Kusema kweli cha maana ni sheria itambue muungano wao maana kwa sasa ikitokea bahati mbaya mmoja akachukuliwa kutoka haya maisha itakuwa ni ngumu mno kwa mwenzake na watoto kupata chochote kisheria! Lakini ingekuwa fresh na Mungu akatambua pia muungano wao...lakini hilo ni juu yao!
ReplyDeletewalichemsha toka mwanzo kunanihii bila sheria. hata hivyo watoto ndio wa kuonewa huruma. kwa kuwa kila mtu hataki kuacha dini yake na kila mmoja anajifanya kichwa ngumu, basi si waendelee hivyo hivyo na uchafu wao kama walivyoamua huko nyuma? au wakafunge ndoa ya serikali, wajinga kweli hao, masikini watoto....
ReplyDeleteKwa kuwa umesema wanapendana sana na wamejaliwa kuwa na watoto tena wazuri sana, na kwakuwa wanazipenda dini zao basi kila mmoja abaki na imani yake na wafunge ndoa ya Kiserikali, ambayo haifungamani na dini yoyote! Katika mafundisho ya dini tunahaswa kuzitii mamlaka kama serikali, hivyo basi taratibu zinazowekwa na serikali ni halali na haziwezi kuwa chukizo machoni pa Mungu.
ReplyDeleteDini ni imani, Dini sio kama Chama au klabu leo upo simba kesho upo yanga. Na imani inakuwa ipo ndani ya moyo wa mtu. Sasa mapenzi yao ni mazuri sana lakini imani za dini zao zimezidi imani ya mapenzi yao. Sasa la muhimu ni kuachana tu kwani hamna aliye tayari kubadili dini yake kwa ajili ya mwenzake. Lakini la muhimu vile vile ni kufikiri watoto maana wao ndio watapata shida.
ReplyDeleteKwangu mimi sioni kama ni busara kama watatengana ukizingatia umri wao pamoja na watoto waliowapata. Mimi naona kama walivyoishi tangu awali kila mtu na dini yake ila tatizo litakuja kwa watoto kwa misimamo ya wazee itawasumbua wapi waelekee kiimani. Kama wamechokana ni ruhusa kutengana lakini kama swala ni imani tayari wameshakosea fomula tangu mwanzo hivyo kupata majibu sasa hivi ni vigumu, nawashauri kama wanapendana waende serikalini wakayamalize ili kila mtu afuate imani yake lakini busara kubwa itumike kuhusu imani za watoto wao. Tunatakiwe tujifunze kupitia huu mfano ili tutengeneze fomula nzuri ya ndoa ili tusije kuwa na migogoro mbele ya safari
ReplyDeleteMdau wa pwani comment yako ni nzuri sana, naiita ni mwaka 2008. Hawa wamechokana wanataka kuweka vikwazo vya kuachana, si waseme tu, wanawasumbua watoto tu, wahana adabu wote!
ReplyDeleteAnonymous wa 3:16 hapo juu kakosea kabisa. Na mimi nina tatizo kama alilolielezea mdau. nimeweleza padre wangu hapa Moshi na akasema hakuna ndoa ya kanisani kati ya muislamu na mkristo. Ndoa mchanganyiko ni possible na waanglicana, walokolole, na waluteri. Wengine hawaruhusiwi.
ReplyDeleteKweili inauma sana kwani unakuta mwenzio unampenda lakini dini inakuwa kikwazo.
kumbuka mkatoliki akifariki akiwa anaishi na mwanamke wa kiislamu hazikwi kamwe na uongozi wa kanisa, wakati mwanamke anayeishi na mkristu yeyote akifariki bado viongozi wake wa kiislamu watamzika kwa heshima za dini yake.
shida ipo hapo wadau. Maisha haya tunaishi sawa, lakini tujue kwamba kuna siku ya siku ambayo tunaitwa kurudi kule tulikotoka kwa mujibu wa imani zetu.
Hapa ndo napaona hapatoshi.Imani ya kidini wakati mwingine inazidi upendo uliopo kati ya wapendanao. Nadhani shida yetu sisi ambao tupo kwenye ndoa mchanganyiko ndo hiyo, kwamba pamoja na kubusiana na kukumbatiana, kila mtu anaelekea kwake kiimani. Inauma sana sanaaaaaa. Tuambieni sisi tunayoishi katika hali hiyo tuwaambieni ndugu zanguni. Tunateseka.
kama ni kweli wanapendana,basi hawawezi kutengana sababu ya dini, ama mmoja kumwambia mwingine haje kwenye dini yake huo kwangu mimi ni upuuzi.nyie oaneni,maombi kila mtu anamuomba mungu,sema majina ya huyo mungu yanatofautiana lakini mlengwa ni huyo mungu, kuhusu watoto wala msiwe na tabu, wataangalia wao wenyewe ni dini hipi inawafaa watafuatwa, labda wataamua wawe na dini ya mungu.(dini ya mungu: kumuabudu yeye na si kuuabudu uslamu wala ukristo)
ReplyDeleteitakuwa ni ujinga wa hali ya juu sana kwa wao kuachana kwa sababu ya dini tuu,na adhabu kubwa itakuwa ni kwa watoto wao maana strees ya divorce kwa watoto ni kubwa sana(God knows),miaka 14 na watoto wazuri na wanasema wanapendana then why kuachia vitu vizuri kama hivyo katika hii dunia just kwa sababu ya tofauti ndogo tuu ya dini ambazo zote zinaamini mungu mmoja...waache uppuzi!
