terni ya mizigo ipitayo reli ya tanga imezinduliwa upya wiki hii baada ya kusitishwa kwa takriban miezi 10 na kuzua malalamiko makubwa miongoni mwa wadau wa huduma hiyo. mdau athumani hamisi aliyeshuhudia hafla hiyo anasema hatua hiyo imepokelewa kwa mikono miwili na wengi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2008

    Train ya CCM au nchi mbona flag....

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2008

    Jamani nielimisheni.

    Hivi huwa kichwa cha treni hakina KIOO. Dereva anaonaje mbele. Au hicho kinachoonekana sio kichwa chwa treni?

    Michuzi saidia please

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2008

    SASA HAPO BENDERA ZA CCM NI ZA NINI?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2008

    SASA HIYO TRENI NI YA CCM?MBONA BENDERA ZA CCM ZIKO JUU?ACHENI KAMPENI ZA UJANJA BWANA...HAPO INGETAKIWA BENDERA YA TAIFA SIO YA CCM.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 20, 2008

    Jamani kama zilivyo Traffic Lights za barabarani,rangi y kijani inaashiria 'ruksa kuondoka' na rangi nyekundu inaashiria 'simama'.Hakuna cha u CCM hapo.Nichukue fursa hii kuwapongeza wote walio husika katika kufanikisha kuanza upya kwa safari za Treni toka Tanga hadi DSM na Vituo vingine nchini.Mabehewa ya Abiria katika Treni ya Kati yaboreshwe ili yafikie kiwango cha kimataifa na huduma ziboreshwe zaidi.Watanzania wengi watapenda kusafiri kwa Treni kuliko Mabasi ya Abiria au hata kwa Ndege especially kutoka Mwanza hadi DSM na kutoka Kigoma hadi DSM.Keep it up!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 20, 2008

    Inaelekea nyie mnaufisadi wa macho na allergy na bendera ya CCM.

    hicho ni kitambaa cha kijani si bendera ya CCM. Umeshaambiwa treni ya mizigo bora wangekuwa abiria labda wangeona hicho unachoita bendera.

    lakini na CUF mnaruhusiwa wakti ikipita kwenye maeneo yenu mpeperushe msibaki kulalama tu. hata mktaka tundikeni kwenye behewa kabisa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 20, 2008

    Wakuu wangu heshima mbele kama kawa, ninaomba kuweka mpya kutoka Dodoma:-

    1. Leo asubuhi Mbunge Chenge, alichukuliwa na polisi na kuepelekwa kituo cha
    polisi Dodoma mjini, kwa mahojiano ya muda wa karibu masaaa matatu kuhusiana na
    kitendo alichokifanya majuzi cha kujaribu kuweka "Uchawi" kwa baadhi
    ya wabunge wenziwe ndani ya bunge, kitendo ambacho kilikamatwa na vinasa picha
    vya jengo vilivyomo ndani ya jengo la bunge, Dodoma.

    2. Mheshimiwa Mkapa, kwa mara ya kwanza leo amehudhuria kikao cha siri cha NEC,
    kinachoendelea toka jana usiku, mjini Dodoma, ameonekana akiwa hoi na amechoka
    sana, wachunguzi wa siasa hawaelewi ni kwa nini baada ya Mkapa kukataa kwa
    makusudi kuhudhuria vikao mbali mbali vya cc na NEC vilivyopita, safari hii
    ametokea bila ya taaarifa kuhudhuria kikao hiki, ambacho kimeitwa ghafla sana.

    3. Gavana wa Benki kuuu Bwana Ndulu, kwa mara nyingine aliiitwa mbele ya kikao
    hiki kutoa maelezo mazito sana, kuhusiana na ishu za EPA, na zingine za
    ufisadi, according to the dataz ni kwamba alishambuliwa sana kwa maswali ya
    wajumbe huko ndani.

    4. Hali ya Mbunge Shujaaa Mwakyembe, sio mbaya sana lakini sio nzuri pia, sasa
    hvii ninapooandika yumo njiani kuepelekwa Dar, kwenda kuangaliwa zaidi kiafya
    na wataaalamu wa juu wa afya nchini, inasemekana kuwa chanzo ni sangoma ya
    Chenge.

