Bado tunakukumbuka

Mwaka sasa umepita, bado tunakukumbuka,
Machozi hatujafuta, bado tunahuzunika,
Jina bado twaliita, kumbe ulishatutoka,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.


Ni vigumu kuamini, kuwa ilishatokea,
Machungu tele moyoni,vigumu kuyazowea,
Hupo tena duniani, mbali umeelekea,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.


Ni kama utani vile, ua letu kunyauka,
Nakumbuka siku ile, kichwani haitotoka,
Umekwenda zako kule, mwisho wako ‘lipofika,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.


Amina mpiganaji, mahiri wetu vijana,
Nasi tulikutaraji, ‘ngetusaidia sana,
Mambo yetu kuyahoji, majibu kupatikana,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.


Uliacha changamoto, kwenye timu ya taifa,
Sasa imepamba moto, yacheza kwa maarifa,
Na sasa tunayo ndoto, itat’ongezea sifa,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.


Bunge uliloliacha, sasa kumepambazuka,
Kwa hakika kumekucha, hoja zinajadilika,
Kwa mafisadi kwachacha, kwao moto unawaka,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.


Ila vita ya madawa, bado inasuasua,
Ingawa wanaelewa, moyoni ‘likusumbua,
Dhati kwao haijawa, bado hawajatatua,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.


Amina dada Amina,rafiki yetu wa kweli,
Kama ingewezekana, kulitenda jambo hili,
Basi tungeomba sana, uturejee kimwili,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.


Kimwili haupo nasi, kiroho tupo pamoja,
Ni kweli tunakumiss, tutakwona siku moja,
Familia yakumiss, Mungu aipe faraja,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.


Naweka kalamu chini, bado sisi twakupenda,
Upumzike kwa amani, mahali ulipokwenda,
Mahala pema peponi, malaika kukulinda,
BADO TUNAKUKUMBUKA, RAFIKI YETU AMINA.




Ewe mdau Fadhili, asante we kwa shairi,
Nakuomba tafadhali, uniweke mstari,
usio mshahadhali, katika hili shauri,
Amina twamkumbuka, masikini na tajiri.


Twamkumbuka Amina, tajiri na masikini,
Na la kufanya hatuna, aliyopanga manani,
Anatajwa kila kona, kwamba awekwe peponi,
Amina twamkumbuka, masikini na tajiri.


Na siku zaenda mbio, kama vile ni utani,
Toka saa za machweo, hadi muda wa jioni,
Twaendeleza vilio, wapi Amina jamani,
Amina twamkumbuka, masikini na tajiri.
Hakika sikunuia, kukushukushuru globuni,
Mradi imetokea, acha na mie nighani,
Uchungu umegusia, ulotukaa moyoni,
Amina twamkumbuka, masikini na tajiri.


Kuna waliosahau, mwezi huu alitutoka,
Asante kwa yako mbiu, muda huu muafaka,
Ye si wa kumsahau, watu wa kila tabaka,
Amina twamkumbuka, masikini na tajiri.


Globu yako e fadhili, nimepita kwa yakini,
sikuona ufedhuli, ulojaa duniani,
Haki utafika mbali, kama si leo mwakani,
Amina twamkumbuka, masikini na tajiri.
Kaditama ninaomba, leo nikomee hapa,
Nikizidi kukuomba, daima usiwe kapa,
Endelea kaza kamba, usije ishia hapa,
Amina twamkumbuka, masikini na tajiri.
Salamu zangu za mwisho, mlio kama Fadhili,
Twahitaji burudish0, katika hapa pahali,
Kama hakuna mipasho, hapa ni penu mahali,
Amina twamkumbuka,masikini na tajiri.
- Michuzi




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2008

    Mashairi yote mawili ni mazuri sana hongereni.
    Sema kwa vile napenda kiswahili sana basi Fadhili naomba unisamehe kwa kukosoa kosa lako dogo tu la neno "kukumiss", hapo ndio umeharibu kutumia "kiswaenglish" .
    Mdau mzawa

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2008

    superb!!!
    hivi vipande vimenikuna, fadhili na misoup keep up!!!