ReplyDeleteKuhusu hawa wawili mmoja muislamu(mwanamume) na mungine mkristo(mwanamume)ambao wameishi kwa muda mrefu kabla hawajaoana na sasa inashaindikana hivyo kutokana na utofauti wa dini maoni yangu yapo hivi: Tukiangalia kwa mtazamo wa dini ya kiislamu mwanamke haruhusiwi kuoana na asiyekuwa muislamu.Hii inatokana na Maagizo ya Muumba kwenye kitabu chake kitukufu yaani Quran.Kama mwanamke ataamua kuoelewa na asiyekuwa Muislamu ajuwe tu kuwa amevunja moja la agizo la Allah.Na pia mwanamke ajiulize mwenyewe swali anafunga ndoa kwa kumridhisha nani? Kwa muislamu aliyemakini jambo analolifanya kwanza anaangalia kama Allah ameridhika, halafu anaangalia maslahi mengine.Yani kwanza maisha ya milele halafu maslahi ya dunia.Kwa upande wa ukristo sijui msimamo uko hasa upande upi yani ukristo unazungumziaje swaala la ndoa kwa ujumla kati ya mkristo na asiyekuwa mkristo. Mtazamo wangu ni huo tu na aliyekuwa na mawazo mengine anaweza kuongezea kwa maslahi ya hawa wawili ili wawe na maisha bora hapa duniani na kesho akhera.Kila la kheri.
ReplyDeleteKabla dini hazikuletwa kwetu, issue ilikuwa ni kabila, je hao ni kabila moja au tofauti? Muhimu sis wote ni wabantu, kama kabila hazina matatizo katika swala hilo waoane kiutamaduni. Imani za dini tuaachie hao wageni walizotuletea. Kumbuka walikuwa na lengo la kututawala. Wabantu wa Tanganyika (Tanzania) tuungane na kuchana na dini za kigeni.
ReplyDeletehivi wewe yanakuhusu nini lakini?au umbea tu wa ndoa za watu.siwapendi visukununu kama nyie,kutwa kufatilia ya watu.embu waacheni
ReplyDeletesina uhakika kama huko haya mambo yapo, lakini nakumbuka kuna kitu kinaitwa bomani ambako huwa watu wanaweza kwenda kufunga ndoa, huku niliko mimi hili swala huwa haliumizi kichwa kabisa kwani kuowa mnakwenda tu na vitambulisho vyenu kotini, mnapewe leseni ya ndowa na mnapewa orodha ya majaji mnachagua wenyewe yupi wa bei nafuu na mnaempendelea,ndoa inafungwa wala haichukui dakika tano ilimradi mke na mume wote wanatakiwa wawe na mashaidi wao wa kutia saini.hii haijali wewe dini gani, rangi gani,mrefu,mfupi,mwembamba, mnene ilimradi wote mmekubaliana kuona basi kinaeleweka kwa kwenda mbele. sasa sioni kwanini iwe vigumu kwa hao watu kama kweli wapo. haya mambo ya mila na desturi sio saa zote yanatakiwa yazingatiwe
ReplyDeleteMbega
MIMI SIJAMUELEWA MTOA MADA KWASABABU SIJUI MAANA YA NDOA RASMI.INAWEZEKANA WAMEFUNGA YA KISERIKALI AMBAYO KWA UELEWA WANGU NI NDOA RASMI PIA.LABDA SASA WANATAKA KUFUNGA YA KIDINI.OTHERWISE MDAU WA A-TOWN FAFANUA HAPO AU STORY INAKUHUSU WEWE SASA UNAJARIBU KUPATA EVIDENCES ILI UKAMSHAWISHI MWENZIO!!
ReplyDeleteNi jambo zuri kujua kwamba NDOA hufungwa na SERIKALI na wala siyo madhehebu za dini. Hili ni swala la kisheria. Madhehebu huwa ni wakala tu. Ndiyo maana vyeti vya ndoa vinavyotolewa huwa ni vya Serikali.
ReplyDeleteKwa hali hiyo, na kama kweli hawa wanataka kuendelea kuishi maisha mazuri kama walivyokuwa hapo mwanzo, basi wafunge ndoa yao serikalini.
Nawatakia kila la heri!