    5. Kwa niaba ya wananchi wengi hapa, tumewasiliana na Mbunge Kimaro, ili aweze
    kuja na kutupa yanayojiri kulingana na haitma yake kiuongozi na all the ishus
    za siasa za taifa kwa ujumla, tunategmea kupata jibu rasmi baadaye kuhusu
    kupatikana kwake na siku, then tutawasilaina na wakulu wengine hapa na hasa
    mkulu MMMJ.

    Ahsante Wakuu, na Mods naomba ikisha expire iepelekwe popote, ni kuhabarishana
    tu kinachoendelea kwenye siasa za taifa letu!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 20, 2008

    mbona mnapenda kusema vitu msivyo jua bendera ya ccm ndio hiyo? ama mnalopoka ccm ni njano nakijani na lama yake ni jembe na nyundo gali moshi linapo ondoka ndio deleva hupewa ishara kwa bendela wale walio tumia leli yakati nadhani wanalijua hilo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 20, 2008

    Ndugu Michuzi,

    Naomba kuwaelimisha wahusika kuwa sasa tuko mwaka wa 2008, teknolojia ya treni hii ni ya miaka ya 1970. So, tuko pale pale, tunadanganywa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 20, 2008

    Anon wa 8:45.. hizo 'engine' hazina VIOO. Dereva anatumia upenyo uliopo kila upande wa engine za namna hii kuangalia mbele.. hivyo anakuwa anaona kwa upande. Ukiangalia hiyo Engine hapo kati kuna uwazi kama ambao ndio mlango, basi ndio hapo anapotizamia mbele. Hata upande wa pili nako pako hivyo hivyo. Hii nadhani ni kwa kuwa hizi engine zinavuta kote kote, mbele na nyuma. Huu ndio ujuzi nilioupata kwa kukaa Tabora na Shinyanga muda mrefu. Pengine wenye maelezo ya kitaalamu wanaweza kusaidia zaidi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 20, 2008

    We Anon wa 2.30 Pm acha FIX wewe umeshawahi kupanda treni lakini?, niulize mimi niliyepata kutoa msimbazi na nikapanda kwenye kichwa cha treni ya mizigo wakati fulani nilikuwa na dharura. Ni kwamba treni ina kioo kwa mbele kama unavyoona kioo cha gari kama toyota pick up vile sema engine yake ni kubwa sana kiasi kwamba hicho unachoona mbele ni bonet na kwa kuwa mpiga picha hii alikuwa chini asingeona kioo kwa juu kutokana na ukubwa wa hilo dubwana. upenyo wa pembeni pia unasaidia lakini kioo kipo. wabheja mwanawane

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 21, 2008

    We anon wa 9:27.. kuna engine mbali mbali. Kama ulipanda treni ya mizigo hapo msimbazi, si kuwa umepanda zote. kuna Engine kubwa (heave duty), za kati, na ndogo (ndogo ambazo mara nyingi huwa zina shuttle short distance.
    Hata kama hiyo engine ina kioo, bado dereva anakaa ubavuni na anatumia uwazi huo kama alivyosema anon aliyetangulia. hebu angalia hiyo engine vizuri.. na kama ujuavyo hizi engine ni multidirectional, sasa kama akitaka kwenda ule upande mwingine ataendaje mbele.. hivyo wanatumia huo uwazi. hivyo usiseme FIX kwani ye kasema wataalamu watafafanua zaidi..

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 22, 2008

    TANGA sio mchezo, GARI,NDEGE,MAJI TRENI (nk...).......UNGO.. hahahaha,

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 23, 2008

    NAMI NAWAUNGA MKONO WADAU HIZI NI PROPAGANDA ZA RAIS NA WASHIKAJI WENZAKE WA CCM. WATANGA AMKE MSIKUBALI NYIE TUMIENI UNGO KAMA KAWAAAAA.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 23, 2008

    we anonymous wa 12;21 sasa toka lini hizo bendera zako za kijani na nyekundu zishikwe na hao vigogo wa ccm..??Then mbona hatuoni hizo nyekundu zikiwa pointed down??? acheni mambo yenu bwana...hao ni hawa mafisadi wadogowadogo walio kwenye dili na hao wahindi....!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...