    ReplyDelete
  3. Pumzika kwa amani amina.

    Huku safari bado ni ndefu.

    Mh alishakabidhiwa orodha ya wazee wa kupika ugali"unga" lakini kauchuna,sijui tatizo nini.

    RIP AMINA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2008

    RIP Amina, i still love u, even more.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2008

    Amina tunakumis sana. Lala unono mpenzi wa Vijana wote tanzania.

    Wadu mimi naona tutafute siku moja vijana tomark Amina Chivupa's day. na itakuwa tunamkubuka kweli kweli.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 26, 2008

    Pumzika kwa amani, tunawaomba Malaika wanzuri wa Mwenyezi Mungu wakuaangazie mwanga! tunakukumbuka daima mpaka naso tutakapoungana na wewe!!

    Hellen

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 26, 2008

    "kamwe sitaisahau hii siku Amina ni kama halfu an hour before nimeambiwa Amina is no more nilikuwa naongea na mtu tena tulikwua tunaangalia habari ya saa mbili usiku kuhusu bungeni na budget and we said Amina has not yet come jamani hivi anaumwa kiasi hicho, then tukanyamaza na kny akili yangu nikajiwazia tu kama kwamba hivi tukisikia Amina amekufa itakuwaje halafu nikakataa mwenyewe no this cannot happen now after few mins the feeling ikapotea na nikasahau after kama half an hour napata msg Amina has died i was shocked...Leo ni mwaka mmoja ,We love you Amina rest in peace you re always a hero hata iweje you did things which most of us could have never done, you re a queen of your own flavour and will remain always. RIP Amina!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 26, 2008

    hivi yule mumewe mnaemwita sijui mpakanjia au mpunga na njia whatever his name is yuko hai? kwani mara ya mwisho tuliambiwa alikuwa akisaidiwa kila kitu kwa mipira kule hosipitali ya kimataifa ya lugalo

    Mbega

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 26, 2008

    Allah ailaze roho yake maali pema peponi. Twamiss sana. Nami peom yangu laja.

    Masalaam

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 26, 2008

    jamani jamani..tutakukumbuka daima milele!!ipo siku mi na wewe,tutaonana tena mpenzi!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 26, 2008

    Very sad to have a year gone without Amina. I knew Amina when we were together at Kisutu Girls Secondary School. It is very heavy to take it in heart that Amina is not with us anymore, I did not see Amina since We finished our Secondary school but I used to hear her beatiful voice on Clouds FM and later in Parliament. That was enough to make happy coz I knew she was moving on with life and achieve what she wanted to be. I thought one day I would meet her. Unfortnately that was not God's plan. Amina was like my young sissy to me. She used to respect me as her sister. I always remember her humble tone when we were at Kisutu. It was rare by then a fellow student to call you dada but Amina did that to me from the heart. For sure I miss her. I pray for her family epecially parents and Rahman.
    Amina lived her life to the fullest. That makes me happy in the middle of sad moments of remembering Amina. We need to thank God for giving us Amina for the time she lived.
    May God rests Amina Chifupa's Soul in Eternal Peace. Amen.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 26, 2008

    we nae mbega acha ushamba..eti hospitali ya kimataifa ya lugalo..nani aliekwambia..au ulimaanisha hospitali ya taifa ya lugalo!!?!??!hamna chochote cha kiumataifa pale

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 26, 2008

    wewe unaemwita mbega mshamba kwa kuiita hosipitali ya lugalo ya kimataifa inaonyesha jinsi gani ushamba na ukapuku unavyokusumbua,umeshindwa kutambua kuwa imetumika kebei hapo

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 27, 2008

    Da ndugu zangu mmenikumbusha machungu.I still love you AMINA u were my star i adored each step u took RIP sweetheart

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 27, 2008

    "hivi yule mumewe mnaemwita sijui mpakanjia au mpunga na njia whatever his name is yuko hai?"

    Hayo maswali yana mwenyewe, pengine Vicky Kamata anayajua....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...