Jamani pole sana maana hapa ndio huwa dini inakuwa ngumu kwenye map[enzi kwani mapenzi hayana dini. Mimi ndio maana enzi hizooo nadeti mtu alikuwa akinipa salamu tuu kama kama kanivutia kabla hatujafikishan mbali bora ukajua kasimamia dini gani , na kama sio dini yako na wewe hauko tayari kubalikika na una msimamo mkali basi bora uende mbali muwe tuu marafiki au sahau. Ushauri wangu mimi kama Mwanamke wa Kiislamu na katika huu upeo wangu mdogo wa dini niliokuwa nao katika uislamu ni kwamba Mwanamke wa Kiislamu haruhusiwi kuolewa isipokuwa na Mwanaume wa Kiislamu, na ukija kwa upande Mwanaume wa Kiislamu basi yeye huwa anaruhusiwa kuoa Mwanamke wa Ahlil-Kitabu yaani aliyetoka katika dini ya vitabu vinne tunavyoamini kuwa vya Mwenyezi Mungu namely Injili , Zaburi Torati FurQan (Qurani) ila hapa sharti lake ni kwamba Watoto wanaotoka katika uhusiano huu ni lazima wawe waislamu yaani wafuate dini ya baba. Narudia tena ninanyoelewa mimi na huu upeo wangu mdogo wa masuala ya dini Hii ina maana ya kwamba Mwanamke wa Kiislamu haruhusiwi kuolewa na dini nyingine kubwa ni kwa sababu ya kizazi chake kwani mtoto huwa anahesabika wa baba ndio maana hata mkioana makabila tofauti watoto kabila wanafuata la baba, kwa mimi ninavyoelewa hii ndio sababu ya msingi ya mwanamke wa kiislamu kuamrishwa asiolewe zaidi ya na muislamu mwenzie, sasa sijui pale ambapo baba atakubali kwa mapenzi yake kuwa watoto wamfuate mama inakuwaje. Lakini ukweli ni kwamba hii ni mara chache sana kutokea kwa mfano hai mimi katika familia yangu ya karibu tuna dini zoote mbili na pande zote zina nguvu sasa watoto wamekuwa wakitangatanga sana na kutokana na hili wanakuwa kama hawana dini na hii imesababisha matatizo mno kwa kweli, sasa imebaki kwa wale waliokuwa na kuoa au kuolewa kufuata dini za mapartner wao. Sasa hapa mimi naomba tuu kumalizia ya kwamba nimetoa mfano wa niliyoyaona kwenye familia yangu na nimeongea jinsi ninavyoelewa mimi soo kam kuna mataaluma huku msinioshee vinywa kama nimekosea nikosoeni mnieleweshe la msingi tu ni kwamba hili swala kwa kweli its about time tulizungumzie humu blogini kwetu kwa sababu ni tatizo sio la mmoja ni la wengi sana tean dini na mapenzi ni ngumu hata mimi ningekuwa sina msimamo wa mapema leo yanngenikuta kama hayo kabisa nimebakia na urafiki wa karibu na muhusika na nashukuru Mungu amenijaalia mwenzi wangu wa dini yangu na watoto wawili tunawafundisha dini kama wajibu wetu na tuna mapenzi ya hali ya juu...... Wahusika nawaombea wavute subira na hapo msilazimishane kubadili dini kwani kubadili dini mtu atake mwenyewe kwa niaba yake sio kwa kulazimishwa, wewe bwana na bibi kila mmoja wenu aamue kuoma dini ya mwenzake aielewe kiokamilifu ka imani yake na ajiulize ni kwa nini mwenzake yuko kwenye dini hiyo ?? Uislamu unasema soma dini na dunia , na kama muislamu tunashuritishwa kutafuta ufahamu wa mambo na kwamba mtu usije ukatumia excuse ya ujinga ana nilikuwa sijui hiyo ni dhambi sasa wewe bibi na bwana kila mmoja wenu nawashauri kabla hamjafikia kuachana kila mmoja wenu kaeni chini muulizane kwa nini wewe uko dini hii sababu za msingi, ukishajua kwa nini dini hii na sio ile chukueni hizo sababu zenu bibi nenda kanisani na bwana nenda msikitini fanyeni "mafundisho" kila mmoja ajifunze dini ya mwenzake aielewe kiundani na nina imani mkifanya hivyo kwa moyo safi bila ya kujiwekea vizingiti basi mmoja wenu ataamua kumfuata mwenzie na mtafikia uamuzi wa mwisho. Sasa hii habari ya kuachan wakati mmeshakuwa woote muda huu wote na watoto mimi naon huo ni Uselfish ndio maana mwanzo nilisema mngeyajua hayo ya dini tangu asubuhi msingesogeleana sasa mnataka kuwachanganya hao watoto mzungu anakwambia " U make yoour bed you lie on it " sasa mmeshafikia hapo mlipo mimi sioni kama kuachana ni solution ........Deal with it !!Jamani kaka Michuzi samahani nimeongea sana duu
ReplyDeleteMichuzi, this topic is very interesting, as it addesses issues realted to the body and soul. What the body loves may be hated by the soul and vise versa.
ReplyDeleteRemember that as one gets older, things pertaining to his spiritual life start taking the lead role in his/her life. Remember that children will become adults and begin their lives one day. As an adult, the next step is old age and eventually death becomes the REALITY.
The material side of one's life is nothing, if his soul is not at peace. That is why I AM DARING to tell the couple in conflit to seperate in peace, so that everybody lives well according to his/her faith.
Children cannot suffer because most of the time they are in school, and they get all possible assistance they want. Remember that they are told that the separation between their parents did not come because of any wrangle among them, but because of their God-searching souls.
Let any decision that you take pleases Gon and not man.
Huko ni kutokuwekana wazi mapema na hili tatizo la kupingana ktk ndoa kutokana na tofauti za kidini linazidi kushamiri siku hadi siku.DAWA YAKE NI UWAZI.Uwazi huu unatakiwa mapema zaidi ili kieleweke whether baba atyakua anaenda church na mama masjid.watoto je wataenda wapi? tuweni makini sana na hili... Nadhani hawa wamechokana.........ILA WATOTO HAO KISHERIA HAWATAMBULIKI...INAUMA SANA
ReplyDeleteAnon unayesema kwamba padre wako kakukatalia habari za ndoa mseto, nadhani huyo padre wako ana sera za kutaka kuongeza waumini, mimi nasisitiza hoja yangu tena kwamba ndoa mseto kwa wakatoliki zinakubalika rasmi. mimi nasema hivyo kwa vile nimeshazishuhudia nyingi sana na pia naifahamu sheria ya ndoa ya kanisa katoliki, ndo maana nasema hivyo, huyo padre wako atakuwa na lake jambo, na kama unabisha hata ukienda katika makanisa mengi tu Dar Es Salaam kuna ndoa kama hizo, mfano nilikuwa chuo kikuu pale Mlimani, nimeshuhudia ndoa kama hizo, pia binamu yangu kaolewa na mwislam kwa ndoa iliyofungwa katika kanisa katoliki, pia nimeishi uaskofuni Songea na nimeshuhudia mwenyewe ndoa mseto zikifungishwa pale, sasa kusema kwamba hazikubaliki, mie napinga, tena hizo mseto ninazokueleza ni mkatoliki na muislam, hivi kama padre wako hapo kakukatalia, wewe nenda uliza sehemu nyingine, kwani kama unaishi mjini makanisa yapo kibao na yanakubali hiyo habari! nasisitiza kwamba ndoa mseto na muilsam zinakubalika na nimeshuhudia mwenyewe, mmojawapo akiwa ni binamu yangu kabisa!!
ReplyDeleteJambo la kwanza kabisa ni kuwa hakuna ndoa ya dini fulani wala dhehebu fulani, ndoa zote ni kwa mujibu wa sheria ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kifupi ndoa zote ni za Serikali. Hivyo hakuna sababu ya kusumbua na eti mimi mkristo wewe budha au vinginevyo.
ReplyDeleteMbili, waroma wanakubali kufungisha ndoa kati ya mroma na mtu anayefuata dini nyingine au hata asiyeamini, na hii ni kwa mujibu wa biblia, haisemi kama ni lazima watu wawe wakristo ndo waoane au lazima ndoa ifungwe kanisani.
Tatu na la msingi, kwa mujibu wa sheria za kiislamu, mtoto huyo waomzaa wakiishi pamoja kama mtu na kimada wake, ni haramu na wala hawezi kuhalalishwa kamwe. Kwa ufupi ni kuwa hawezi kuwa muislam. Kwa hiyo iwapo hawa watu watafunga ndoa kanisani mtoto aweza batizwa na kuwa mkristo safi tu na ndoa yao ikawa halali machoni pa mungu na serikali na jamii. Na iwapo mama ataamua kubadili dini na kuwa mkristo itakuwa bora zaidi kwa kuwa familia nzima watakuwa wakiabudu pamoja. Katika hali aliopo sasa, hasa mama, sijui kwa undani sana sheria za uislamu zinasemaje kuhusu mwanamke anayezaa nje ya ndoa, ila nakumbuka yule mama wa Nigeria aiyekuwa apigwe mawe mpaka kufa. Kama hii inaaply kwa mama huyu pia, sioni ni kwa nini aendelee kung'ang'ania kuwa muislamu, ni heri akabadili dini na kuwa mkristo tu kwani huko wote wapokelewa kwa raha na amani, hakuna kuadhibiana.
Nne, ndoa ni ya watu wawili wanaopendana na wameamua kuishi pamoja mpaka kufa kwa shida na raha. Iwapo kuna mmoja wao anaona kuwa siku za karibuni anawea kuamua kuishi kivyake, ni bora wasioane. Au kama kuna mmoja hampendi mwenzake ni heri kutofunga ndoa kabisa nakila mmoja achukue ustaarabu wake, isipokuwa hatima ya mtoto iamuliwe kutokana na hali halisi na maslahi ya mtoto mwenyewe. Ushauri wangu, mtoto hakubaliki katika uislamu, hivyo ni bora wampeleke kanisani akabatizwe tu.
Tano, Kwa kuwa kama nilivyoeleza awali kuwa, ndoa ni ya watu wawili mwnamume na mwanamke wanaopendana na wameamua kuishi pamoja mpaka kufa, ndugu hawana nafasi katika kuamua nani amuoe au aolewe na nani, haipo katika uislamu wala ukristo hata upagani. Mtu halazimishwi mtu wa kumuoa wala kuolewa naye, hivyo kusema kuwa ndugu hawakubaliani na muungano wenu ni kisingizio tu cha kuficha ukweli kuwa hakuna mapenzi wala nia ya kuoana kati yenu. Waamuzi wa hatima ya maisha yenu ni ninyi wenyewe wawili, mkizingatia maslahi ya mwanenu na yenu pia.
Narudia kusema, kama mapenzi hamna kati yenu, msioane na kama mnapendana kwa dhati na mpo tayari kufunga ndoa, hakuna wa kuwazuia wala kuwaamulia mfungaje bali mfungie wapi, hamuwezi kufunga ndoa msikitini hata baba akislimu kwa kuwa mmesha lala na kuzaa pamoja kabla ya ndoa. Msikitini hamkubaliki kwa hali yeyote labda mdanganye, kitu ambacho ni upuuzi iwapo ninyi mnataka kuishi halali machoni pa Mungu na jamii.
Hitimisho, kaeni chini mfikiri na kuzingatia ujumbe huu, fanyeni maamuzi kutokana na nyoyo zenu zinavyowatuma. Ninyi ndo mnaotaka kuishi pamoja na ni ninyi mtakaojibu maswali siku parapanda likilia.
Kwanza hapo walipo wapo kwenye ndoa! Sheria inasema mkiishi miezi 6, mnatambuliwa kama mume na mke! Waseme wanataka kuhalalisha maana wapo kwenye ndoa kwa muda mrefu!
ReplyDeleteSwala la kutengana ni choice kama walivyokua na choice ya kuishi pamoja! BTW wakati wanaanza kuishi walimshirikisha nani?
Hivi tukisema waachane halafu wasiachane, si tutaonekana tuna kiherehere na hatuwatakii mema! And who cares kwa kuwa pamoja au kutokua pamoja!
Nafikiri swala la kutengana ni CHOICE yao wawili, mtu huwezi ingilia CHOICES za watu!
Ushauri wa bure tu kwa wadau wote ni kwamba kama un imani na dini yoyote ile halali basi hakuna ndoa inayochnganya dini,ama mume amfate mke au mke amfuate mume na si kinyume chake.
ReplyDeleteNdoa ya kiserikali(bomani) inakubalika tu kiserikali lakini kwa mujibu wa imani zetu za dini (hasa wakatoliki)hapa ndugu hujaoa bado,upo kwenye uzinifu kama yule ambaye hajaoa kabisa.
Hivyo ndugu licha ya kupendana pia suala la dini lina nafasi yake,kwa maana ya kwamba chaguaneni wale tu mnaofanana dini ili kuomdoa mgogoro ambao ni lazima utakuwapo pindi linapokuja suala la kufunga ndoa hasa mkiwa dini tofauti.
me nahisi upendo umeisha hapa na dini sio kigezo cha wao kutokufunga ndoa na pia nashaka sana na baba kuwa kweli anazijua sheria za ndoa za kikatoliki
ReplyDeleteushauri wa bureee....
wafunge ndoa ya mseto pale kanisani (katoliki) kila mtu atabaki na ndoa yake
hata hivyo nampa pole baba huyo hao watu ni vigeugeu sana
anony June 24, 2008 4:20 PM, nijuavyo mie kislamu unatumia ubin au ubinti wa mama yako. mfano waulize wanaoandika vibao vya alama za makaburini.
ReplyDeleteHuyo bwana anayejiita NGWENGWE, kweki ni ngwenge, busara zimepungua. Lakini ndoa ya nini aada ya miaka 14? Kwa nini muanze kuzungumzia dini sasa hivi? Au mmoja wenu ana 'upper hand', na anajaribu kutingisha kibiriti? Nakubaliana na wengine, mmoja kamchoka mwenzie!
ReplyDeleteLakini, ndoa za mseto maanake nini? mimi mwislamu, nikapige goti kanisani na kubatiza wanangu --maana hili hamlisemi--ukifunga ndoa mseto kikatoliki, wanao watabatizwa!
Dini si vitu vya mchezo, hatuwezi kuvi-discuss humu Bw. michu! Penzi ni bahari nyingine--kila mtu anajua yake--wengine hufumania,baadae wakawaomba msamaha wenzao, kwanini walienda kwenye fumanizi.
Wako wanaoamini ndoa ni mkataba wa milele, wengine tunaamini ni mkataba wa hiyari na unaweza kuvunjwa 'by mutual consent' au kwa shinikizo.
Hao watu wasituzingue, kama wanataka ku-call it quits, let them do so. Wakubaliane watoto ni vipi!
NB. Bw Ngwenge, hakuna watoto wa haramu kwenye Uislam, wako watoto wa zinaa! Watoto wa haramu ni 'concept' ya wazungu--naamini siyo ya Wakristo! Kwa lugha ya wenzetu, wanaitwa 'bastards', kudadadeki!!
Watoto wa haramu ni wale wanaolishwa mali ya haramu kama mali ya uizi, rushwa au ufisadi.
Mimi ni mzee wa kanisa. Yaani Kiongozi wa jumuiya na kanda katika kanisa katoliki. Katoliki wanaruhusu kufunga ndoa mseto na kila mtu akaendelea na imani yake. Isipokuwa watoto walelewe katika imani ya kikatoliki. Hapo ina maana kuwa mama akafunge huko kanisani. Upande wa pili kwa Waislamu kama sikosei hiyo wao hawaitambui kama ndoa bado ataonekana anaishi na hawara mpaka hapo watakapofunga ndoa ya kiislamu. Kama wanapendana wasali sana li roho mtakatifu awaongoze na kufikia maamuzi yenye faida katika familia yao. Mama wa kambo, baba wa kambo kwa watoto ni hadithi moja ndefu na mpya kabisa. Ombeni mtapewa, pigeni hodi mtafunguliwa kwa maombezi yenu
ReplyDeletekaka michuzi hili swala la dini si la mzaha kabisa, watu wengi huwa wanalichukulia kirahisi rahisi sana, dini ni imani ya mtu alionayo kwa Mungu wake mi binafsi huwa siafiki swala la wawili waliamua kuwa pamoja wakiwa na dini tofauti mmoja kumlazimisha mwenzie abadili, kamwe huwezi badili imani ya mtu na mmoja(mlazimishaji ) anakuwa hamtendei haki mwenzie. mimi naamini kuwa Mungu ndo anaweza kumbadilisha mtu kutoka hali flani kwenda hali flani na sio mwanadamu, mimi kama mkirsto ninae amini biblia sioni sababu ya kulazimishana kubadili nanukuu kitabu cha 1 wakorintho 7:12-17 inasema (iwapo ndugu mmoja ana mke asieamini na anakubali kukaa nae asimwache vivyo hivyo kwa mke kwa maana yule mume hutakaswa kwa mkewe na mke pia hutakaswa kwa mkewe. lakini yule asieamini akiondoka na aondoke na hapo mke au mume hafungiki, lakini Mungu ametuita kwa amani. kwa maana wajuaje wewe mume kama utamwokoa mkeo na wewe mke kama utamwokoa mumeo,lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu na kama Mungu alivyomwita kila mtu aenende vivyo hivyo.jamani kama mtu unaona unamsimamo mkali bora tafuta wa imani yako kuepusha matatizo baadae.
ReplyDeleteMs Bennett
anonymous wa 3:53 Maoni mazuri
ReplyDeleteKi ukweli Imani ni jambo lichanganyalo sana.
Nani mkweli?Islam,Budha,mkristo,sikki,mlokole?
Jamani watoto!Nyie mmeshapata mlichokuwa mnataka.
Huyu aliyetoa hoja hii, naomba airekebishe, haina ukweli, ina ajenda ya siri, eti`Tatu na la msingi, kwa mujibu wa sheria za kiislamu, mtoto huyo waomzaa wakiishi pamoja kama mtu na kimada wake, ni haramu na wala hawezi kuhalalishwa kamwe.
ReplyDeleteHakuna mtoto `haramu', tendo ndilo la haramu. Mashekhe mpo wapi, angalieni sana hizi nukuu zilizokosewa.
m3
kama tatizo ni dini na wanataka wafunge ndoa waende kwa mkuu wa wilaya huyo anon no,1 anasema katoliki watawafungishia ndoa huyo ni muongo kabisa hakuna kitu kama hicho ni lazima mmoja abadilishe dini kama wote wanaimani yao wenyewe basi waende huko nilikosema na kila mtu abaki na imani yake mwenyewe
ReplyDeletesweet
Arusha
kama huyo mwanamke aliahidi kubadili dini kumfuata mume wake na kuolewa kanisani na sasa hataki, anamfanya mwanaume wake awe anaishi maisha ya uzinzi.Kama mwanamke hataki kabisa kubadili dini basi ushauri wangu kwa huyo mkatoliki ni kwenda kumuona paroko wake amueleze kila kitu kwa uwazi na ukweli ampe ushauri utakaofaa kwa ajili ya kuokoa roho yake. kumbuka mwili utakufa na kuoza lakini roho inaishi milele. uchaguzi ni wako maana mungu ametupa akili na utashi na ndio maana hamshurutishi mtu kufuata amri zake lakini ametupa ili tuchague: tuzitekeleze tukaishi naye au tuzipuuze tukaishi na shetani motoni. hakuna midway.
ReplyDeleteHao wanandoa walishalikoroga sasa walinywe. Kwa maana kwamba wao hayo wangeyaelewa kwanza kabla hawajaoana, kuwa eti dini imekuwa kikwazo sasa? na ni kipi kilowashtua sasa, na kuvumbuka kwenye upofu wa mapenzi walokuwa nayo mpaka wakatanabahi kuwa wanatakiwa walingane kiimani? Biblia inasema msifungamane na wasioamini na uislam unasema tusioe manasara(wenye imani tofauti)kwanza waslimisheni mkisha muwaoe/muolewe. Hekima hiyo ni tangu enzi za mitume na masahaba, na ina maana zake moja ni hiyo inayojitokeza hapo ingawa wameshindwa kutwambia kuwa walishachokana au wanauroho wa kugombea watoto wawe imani ipi, sasa wanakuja na misimamo ya kuogopa kuwa makahaba wa imani, kwa maana ya kukataa kutangatanga na kuingia katika imani nyengine. Ukweli ni kuwa mmeshachelewa, sasa hivi kuwa na mvuto wa kumrejeza mwenzako kwenye imani yako ilitakiwa kipindi kile cha mahaba motomoto ndo pakushawishiana au kuachana kabla, watani wanasema "mchuzi wa mbwa huliwa wamoto ukishapoa haunyweki" sio sasahivi washajuana madhaifu na kuchokana, mnatia vipingamizi vya dini ili muachane.
ReplyDeleteUshauri ninaowapa hao wahusika wajifunze kuhusiana imani zao zinasemaje juu ya kila mmoja kwa kuwapa msaada mdogo we muislam katafute kanda za shekh Nassour Bachu mhadhiri huyu alielezea vizuri amechanganya maelezo yote akitoa kwenye biblia na kuraani.Mkristo soma biblia inasemaje hasa wakorinto wakwanza mlango wakumi na tatu, mpashane khabari lipi litakalo wafaa kwa sasa kwa faida yao ya maisha ya baadae au ya sasa. na kwa kuwaongoza watoto wao katika njia ya haki, na isiwe kwa kulazimishana,ni kwa kuridhiana.
kweli huyu anayejiita Ngwengwe inaonekana busara zimempungua kama hazijamuishia. jamani mtu kama huna ufahamu wa dini fulani usitoe mtazamo kwani inakuwa ni upotoshaji kabisa. watu wengine madhali tu wachangie waonekana wanaandika sana. Halafu blaza michu uache kutuchokonoa ukiona tumetulia unaibuka na kitopic kipya. Wadau mnachonga sana kuliko kutoa ushauri kwa aliyeuliza.
ReplyDeleteThis is too ridiculous ,sacrificing your marriage because o religion it's too crazy.Where do they want to go and do kama si ufuska tu wanaenda kufanya.Just seat together and sort out your issues >14 years ni nyingi mno and could not let them go easily like that.Kama mmechokana sema ukweli lakini si dini.Where do you want your kids to go or because you've money that's why .I'm telling you bitterly ,you will see the consequences in few days to come.And none of your Gods in either side you will be serving nor pleasing unless you are not praying a real living God.
ReplyDeleteTake Care my friends and don't take this for Granted
Haya somo tosha kabisa hilo!, wengine mjifunze kupitia hapa mana hata km umependa vp wakati mwingine inabidi uwe na vigezo ili baadae usije kujuta
ReplyDeletesalaam
mdauXXXL
Hawa bwana WAMECHOKANA haiwezekani leo mwaka wa 14 ndio wajue tofauti zao za kidini, hapa mwanaume kesha pata dogodogo nyingine ndio anataka kumwacha mwanamke au mwanamke kesha pata bwana mwingine, lakini inakuwaje mwanamke mwanzo akubali kuwa atakubali kubadili dini na badae ageuke? Mie na hisi mwanaume amemkosea huyu mama kiasi mwanamke haoni sababu za kubadili dini wakati mwanaume heshima hakuna tena. ILA mie ningependa kuwatahadharisha wawili hawa kuwa mafanikio ambayo kila mmoja ameyapata kwa kipindi walichokaa ni nyota zao zimeendana sasa wasione ajabu watakapo tengana mambo yao au mmoja wapo maisha yakaanza kumwendea kombo hili waliweke akilini pia, alafu pia mbona wanakuwa mafedhuli je watoto wao wataishi maisha gani baada ya wao kutengana? je wamelifikiria hilo pia au wanajifikiria wenyewe tu na raha zao?
ReplyDeleteNgwengwe kakosa nini jama?
ReplyDeleteHebu someni hapa: http://www.uislamu.org/nasaha/nasaha8.htm na hapa
http://groups.yahoo.com/group/jifunzeuislamu/message/721 pia hapa
http://www.uislam.net/ukumbi/archive/index.php?t-894.html
Nanukuu "kwanza
zinaa ni haramu, na sifikiri kuwa kuna mtu anajawizisha, la pili,
yule mtoto wa zinaa ni mtoto wa haramu, na hapewi nasaba ya baba
yake kwa lolote liwalo, na kuoana kwao hakuhalalishi yule mtoto.
" Hii inapatikana hapa http://groups.yahoo.com/group/jifunzeuislamu/message/435
Msiwapotoshe hawa ndugu, baba, mama wanapaswa kupigwa mawe kwa uislamu na watoto ni mashaka tupu. Kama kweli wataka oana njia pekee ni kuingia kanisani na kuwa wakristo, kwa kuwa huko wote wakubalika.
Unadai hakuna watoto wa haramu bali wa zinaa, je, zinaa ni nini? si ni haramu? hivyo basi inafanya watoto wa zinaa = watoto wa haramu.
ReplyDeleteMsitake kukwepesha hoja. Namuunga mkono Ngwengwe
uislamu unasema: Ndoa baada ya zinaa haisihi, na watakaooana kwa namna hiyo huwa wamo katika hukumu ya zinaa maisha yao wasipotengana kwa kauli tunayoitegemea, nayo imepokewa kutoka kwa Masahaba kadha akiwemo Aliy, Bibi Aisha na Ibnu Mas'oud -Allah awaridhie. WaLLahu A'lam.
ReplyDeleteNgwengwe hongera, umefanya uchambuzi halisia kutokana na hoja hasa ya wahusika. Kama kuna upungufu ni mdogo sana, ila ukweli na suluhisho ulilolitoa ni la msingi mno. Watu wote hawa, mume, mke na watoto wao wapo katika mtihani mkubwa mno unaotegeea maamuzi ya baba na mama huyu. Ni kweli iwapo kama kweli wao ni wacha Mungu na wanataka kweli kwnda mbinguni baada ya zinaa waliyoitenda wanapaswa waamue kwa makini sana. Hawwezi kwenda bomani kwa kuwa wao ni wacha Mungu au wanataka kumcha Mungu, wakienda katika Uislam wanapaswa kupigwa mawe na baba atawakosa watoto wote kwa kuwa kiislam si wake ni wa mama. Na kubwa zaidi baba na mama wanapaswa kupigwa mawe au kula mijeredi. Sidhani kama ni uamuzi sahihi.
ReplyDeleteUshauri wangu waende kanisani kwa bwana watubu dhambi na waoane. Kwa njia hiyo familia nzima itakuwa pamoja na watatambulika kwa Mungu pia, kwa kuwa wote watapokelewa mbele ya macho ya Bwana Yesu. Hilo ndilo suluhisho. Kuachana siafiki kwa kuwa hata kama kuna mmoja wao katembea nje ya uhusiano wao, bado hawana ndoa iliyohalalishwa hivyo hawafungiki. Ingawa kisheria watu hawa wameshakaa zaidi ya miaka 14 pamoja na kuzaa watoto wanatambulika wanandoa, ingawa hajafunga. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya jamhuri ya muungano wa TZ. Wazinzi acheni kumshambulia Ngwengwe
HAWA WOTE NI WAZINZI. USHAURI FANYENI HIMA NENDENI KANISANI MTUBU, MUOANE MUMREJEE MOLA KABLA HAMJAFA.
ReplyDeleteKWA SASA HAKUNA HATA MMOJA WENU ANAYEMCHA MUNGU HAPO MLIPO MNAJIDANGANYA TU KWA KUWA HAMJAOANA NA BADO MNAENDELEZA ZINAA. HAMKUBALIKI KATIKA UISLAMU HATA MKIANA. KIMBILIENI KWA YESU, ATAWAOKOA WOTE NA WANENU. ACHENI UPUUZI
wewe SETH there is only one GOD,the one above!!!!shauri zenu...when parapanda ikilia,atleast you were told!!!... Bibles are there,Quarans are there,Wainjili are there,Manabii are there.. YOU WERE TOLD,BUT YOU DID NOT FOLLOW!IF YOU SHALL PERISH UNDER THE SUN IN THE LAST DAY,KNOW THAT YOU WERE TOLD.AM ONLY DOING MY JOB AS A MESSENGER..AM ONLY LETTING YOU KNOW..
ReplyDeleteHAWA SIWALIKUWA MAREKANI HAWAKUJUA KAMA DINI NI KIKWAZO WAMESUBIRI MPAKA WAPATE WATOTO NDIYO WANALETA HAYA MANENO YA UDINI? LABDA MMOJA WAO KAPATA DILI ANATAFUTA SABABU TU HAKUNA CHA DINI WALA NINI WAMECHOKANA TU
ReplyDeleteKwa kuwa Mungu ni mmoja, na Waislam na Wakristo wote wanamuamini Mungu huyo huyo mmoja, hakuna sababu ya kutengana kwa sababu ya imani ya kidini.
ReplyDeleteWameishi muda mrefu pamoja, miaka 14. Kilichowafanya waishi hivyo bila kutengana ni nini na kinachowafanya mpaka wafikirie kutengana leo ni nini?
Kila mtu aendelee na imani yake, kwani kila mtu atahukumiwa kwa mazuri na mabaya yake, kutokana na imani yake.
Ni hayo tu.